Pages

KAPIPI TV

Saturday, November 28, 2015

NHIF YAKABIDHI KITUO CHA MATIBABU CHA MFANO DODOMA

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Michael Mhando akionesha funguo za Jengo la Kituo cha Mfano cha NHIF Dodoma mara baada ya kukabidhiwa jengo

Ujumbe wa NHIF na Hospitali ya Mkoa Mara baada ya kupokea Jengo
Kituo cha Matibabu cha Mfano cha NHIF Dodoma
Kituo cha Matibabu cha Mfano cha NHIF Dodoma_sehemu ya mapokezi

 MFUKO wa taifa wa bima ya afya (nhif) umekabidhiwa kituo chake cha
matibabu cha mfano mara baada ya ujenzi wa kituo hicho kukamilika.

Makadhiano hayo yamefanyika mjini hapa jana (leo) katika hafla fupi
iliyohudhuriwa na Uongozi wa nhif, hospitali ya mkoa na timu ya
wakandarasi akiwemo mshauri mkuu wa mradhi huo kampuni ya Nosuto
Associates.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Michael Mhando amesema kukamilika kwa
jengo hilo ni hatua kubwa iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na kazi
iliyoko sasa ni ya ununuzi wa vifaa na samani za jengo ili lianza
kutoa huduma kabla ya sikukuu ya Krismasi.

Amesema timu ya wataalamu kutoka Sekteratarieti ya mkoa tayari iko
jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuchagua vifaa tiba mbalimbali
vitakavyotumika. Ameongeza kuwa vifaa vyote hivyo pamoja na samani za
jengo hili vitalipiwa na Mfuko wa NHIF.

Kituo hicho cha matibabu cha kisasa kinayo mifumo mbalimbali ya TEHAMA
katika utoaji wake wa huduma ikiwemo miito kwa wauguzi,  utayarishaji
wa madai na utambuzi wa wagonjwa.

Amesema malengo makuu ya ujenzi wa kituo hicho ni kuwa na kituo cha
kisasa kitakachowezesha wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na
umma wa watanzania kwa ujumla kupata huduma bora za matibabu
wanapokuwa Dodoma katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa.

Naye Mkurugenzi wa fedha,mipango na uwekezaji wa nhif bw Desudedit
Rutazaa amesema Kituo hicho vilevile kitasaidia kuwepo na watalamu
wenye uzoefu nchini kwani itakuwa ni sehemu ya kujifunzia kwa
wataalamu wa kada mbalimbali za udaktari na utabibu wawapo masomoni
katika mkoa wa Dodoma na mikoa mingine ya Tanzania.

No comments: