Pages

KAPIPI TV

Wednesday, December 23, 2015

SHIRIKA LA NYUMBA NHC LAZINDUA UUZAJI WA NYUMBA ZA MRADI WA 711 KAWE

k1
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Mchechu Kyando akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa uuzaji wa nyumba za mradi wa 711 uliopo Kawe jijini Dar es salaam, Nyumba hizi ziko kwenye majengo 7 yenye ghorofa 11 kila moja ambayo yanatarajiwa kuchukua watu 1000 kwa na huu ni utangulizi wa ujenzi wa mji mpya wa kisasa unaotarajiwa kujengwa eneo la Tanganyika Pakers Kawe jijini Dar es salaam ambao ukikamilika utaweza kuchukua watu 15000.
Watu wanaohitaji kununua nyumba hizo wanatakiwa kufika ofisi za NHC Kinondoni au Makao Makuu ya Shirika la Nyumba NHC Upanga au wanaweza kutembelea kwenye mtandao wa shirika hilo kwa maelezo zaidi ili kununua nyumba hizo hafla ya uzinduzi wa nyumba hizo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika makao makuu ya shirika hilo Upanga.(PICHA NA JOHN BUKUKU WA FULLSHANGWE)
k4
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Mchechu Kyando akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa uuzaji wa nyumba za mradi wa 711 uliopo Kawe jijini Dar es salaam. k17
Meneja wa Masoko na Mauzo wa NHC, Tuntufye Mwambusi akizungumza na Monica Joseph Mkurugenzi wa Kampuni ya Monifinace Investment Group Limited wakati wa uzinduzi huo.
k18
Meneja wa Masoko na Mauzo wa NHC, Tuntufye Mwambusi akimsikiliza Bw. David Shambwe Mkurugenzi wa Fedha Maendeleo ya Biashara NHC katika uzinduzi huo kulia ni Mwita Makenge Mkurugenzi wa Kampuni ya Wegmar Limited na kushoto ni William Genya Meneja Maendeleo ya Biashara NHC .
k19Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Nehemia Mchechu katikati na Felix Maagi, Mkurugenzi wa Fedha wa NHC wakimsikiliza Linley Kapya kutoa Benki ya NBC wakati alipokuza akizungumza jambo katika uzinduzi huo.
k5
Meneja wa Masoko na Mauzo wa NHC, Tuntufye Mwambusi akizungumza na kuelezea jinsi mradi huo utakavyokuwa na mambo muhimu yaliyopo katika mradi huo huku akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa shirika hilo..
k06
Baadhi ya wafanyakzi wakipozi kwa picha w.akati wa hafla hiyo
k6
Meneja wa Masoko na Mauzo wa NHC, Tuntufye Mwambusi akifafanua jambo mbele ya waalikwa wakati alipokuwa akiuelezea mradi huo.
k07
Baadhi ya wageni walikwa wakifuatilia maelezo mbalimbali kuhusu mradi wa 711 wa Kawe jijini Dar es salaam.
k7
Meneja Masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Aden Kitomari akifafanua mambo mbalimbali wakati akiuelezea mradi wa 711 uliopo Kawe jijini Dar es salaam.
k08
Wageni waalikwa wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa na maofisa mbalimbali wa shirika la Nyumba NHC.
k8
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Mchechu pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo wakifuatilia video zilizokuwa zikionyesha jinsi mradi huo utakavyokuwa wakati wa uzinduzi uliofanyika Makao Mkuu wa shirika hilo Upanga.
k10
Baadhi ya wageni waalikwa kutoa taasisi mbalimbali wakifuatilia uzinduzi huo.
k12
Kutoka kulia ni Meneja wa Masoko na Mauzo wa NHC, Tuntufye Mwambusi na Meneja Masoko wa NHC Bw. Aden Kitomari wakimsikiliza Taji Liundi aliyekuwa MC wa uzinduzi huo.
k14 k15 k16
Wageni mbalimbali walihudhuraia uzinduzi huo.

MSHINDI WA SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2015 CAROLINE CHELELE, AKABIDHIWA RASMI ZAWADI ZA VIFAA VYA KILIMO ZENYE THAMANI YA TSH MIL.20 IFAKARA.


Mshindi wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula Msimu wa nne Bi. Caroline Chelele aliyekaa kwenye Pawatila akifurahia zawadi zake, Muda mfupi baada ya kukabidhiwa.
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombelo Bw. Yahya Naiya (wa pili kushoto) aliye muwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kilombelo akikata utepe kuashiria tukio la kumkabidhi zawadi rasmi mama shujaa wa chakula msimu wa nne 2015 Bi. Caroline Chelele, wa kwanza kushoto ni Mercy Minja Kaimu mkurugenzi wa wa mji wa Ifakara, wa tatu kutoka kulia ni Mama Shujaa wa Chakula Bi. Caroline Chelele na Mbunge wa Jimbo la Kilombelo Mh. Peter Lijuakali
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombelo Bw. Yahya Naiya (wa pili kushoto) aliye muwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kilombelo akimpongeza Mama shujaa wa chakula 2015 baada ya kukabidhiwa zawadi ya vifaa vya kilimo vyenye thamani ya Tsh Milioni Ishirini(20,000,000)
 Vifaa  vya kilimo ambavyo alikabidhiwa  mama Shujaa wa Chakula Msimu wa nne 2015, ikiwa ni Pawatila na Mashine ya kumwagilia na Shamba lenye Hekta 7 ambalo halipo pichani.
 Mshindi wa Shindano la Mama shujaa wa chakula linalo endeshwa na Oxfam kupitia Programu yake ya Grow Bi Caroline Chelele akitoa neno la Shukurani baada ya kukabidhiwa zawadi.
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombelo Bw. Yahya Naiya (wa pili kushoto) aliye muwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kilombelo, akitoa neno la shukurani kwa Shirika la Oxfam kwa jinsi wanavyo wajali na kuwawezesha wakulima wadogo wadogo.
Mbunge wa Kilombelo Mh. Peter Lijuakali akimpa pongezi mama shujaa wa Chakula 2015 kwa kuleta ushindi mkubwa wilayani hapo na kuwasihi akinamama wengine wajitokeze kushiriki kipindi ambacho nafasi inatokea tena na kurudisha ushindi huko.
Meneja wa Ushawishi na utetezi kutoka Oxfam Eluka Kibona akielezea kwa undani kuhusiana na shindano la Mama shujaa wa Chakula.
Mtaalam wa Kilimo hai kutoka SOAM wa tatu kutoka kushoto akitoa maelezo ya namna ya kutengeneza mbolea asiyo na kemikali yoyote kwa kutumia Majani,Magugu, Majivu,Maji na Udongo
Baadhi ya wanakijiji wakifanya kazi kwa vitendo kwa kusombelea nyasi kavu pamoja na magugu kwa ajili ya kutengeneza Biwi
Shamba darasa la utayarishaji wa Biwi likiwa linaendelea 
Baadhi ya wanakijiji ambapo mama Shujaa wa Chakula alipokabidhiwa zawadi zake, wakifuatilia kwa makini shamba Darasa
 Mshindi wa shindano la Mama Shujaa wa chakula 2015 msimu wa nne Bi. Caroline chelele (Kulia) akimkabidhi zawadi Kaimu Mkurugenzi wa Mji wa Ifakara Bi. Mercy Minja kwa niaba ya Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombelo
 Bi.Caroline chelele akikabidhi zawadi yake ya Kigoda kwa Shirika la Oxfam, kutoka kushoto ni Narsis Silvesti, Eluka Kibona na wa kwanza kulia ni Suhaila Thawer wote kutoka Oxfam Tanzania
 Mama Shujaa wa chakula akikabidhi zawadi ya Picha kwa Shirika la Oxfam
 Watalam wa Kilimo hai kutoka SOAM wakimkabidhi vipeperushi vinavyozungumzia kilimo hai Mama Shujaa wa Chakula 2015 Bi. Caroline Chelele
 Baadhi ya wananchi waliokuwa katika sherehe hizo za kukabidhiwa zawadi mama shujaa wa Chakula.
Picha ya pamoja ya viongozi wa Wilaya ya Kilombelo, Shirika la Oxfam na Mshindi wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula Msimu wa nne 2015 Bi.Caroline Chelele

Mshindi  wa shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015, Linaloendeshwa na Shirika la Oxfam kupitia program yake ya Grow msimu wa nne Caroline Chelele amekabidhiwa zawadi ya vifaa vya kilimo vyenye thamani ya kiasi cha shilingi Millioni 20, nyumbani kwake kata ya Ifakara mkoani Morogoro.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo ya zawadi  Mkoani Morogoro wilayani  Kilombero kata ya Ifakara,Meneja Ushawishi na Utetezi kutoka Shirika la Oxfam,Eluka Kibona alisema zawadi hiyo ni moja ya utekelezaji wa shindano hilo kwa mshindi aliyeshinda shindano hilo la Mama shujaa wa Chakula 2015.

Alisema shirika lao linatoa takribani Milioni 20 kwa mshindi ambapo mshindi  anatakiwa kuchagua zawadi ya vifaa vya kilimo ili kuweza kumuwezesha zaidi. Kibona alisema Mshindi huyo alikabidhiwa Pawatila kwa ajili ya kubebea Mazao,vifaa vya umuagiliaji pamoja na Shamba lenye Ekali 7. "Huu ni muendelezo wa shindano la mama shujaa wa Chakula kukabidhi zawadi kwa ajili ya kuwainua wakulima wadogo wadogo kuonekana na Serikali kama wao wanamchango mkubwa kwa jamii kutokana na Chakula wanacholima ndicho kinacholisha taifa,"alisema Kibona . Aliongeza shindano hilo lipo chini ya Kampeni ya GROW yenye lengo la kuwainua wakulima wadogo wanaokumbana na changamoto mbalimbali katika kilimo.

Kwa Upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombero , Yahya Naniya aliishukuru shirika hilo kwa hatua ya kuwathamini na kuwapigania wakulima wadogo ambao asilimia kubwa kati yao ni wanawake.Alisema  kupitia shindano hilo linaweza kuongeza Chachu kwa wakulima kufanya  shughuli za kilimo kwa kasi na kuongeza wigo mpana wa kupata mazao mengi kutokana na Mashirika mbalimbali kuwawezesha.

Naye Mshindi wa Shindano hilo 2015,Caroline Chelele alisema  atahakikisha zawadi hizo anazifanyia kazi ipasavyo itakayomuwezesha kumuongezea mazao mengi zaidi. Aliomba Serikali pamoja na mashirika mbalimbali kuendelea kuasidia wakulima wadogo na kuhakikisha nao wanathaminiwa kama wakulima wakubwa.

UJUMBE WA SHIRIKA LA NYUMBA UGANDA WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO NHC TANZANIA

Ujumbe wa Shirika la Nyumba la Taifa la Uganda (NHCC) ukiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo, Parity Twinomujuni (aliyeketi mbele ya logo ya NHC) ukijadiliana masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya nyumba nchini na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa la Tanzania, Nehemia Kyando Mchechu. Ujumbe huo umekuwapo katika ziara ya siku mbili ya mafunzo nchini kujifunza namna utendaji wa Shirika la Tanzania unavyofanyika ili waweze kupata njia za kuweza kuboresha Shirika zaidi Shirika la NHCC Uganda.
Ujumbe wa Shirika la Nyumba la Taifa la Uganda (NHCC) ukiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu Parity Twinomujuni (aliyeketi mbele ya logo ya NHC) ukijadiliana masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya nyumba nchini na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa la Tanzania, Nehemia Kyando Mchechu. Ujumbe huo umekuwapo katika ziara ya siku mbili ya mafunzo nchini kujifunza namna utendaji wa Shirika la Tanzania unavyofanyika ili waweze kupata njia za kuweza kuboresha Shirika zaidi Shirika la NHCC Uganda.
Mojawapo ya nyumba za NHC Mwongozo zilizotembelewa na Ujumbe wa Shirika la Nyumba la Taifa la Uganda (NHCC) ukiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu Parity Twinomujuni. Ujumbe huo umekuwapo katika ziara ya siku mbili ya mafunzo nchini kujifunza namna utendaji wa Shirika la Tanzania unavyofanyika ili waweze kupata njia za kuweza kuboresha Shirika zaidi Shirika la NHCC Uganda.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Nyumba la Taifa la Uganda (NHCC) Balozi Agnes Kadama Kalibbala na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa la Uganda (NHCC) Parity Twinomujuni wakifuatilia mawasilisho yaliyokuwa ya kifanywa na Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa la Tanzania jana.
Mkurugenzi wa Ubunifu wa Shirika la Nyumkba la Taifa la Tanzania (NHC), Issack Peter akitoa mada kuhusu utendaji wa Shirika hilo kwa Ujumbe wa Shirika la Nyumba la Taifa la Uganda (NHCC) ukiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu Parity Twinomujuni Ujumbe huo upo nchini katika ziara ya siku mbili ya mafunzo nchini kujifunza namna utendaji wa Shirika la Tanzania unavyofanyika ili waweze kupata njia za kuweza kuboresha Shirika zaidi Shirika la NHCC Uganda.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Maagi (Wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa Shirika la Nyumba la Taifa, Haikamen Mlekio wakiagana na Ujumbe wa Shirika la Nyumba la Taifa la Uganda (NHCC) uliokuwa ukiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu Parity Twinomujuni. Ujumbe huo upo nchini katika ziara ya siku mbili ya mafunzo nchini kujifunza namna utendaji wa Shirika la Tanzania unavyofanyika ili waweze kupata njia za kuweza kuboresha Shirika zaidi Shirika la NHCC Uganda.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa la Uganda (NHCC) Parity Twinomujuni akiwa katika ziara ya mradi wa Mwongozo, Kigamboni Dar es Salaam.
Mojawapo ya nyumba za NHC Mwongozo zilizotembelewa na Ujumbe wa Shirika la Nyumba la Taifa la Uganda (NHCC) ukiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu Parity Twinomujuni. Ujumbe huo umekuwapo katika ziara ya siku mbili ya mafunzo nchini kujifunza namna utendaji wa Shirika la Tanzania unavyofanyika ili waweze kupata njia za kuweza kuboresha Shirika zaidi Shirika la NHCC Uganda.
Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa Shirika la Nyumba la Taifa, Haikamen Mlekio akimzungumza jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa la Uganda (NHCC) Parity Twinomujuni walipofanya ziara ya mradi wa Mwongozo.
Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa Shirika la Nyumba la Taifa, Haikamen Mlekio akimzungumza jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa la Uganda (NHCC) Parity Twinomujuni walipofanya ziara ya mradi wa Mwongozo.
Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa Shirika la Nyumba la Taifa, Haikamen Mlekio akimzungumza jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa la Uganda (NHCC) Parity Twinomujuni walipofanya ziara ya mradi wa nyumba za gharama nafuu Kibada.
Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa Shirika la Nyumba la Taifa, Haikamen Mlekio akimzungumza jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa la Uganda (NHCC) Parity Twinomujuni walipofanya ziara ya mradi wa nyumba za gharama nafuu Kibada
mojawapo ya nyumba za gharama nafuu NHC Kibada Kigamboni Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa Shirika la Nyumba la Taifa, Haikamen Mlekio akimzungumza jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa la Uganda (NHCC) Parity Twinomujuni walipofanya ziara ya mradi wa nyumba za gharama nafuu Kibada.

Sunday, December 13, 2015

MAKAMU WA RAIS MGENI RASMI TAMASHA LA AMANI.

msa1
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kinondoni wakati alipomtangaza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Samia Hassan Suluhu kuwa mgeni rasmi wa Tamasha la Kushukuru kufuatia kufanyika kwa uchaguzi wa amani na utulivu tarehe 25 mwezi Oktoba mwaka huu nchini kote huku nchi ikiendelea kuwa na utulivu na amani ya hali ya juu. Kushoto ni Mratibu Tamasja la Kushukuru masuala ya usalama Bw. Hamisi Pembe
msa2
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama na Mratibu Tamasja la Kushukuru masuala ya usalama Bw. Hamisi Pembe wakifurahia jambo wakati walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari leo.
msa3
Mratibu Tamasha la Kushukuru masuala ya usalama Bw. Hamisi Pembe akifafanua mambo mbalimbali kuhusu usalama wa tamasha hilo, huku Mkurugenzi wa Msama Promotion akimsikiliza kwa makini wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari
............................................................................
NA MWANDISHI WETU
·Munishi aliyeimba Malebo naye ndani
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Samia Suluhu Hassan amethibitisha kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Krismass litakalofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mwewnyekiti wa kamati ya maandalizi ya kamati hiyo Alex Msama amesema kuwa Makamu wa Rais amethibitisha na wanaendelea kujipanga ili kulinogesha Tamasha hilo.

Alisema wanashukuru kwa Makamu wa Rais kushiriki katika Tamasha hilo kama mgeni rasmi licha ya muda mfupi tangu aingie madarakani.

Msama alisema, mama Samia ameonyesha kuwa ni mzalendo wa kweli kwani muda sio mrefu amemaliza kampeni za Uchaguzi Mkuu na kuzunguka nchi nzima hivyo kuwa na uchovu mwingi lakini amekubali kitu ambacho kimetoa faraja kwa wakazi wa Dar es salaam ambao wanatarajia kumiminika kwa wingi kushiriki tamasha hilo.

“Napenda kuwatangazia kuwa mgeni rasmi wa Tamasha la Krismass lenye lengo maalum la kushukuru mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu kuwa mgeni rasmi ni mama yetu mpendwa Samia Suluhu Hassan,” alisema Msama.

Msama amesema kutokana na Makamu wa Rais kuwa mwanamke wa kwanzakushika nafasi hiyo hapa nchini kuna kila sababu ya mashabiki kujitokeza kwa wingi siku hiyo.

Katika hatua nyingine Msama pia amemtangaza mwimbaji wa injili mkongwe hapa nchini anayefanya shughuli zake nchini Kenya Faustine Munishi ambaye ameimba nyimbo maarufu inayojulikana kama Malebo.

Amesema Munishi amethibitisha na yuko katika mazoezi ya nguvu kuhakikisha kuwa kila kitu kinakwenda sawa siku hivyo na amepanga kuimba nyimbo zote ambazo alikuwa akiimba zamani ikiwemo malebo.

Aidha mjumbe wa kamati ya Tamasha hilo Khamis Pembe alisema, kila kitu kimekamilika ili kuhakikisha washiriki akiwemo Makamu wa Rais wanakuwa salama.

Alisema wamejipanga vizuri na watahakikisha hakuna tatizo lolote la ulinzi siku hiyo ili kuendeleza hali hiyo kama ilivyokuwa katika matamasha mengi ambayo yamekuwa yakiandaliwa na Msama Promotions.

INTERSWITCH LAUNCHES IN TANZANIA

CEO, Bernard Matthewman
INTERSWITCH, the leading integrated digital payments and commerce provider focused on Africa has today announced its entry into Tanzania and unveiled its new corporate identity. This marks a new phase inInters witch’s expansionacross Africa with operations now in six (6) countries.

The entry into East Africa follows the completion of the merger with leading East African e-payments provider Paynet Group.  Effectively, Paynet Tanzanianowbecomes Interswitch.

Paynetbegun operations  in 2003 and isbest known for a number of innovations includinglinking ATMs with M-PESA in Tanzania (Vodacom M-Pesa) and Kenya (Safaricom- M-Pesa), and driving the adoption of EMV Chip cards across Tanzania, Uganda and Kenya.

Following these announcements, Tanzania becomes the sixth country where Interswitch has rebranded its operations in Africa with its new corporate identity seeking to establish uniform brand values and identity across Africa.

Speaking during the launch held at the Hyatt Regency- the Kilimanjaro in Tanzania, Interswitch East Africa CEO Bernard Matthewman said the launch of the new brand in Tanzania was a statement of Interswitch’s leading position in the market and reflects its ambition to continue to grow its world class service across the African continent.

“Interswitch’s new logo and brand is a confident statement of our leading position in the market and sets us apart from the competition. The bold design clearly reflects the best-in-class service we provide our customers, our ambitious pan-African expansion plans and our relentless pursuit of new and innovative e-payment solutions for the African market. At Interswitch we continue to push the frontiers of not just digital payments but commerce as a whole.

He added:
“We now have an unrivalled, truly borderless pan-African payment infrastructure under Interswitch which we will leverage to enable faster transactions, innovation and even greater value for our partners and the community.”
Cynthia Kantai

Regional Head of Marketing & Corporate Communications Cynthia Kantai said the new identity celebratesInterswitch’s continuous drive to innovate e-payment solutions tailored to the African market with the aim of delivering ‘intuitive exchange’, where transactions happen at the speed of thought.

She said the new bold yet simple design encapsulates the personality, drive and values of integrity and trust that are central to the Interswitch brand.


Since launching in 2002, Interswitch has grown rapidly and consistently, resulting in a current transaction volume of over 350 million transactions per month and more than US$32 billion a year across its platforms. Interswitch, according to Deloitte, is the fastest growing tech company in Africa with revenue growth of 1226% in the last five years.


During the event,Interswitch also announced the launch of   Verve, an exciting new card and payment scheme offered by Verve International, an Interswitch Group company.

Verve is the biggest payment card brand in Nigeria with more than 30 million payment tokens, and is rapidly expanding issuance and acceptance across the African continent and is now issued by over 40 banks in Africa. The launch of the card now expands Verve card operations into Tanzania, Kenya, Burundi, South Sudan and Rwanda with integration into existing operations in Uganda.

 Verve already hasa strategic partnership with UBABankand KCB for both ATMs and merchant POS. . . . This announcement now expands Verve card acceptance and payment services into five key East African markets.

Verve International is pursuing acceptance of the Verve card around the world. In 2013 the company signed a partnership agreement with Discover Financial Services (DFS), the owners of Diner’s Club, which will give Verve cardholders access to the Discover global network of over 185 countries and territories across the world.

Richard Coate, Verve International Regional head in East Africa said:

“We are seeing rapidly expanding trade flows between East and West Africa and with that increased travel. Expansion of Verve acceptance across Africa and around the world is part of the long-term strategic vision for our business. It will also foster closer business partnerships between East and West Africa and improve the ease of doing business on the continent, thereby encouraging even stronger growth. We have created Africa’s first truly global payment card brand and an important symbol of Africa’s economic power.”
Note That

Interswitch is an Africa-focused integrated digital payments and commerce company that facilitates the electronic circulation of money as well as the exchange of value between individuals and organizations on a timely and consistent basis.

The company started operations in 2002 as a transaction switching and electronic payments processing company that builds and manages payment infrastructure as well as deliver innovative payment products and transactional services throughout the African continent.

Interswitch provides technology integration, advisory services, and payment infrastructure to government, banks and corporate organizations. We process transactions from various channels namely: ATMs, mobile, PoS, online (web) and IVR;

For more about Interswitch, log on to: www.interswitchgroup.com

About Verve International

NHIF ILIVYOADHIMISHA 9 DESEMBA KWA KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA








 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko Michael Mhando akiwaongoza Watumishi wa Mfuko kufanya usafi maeneo yanayozunguka makao makuu ya Mfuko na hatimaye kutoa mashuka 100 kwa Hospitali ya Jeshi la Polisi Kilwa Road.