Pages

KAPIPI TV

Wednesday, May 2, 2012

AJALI YA BASI YAUA SABA IGUNGA TABORA.


AJALI TABORA - IGUNGA


                         Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Anthony Rutha.

WATU saba wamefariki dunia leo hii asubuhi na wengine 54 wamejeruhiwa vibaya kufuatia ajali ya basi la kampuni ya NBS lililokuwa likifanya safari ya kutoka Tabora kuelekea Arusha.

Kwamujibu wa kamamnda wa polisi mkoa wa Tabora ACP Anthony Rutha ajali hiyo imetokea umbali wa kilomita mbili kabla ya kuingia katika mji wa Igunga ambapo amebainisha kuwa miongoni mwa watu hao saba wanaume ni watatu,wanawake watatu pamoja na mtoto mdogo wa kiume ndio waliofariki katika ajali hiyo huku akibainisha kuwa jeshi la Polisi bado linaendelea na uchunguzi.

Aidha kamanda Rutha amelitaja basi lililohusika katika ajali hiyo ni la kampuni ya NBS lenye nambari za usajiri T 978 ATM lililoanza safari yake majira ya saa 12 alfajiri kutoka Tabora kuelekea Arusha likiwa linaendeshwa na dereva Idd Shabani ambaye kwasasa yuko mahututi.


Kwaupande wake mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Igunga Dr.Joseph Kisola amesema majeruhi wapatao 54 wamepokelewa katika hospitali hiyo huku watano kati yao  hali zao ni mbaya.


Dr.Kisola amebainisha kuwa majeruhi waliobaki huenda wakaruhusiwa kurudi makwao kutokana na hali zao kuendelea vizuri.

No comments: