Pages

KAPIPI TV

Sunday, February 14, 2016

WAZIRI UMMY MWALIMU ATEMBELEA MUHIMBILI KUKAGUA UTEKELEZAJI WA AGIZO LA RAIS MAGUFULI

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ametembelea hospitali ya Taifa Muhimbili kukagua utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli la kuwataka watumishi wa wizara hiyo waliokuwa wakilitumia jengo la Kitengo cha Afya ya Uzazi na Mtoto kuhamisha ofisi zao na kuliacha kwa ajili ya matumizi ya wodi ya wazazi.
Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo katika hospitali hiyo, Waziri Ummy amesema kuwa mpaka kufikia kesho tayari jengo hilo litakuwa limeanza kutumika kwa kuwa watafanya kazi ya kuhamisha makabrasha ya watumishi hao usiku kucha kuhakikisha agizo la Rais John Magufuli linatekelezwa mara moja.
FSA_6533

Picha mbalimbali zinaonesha Waziri Ummy Mwalimu akikagua utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli pamoja na watumishi na vibarua wakihamisha nyaraka na makabrasha mbalimbali kutoka kwenye jengo lililokuwa likitumiwa kama ofisi na watumishi wa wizara hiyo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam.

FSA_6443
FSA_6416
????????????????????????????????????
FSA_6540
????????????????????????????????????

DK. KINGWANGALLA ATOA SIKU 60 KWA HOSPITALI YA KANDA YA RUFAA MBEYA, KUNUNUA MASHINE YA CT-SCAN

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla amefanya ziara, Februari 12, 2016 katika Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Nyanda za juu kusini- Mbeya, na kutoa maagizo mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa mashine CT-Scan ndani ya siku 60 huku akibainisha kuwa endapo watazembea basi watawachukulia hatua kali na kuwajibishwa watendaji na uongozi wa Hospitali hiyo.
Dk. Kigwangalla alifika hospitalini hapo majira ya saa tisa alasiri na kutembelea idara mbalimbali za hospitali hiyo kuona jinsi ya ufanyaji kazi ambapo ndipo alipobaini ukosefu wa mashine hiyo ya CT-Scan pamoja na vifaa vingine muhimu ambavyo alibainisha kuwa hata uongozi wa Hospitali hiyo walikuwa na uwezo wa kuvinunua bila kutegemea Serikali.
Baadhi ya idara ambazo, Dk. Kingwangalla alitembelea ni pamoja na kitengo cha kutolea huduma kwa wagonjwa (OPD), Kitengo cha upasuaji, wodi ya upasuaji, duka la dawa la hospitali hiyo, wodi ya wanawake, wodi ya wanaume, watoto na kitengo cha Maabara ambapo kisha alipata kuongea na wafanyakazi pamoja na uongozi mzima wa Hospitali.
Dk.Kigwangalla alitoa wasaha mwingi kusikiliza kero za wafanyakazi hao kuongea lile linalowakabili bila kuogopa ili aweze kujua matatizo na changamoto zinazowakabili.
"Hospitali kubwa kama hii hapa Mbeya na wataalam wote mlionao mnashindwa kufanya biashara!, Mnategemea tu Serikali? lini mtakuwa na CT-scan kwa upande wenu? wakati mnaingiza Milioni 500 kwa mwezi?" alihoji Dk. Kigwangalla.
Dk.Kigwangalla aliwaambia uongozi wa hospitali hiyo ina fursa na uwezo wa kufanya jambo kubwa kwani pia ina uwezo hata wa kukopa fedha kutoka mashirika ya bima ya afya.
Aidha, Dk Kigwangalla amewataka uongozi wa Hospitali hiyo kuwa wabunifu katika uendeshaji wao ikiwemo kutengeneza jengo la kisasa la matibabu ya kulipia, kujenga nyumba za wafanyakazi ambapo amewapa mikakati hiyo imeanza na pindi atakaporejea tena hospitali hiyo.
Imeandaliwa na Andrew Chale, modewjiblog, Mbeya

DSC_3499

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akisisitiza suala la Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Nyanda za juu kusini- Mbeya kununua mashine ya CT-scan ndani ya siku 60, huku akiahidi kuwachukulia hatua kali ya kuwawajibisha watendaji watakaozembea katika hilo.

kigwangalambeya2

Baadhi ya wafanyakazi na madaktari wa hospitali hiyo wakifuatilia mkutano huo wakati Naibu Waziri Dk.Kigwangalla (hayupo pichani) wakati wa alipofanya ziara Februari 12,2016. Wafanyakazi hao waliweza kutoa maoni yao mbalimbali ikiwemo suala la motisha na uboreshaji wa mishahara pamoja na ukosefu wa vitendea kazi ikiwemo kitengo cha maabara.

kigwangala mbeya

Mmoja wa madaktari wa hospitali hiyo ya rufaa Mbeya akiuliza akitoa maoni yake kwa Naibu Waziri Dk.Kigwangalla.

kigwazz

Kaimu Mkurugenzi wa hospitali ya Kanda ya rufaa Mbeya, Thomas Isidori akitoa fursa kwa Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla (kulia) kuzungumza na wafanyakazi katika mkutano wake huo.

kigwangala2

Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla akipita katika moja ya maeneo ya hospitali hiyo ya Kanda ya rufaa Mbeya sambamba na wenyeji wake...

kigwaz

Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akitazama moja ya kipimo cha mgonjwa ambacho hata hivyo ilieleza kuwa kilipimwa nje ya Hospitali hiyo na kuletwa hapo ambapo alipotaka kujua kwa nini imekuwa hivyo kwa hospitali kubwa kama hiyo alielezwa kuwa hawana mashine ya CT-Scan ndipo alipoutaka uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha mashine hiyo inapatikana ndani ya siku 60 kuanzia hiyo Februari 12.

kigwangala mbeya6

Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla akipata maelezo ya moja ya mashine ndani ya maabara ya hospitali hiyo ya Kanda ya rufaa Mbeya. Hata hivyo ameelezwa mashine hiyo ni ya zamani sana hivyo ufanisi wake ni mdogo huku wakimweleza kuwa inatakiwa wapatiwe mpya ilikuendana na kasi.

kigwangaz

Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla akimjulia hali Mtoto Edger Emmanuel (2) anayepatiwa matibabu ya mguu wake katika wodi hiyo ya watoto kitengo cha upasuaji.

kigwaz11

Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla na Kaimu Mkurugenzi, Thomas Isidori wakimjulia hali Mzee Lazaro Mwakapunga aliyelazwa hospitalini hapo.

kigwanga1

Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla akipatiwa maelezo namna ya mfuko wa malipo wa ki-elektroniki unaotumiwa hospitalini hapo na Kaimu Mkurugenzi, Thomas Isidori. Hospiatli hiyo inatumia mfumo huo ambapo imeweza kufanikiwa katika ukusanyaji wake wa mapato.

kigwangala

Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akipokelewa na Katibu wa Hospitali hiyo, Maryam Msalale wakati wa kuwasili katika ziara hiyo. (Picha zote na Andrew Chale, modewjiblog, Mbeya).

TAASISI YA KUTETEA HAKI ZA WANAWAKE KATIKA MASUALA YA UMILIKI WA ARDHI "MAMA ARDHI ALLIANCE"YAZINDULIWA

1
Mkurugenzi wa Woman Fund Tanzania Mama Mary Lusindi pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Imelda Lulu Urio kushoto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya(Mama Ardhi Alliance)wakizindua rasmi taasisi hiyo ambayo kazi yake kubwa ni kuwatetea wanawake katika masuala mbalimbali yanayohusu umiliki wa Ardhi, uzinduzi huo umefanyika mwishoni mwa wiki katika ofisi za shirika la Tanzania Women Lawyers Association (TAWLA) Ilala jijininDar es salaam.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
2
Mkurugenzi wa Woman Fund Tanzania Mama Mary Lusindi pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Imelda Lulu Urio kushoto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya(Mama Ardhi Alliance)wakikata utepe kama ishara ya kuzindua rasmi taasisi hiyo ambayo kazi yake kubwa ni kuwatetea wanawake katika masuala mbalimbali yanayohusu umiliki wa Ardhi.
3
Mkurugenzi wa Woman Fund Tanzania Mama Mary Lusindi akionyesha huku Kaimu Mkurugenzi wa Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Imelda Lulu Urio kushoto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya(Mama Ardhi Alliance) na wanachama wenzake wakifurahia mara baadea ya kuzindua rasmi taasisi hiyo ambayo kazi yake kubwa ni kuwatetea wanawake katika masuala mbalimbali yanayohusu umiliki wa Ardhi, Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TAWLA Tike Mwambipile.
4
Mkurugenzi wa Woman Fund Tanzania Mama Mary Lusindi akimpongeza Kaimu Mkurugenzi wa Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Imelda Lulu Urio kushoto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya(Mama Ardhi Alliance)mara baada ya kuizindua rasmi taasisi hiyo ambayo kazi yake kubwa ni kuwatetea wanawake katika masuala mbalimbali yanayohusu umiliki wa Ardhi
6
Kaimu Mkurugenzi wa Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Imelda Lulu Urio kushoto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya(Mama Ardhi Alliance) akisaini kulia ni Naemy Silayo Program Officer Gender And Children Unit wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)
7
Mkurugenzi wa Woman Fund Tanzania Mama Mary Lusindi akizungumza jambo katika kikao hicho kutoka kulia ni Bi.Lilian Liundi kutoka TGNP na katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa TAWLA Bi. Tike Mwambipile.
8
Jaquiline Waya Afisa Mipango wa Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo Afrika WILDAF akizungumza jambo katika mkutano huo kulia ni Loyce GondweOfisa wa Sheria katika shirika la Tanzania Media Women Association (TAMWA)
10
Kaimu Mkurugenzi wa Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Imelda Lulu Urio kushoto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya(Mama Ardhi Alliance) pamoja na baadhi ya wajumbe wa mkutano huo wakiendelea na majadiliano.
11
Wajumbe wa Taasisi ya Mama Ardhi Alliance wakipitia nyaraka kabla ya kusainiwa na kuzindua taasisi hiyo.
12
Mkurugenzi Mtendaji wa TAWLA Tike Mwambipile akizungumza jambo katika kikao hicho
13
Mkutano ukiendelea

RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI AZUNGUMZA NA WAZEE WA DAR ES SALAAM, ASKOF GWAJIMA NDANI

1
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Meck Sadik wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee tayari kwa kuongea na wazee wa mkoa wa Dar es salaam leo ambapo mkutano huo pia ulihudhuriwa na Makamu wa Rais Mama Samia Hassan Suluhu na Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa.
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amehudhuria katika mkutano huo ambapo alionekana mtu mwenye kufurahia hotuba hiyo, Kamera ya Fullshangwe ilimnasa askofu huyo maarufu kwa matamshi yake ya "Wakale Malimao" akiwa na tabasam kubwa akionekana kufurahia kuhudhuria kwake katika mkutano huo.
Mwanzo wakati alipofika ukumbini hapo alikuta ratiba inaendelea hivyo ilibidi akae viti vya nyuma lakini Shekh Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhadi Mussa Salim alimpigia simu na kumwambia aende mbele akakae pamoja na viongozi wenzake wa dini na ndipo alipoenda kukaa eneo hilo.
(PICHA NA JOHN BUKUKU- FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
2
Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ukiwasili kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee leo wakati alipoongea na wazee wa mkoa wa Dar es salaam.
3
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Wazee wa mkoa wa Dar es salaam mzee Hemed Mkali kutoka kulia ni Mkuu wa mkoa wa dar es salaam Mh. Raymond Mushi na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ndugu Ramadhan Madabida.
4
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa wazee wa mkoa wa Dar es salaam wa zamani Mzee Idd Simba, Kulia ni mfanyabiashara Abdullah Mohamed.
5
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa.
6
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mama Samia Hassan Suluhu na Waziri Mkuu Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa na Mke wa Rais Mama Janet Magufuli wakiwa meza kuu pamoja na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Dar es salaam.
7
Baadhi ya mawaziri wa wizara mbalimbali katika serikali ya awamu ya tano wakiwa katika mkutano huo.
8
Baadhi ya viongozi wa dini ya Kikristo na ya Kiislamu wanaounda kamati ya Amani wakiwa katika mkutano huo
15
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima hakubaki nyuma na yeye amehudhuria katika mkutano huo na hapa akionekana mwenye furaha na bashasha kama alivyonaswa na kamera yetu.
06
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima akiwa amekaa pamoja na viongozi wenzake wa dini katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam wakati Rais Dk. John Pombe Magufuli alipozungumza na wazee wa mkoa wa Dar es salaam.
9
Baadhi ya wazee wa Dar es salaam wakitambulishwa katika mkutano huo.
11
Baadhi ya mawaziri waliohudhuria katika mkutano huo kutoka kulia ni Mh. Profesa Sospeter Muhongo, Dk. Abdallah Posi, Nape Nnauye, Januari Makamba na Ummy Mwalimu.
12
Baadhi ya wazee wakifuatilia kwa makini wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli alipokuwa akihutubia mkutano huo.
13 14
16
Makamu wa Rais Mama Samia Hassan Suluhu akisalimia wazee katika mkutano huo.
17
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa akisalimia wazee katika mkutano huo.
18
Mwenyekiti wa Wazee wa mkoa wa Dar es alaam Mzee Hemed Mkali akihutubia katika mkutano huo na kumkaribisha Rais Dk. John Pombe Magufuli ili kuwahutubia wazee hao.
19
Wazee hawa wakionekana kuhamasika na hotuba ya Rais Dk. John Pombe Magufuli.
20
Rais Dk. John Pombe Magufuli akihutubia katika mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.

Friday, February 12, 2016

UN YAIPONGEZA TANZANIA KWA JUHUDI ZINAZOFANYWA NA SERIKALI KUKABILI UKATILI DHIDI YA WANAWAKE

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.[/caption]
UMOJA wa Mataifa umepongeza mashirika mbalimbali na serikali ya Tanzania kwa kuchukua hatua kukabiliana na vitendo vya kikatili vya ukeketaji.
Aidha imepongeza wito kutoka katika mashirika mbalimbali ya kutaka kuwapo na mabadiliko katika sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ili kuzuia ndoa za utotoni.
Katika taarifa iliyotolewa na ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Dar es salaam imesema kwamba kitendo cha kuwapo na ushawishi wa kutaka mabadiliko kwa sheria hiyo ya ndoa ni dalili kwamba watanzania wanataka kuona kwamba ndoa za utotoni zinamalizwa.
Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Hoyce Temu amesema katika taarifa hiyo kwamba kitendo cha saini kuendelea kuchukuliwa wakati wa siku ya kimataifa ya kupiga vita ukeketaji Februari 6 mwaka huu kunaonesha kwamba watanzania wako tayari kuzuia ndoa za utotoni.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanyika mwaka 2010, asilimia 15 ya watanzania wamekeketwa, huku wengi wakiwa mkoa wa Manyara asilimia 77.
Kwa mujibu wa Azimio la Beijing dunia ilikubaliana kwamba mtoto wa kike asilazimishwe kuolewa na pia umri wa kuolewa unapaswa kuwa miaka 18.
Kwa mujibu wa sheria ya Tanzania mtoto wa miaka 15 anaweza kuolewa huku akiwa na miaka 14 mahakama inaweza kuridhia ndoa.
Taarifa ya Umoja huo imesema kwamba Tanzania pamoja na nchi nyingine ubaguzi kwa mwanamke unaendelea kupitia sheria na tamaduni mbalimbali huku imani za kidini zikiimarisha ubaguzi huo.
wanawake
Umoja wa Mataifa umesema kwamba unajisikia fahari kufanyakazi na serikali ya Tanzania kutekeleza makubaliano ya kimataifa kubadili umri wa kuozwa na kuoa kwa vijana wake.
“Umoja wa Mataifa unafurahi kushirikiana na serikali ya Tanzania kuhakikisha kwamba haki za wasichana zinalindwa. Pia juhudi za jamii kumaliza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana zinakaribishwa. “ilisema taarifa hiyo.
Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo mwaka 2015 zilitia saini utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu yenye lengo la kuwezesha mabadiliko kubadili yanayostahiki karne ya 21.
Malengo hayo yamelenga kukabili changamoto za umaskini,usawa na ukatili dhidi ya wanawake.
Katika malengo hayo uwezeshaji wa wanawake ni sharti mojawapo na imeelezwa wazi katika lengo namba tano la usawa na uwezeshaji.
Lengo hilo limedhamiria kuondokana na tabia mbaya kama za ndoa za lazima na ukeketaji.