Halima Mdee Mbunge wa Kawe akigeukia pembeni na kuonyesha ishara ya kukataa kuigusa keki ya Shay Rose Banji huku akicheka.
Wabunge
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi
waliangua Vicheko pale wenzao wa CHADEMA walipoikwepa kuigusa nakuila
Keki ya Birthday ya Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Shy Rose Banji
wakati wa tafrija yake iliyofanyika Nyumbani Longe Jijini Dar es Salaam.
Wabunge
hao wa CHADEMA ni Halima Mdee (Kawe) ambaye anaonekana picha ya juu
akiikataa keki hiyo iliyotolewa na Wakurugenzi wa Nyumbani Longe, Gadna
G Habash na Mkewe Lady Jay Dee, huku Mbunge wa Viti Maalum, Lucy Kiwelu
picha ya chini nae akijificha asiitazame kwa karibu.
Wabunge hao waliigwaya Keki hiyo kutokana na jinsi ilivyopambwa rangi za CCM.
Huku
Wabunge wa CCM wakishangilia wakimtaka Halima Mdee aongoze Ukataji wa
Keki hiyo ambayo ilitolewa baada ya keki ya awali iliyoandaliwa na Baby
Girl Shy Rose kuliwa, ilishindikana kuliwa na kuhifadhiwa.
Watu
mbalimbali walihudhuria tafrija hiyo ndogo wakiwepo Wabunge, wanasiasa,
Wasanii muziki, Watangazaji na Wanahabari ambapo kila aliye simama
kuongea alimpongeza sana Shy Rose kwa kuwa Mpambanaji wa Ukweli katika
kutafuta kile anachotaka na kumuombea kwa Mungu amuongoze vyema katika
kazi yake.
No comments:
Post a Comment