Pages

KAPIPI TV

Sunday, November 29, 2015

HAPA KAZI TU” YAWAWEKA SAWA WAFANYAKAZI WA DAWASCO.

 Ofisa Mtendaji wa Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (Dawasco), Mhandisi Cyprian Luhemeja, akizungumza katika mkutano na wafanyakazi uliofanyika hivi karibuni Makao Makuu ya Dawasco jijini Dar es Salaam kuhusu utendaji kazi wa kazi.
 Wafanyakazi wa Dawasco wakimsikiliza Ofisa Mtendaji 
Mkuu wao.


Na Mwandishi, Maalumu

Ule usemi maaarufu wa Hapa kazi tu” 

unaendelea kuimbwa na kufanyiwa kazi na watanzazia wengi hususani watumishi wa Umma na serikali ili kuendana na kasi ya awamu ya Tano ya Raisi Magufuli. Kauli mbiu hiyo imekumbushwa tena na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Eng Cyprian Luhemeja wakati wa kikao cha pamoja na  wafanyakazi wa shirika hilo mapema wiki hii.

“lazima tuendane na kasi na speed ya Mheshimiwa Rais, tabia ya kufanya kazi kwa mazoea, kutojali malalamiko ya Wateja sasa ni mwisho” aliongeza Luhemeja

Aliwataka wafanyakazi kujali muda wao wa Kazi kwa kutenda yale ambayo yataondoa kero ya Maji kwa Wateja hususani kuziba mivujo ya Maji katika maeneo mengi ya Jiji pamoja na kupambana na wizi wa Maji ili kila mwananchi apate huduma ya Maji kihalali.

Alimalizia kwa kuwataka wafanyakazi wa DAWASCO kutekeleza kauli ya Rais aliyoitoa mapema wakati akifungua Bunge katika sekta ya Maji pale aliposema “LAZIMA TUWATUE KINA MAMA NDOO KICHWANI” kwa kuhakikisha huduma ya Maji inamfikia mwananchi na kuondokana na malalamiko ya upatikanaji huduma hiyo kwa maeneo stahili.


CHAMA CHA WASHIRIKA-WAUGUZI TANZANIA KUKUTANA DESEMBA 12, 2015 JIJINI DAR ES SALAAM KUJADILI MAENDELEO NA CHANGAMOTO ZAO


 Ofisa Ushirika wa Wilaya ya Kinondoni jijini  Dar es Salaam, Omary Mkamba (kulia), akimkabidhi cheti cha Usajili wa Chama cha Ushirika -Wauguzi Tanzania  (Tanna Saccos Ltd) , Mwenyekiti wa chama hicho, Kapteni Adam Leyna katika mkutano uliofanyika hivi karibuni. Mkamba ni mlezi wa chama hicho.
 Mwenyekiti wa chama hicho, Kapteni Adam Leyna (katikati), akizungumza na wanachama wapya waliojiunga na chama hicho mkoani Kagera.
 Wanachama wakijadiliana.
 Wanachama wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa wamevalia fulana rasmi mkoani Kagera
Viongozi wa chama hicho na wanachama wakiwa katika picha ya pamoja.

Na Dotto Mwaibale

CHAMA cha Washirika-Wauguzi  Tanzania (Tanna Saccos Ltd) kinatarajia kujadili mafanikio na changamoto zao mbalimbali katika mkutano wao mkuu , utakaofanyika Desemba 12, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, 
Mwenyekiti wa Tanna Saccos Ltd, Kapteni Adam  Leyna alisema mkutano huo ni muhimu sana kwao kwani unawakutanisha wauguzi washirika nchi nzima na kuweza kujadili mafanikio, changamoto mbalimbali na maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

"Ni mkutano muhimu sana kwetu kwani unatusaidia kubadilishana uzoefu wa ushirika kutoka kwa washirika wenzetu kama Ngome Saccos, Walimu Saccos na Magereza Saccos na kujua changamoto zetu ikiwa ni pamoja na kuzitafutia ufumbuzi' alisema Leyna.

Aliongeza kuwa mkutano huo ambao utafanyika Ukumbi wa Makuti katika Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa Mgulani ni mikutano ambayo hufanyika kila mwaka ili 
kuzungumzia maendeleo ya chama na uboreshaji wa uchumi wa muuguzi na ustawi wa  jamii kwa ujumla.

Leyna alisema pamoja na mambo mengine katika mkutano huo 
watajadili taarifa ya maendeleo ya chama na kuweka mpango 
kazi wa kutekeleza mwaka wa fedha 2016.

Mwenyekiti huyo ametumia fursa hiyo kuwaomba wauguzi washirika wa tanna saccos ltd kujitokeza kwa wingi katika mkutano huo muhimu kwao.

Chama cha Ushirika -Wauguzi Tanzania (Tanna Saccos Ltd)  ni 
chama cha ushirika kinachowaunganisha  wauguzi na wakunga 
Tanzania ambacho kinasimamia utoaji wa mikopo, elimu ya ujasiriamali na maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wauguzi.

MSD YAKARABATI JENGO LA DUKA LA DAWA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI KWA KASI KUBWA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS DK.MAGUFULI

Mafundi wakikarabati jengo ambalo Bohari ya Dawa (MSD), itafungua duka la dawa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MSD) Dar es Salaam jana kwa ajili ya kuhudumia wananchi kwa karibu zaidi vikiwemo vifaa tiba. Duka hilo linatarajiwa kufunguliwa kesho kutwa.
Fundi akitoboa ukuta sehemu litakapo fungwa beseni la kunawia katika duka hilo.
Mafundi wakiendelea na ukarabati wa jengo hilo lililopo jirani na wodi ya Kibasila linalotizamana na maegesho ya magari.
Fundi akipaka rangi ndani ya jengo hilo.
Jengo la duka hilo la MSD linavyoonekana kwa nje. Hapa mafundi wakiendelea na kazi ya ukarabati.

Na Dotto Mwaibale

BOHARI ya Dawa (MSD) imejiimarisha na kuhahikisha inatekeleza kwa wakati agizo la Rais Dk. John Magufuli la kuweka maduka ya dawa katika hospitali za rufaa na kanda nchini.

Katika kutekeleza agizo hilo MSD imeanza kwa kasi kubwa ya kukarabati jengo la duka la dawa katika  Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), ambalo linatarajiwa kufunguliwa kesho.

Mwandishi wa habari hii alishuhudia jana kasi kubwa ya mafundi ujenzi wakikarabati  jengo hilo ambalo awali lilikuwa likitumika kama stoo ya kuhifadhi vitu mbalimbali vya hospitali hiyo.

Akizungumza na vyombo vya habari hivi karibuni kuhusu ufunguzi wa maduka hayo, Mkurugenzi Mkuu wa  MSD, Laureane Bwanakunu alisema  agizo la Rais la kuitaka MSD kuanzisha duka la dawa karibu na hospitali limekuja wakati muafaka kwani  kwenye mpango mkakati wa miaka sita wa MSD tayari ilikuwa na mpango wa kufungua maduka hayo kwa ajili ya kusogeza huduma karibu a wananchi.

Alisema maduka ya MSD ambayo yatafunguliwa kwenye hospitali za rufaa na kanda yatafanya kazi masaa 24 na kuuza dawa na vifaa tiba  chini ya bei ya soko pia yatahudumia watu binafsi na wale waliopo kwenye taratibu za Bima ya afya kote nchini.

"Ili kudhibiti watumishi wasio waaminifu kuiba dawa MSD inafanya kazi za uagizaji, uhifadhi  na usambazaji kwa kutumia mfumo wa mtandao wa E9 na tangu mwaka wa fedha uliopita tumeanza kuziwekea alama ya GOT bidhaa zetu ikiwa ni pamoja na vidonge." alisema Bwanakunu.  


Alisema vidonge ambavyo tayari vimewekewa nembo ya GOT vipo 45 na wanaendelea kuwapa maelekezo wazabuni ili vyote viwekwe alama hizo..,nembo ya serikali inaonekana kwenye dawa za serikali kama Diclofenac, moxillin, iprofloxacin, Contrimoxale,paracetamol,
na magnesium.

Alisema wanatarajia kuanzisha huduma ya kutoa taarifa kwa njia ya simu pale wananchi watakapoona kuna wizi wa dawa za serikali na kwamba wananchi  wanaelimishwa kutoa taarifa pale wanapoona dawa za serikali mitaani.

Alisema, pamoja na serikali kuanza kupunguza deni lake linalodaiwa na MSD bado inadaiwa Sh.bilioni 53.



MO APATA TUZO NYINGINE, ADHIHIRISHA TAMAA YA KUWATUMIKIA WATANZANIA

IMG_3351
Mfanyabiashara maarufu ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akitembea kwenye 'Red Carpet' mara baada ya kuwasili katika hotel ya Hilton Sandton jijini Johannesburg, Afrika Kusini kwenye hafla ya utoaji tuzo iliyoandaliwa na jarida maarufu la Forbes na kutunukiwa tuzo ya "Forbes Africa Person Of the Year 2015".(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Na Modewjiblog team
MFANYABIASHARA na mtu mwenye taasisi ya kusaidia jamii, Mohammed Dewji maarufu kama Mo ametunukiwa tuzo ya jarida maarufu la Forbes ya "Forbes Africa Person Of the Year 2015" katika hafla iliyofanyika Novemba 27 mwaka huu jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
Mfanyabiashara huyo pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya Mohammed Enterprises T Ltd (MeTL Group) kampuni iliyoanzishwa na na baba yake katika miaka ya 1970 ambayo sasa imekua na kujikita katika viwanda vya nguo, usagaji nafaka, utengenezaji wa vinywaji baridi, usindikaji wa mafuta ya kula, usindikaji wa chai na kuendesha mashamba ya mkonge ambapo tayari anashea ya asilimia 40 ya soko.
Mo ametwaa tuzo hiyo kwa kuwashinda watu watano mashuhuri barani Afrika. Watu hao ni Nkosazana Dlamini Zuma, mke wa Kwanza wa Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma. Mama huyo kwa sasa ndiye Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU). Mwingine ni Rais wa sasa wa Nigeria, Muhammadu Buhari aliyetambuliwa kutokana na kuanzisha vita dhidi ya rushwa nchini mwake.
Aidha wapo Arumna Otei, mchumi mahiri raia wa Nigeria ambaye kwa sasa ni Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia. Pia alikuwemo Mwandishi maarufu wa vitabu wa Nigeria, Chimanda Ngozi Adichie ambaye moja ya vitabu vyake vinaelezea picha halisi ya Afrika inavyofikiriwa duniani.
Akitoa neno la shukurani baada ya kukabidhiwa kwa tuzo hiyo Mo, alisema anatoa tuzo hiyo kwa vijana wa Kitanzania kwani ndio nguvu kazi inayobeba uchumi wa nchi.
Mo ambaye kampuni yake ya MeTL inaongoza kwa kutoa ajira nchini, ikiwa imetoa ajira 26,000 kote katika viwanda vyake 31 vilivyopo nchini na katika mataifa matano ya Afrika, alisema amefurahishwa na tuzo hiyo ambayo anaitoa kwa vijana kwa kutambua pia wajibu mkubwa walionao katika kukabiliana na umaskini.
IMG_3317
Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akifurahi jambo na baadhi ya wageni waalikwa nje ya ukumbi wa hafla hiyo ya utoaji tuzo iliyoandaliwa na jarida la Forbes.
Alisema ajira 26,000 zimegusa watu wengi nchini na kwamba ana matumaini makubwa ya siku za usoni kutoa ajira zaidi kutokana na biashara zake kuendelea kukua.
"Heshima yangu kubwa haitokani na utajiri, maana kama utajiri wako hauna msaada wala kugusa watu masikini hauna maana yeyote, hivyo basi heshima hii ni kutokana na kwanza bidhaa zangu kugusa maisha ya watu kila siku kuanzia sukari na majani ya chai asubuhi pamoja na unga wa ngano, lakini pia chakula cha mchana kwa unga wa sembe, mafuta ya kupikia na maji ya kunywa, bidhaa zote hizo za Mohammed Enterprises zinagusa maisha kila nyakati katika siku.
"Nina viwanda 31 ambavyo vimekuwa vikitengeneza bidhaa za Kitanzania na kuziuza kwa Watanzania kwa bei yenye unafuu mkubwa, mathalani tunauza maji kwa bei chini ya dola moja kwa shilingi za Kitanzania 200, hakuna hata Ulaya, nina kiwanda cha khanga na vitenge ambacho malighafi zake zote ni za Kitanzania, hivyo kuna kusaidia serikali kwa kulipa kodi ipasavyo, lakini pia kusaidia moja kwa moja ajira za Watanzania walio wengi ambao tatizo lao kubwa katika kundi la vijana ni ajira"
Alitumia fursa hiyo kumshukuru na kumpongeza baba yake kwa kumwita mjasiriamali shujaa ambaye alitoka kuanzia dereva wa malori baada ya kuhitimu kidato cha nne mwishoni mwa miaka ya 1960 hadi kufikia ubilionea. Alisema alipata maono ya utajiri hasa kutoka kwa baba yake huyo aliyekuwa akimshirikisha biashara tangu akiwa mdogo.
“Mwanaume mwenye ndoto huhitaji mwanamke mwenye maono. Na nimebarikiwa mwanamke ambaye kwa miaka 15 amekuwa akinipa sapoti isiyoyumba.
IMG_3362
Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akibadilishana 'Business card' na mmoja wa wageni waalikwa katika hafla hiyo.
“Saira, nina shukurani nyingi kwako kwa kuwa nguzo ya familia yetu, mama wa heshima kwa watoto wetu watatu,” alisema Mo kwenye hafla hiyo.
Kwa utulivu, Mo alisema: “Baba, zawadi kubwa ambayo ulinipa katika maisha yangu ni muda wako, na kwa hilo nitakuwa mwenye deni la shukurani kwako siku zote za maisha yangu.”
Mo ambaye moyo wake wa binadamu ulimfanya awanie uwakilishi Jimbo la Singida Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kushinda nafasi hiyo na hivyo kuwawakilisha wanasingida kuanzia 2005 na 2015 amesema maisha ni changamoto kubwa inayobadilishwa kwa utumishi wenye nia ya dhati kwa umma.
Alisema alipowania uwakilishi alikuwa na sababu: “Nilikuwa na umri wa miaka 24, nilikwenda Singida kutoa heshima kwenye kaburi la marehemu babu yangu. Sikuwa nimefika huko tangu nilipoondoka nikiwa na umri wa miaka mitatu.
“Nilipokuwa njiani, nilimuona mzee akiwa na maji yenye rangi ya njano, machafu ambayo aliyatumia kwa kunywa. Nilishangaa, maana hali ile sikuwahi kufikiri kama ipo vile. Kipindi hicho nilikuwa nimemaliza Chuo Kikuu cha Georgetown, Marekani.”
Mo anasema kuwa aliingiwa na hisia kutaka kujua nini hasa alichokuwa anahitajika kufanya, alimfuata yule mzee aliyekuwa na maji yale, alipozungumza naye, aliwazungukia watu wengine na kuridhika kuwa ile ndiyo hali halisi, hapo ndipo fikra ya kwa nini agombee ubunge ilipoanzia.
Anasema kuwa baada ya kujiridhisha hivyo, alirudi kwa mzee wa kwanza, alizungumza naye na kumuuliza ni kwa nini shida ile ilikuwa haizungumzwi kwa upana katika mamlaka husika.
IMG_3434
Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji pamoja na ujumbe wake alioambatana nao kutoka Tanzania.
“Nilipojitambulisha yule mzee alisema anamkumbuka babu yangu, kisha akanishauri nigombee ubunge, alinisisitiza mno ili nisaidie kuondoa lile tatizo la watu wa Singida kunywa maji machafu,” alisema Mo.
Anaeleza kuwa alipokuwa njiani kurejea Dar es Salaam, alilifikiria tatizo hilo kwa mapana zaidi, akalifanyia utafiti na kubaini kwamba katika kila watu 10, watatu walikuwa wakipoteza maisha kutokana na maradhi yanayosababishwa na maji machafu.
Anaendelea kusema kuwa aligundua kuwa Singida kulikuwa na tatizo kali la maji safi na salama. Anasema kuwa alibaini uwepo wa tatizo la elimu kuhusu matatizo ya maji.
Jambo lingine ambalo anasema aliligundua ni uwepo wa tatizo la huduma za afya. “Niliwafikiria watoto wangu, jinsi ninavyowapenda, na namna ambavyo kila mzazi anavyompenda mwanaye. Nilipingana na hali kuwa watoto wa Uingereza na Marekani wamependelewa zaidi. Maisha ni sawa bila kujali chochote,” anasema Mo.
IMG_3359
Sehemu ya ujumbe kutoka Tanzania uliombatana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji kwenye hafla hiyo.
“Niliona lazima nitimize wajibu wangu. Kutimiza malengo yangu ya kusaidia jamii, kufanikiwa katika biashara. Mambo hayo mawili hisani na biashara nimeyaweka pamoja na ndiyo maana nimefika hapa leo, tunajivunia sana kuitwa METL nembo ya Watu. Katika miaka yangu 10 kama mbunge, nimefanya mabadiliko mengi. Nilikuwa na sababu ya kupata mkopo nafuu wa dola milioni 35, ambao ulisababisha kuwekwa kwa miundombinu ya maji safi na salama Manispaa ya Singida.
“Niliitumia MeTL, tuliweza kudhamini shughuli nyingi za maendeleo ya kijamii. Kuhusu elimu, nilifanikisha kujenga shule 15, zikawa 17, kabla ya hapo tulikuwa na shule mbili tu. “Kuhusu huduma za afya, hapa nimshukuru mke wangu kwa jitihada zake. Alikuwa Mwenyekiti wa taasisi ya Tumaini la Maisha ambayo imekuwa ikisaidia watu wengi, hasa watoto dhidi ya maradhi ya saratani.”
IMG_3469
Burudani mbalimbali zikiendelea ukumbini hapo.
IMG_3548
Mkurugenzi Mtendaji wa Jarida la Forbes Afrika, Sid Wahi akitoa neno la ukaribisho kwa wageni waalikwa. Kulia ni Head of Events wa ABN Productions, Alexander Leibner.
DSC_4663
Mwanzilishi na mchapishaji wa jarida la Forbes Afrika, Bw. Rakesh Wahi ( wa pili kushoto) akikamkabidhi Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania na Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji (wa pili kulia) tuzo ya Heshima Barani Afrika "2015 Forbes Africa Person of the Year" iliyotolewa na Jarida la Forbes Afrika kwa kutambua mchango wake katika kusaidia jamii ikiwemo kutoa ajira kwa zaidi ya watu 26,000 nchini na mambo mengine yanayoigusa jamii. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi Mtendaji wa Forbes Afrika, Sid Wahi (kulia) na MEC Panyaza Lesufi kutoka kitengo cha elimu, Gauteng Province (kushoto).
IMG_3780
Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania na Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akitoa neno la shukurani baada ya kukabidhiwa kwa tuzo, alisema anatoa tuzo hiyo kwa vijana wa Kitanzania kwani ndio nguvu kazi inayobeba uchumi wa nchi.
IMG_3776
IMG_3825
MO akiteta jambo na Mchumi mahiri raia wa Nigeria ambaye kwa sasa ni Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, Arunma Oteh (kulia) ambaye walikuwa pamoja kwenye kinyang'anyiro cha kuwania tuzo hiyo ambapo pia alimpongeza sana.
IMG_3849
Pichani juu na chini MO akiendelea kupongezwa na wadau mbalimbali walioalikwa kwenye hafla hiyo.
IMG_3866
IMG_3875
Pongezi kwa MO zikiendelea kutolewa.
IMG_3889
IMG_3857
MO katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Jaguar Land Rover ambao ni miongoni mwa wadhamini wa sherehe za tuzo hizo.
IMG_3940
MO katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Makampuni ya MeTL Group, Vipul Kakad mara baada ya kutwaa tuzo hiyo.
IMG_3925
Makamu wa Rais wa MeTL GROUP, Vipul Kakad na Shemane Amin wakipitia moja ya taarifa iliyowavutia kwenye jarida la Forbes Afrika.
IMG_3911
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Jaguar Land Rover ya Afrika Kusini wakipozi kwenye 'Red Carpet'.

Saturday, November 28, 2015

MKURUGENZI WA AMANA BANK AFUNGUA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA TAWI LA MWANZA

Mkurugenzi wa benki ya Amana  Dk Muhsin Masoud  akimkabidhi  zawadi mteja Yasmin Ismail Mussa kwa utunzaji bora wa fedha katika tawi la Mwanza.


Benki ya Amana leo hii imehitimisha wiki ya huduma kwa wateja ambapo katika tawi la Mwanza mkurugenzi wa benki hiyo Dk Muhsin Masoud alitoa zawadi mbali mbali kwa wateja wenye sifa tofauti tofauti kama ioneshavyo pichani. 

Mkurugenzi huyo alikutana na wateja mbali mbali tawini  hapo ili kubadilishana nao mawazo na pia kupokea maoni toka kwao katika kuboresha huduma kwa wateja wa benki hiyo pekee ya Ki Islamu nchini. 

Kilele hicho cha wiki ya huduma kwa wateja kimefanyika katika matawi yote ya benki hiyo ambayo kwa Dar es Salaam ni Tandamti, Lumumba, Nyerere na Main, vile vile Arusha na Mwanza.
Mkurugenzi wa Amana Bank Dk Muhsin Masoud akimzawadia Bw Juma Kivuruga kwa kuwa mfanyakazi bora kwa tawi la Mwanza, Kivuruga alipigiwa kura na wafanyakazi wenziye wa tawi hilo.
Daud Lweno akizawadiwa na Mkurugenzi wa Amana Bank kama mteja mzuri kulipia miamala ya TRA katika tawi la Mwanza.
Mteja Yasmin Ismail akikata keki ya kuadhimisha miaka minne tangu kufunguliwa kwa benki hiyo, huku wafanyakazi wa benki hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi wao wakifuatilia tukio hilo kwa umakini.
Bw Juma Msabaha meneja huduma kwa wateja wa Amana bank akijibu baadhi ya maswali kuhusu benki hiyo toka kwa waandishi wa habari.
Meneja wa tawi la Mwanza Saleh Awadh akiongea na mteja wa benki hiyo.
Hawa Maftah wa Amana Bank akimhudumia mteja mapema leo katika tawi.
Mkurugenzi Dk Muhsin Masoud akiongea na mmoja wa mamia ya wateja aliokutana nao leo katika tawi la jijini Mwanza ambako alikuja rasmi kwa shughuli ya ufungaji wa wiki ya huduma kwa wateja.
Picha ya pamoja wafanyakazi wa benki hiyo na mkurugenzi wao.
Zainab Barker ambaye ni meneja huduma kwa wateja wa tawi la Mwanza.
Ibtisam Akrabi akimhudumia mteja katika tawi la Mwanza.
Mahmoud Maimu akimhudumia mteja.

KAMPENI YA ABIRIA PAZA SAUTI YAZINDULIWA RASMI JIJINI DAR ES SALAAM

Mkuu wa Kitengo cha Elimu kwa Umma wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Abel Swai (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo, kuhusu kampeni ya Abiria Paza Sauti iliyozinduliwa Dar es Salaam leo asubuhi.

Na Dotto Mwaibale

MKUU wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna wa Polisi, Mohamed Mpinga amesema kila mwananchi anawajibu kuzuia ajali za barabarani badala ya kudhani kazi hiyo ni ya polisi pekee.

Mpinga alitoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Abiria Paza Sauti iliyozinduliwa Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam leo asubuhi, ambao ulikwenda sanjari na mabalozi wa Usalama barabarani  (RSA) ambao walitoa elimu  kwa abiria kuhusu usalama barabarani.

"Abiria pazeni sauti pale mtakapoona dereva anaendesha gari lake ndivyo sivyo na kama mtapaza sauti itasaidia kupunguza ajali hapa nchini" alisema Kamanda Mpinga.

Mwakilishi  wa Mwenyekiti wa Usalama Barabarani ambaye ni Mratibu wa kampeni hiyo , Jackson Kalikuntima, alisema kampeni hiyo itaendelea nchini kote kwa njia ya kutoa elimu, haki na wajibu wa raia wanapokuwa safarini.

Alisema abiria wanaowajibu wa kuzuia ajali wakishirikiana na mabalozi watakao kuwa ndani ya mabasi kuhimiza abiria kupaza sauti.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Elimu kwa Umma wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Abel Swai alisema kumekuwa na changamoto kubwa kwa baadhi ya madereva kukiuka sheria na kusababisha ajali kwa makusudi.

Alisema kampeni hiyo inalengo la kutoa elimu kwa abiria waweze kujiamini na kutoa taarifa pale wanapoona dereva anakwenda kinyume na sheria kwa kutumia namba za kutoa taarifa kwa polisi na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) ambazo ni 0800110019 au 0800110020.

Swai alisema madereva wanapaswa kutii sheria bila shuruti na kuwa wana amini kila mmoja atakuwa makini na kuzingatia sheria ajali zitapungua kama sio kuisha kabisa.


NHIF YAKABIDHI KITUO CHA MATIBABU CHA MFANO DODOMA

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Michael Mhando akionesha funguo za Jengo la Kituo cha Mfano cha NHIF Dodoma mara baada ya kukabidhiwa jengo

Ujumbe wa NHIF na Hospitali ya Mkoa Mara baada ya kupokea Jengo
Kituo cha Matibabu cha Mfano cha NHIF Dodoma
Kituo cha Matibabu cha Mfano cha NHIF Dodoma_sehemu ya mapokezi

 MFUKO wa taifa wa bima ya afya (nhif) umekabidhiwa kituo chake cha
matibabu cha mfano mara baada ya ujenzi wa kituo hicho kukamilika.

Makadhiano hayo yamefanyika mjini hapa jana (leo) katika hafla fupi
iliyohudhuriwa na Uongozi wa nhif, hospitali ya mkoa na timu ya
wakandarasi akiwemo mshauri mkuu wa mradhi huo kampuni ya Nosuto
Associates.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Michael Mhando amesema kukamilika kwa
jengo hilo ni hatua kubwa iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na kazi
iliyoko sasa ni ya ununuzi wa vifaa na samani za jengo ili lianza
kutoa huduma kabla ya sikukuu ya Krismasi.

Amesema timu ya wataalamu kutoka Sekteratarieti ya mkoa tayari iko
jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuchagua vifaa tiba mbalimbali
vitakavyotumika. Ameongeza kuwa vifaa vyote hivyo pamoja na samani za
jengo hili vitalipiwa na Mfuko wa NHIF.

Kituo hicho cha matibabu cha kisasa kinayo mifumo mbalimbali ya TEHAMA
katika utoaji wake wa huduma ikiwemo miito kwa wauguzi,  utayarishaji
wa madai na utambuzi wa wagonjwa.

Amesema malengo makuu ya ujenzi wa kituo hicho ni kuwa na kituo cha
kisasa kitakachowezesha wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na
umma wa watanzania kwa ujumla kupata huduma bora za matibabu
wanapokuwa Dodoma katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa.

Naye Mkurugenzi wa fedha,mipango na uwekezaji wa nhif bw Desudedit
Rutazaa amesema Kituo hicho vilevile kitasaidia kuwepo na watalamu
wenye uzoefu nchini kwani itakuwa ni sehemu ya kujifunzia kwa
wataalamu wa kada mbalimbali za udaktari na utabibu wawapo masomoni
katika mkoa wa Dodoma na mikoa mingine ya Tanzania.