Pages

KAPIPI TV

Thursday, August 6, 2015

WASHIRIKI WA SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2015 WAWASILISHA MIRADI YAO YA KILIMO NA MAZINGIRA KWA WANAKIJIJI CHA KISANGA WILAYANI KISARAWE PWANI


 Washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015 wakiwa katika Bwawa la Lamboni wakipata maelezo kutoka kwa wanakijiji hii ikiwa ni moja ya sehemu ya ziara yao jana .
 Wenyeji pamoja na  Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula wakielekea Mabondeni..Ilikuwa ni nafasi yao ya kufahamu maeneo mbalimbali Kijijini hapo...
 Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa chakula wakioneshwa Madhari ya shule ya Msingi ya Kisanga na mmoja wa wanakijiji aliyesimama Mbele Kulia.
 Hapa washiriki wa Shindano la Mama Shijaa wa chakula 2o15 linalo andaliwa na Oxfam kupitia kampeni yao ya Grow , kipindi kinachoruka kila siku ITV kuanzia Saa Kumi na mbili  Jioni na Kurudiwa saa Tano na nusu asubuhi  wakiwa katika ofisi ya Kusindika zao la Mihogo
 Hapa washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 msimu wa nne wakiwa katika moja ya kisima ambacho maji yake yananukia Mafuta, maji haya yanatumika zaidi katika shughuli za Kufulia Nguo.
 Mwakilishi kutoka Oxfam Eluka Kibona aliyesimama (Kulia) akizungumza na Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula Pamoja na wanakijiji katika Kijiji Cha Kisanga jana.
 Kundi la kwanza la Washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015 wakiwasilisha Mradi wao wa Mazingira..
 Wanakijiji na Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 wakiwasikiliza jinsi Miradi inavyo wasilishwa.
 Kundi la pili la washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 wakiwasilisha Mradi wao wa Kilimo Bora.

 Kundi la Tatu la washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 wakiwasilisha Mradi wao wa Kilimo Bora cha Mboga Mboga na Hihogo.
********
Ni siku nyingine tena katika kijiji cha Kisanga, jua la saa nne asubuhi ni kali huku  mti huu mkubwa wa mkorosho uliopo eneo la makutano unatusitiri. Washiriki wa shindano la Mama shujaa wa Chakula Shindano lililiondaliwa na Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow, walikuwa wamesimama vikundi vikundi, bila shaka walikuwa wanahadithiana chakula walichowapikia wenyeji wao jana. 

Siku ya ilikuwa  inaanza kwa waandaaji wa shindano kutengeneza makundi matatu ya kina Mama Shujaa wa Chakula watano watano. 

Kwa muda watakaokaa hapa kijijini Kisanga, kila kundi linatakiwa kutengeneza mradi wa maendeleo endelevu kwa manufaa ya kijiji cha Kisanga. Ili kufahamu fursa na changamoto zilizopo, uongozi wa kijiji unawatembeza sehemu nne. 

Upatikanaji wa maji ya uhakika kijijini hapa ni changamoto. Kina Mama Shujaa wa Chakula wanaletwa sehemu hii yenye bwawa, wenyeji wanaiita lamboni. Inasadikika kuwa zamani kulikuwa na kisima, ila kwa sasa kimefunikwa na wingi wa maji. Pia kuna viumbe wakali kama vile chatu. 

Elimu ya msingi katika kijijini Napo inatolewa katika shule ya msingi Kisanga. Wakina Mama Shujaa wa Chakula wanaoneshwa mandhari ya shule na mwenyeji. 

Wakazi wa kijiji cha Kisanga wanapata maji ya kunywa na kupikia katika visima vilivyopo eneo hili linaloitwa Mfuru. Kufuatia msimu wa mvua ulioisha, visima vyote vinne vina maji ya kutosha, japo kisima kimoja maji yake hayatumiwi kwa kunywa kwani yana harufu inayosadikika kuwa ni ya mafuta. Hata hivyo, wakati wa kiangazi kina mama (wenyeji) wanalazimika kuamka saa tisa alfajiri kutokana na uhaba wa maji, na kibaya zaidi usalama wao wakiwa njiani ni wa mashaka kwani hawapewi msaada na waume zao (kwa walioolewa). 

Ziara ya kutembelea kijiji inafika kwenye hospitali/kituo cha afya cha Kisanga. Kina Mama shujaa wa chakula wanashangaa kuambiwa bei kubwa ya matibabu katika kituo hicho, ambacho kwa siku ya leo kimefungwa. 

Zao kuu la Kisanga ni mihogo. Ziara ya kina Mama Shujaa wa Chakula inaishia katika kituo cha kusindika mihogo. Hapa kunasagwa unga wa mihogo, pia tambi na keki za unga wa mihogo zinatengenezwa hapa. 

Naam, muda wa makundi kuwasilisha mapendekezo ya mradi wa maendeleo endelevu waliopanga mbele ya wanakijiji wa Kisanga unawadia.

KUNDI LA KWANZA 

Kutoa elimu juu ya mazingira, Kuchimba mashimo ya taka. Wafanyabiashara wanawake walio barabarani wafunike chakula ili vumbi lisiingie.Wana Kisanga wote watahitajika kufanya usafi jumamosi.  Kuanzisha shamba darasa na kutoa elimu.

KUNDI LA PILI
Biashara cha mboga na matunda kwenye bonde (karibu na bwawa) kwa kutumia mbolea asili na maji yaliyopo. Kutoa elimu kwa kupitia shamba darasa jinsi ya kutumia rasilimali za kijiji kwa ajili ya maendeleo ya kijiji

KUNDI LA TATU
Mradi wa kilimo bora. Kilimo cha mbogamboga na kilimo cha mihogo na mahindi kwenye muinuko wa bonde. Wananchi kupewa elimu ya kilimo bora, kutumia wataalamu waliopo

Siku inaisha kwa waandaaji kupanga makundi matatu mapya ambayo watapewa kazi ambayo lazima iishe kesho hiyohiyo.

ILI KUMPIGIA KURA MSHIRIKI  BOFYA HAPA>>>

MKUTANO MKUU ADC WAMPITISHA, CHIEF LUTASOLA YEMBA KUWA MGOMBEA URAIS TANZANIA BARA, SAID MIRAJI ABDULLAH MGOMBEA MWENZA

 Mgombea urais wa chama cha ADC,  Zanzibar, Hamad Rashid Hamad, akihutubia katika mkutano huo.
 Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bara kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Chief Lutasola Yemba (katikati), akimtambulisha mgombea mwenza wake, Said Miraji (kulia), katika mkutano mkuu wa tatu wa chama hicho uliofanyika Dar es Salaam leo. Kushoto ni mgombea urais wa chama hicho, Zanzibar, Hamad Rashid Hamad.
 Makamu Mwenyekiti wa ADC, Zanzibar, Faki Hamisi Silima, akizungumza katika mkutano huo.
 Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bara kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Chief Lutasola Yemba (kulia), na mgombea mwenza wake, Said Miraji, wakiwapungia mkono wanachama wa chama hicho katika mkutano mkuu huo.
 Katibu Mkuu wa chama hicho, Lydia Bendera akimpongeza. Said Miraji kwa kuteuliwa kuwa  mgombea mwenza.
 Makada wa chama hicho wakiwa na furaha kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea. 

NCHI WAHISANI WATOA DOLA ZA MAREKANI MILIONI 802.15 KUKABILI MABADILIKO YA TABIA NCHI

IMG_1116
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akimkaribisha ofisini kwake Mwakilishi wa mtandao wa FANPRAN, Sithembile Ndema kwa ajili ya kusaini kitabu cha wageni kabla ya kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Na Mwandishi wetu
JUMLA ya dola za Marekani milioni 802.15 zimetolewa na nchi wahisani katika kusaidia mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi katika kipindi cha miaka miaka mine iliyopita.
Hayo yalielezwa na Mkurugenzi wa Kituo cha Mabadiliko ya tabia nchi Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Profesa Pius Yanda wakati alipokuwa akitoa mada kuhusu utafiti alioufanya yeye na wenzake kuhusu mchango wa uwezeshaji mapambano hayo kutoka nchi marafiki.
Alisema kiasi hicho cha fedha ni sawa na wastani wa dola milioni 200 kila mwaka zilizokuwa zikipelekwa katika sekta mbalimbali nchini.
Alisema utafiti walioufanya ambao ulilenga kuona kiasi cha fedha zilizotoka kwa wafadhili kwa ajili ya miradi mbalimbali ni awamu ya pili ya utafiti ambao awali ulijikita kuona bajeti ya taifa inavyotumika kukabili mabadiliko ya tabia nchi.
Profesa Yanda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere cha Mazingira amesema kwamba sehemu kubwa ya fedha ipo katika miradi ya maendeleo ambayo utekelezaji wake pamoja na kutosema kwamba unakabili mabadiliko ya tabia nchi, matokeo yake ndiyo yanayobainisha.
IMG_1128
Mkurugenzi wa Kituo cha Mabadiliko ya tabia nchi Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Profesa Pius Yanda (kushoto) akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (wa pili kushoto) huku wengine wakishuhudia zoezi hilo, Kulia ni Mwakilishi wa FANPRAN, Sithembile Ndema na wa pili kulia Mtafiti msaidizi kutoka ESRF, Ian Shanghvi.
Alitolea mfano kuwa miradi ya kusambaza umeme vijijini ( REA) nchini ambayo ilipata fedha nyingi katika miaka ya 2011 na 2012 ni miradi ya maendeleo lakini hatima yake ni kuzuia ukataji hovyo wa miti kwa ajili ya nishati.
Akifafanua fedha hizo zaidi alisema kwamba Tanzania mwaka 2010 jumuiya ya kimataifa zilitoa dola za Marekani milioni 171.93, mwaka 2011 dola za Marekani milioni 225.35, mwaka 2012 dola za Marekani milioni 229.74 na mwaka 2013 Tanzania ilipata dola za Marekani milioni 175.14.
Utafiti huo ambao uligharamiwa na COMESA, EAC na SADC umewasilishwa katika mkutano wa kitaifa wa uwezeshaji wa miradi ya kukabili tabia nchi kwa mfumo wa ndani ambapo pia Mwakilishi wa mtandao wa FANRPAN, Sithembile Ndema alikuwepo kuelezea maana ya mikutano ya kisera katika nchi zinazounda mtandao huo.
Mtandao huo ambao ulianzishwa mwaka 1994 baada ya mkutano wa mawaziri wa kilimo wa nchi za SADC, EAC na COMESSA na makao makuu yake kuwa nchini Zimbabwe ulianza kazi mwaka 1997 na sasa makao makuu yapo nchini Afrika Kusini.
Mtandao huo umelenga kuwezesha mataifa ya Afrika kuendesha kilimo na ufugaji unaozingatia mabadiliko ya tabia nchi na hivyo kutunza mazingira na kuongeza tija.
Mikutano ya aina hiyo pia inafanyika Uganda, Ethiopia, Kenya na Zambia.
Profesa Yanda alisema kwamba pamoja na fedha hizo kuonekana nyingi kiukweli ni haba kutokana na hali halisi ilivyo sasa na hasa ikizingatiwa kwamba kunatakiwa pia fedha za mabadiliko tabia nchi yenyewe badala ya kutumia miradi ya maendeleo ambao matokeo ni kukabili mabadiliko ya tabia nchi.
IMG_1149
Mshehereshaji Hanif Tuwa kutoka ESRF, akitoa mwongozo wa yatakayojiri kwenye mkutano wa kitaifa wa kujadili sera ya uwezeshaji kifedha mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za ESRF.
Alisema takwimu walizopata kuhusu fedha zilizofika nchini kutoka katika jumuiya ya kimataifa zililingana na taarifa zilizopo Hazina na kuonesha kwamba fedha hizo zilienda kutumika katika makadirio yaliyokusudiwa.
“tofauti iliyopo ni tafsiri ya miradi ya mabadiliko ya tabianchi. Miradi ya maendeleo, inatamkwa kama miradi ya maendeleo lakini ukiangalia mwishoni ni miradi hiyo kusaidia katika kukabili mabadiliko ya tabia nchi” alisema katika mahojiano baadae na na waandishi wa habari.
Alisema kama Mkurugenzi wa Kituo cha mabadiliko ya tabia nchi anashauri serikali kuhimiza wananchi wake kuendelea kusimamia mazingira vyema huku wakulima na wafugaji wakisikiliza maofisa ugani kwa ajili ya kuwa na kilimo na ufugaji bora usioharibu mazingira..
Alisema tafiti mbalimbali zinaonesha kuwepo kwa athari kubwa ya mabadiliko ya tabia nchi ambapo sasa hata sehemu za baridi za nyanda za juu zimeanza kuwa na magonjwa ya Malaria huku wakulima wakiwa hawajui muda wa kupanda kutokana na mabadiliko ya joto na pia unyeshaji wa mvua.
Alisema pia nyanda za juu sasa zinakabiliwa na wadudu waharibifu wa mazao vitu ambavyo awali havikuwepo.
Alisema kwamba bado taifa linahitaji kufanya tafiti nyingi zaidi na kuzitumia kuelimisha umma kuhusu nini kinatokea na nini kinastahili kufanywa kukabili mabadiliko hayo.
IMG_1174
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akihutubia mkutano wa kitaifa wa kujadili sera ya uwezeshaji kifedha mabadiliko ya tabia nchi. Mkutano huo umefanyika jana jijini Dar es salaam katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za ESRF na kujadili taarifa ya utafiti uliofanywa kwa miaka minne kuhusiana na uwezeshaji.
Mkutano huo wa kitaifa ulifunguliwa na Mkurugenzi wa Taasisi huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) Dk. Tausi Kida ambaye alisema lengo la mkutano huo ni kuchambua utafiti uliofanywa na kuja na maazimio yatakayosaidia kuboresha kilimo na kuhifadhi mazingira katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.
Aliwaambia washiriki kuiangalia kwa makini tafiti ya Profesa Pius Yanda na kuhakikisha kwamba wanakuwa na uelewa wa maudhui na kuwezesha kutoa dira ya utekelezaji katika siku za usoni.
Alisema wakati taifa linajipanga kutekeleza mpango wake wa maendeleo wa kuelekea katika uchumi wa viwanda suala la mabadiliko tabia nchi haliwezi kuachwa na hivyo wajumbe wa mkutano walitakiwa kuangalia na kuja na mapendekezo yao.
Mapendekezo hayo ni pamoja na kuwa na kilimo na ufugaji wenye tija unazoingatia ufanisi katika hifadhi ya mazingira na namna uwezeshaji wa ndani unavyoweza kuendeleza mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.
Alisema ni muhimu kilimo kuwa ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
ESRF ni taasisi yinayojishughulisha na tafiti mbalimbali za jiuchumi na kijamii zinazotoa mwelekeo wa utekelezaji wa sera na kanuni mbalimbali za maendeleo na ustawi wa jamii.
Pmaoja na kuratibu mkutano huo pia ilitoa nafasi ya ukumbi wake kutumika na kutoa mwelekeo wa mkutano na umuhimu wake katika mpango wa pili wa maendeleo wa taifa ambao unatakiwa uzingatie mabadiliko ya tabia nchi.
IMG_1161
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akisoma hotuba na kuwakaribisha washiriki wa mkutano wa kitaifa wa kujadili sera ya uwezeshaji kifedha mabadiliko ya tabia nchi. Kulia ni Mwakilishi wa FANPRAN, Sithembile Ndema na kushoto ni Mkurugenzi wa Kituo cha Mabadiliko ya tabia nchi Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Profesa Pius Yanda.
IMG_1203
Mwakilishi wa FANPRAN, Sithembile Ndema akielezea mradi wa COMESA wa uwezashaji wa ndani wa fedha kwa ajili ya mabadiliko ya tabia nchi katika mkutano huo.
IMG_1249
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (katikati) na Mkurugenzi wa Kituo cha Mabadiliko ya tabia nchi Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Profesa Pius Yanda (kulia) wakifuatilia ka umakini 'presentation' ya Mwakilishi wa FANPRAN, Sithembile Ndema (hayupo pichani).
IMG_1318
Mkurugenzi wa Kituo cha Mabadiliko ya tabia nchi Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM), Prof. Pius Yanda, akitoa mada ya ufadhili wa kimataifa wa uwezeshaji wa kifedha wa mabadiliko ya tabianchi Tanzania katika mkutano huo.
IMG_1370
Pichani juu na chini washiriki wakichangia mawazo yao kuhusu namna sera ya uwezeshaji kifedha mabadiliko ya tabia nchi inavyopaswa kuwa katika mkutano huo.
IMG_1343
IMG_1150
Pichani juu na chini ni washiriki kutoka taasisi mbalimbali za serikali na zisizo za serikali, watafiti, na wadau wa maendeleo waliohudhuria mkutano wa kitaifa wa kujadili sera ya uwezeshaji kifedha mabadiliko ya tabia nchi.
IMG_1155
IMG_1231 IMG_1260
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano wa kitaifa wa kujadili sera ya uwezeshaji kifedha mabadiliko ya tabianchi.
IMG_1256
Picha ya pamoja ya washiriki.

Tuesday, August 4, 2015

BALOZI LIBERATA MULAMULA ATINGA NDANI YA STUDIO YA KILIMANJARO

 Balozi Liberata Mulamula akiwasili nje ya jengo lenye studio ya Kilimanjaro tayari kuongea LIVE katika kipindi cha Jukwaa langu kinachorushwa kila siku ya Jumatatu kuanzia saa 12 jioni mpaka saa 2 usiku saa za Mashariki za Marekanui. anayemfungulia mlango ni Abdul Malik
 Balozi Liberata Mulamula akiingia ndani ya studio akiwa amesindikizwa Harriet Shangarai (kushoto) ambaye pia ni Mkurugenzi wa studio hiyo, kulia ni Afisa Ubalozi Swahiba Mdeme na Abdul Malik
 Balozi Liberata Mulamula akipata maelezo kutoka kwa studio meneja ambaye pia ni mtangazaji na mtayarishaji wa kipindi cha Jukwaa langu, Bwn. Mubelwa Bandio (hayupo pichani) Kushoto ni Afisa Ubalozi Swahiba Mdeme akifuatilia maelezo hayo.
 Mhe. Liberata Mulamula akiendelea kusikiliza maelezo kutoka kwa meneja wa studio Mubelwa Bandio ambaye ni mtangazaji na mtayarishaji wa kipindi cha jukwaa lako. Kati ni matangazaji maarufu wa Radio ya Times FM na aliyewahi kutangaza  Radio One Bi. Rose Chitalah ambaye pia anamsaidia Mubelwa Bandio katika utangazaji na kuchangia hoja mbalimbali katika kipindi cha Jukwaa langu.
 Balozi Liberata Mulamula akiendelea kujibu maswali ya watangazaji mahiri Mubelwa Bandio (kulia) na Rose Chitalah (hayupo pichani ) na wasikilizaji waliokua na shahuku ya kumuuliza maswali.
  Balozi Liberata Mulamula akiendelea kujibu maswali ya watangazaji mahiri Bwn. Mubelwa Bandio (hayupo pichani ) na Rose Chitalah (kushoto)
 Afisa Ubalozi Swahiba Mdeme akisikiliza mahojiano na kunakili baadhi ya vipengele katika mahojiano hayo.
 Kutoka kushoto ni Afisa Ubalozi Swahiba Mdeme, Mhe. Balozi Liberata Mulamula na mtangazaji mahiri Rose Chitalah wakiwa katika picha ya pamoja.
 Kutoka kushoto ni Dj Luke Joe, Meneja wa studio ya Kilimanjaro,  Mubelwa Bandio, Mhe. Balozi Liberata Mulamula na mtangazaji mahiri Rose Chitalah wakipata picha ya kumbu kumbu na Balozi Liberata Mulamula anayemaliza muda wake kama Balozi wa Tanzania nchini Marejkani na Canada na sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa

TANZANIA YAWA KIVUTIO KATIKA MAONESHO YA AFRIKA MASHARIKI YANAYOFANYIKA NAIROBI NCHINI KENYA

Ufunguzi wa maandamano ya maonyesho ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yajulikanayo kama JAMFEST yaliyoanza leo katika Viunga vya Ukumbi wa Kimataifa wa Kenyata uliopo jijini Nairobi Kenya.
Muongozaji wa bendi ya polisi nchini Kenya akiongoza maandamano ya Ufunguzi wa Maonyesho ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo nchi zote za Afrika Mashariki zimeshiriki maonyesho hayo yanayoanza leo katika viunga vya Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyata.
Msafara wa uzinduzi wa maonyesho ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ukiwa unatoka katika viwanja vya Uhuru Park uliopo ndani ya jiji la Nairobi kuelekea katika Viunga vya Ukumbi wa Kimataifa wa Kenyata ambapo baadhi ya wakazi wa nchi mbalimbali kutoka Afrika Mashariki wakionyesha bidhaa zao.
Watanzania wakiwa na bendera ya nchi kabla ya maandamano kuanza Katika viwanja vya Uhuru Park jijini Nairobi
Watanzania wakiwa na furaha ya kushiriki maonyesho ya jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoanza kufanyika katika Viwanja vya KICC Nairobi Kenya.
Watanzania wakitoa burudani katika viwanja vya Uhuru Park kabla ya Maandamo ya Ufunguzi wa Maonyesho ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoanza leo katika viwanja vya KICC Nairobi Kenya.
Tanzania Kwanza mengine baadae..
Wadau wa Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja.Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

"BAADA YA KURA ZA MAONI RAGE KUMFUATA LOWASSA CHADEMA"?



Na Mwandishi wetu,Tabora mjini.


SIKU CHACHE mara baada ya kufanyika uchaguzi wa kura za maoni za kuchagua Mgombea atakayeteuliwa  kuwania  Ubunge wa Jimbo la Tabora mjini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi,baadhi ya wananchi mjini Tabora wakiwemo wanachama wa CCM wamejikuta wakijiuliza maswali yasiyokuwa na majibu ya haraka kuhusu aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Tabora mjini Bw.Aden Rage kuwa ataendelea kuwa mwanachama wa chama hicho au atakihama kutokana na matokeo ya kura za maoni ambapo alipata kura ambazo hakutarajia kuzipata.

Mtazamo huo wa wananchi  wa Jimbo  la  Tabora mjini na pengine wa baadhi ya makada wa Chama cha Mapinduzi kuona viongozi wanaoona dalili ya kushindwa kwenye uchaguzi wa kura za maoni na kukimbilia kwenye vyama vya upinzani umekuja kufuatia hasa baadhi ya wabunge ambao walikuwa wakionesha kuwa ni maswahiba wa karibu wa Waziri mkuu mstaafu Bw.Edward Lowassa kumfuata kwenye chama alichohamia sasa Chadema.

Rage baada kupata kura 4133 akiwa  ameshika nafasi ya pili kinyume na matarajio yake  ambapo mshindi wa kwanza Emmanuel Mwakasaka  alipata kura 13,335,Wananchi wamekuwa wakijiuliza kuwa huenda kiongozi huyo akakihama Chama cha Mapinduzi kutokana na matokeo hayo ambayo yanadhihirisha kutokukubalika kwake na wengi kama alivyodhani na pengine kupewa moyo na wapambe wake wa karibu huku dalili za wazi zikidhihirisha kuwa kutokana na ukaribu wake na Bw.Lowassa huenda nae akafanya maamuzi magumu ya kumfuata Chadema.

Aidha mtazamo mwingine wananchi ambao umekuwa ukizidi kuwapa ukweli wa madai kwamba huenda Rage akahamia Chadema na pengine chama chochote cha siasa ni pale wanaposikiliza Redio anayoimiliki ikiendelea kuwaponda baadhi ya viongozi wa CCM na hata kufikia hatua ya kuwashawishi wananchi katika uchaguzi mkuu wa oktoba wachague viongozi wa Upinzani kwa madai kwamba CCM imepoteza dira.

Hata hivyo mtandao huu unaendelea kumtafuta Rage ili aweze kubainisha ukweli wa madai ya kuhamia Chadema kama ilivyozagaa katika maeneo mbalimbali Jimbo la Tabora mjini ikiwemo katika vikundi vya mitandao  ya kijamii  maarufu Whatsap.

Habari za ndani kutoka Chadema:-
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema jimbo la Tabora mjini kimekuwa kikiomba Mungu usiku na mchana CCM iweze kuliteua jina la Bw.Aden Rage ili awe mgombea Ubunge jimbo la Tabora mjini kwakuwa uteuzi huo utakuwa na neema kubwa kwa Chadema kupata kirahisi ushindi mkubwa wa Jimbo hilo.

Habari zaidi zinasema kuwa kutokana na madai kwamba Rage hakufanya lolote katika kipindi chote alichokuwa madarakani hivyo kwa upande wa Chadema itawarahisishia namna ya kumuelezea wakati wa mchakato wa kampeni za uchaguzi mkuu.

Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Tabora mjini Bw.Simon Lameck akizungumza na Mtandao huu wa KAPIPIJhabari.COM alisema CCM kutokana na kuwakumbatia Wabunge wasiowajibika na kuwatumikia vyema wananchi kitakacho wapata safari hii wasitafute mchawi kwakuwa itakuwa imetokana na mfumo uliopo ndani ya chama hicho wa kushindwa kuwawajibisha Wabunge ambao hawawakilishi wananchi na kero walizonazo katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zaidi ya kupongeza kila kitu hata kama kinawaumiza wapiga kura wao.

Habari za ndani kutoka CCM:-
Mmoja kati ya viongozi wa CCM ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema kumekuwa na taarifa hizo zimeenea katika maeneo mengi lakini hawana sababu ya kufuatilia kwani hakuna mtu anayelazimishwa kuwepo ndani ya CCM kwakuwa chama hicho ni chama makini na hakiwezi kushughulikia mtu mmoja anapotaka kuhama kwani hakuna maslahi ya kijamii kufanya hivyo.
 

   

MUWANIA UBUNGE JIMBO LA KAWE WAKILI ELIAS NAWERA KUMPA USHIRIKIANO ATAKAYEPITISHWA NA CCM, AELEZEA KUHUSISHWA NA RUSHWA

  Mgombea nafasi ya kuwania ubunge Jimbo la Kawe, Wakili Elias Nawera (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi.
 Mgombea nafasi ya kuwania ubunge Jimbo la Kawe, Wakili Elias Nawera (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu kumpa ushirikiano mgombea wa nafasi hiyo aliyeshinda kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika jimbo hilo na kukamatwa kwake na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa madai ya kutoa rushwa.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

MGOMBEA nafasi ya kuwania ubunge Jimbo la Kawe, Wakili Elias Nawera amesema atampa ushirikiano mgombea wa nafasi hiyo aliyeshinda kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuhakikisha CCM inapata ushindi.

Nawera aliyasema hayo jijini Dar es Salaam leo asubuhi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mchakato wa kura za maoni katika jimbo hilo na kuhusishwa na kukamatwa kwake na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa madai ya kutoa rushwa.

"Nampongeza mwenzangu aliyeongoza kura za maoni katika jimbo la Kawe na ninaahidi kushirikiana na mgombea mwenzangu atakaye teuliwa na vikao vya uteuzi vya CCM kupeperusha bendera katika uchaguzi mkuu na kuwa ushindi wa kishindo kwa CCM kuanzia udiwani, ubunge na urais".  alisema Nawera.

Akizungumzia kuhusu mchakato huo na kuhusishwa na rushwa aliilalamikia Takukuru kwa kumuhusisha na tukio hilo kuwa walikuwa na nia ya kumsaidia mmoja wa wagombea nafasi hiyo na yeye kumpunguza nguvu kisiasa.

Nawera alisema licha ya kutoa taarifa za vitendo vya rushwa katika mchakato huo hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa lakini katika mazingira ambayo hakuyategemea amebambikiwa tuhuma hizo ambazo hakuwa nazo.

Aliongeza kuwa wakati wa ukamatwaji wake hawakumjulisha kuwa yupo chini ya ulinzi, pia hawakujitambulisha na wala hawakumuambia anatuhumiwa kwa kosa gani na bila kumpa nafasi ya kuwasiliana na ndugu zake au mwanasheria na kumpeleka kituo cha polisi Magomeni.

Nawera alisema si jambo zuri kwa vyombo vya dola kumkamata mwananchi na kumuhusisha na tuhuma mbalimbali hiyo si sahihi na ni matumizi yasiyofaa ya rasilimali za nchi na matumizi mabaya ya madaraka.

Muwania ubunge huyo Julai 30, 2015 saa mbili usiku alikamatwa na maofisa wa Takukuru kwa kuhusishwa na rushwa na baada ya mahojiano alisweka rumande kwa masaa 10 na kuachiwa kwa kujidhamini mwenyewe. 
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

JARIDA LA EUROMONEY LA UINGEREZA LATOA TUZO YA UFANISI KWA BENKI YA NMB TANZANIA

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kushoto), akiwaonesha waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, Tuzo ya Ufanisi wa kibenki nchini Tanzania iliyotolewa na Shirika la Euromoney la Uingereza  kwa benki hiyo ijulikanayo Euromoney 2015 Award for Excellence. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa benki hiyo, Joseline Kamuhanda.
 Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa benki hiyo, Joseline Kamuhanda (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

BENKI ya NMB imetajwa kuwa Benki bora Tanzania kwa mwaka 2015, na kujinyakulia tuzo ikiwa ni kwa miaka mitatu mfurulizo.

Tuzo hiyo ilitolewa jijini London nchini Uingereza na Jarida la Euromoney linalojihusisha na masuala ya fedha.

Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Ineke Bussemaker alisema Jarida ilo huandaa hafla ya kuyatambua Zaidi ya Makundi 20 ya bidhaa za taasisi za kifedha, ili kutazama benki bora.

Alisema Tuzo hiyo huzitambua pia taasisi za kifedha duniani kote ambazo zimepata mafanikio ya hali ya juu katika shughuli zake, hasa kwa kuonesha ubunifu na kupata mafanikio ya kifedha kila mwaka.

Alifafanua kuwa kazi ya kutafuta washindi, ufanywa na  Jopo la wataalam kutoka mataifa mbalimbali na wenye utaalamu mbalimbali, ambao hupitia taarifa zinazowasilishwa na taasisi zote za kifedha duniani na kutangaza washindi.

"Katika miezi 12, benki ya NMB imeanzisha huduma mbali mbali za kibenki na hivyo kuendelea kuwafikia wateja wa huduma za kibenki kuanzia kuweka akiba, kutoa na kuchukua fedha mijini na vijijini"alisema

Bussemaker alitoa shukrani kwa wateja wa Benki hiyo, wafanyakazi na washika dau wote kwa kuwa sehemu ya mafanikio hayo.

Aliongeza kuwa tuzo hiyo inaongeza kwenye hazina ya tuzo ambazo benki imezipata katika miezi 12 huku akizitaja baadhi kuwa ni benki bora ya mwaka kutoka jarida la Banker, Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) wakiipa NMB tuzo ya mlipakodi anaefuata sharia katika taasisi za kifedha nchini.