Pages

KAPIPI TV

Friday, February 12, 2016

UN YAIPONGEZA TANZANIA KWA JUHUDI ZINAZOFANYWA NA SERIKALI KUKABILI UKATILI DHIDI YA WANAWAKE

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.[/caption]
UMOJA wa Mataifa umepongeza mashirika mbalimbali na serikali ya Tanzania kwa kuchukua hatua kukabiliana na vitendo vya kikatili vya ukeketaji.
Aidha imepongeza wito kutoka katika mashirika mbalimbali ya kutaka kuwapo na mabadiliko katika sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ili kuzuia ndoa za utotoni.
Katika taarifa iliyotolewa na ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Dar es salaam imesema kwamba kitendo cha kuwapo na ushawishi wa kutaka mabadiliko kwa sheria hiyo ya ndoa ni dalili kwamba watanzania wanataka kuona kwamba ndoa za utotoni zinamalizwa.
Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Hoyce Temu amesema katika taarifa hiyo kwamba kitendo cha saini kuendelea kuchukuliwa wakati wa siku ya kimataifa ya kupiga vita ukeketaji Februari 6 mwaka huu kunaonesha kwamba watanzania wako tayari kuzuia ndoa za utotoni.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanyika mwaka 2010, asilimia 15 ya watanzania wamekeketwa, huku wengi wakiwa mkoa wa Manyara asilimia 77.
Kwa mujibu wa Azimio la Beijing dunia ilikubaliana kwamba mtoto wa kike asilazimishwe kuolewa na pia umri wa kuolewa unapaswa kuwa miaka 18.
Kwa mujibu wa sheria ya Tanzania mtoto wa miaka 15 anaweza kuolewa huku akiwa na miaka 14 mahakama inaweza kuridhia ndoa.
Taarifa ya Umoja huo imesema kwamba Tanzania pamoja na nchi nyingine ubaguzi kwa mwanamke unaendelea kupitia sheria na tamaduni mbalimbali huku imani za kidini zikiimarisha ubaguzi huo.
wanawake
Umoja wa Mataifa umesema kwamba unajisikia fahari kufanyakazi na serikali ya Tanzania kutekeleza makubaliano ya kimataifa kubadili umri wa kuozwa na kuoa kwa vijana wake.
“Umoja wa Mataifa unafurahi kushirikiana na serikali ya Tanzania kuhakikisha kwamba haki za wasichana zinalindwa. Pia juhudi za jamii kumaliza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana zinakaribishwa. “ilisema taarifa hiyo.
Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo mwaka 2015 zilitia saini utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu yenye lengo la kuwezesha mabadiliko kubadili yanayostahiki karne ya 21.
Malengo hayo yamelenga kukabili changamoto za umaskini,usawa na ukatili dhidi ya wanawake.
Katika malengo hayo uwezeshaji wa wanawake ni sharti mojawapo na imeelezwa wazi katika lengo namba tano la usawa na uwezeshaji.
Lengo hilo limedhamiria kuondokana na tabia mbaya kama za ndoa za lazima na ukeketaji.

No comments: