Pages

KAPIPI TV

Wednesday, July 27, 2016

TANZANIA YASHEHEREKEA SIKU YA MERIT KWA KUKUTANISHA VIJANA KUWAPA ELIMU KUHUSU SDGs




Katika kusherekea Siku ya Merit ambayo huadhimishwa kila Julai, 24 ya kila mwaka, vijana mbalimbali nchini wamekutanishwa kwa pamoja ili kuweza kujadili kuhusu Maendeleo Endelevu (SDGs) pamoja na kuweka mipango jambo gani lifanyike ili kuhakikisha kila raia anapata elimu kuhusu SDGs.

Akizungumza na Mo Blog kuhusu siku hiyo, Mwanaharakati wa Maendeleo Endelevu, Rose Mmbaga alisema kwa Tanzania mwaka huu wamekutanisha vijana kwa pamoja na kujadili jinsi gani wanaweza kusaidia watu wengine kujiunga katika utekelezaji wa Maendeleo Endelevu (SDGs).

Mwanaharakati wa Maendeleo Endelevu, Rose Mmbaga akitoa neno la ufunguzi katika kongamano lililokutanisha vijana ikiwa ni katika kusherekea Siku ya Merit. (Picha zote na Rabi Hume, MO Blog)

Alisema pamoja na kukutanisha vijana pia wamekutanisha mashirika mbalimbali ya ndani na nje ya nchi ambayo yataweza kuelezea jinsi gani yanafanya kazi, jinsi ambavyo yanaweza kuwasaidia vijana na jinsi ambavyo wanaweza kusaidiana na Umoja wa Mataifa (UN) ili kutekeleza Mipango ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

"Kwa mwaka huu tumekutanisha mashirika ambayo yameungana nasi katika kuadhimisha Siku ya Merit lakini pia tuna vijana ambao wameshamaliza vyuo kwa sasa wanatafuta ajira, vijana waliomaliza kidato cha sita na wengine wamemaliza kidato cha nne," alisema Rose.

Mwanaharakati wa Maendeleo Endelevu, Rose Mmbaga akizungumza katika kongamano lililokutanisha vijana na kupata elimu kuhusu Mipango ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

Alisema kuwa wameamua kukutanisha vijana wakiamini kuwa bado wana nguvu na wanauelewa mpana hivyo ni rahisi kwa wao kutumika kutoa elimu kwa watu wengine ambao bado hawajawa na uelewa kuhusu SDGs

Aidha alisema hiyo ni moja ya hatua za awali ambazo wanazifanya kwani wanatambua kuwa kundi kubwa la vijana bado lipo mtaani na hivyo baadhi yao wanataraji kwenda katika mkutano wa kujadili Maendeleo Endelevu (SDGs) utakaofanyika New York, Marekani na baada ya kurejea watarudi na mipango mkakati ambayo wataitumia kufikisha elimu kwa kila mtu ili ajue SDGs ni nini na jinssi gani inaweza mfikia. (Na Rabi Hume - MO Blog)

Mwanaharakati wa Maendeleo Endelevu, Rose Mmbaga akiendelea kuzungumza na vijana kuhusu SDGs.

Mwanaharakati wa Maendeleo Endelevu (SDGs), Nicolaus Mukasa akiwapa elimu washiriki kuhusu SDGs.

Baadhi ya wawakilishi wa mashirika yaliyoshiriki kongamano hilo wakielezea jinsi mashirika yao yanafanya kazi, jinsi yanavyoweza kuwasaidia vijana na kushirikiana na Umoja wa Mataifa (UN) ili kusaidia kusaidia kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).











Baadhi ya washiriki waliohudhuria kongamano hilo.





Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.

Saturday, July 23, 2016

MBUNGE WA VITIMAALUM MKOA WA TABORA BI.HAWA MWAIFUNGA ATOA MSAADA WA CHEREHANI KWA MWANACHAMA WA CCM

Mbunge wa vitimaalum mkoa wa Tabora Bi.Hawa Mwaifunga akimkabidhi Cherehani mmoja kati ya Wanawake wa Tabora mjini kwa lengo kumsaidia ili aweze kujikimu kimaisha baada ya kutengwa  na mumewe kufuatia kuugua kwa muda mrefu.
Hawa Mwaifunga akijaribu kuifunga vizuri Cherehani hiyo mpya kabla ya kumkabidhi Mwanamke huyo mwenye familia ya watoto watatu akitegemea kuendesha maisha yake kwa kufanya vibarua vya kufyatua matofali ya kuchoma.


JESHI LA POLISI MKOA WA DAR ES SALAAM LAINGIZA SH.MILIONI 198 KATIKA ZOEZI LA KUHAKIKI SILAHA 14107

 Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna, Simon Sirro, akisisitiza jambo wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Ofisini kwake Dar es Salaam leo mchana alipokuwa akitoa taarifa ya matukio mbalimbali ya uhalifu pamoja na mchakato wa uhakiki wa silaha.
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna, Simon Sirro, akiwaonesha waandishi wa habari bunduki aina ya gobore walioikamata kabla ya kutumika kwa ujambazi wakati akitoa taarifa ya matukio mbalimbali ya uharifu pamoja na mchakato wa uhakiki wa silaha mkoani humo leo mchana.
 Kamanda Sirro akionesha simu walizokutwa nazo watu wanaodaiwa vinara wa kupora simu kwa kutumia pikipiki katika maeneo mbalimbali ya jijini.

 Wapiga picha za vituo mbalimbali vya televisheni wakichukua taarifa hiyo.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.


Na Dotto Mwaibale

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limefanikiwa 
kuliingia mapato taifa ya sh.milioni 198 kutokana na zoezi la uhakiki wa silaha lililofanyika mapema mwaka huu.

Jeshi hilo limefanikiwa kuhakiki jumla ya silaha 14,107 kwa kipindi cha kuanzia Machi Mosi hadi Juni 30 mwaka huu, vile vile Jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata jumla ya watuhumiwa sugu 1,065.

Hayo yameelezwa leo na Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Simon Sirro wakati akitoa taarifa za matukio mbalimbali ya uhalifu pamoja na zoezi la kuhakiki wa silaha hizo.

Alisema zoezi la uhakiki wa silaha lilihusisha mikoa ya kipolisi ya Temeke, Ilala na Kinondoni.

"Idadi ya watu waliojitokeza kuhakiki silaha kwa mikoa yote ni 11,602, na silaha zilizohakikiwa ni pistol 5,073, shotgun 4,707 na rifle 2,974," alisema.

Kamishna Sirro alisema dosari ndogo ndogo zilizojitokeza katika zoezi hilo ni kama vile wamiliki wa silaha kuwa na umri mkubwa zaidi ya miaka 70, na wengine kumili silaha za marehemu kinyume na taratibu.

"Hawa kwa kweli hatukuwaruhusu waendelee kumiliki hizo silaha, hivyo tulibaki nazo na wale walioshindwa kuzilipia silaha zao kwa muda mrefu pia tulibaki nazo," alisema.

Kamishna Sirro alisema kutokana na sababu hizo jumla ya silaha 66 walibaki nazo (kusalimishwa), ikiwa ni shotgun 36, rifle 10 na pistol 20.

Katika operesheni maalumu iliyowezesha kukumata watuhumiwa sugu 1,065, Kamishna Sirro alisema watuhumiwa hawo walikatwa kwa makosa mbali mbali yakiwemo ya makosa ya unyang'anyi wa kutumia nguvu.

"katika hawa tumefakiwa kuwakamata watengenezaji wa pombe haramu ya gongo wakiwa na lita 952 pamoja na mitambo mitatu, vile vile kuna wavutaji wa bangi na puli zao 277.

"Matukio mengine ni pamoja na kukamatwa kwa kete 210, misokoto 144, pamoja na wacheza kamari," alisema.

Katika hatua nyingine Jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu  kwa makosa ya uporaji  wa simu katika maeneo mbali mbali ya kinondoni, mtuhumiwa wa kwanza ni Richard Augustino 18 aliyekamatwa Julai 11 mwaka huu maeneo ya Coco Beach akiwa na sumsung yenye thamani ya sh. 500,000.

"Wengine ni Abdalah Chande 36 aliyekematwa Julai 11 mwaka huu maeneo ya Magomeni Mapipa akiwa na simu 11 za wizi, na Abdalah Saidi 22 ambaye alikamatwa maeneo ya Mapipa julai 14 mwaka huu akiwa na pikipiki aina ya boxer ambayo ilikuwa ikitumika katika matukio ya ukuporaji simu," alisema. 



NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII,MHANDISI RAMO MAKANI ATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA KISIWA CHA RUBONDO

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akiwasili katika Hifadhi ya Taifa ya Rubondo.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akipokelewa na Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Kasheku (Msukuma) mara baada ya kuwasili katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akisalimiana na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Geita ,Herman Kapufi mara baada ya kuwasili katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha  Rubondo. 
 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Utalii katika Shirika la Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akisalimiana na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo ,Missana Mwishawa muda mfupi baada ya kuwasili katika hifadhi hiyo.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya kisiwa cha Rubondo.
  Mkurugenzi wa Idara ya Utaliii wa Shirika la Hifadhi za Taifa,(TANAPA) Ibrahimu Musa akiteta jambo na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani kabla ya kuanza kikao na watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
Mkurugenzi wa Idara ya Utaliii wa Shirika la Hifadhi za Taifa,(TANAPA) Ibrahimu Musa akizungumza wakati wa kikao cha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani na watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
Baadhi ya Madiwani wa mkoa wa Geita wakiwa katika kikao hicho.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo ,Missana Mwishawa akisoma taarifa ya hifadhi hiyo kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani.
Mkuuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo,Missana Mwishawa akimkabidhi Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani taarifa ya Hifadhi hiyo.
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Geita ,Herman Kapufi akizungumza katika mkutano wa Naibu Waziri wa  Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani (kulia kwake) alipotembelea Hifadhi ya Taifa ya kisiwa cha Rubondo.kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Utalii wa Shirika a Hifadhi za Taifa (TANAPA) Ibrahim Musa.
Baadhi ya watumishi katika Hifadhi ya taifa ya kisiwa cha Rubondo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akisisitiza jambo wakati wa kikao chake na watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo alipofanya ziara ya siku moja katika Hifadhi hiyo.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo pamoja na viongozi wengine wa serikali wa mkoa wa Geita mara baada ya kumalizika kwa kikao na watumishi wa hifadhi hiyo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Geita mara baada ya kumaliza kikao na watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo. 

Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog kanda ya Kaskazini.

Friday, July 22, 2016

WANACHAMA WA CUF KUPIGA HODI KWA IGP MANGU ENDAPO ATAENDELEA KUKIFUATILIA CHAMA HICHO

Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Tanzania Bara, Shaweji Mketo, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam , wakati wa kutoa msimamo wa chama hicho kuhusu mikakati ya Jeshi la Polisi dhidi ya vyama vya siasa hasa cha Cuf. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Ulinzi Taifa, Mustafa Wandu na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrul.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrul (wa nne kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa msimamo wa chama hicho kuhusu mikakati ya Jeshi la Polisi dhidi ya vyama vya siasa hasa cha Cuf. Wengine ni maofisa mbalimbali wa chama hicho.

Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Tanzania Bara, Shaweji Mketo, akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

MKURUGENZI wa Uchaguzi wa Chama cha Wananchi (CUF) Shaweji Mketo amesema iwapo Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu ataendelea kukifuatilia chama hicho wanachama wa chama hicho watekwenda ofisini kwake kumsalimia.

Mketo ameyasema hayo Makao Makuu ya Chama hicho Buguruni leo Dar es Salaam leo wakati Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrul alipo kuwa  akizungumza na waandishi wa habari kuhusu msimamo wa chama hicho kuhusu mikakati ya Jeshi la Polisi dhidi ya vyama vya siasa hasa cha Cuf.

"Tunasema sisi Cuf hatumuogopi IGP na kama ataendelea kutufuatafuata haita pita wiki mbili tutamfuata kwenda kumsalimia ofisi kwake" alisema Mketo.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrul
alisema chama hicho kimesikitishwa na kauli ya IGP aliyoitoa hivi karibuni wakati akihojiwa Tido Mhando wa Kituo cha Televisheni cha Azzam kuwa jeshi hilo wakati wowote litamkamata  Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad kwa kuwachochea  wafuasi wake ili waichukie serikali iliyopo madarakani.

Alisema baada ya kuitafakari kauli hiyo ya IGP wamebaini kwamba hivi sasa IGP  Mangu ameamua kuwathibitishia watanzania kuwa jeshi la polisi ni idara maalumu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mazrul  alisema kwa muda mrefu IGP Mangu amekuwa akilitumia jeshi la polisi kushiriki katika matukio mbalimbali ya kuhujumu demokrasia na kukiuka haki za binadamu kwa lengo la kukinusuru Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokana na anguko kubwa la kukataliwa na wananchi kama ilivyothibitika kabnla na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka jana.

Alisema jeshi la polisi limekuwa na utaratibu wa kukamata raia, kuwapiga kuwabambikia kesi, kuwashikilia na kuwatesa katika vituo vya polisi bila ya kuwafikisha mahakamani.

Mazrul alisema  hadi sasa zaidi ya wananchi 400 wameathiriwa kutokana na hujuma za jeshi la polisi kwa kuwabambikia kesi.









DKT. REGINALD MENGI AMTUMIA UJUMBE MZITO WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA

Katika kufikia malengo ya Tanzania kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025, Mwenyekiti wa Taasisi za Sekta Binafsi (TPSF), Dkt. Reginald Mengi amemtumia Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ujumbe kupitia kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana, Wazee na Wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama, ujumbe ambao anaamini kama ukifanyiwa kazi Tanzania itaweza kufikia malengo yake kwa haraka zaidi.
Dkt. Mengi ambaye pia ni Mwenyekiti wa makampuni ya IPP alituma ujumbe huo kwa Waziri Mkuu wakati ufunguzi wa Kongamano la Mashauriano ya Ushiriki wa Watanzania katika Uwekezaji ambalo linafanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam, kongamano lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).

Alisema kuwa pamoja na serikali kufanya jitihada nyingi ili kuwashirikisha wananchi wake katika uwekezaji kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi lakini bado kuna changamoto nyingi ambazo zimekuwa zikijitokeza na zinahitaji kufanyiwa kazi.

Mwenyekiti wa Taasisi za Sekta Binafsi (TPSF), Dkt. Reginald Mengi akizungumza katika Kongamano la Mashauriano ya Ushiriki wa Watanzania katika Uwekezaji kwa niaba ya TPSF ambapo alitumia fursa hiyo kuishauri serikali mambo ambayo anaamini serikali ikiyafanyia kazi uchumi wa Tanzania utakua kwa kasi tofauti na sasa.(Picha na Modewjiblog)

"Serikali imekuwa ikitumia pesa kuwapeleka vijana kusoma nje lakini nikakutana na kijana mmoja akaniambia kasoma nje lakini bado hana ajira na alipelekwa kusomea digrii ya mambo ya mafuta na gesi,

"Nadhani ni vyema serikali ikabidili mwenendo wake na kuhakikisha vijana wote ambao wanapelekwa kusoma nje wakirudi nchini wapewe nafasi za kazi ili kulisaidia taifa kwa hiyo naomba utufikishie ujumbe kwa Waziri Mkuu ukienda Dodoma katika mkutano mkuu wa chama," alisema Dkt. Mengi.

Pia alisema nchi yetu imekuwa ikitegemea zaidi kilimo hivyo iwekeze katika kilimo na iache kuagiza nje bidhaa ambazo zinatengenezwa na vyakula ambavyo vinapatikana nchini lakini pia kuwapa vipaumbele wawekezaji wazawa na hata wanapokuja wageni ihakikishe na watanzania wanashiriki kikamilifu katika kuwekeza.

Mwenyekiti wa Taasisi za Sekta Binafsi (TPSF), Dkt. Reginald Mengi akizungumza katika Kongamano la Mashauriano ya Ushiriki wa Watanzania katika Uwekezaji lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.

"Nchi yetu kwa miaka mingi tunajulikana kuwa tunafanya zaidi kilimo na nadhani hapa kunahitaji ushirikishwaji mkubwa wa watanzania na tuache kulima nanasi na hapo hapo tunaagiza juisi ya nanasi nje ni muhimu watanzania watambue kuwa nchi yao ni tajiri na wakishiriki kikamilifu itafika mbali," alisema Dk. Mengi.

Kwa upande wa Waziri Mhagama ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi alikiri kuwepo kwa baadhi ya changamoto ambazo zimekuwa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lakini serikali inalifahamu hilo na wameanza kufanya mabadiliko ya sheria na sera wanazozitumia kwa sasa.

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri mkuu Kazi, Ajira, Vijana, Wazee na Wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama akitoa hotuba katika kongamano hilo pamoja na kujibu baadhi ya hoja alizotoa Dkt. Mengi.

"Serikali inalifahamu jambo hilo kama kuna umuhimu wa kufanya mabadiliko ili kuwasaidia Watanzania kukuza uchumi wao na wa taifa, kwa sasa tumeanza kufanya mabadiliko kwa baadhi ya sheria na sera na tutaendelea kuangalia ni wapi kunahitajika mabadiliko ili kila jambo lifanyike kwa faida ya watanzania wote," alisema Waziri Mhagama.

Akielezea kongamano hilo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng`i Issa alisema malengo ya kongamano ni kubadilishana mawazo na wadau mbalimbali wa serikali na sekta binafsi lakini pia kushirikisha mashirika ya nje ya nchi ili kuweza kupata njia bora ambayo itakwenda kutumika katika kuwashikirikisha watanzania wote ili kila mmoja ashiriki kukuza uchumi wa taifa.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng`i Issa akielezea malengo ya kongamano hilo la siku mbili.

Baadhi ya wageni waalikwa ambao wamehudhuria kongamano hilo la siku mbili.



Wageni rasmi wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa kongamano.