Pages

KAPIPI TV

Tuesday, June 30, 2015

KONGAMANO LA JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA WANAWAKE TANZANIA (TANZANIA BUSINESS ENTREPRENEURS) LAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

 Mwenyekiti wa Tanzania Business Entrepreneurs for Women,  Haika Lawere akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa Kongamano hilo lililofanyika Hoteli ya Mbezi Guarden Dar es Salaam.
 
 Wadau wa kongamano hilo wakiwa wamejipanga kisawasawa. Kutoka Kulia ni Getrude Kilyabusebu, Haika Lawere, Hilda Mgaja na  Julieth Mjale.
 Mwezeshaji wa Kongamano hilo, James Mwang'amba 
akitoa mada.
 Muwezeshaji wa kongamano hilo, Chriss Rupia (kulia), akitoa maelezo juu ya namna ya kuanzisha Kampuni na hatua mbalimbali ambazo mtu anatakiwa azifuata wakati wa kufungua kampuni hasa binafsi.
 Mwenyekiti wa Tanzania Business Entrepreneurs for Women Haika Lawere (wa kwanza kulia) pamoja na wadau wengine wakiangalia bidhaa mbalimbali wakati wa kongamano hilo. 
 Mmoja wa majaji akiangalia bidhaa mbalimbali zilizopangwa kwenye meza zilizotokana na ubunifu wa wanawake waliohudhuria kongamano hilo.
Kongamano likiendelea
Baadhi ya wajasiriamali na wadau mbalimbali wakiwa katika Kongamano hilo.
Mmoja wa waratibu wa kongamano hilo Getrude Kilyabusebu (Kulia) akiweka sawa  kumbukumbu ya wadau waliofika katika kongamano hilo.
Bidhaa mbalimbali zikioneshwa.
Maonyesho ya bidhaa mbalimbali yakiendelea.

Baadhi ya wajasiriamali wakionesha kazi zao.
  Wadau mbalimbali wakitizama bidhaa mbalimbali katika Kongamano hilo.

Na Dotto Mwaibale

WAJASIRIAMALI wanawake nchini wametakiwa kuwa na moyo wa uthubutu ili kupiga hatua ya maisha na kiuchumi badala ya kuwa waoga.

Mwito huo umetolewa na Mratibu wa Kongamano la Jumuia ya Wafanyabiashara Wanawake Tanzania, Julieti Mjale wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kongamano hilo lililofanyika Hoteli ya Mbezi Garden Dar es Salaam jana.

"Uthubutu katika jambo lolote ni muhimu kwani unamfanya muhusika kupiga hatua ya maendeleo" alisema Mjale

Alisema wajasiriamali waliowengi wamekuwa na mipango mizuri ya kubuni biashara fulani lakini wanakuwa na hofu ya kupoteza fedha zao na hiyo inatokana na kushindwa kuthubutu au kuchukua maamuzi magumu ya kuanza kufanya biashara waliyoikusudia.

Akijitolea mfano yeye alisema alithubutu kwa kuanza kufanya biashara za chini lakini leo hii ana nyumba za kupangisha na kufikia hatua ya kufanya biashara za kwenda nje ya nchi na kuandaa makongamana ya namna hiyo kwa ajili ya kutoa elimu ya biashara.

Mwenyekiti wa Jumuia hiyo, Haika Lawere alisema lengo la kongamano hilo ni kuwakutanisha wajasiriamali wanawake ili kupeana uzoefu wa biashara na kujua changamoto walizonazo na kuzitafutia ufumbuzi pamoja na kupanua wigo wa shughuli zao na kutafuta masoko mapya ya bidhaa zao.

Katibu wa Jumuia hiyo, Hilda Ngaja, alisema changamoto kubwa waliyonayo wajasiriamali wanawake ni kutokuwa na uelewa mkubwa wa kufanyabiashara zao na kujikuta wakirudi nyuma kimaendeleo na ndio maana wamekuwa wakitumia fursa za semina na makongamano kwa ajili ya kuelimishana.
(Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba-0712-727062)



MWILI WA MKE WA MWANAHABARI THOBIAS MWANAKATWE WA KAMPUNI YA THE GUARDIAN ALIYEFARIKI KWA KUGONGWA NA GARI NJE YA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE WAAGWA JIJINI DAR ES SALAAM KUZIKWA KARATU MKOANI ARUSHA

 Mhariri wa Gazeti la Nipashe, Jesse Kwayu (kushoto), na waombolezaji wengine wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa mke wa mwanahabari wa Kampuni ya The Guardian, Thobias Mwanakatwe, Levina Genda wakati wakilipekeka kwenye gari tayari kwa safari ya kwenda Karatu mkoani Arusha kwa mazishi yatakayofanyika kesho.
 Mwanahabari wa Kampuni ya The Guardin Ltd, Thobias Mwanakatwe akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa mke wake, Levina Genda wakati wa ibada ya kumuaga iliyofanyika Hospatali ya Amana Dar es Salaam leo a. Mke wa Mwanakatwe alifariki kwa kugongwa na gari maeneo ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mwishoni mwa wiki.
 Waombolezaji wakiwa kwenye ibada ya kumuaga Levina Genda, iliyofanyika Hospitali ya Amana Ilala Dar es Salaam leo asubuhi.
 Hapa ni huzuni umetawala.
 Wafanyakazi wenzake na Thobias Mwanakatwe wa Kampuni ya The Guardian wakiwa wamejiinamia kwa huzuni.
 Thobias Mwanakatwe (katikati), akiwa na wafanyakazi wenzake waliofika kumfariji.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Levina na waombolezaji wengine wakiwa kwenye ibada ya kumuaga mpendwa wao.
 Kiongozi wa dini kutoka kanisa la Katoliki akiongoza ibada ya kumuombea marehemu.
 Ibada ikiendelea.
 Mwakilishi wa wanahabari kutoka mkoani Mbeya ambako Mwanakatwe alikuwa akifanyakazi kabla ya kuhamia Dar es Salaam, Patrick Kosima akitoa akizungumza katika ibada hiyo kabla ya kutoa rambirambi ya sh.220,000.
 Mhariri wa Gazeti la Nipashe, Jesse Kwayu (katikati), akizungumza katika ibada hiyo wakati akiwasilisha salamu za rambirambi za Kampuni ya The Guardian.
 Mdau Fabiola Bula wa Karatu, akitoa heshima za mwisho kwa marehemu. 
 Heshima za mwisho kwa marehemu zikiendelea.
 Wafanyakazi wa Kampuni ya The Guardian wakitoa heshima za mwisho kwa wifi yao, Levina Genda. 'Hakika ni huzuni tupu'
Jeneza likiingizwa kwenye gari tayari kwa safari ya kwenda Karatu kwa mazishi.
(Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba -0712-727062)

Monday, June 29, 2015

TAASISI YA KIISLAM YADAIWA KUNYANYASA NA KUWAFANYIA UKATILI WATOTO MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI

Mmoja kati ya Wanafunzi wa Shule ya Arba Light akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu adha wanayofanyiwa na Uongozi wa Kutayba Saccos ikiwa ni pamoja na kufungiwa huduma za choo wakati wakiwa shuleni hapo jambo ambalo limetafsilika kuwa ni manyanyaso na ukatili wa hali ya juu.
Bi.Fatuma Kidori mkazi wa Kanyenye akizungumzia Ukatili huo wa kuzuia Watoto wasipate elimu katika Shule hiyo kwa zaidi ya siku tano baada ya kuwafungia Mageti kitendo kilichofanywa na Uongozi wa Kutayba Saccos taasisi inayomilikiwa na Baraza kuu la Jumuiya ya Taasisi za Kiislam nchini.
Mwalimu Dolla Fungameza mkuu wa Shule hiyo ya Arba Light akizungumza masikitiko yake kufuatia kitendo hicho cha kikatili dhidi ya watoto kilichofanywa na Uongozi wa Kutayba Saccos
Baadhi ya watoto Chekechea wanaosoma katika Shule ya Arba Light iliyopo kata ya Kanyenye Manispaa ya Tabora wakiwa wamekaa nje ya Shule yao baada ya mmoja kati ya viongozi wa Taasisi ya Kutayba Saccos kufunga mageti akizuia watoto hao wasipate haki yao ya msingi ya elimu kufuatia mgogoro uliopo baina ya Uongozi wa Kutayba Saccos na Wamiliki wa majengo ya shule hiyo.
Geti likiwa limefungwa na Uongozi wa Kutayba Saccos wakizuia Watoto na walimu wao wasiingie madarasani jambo ambalo ni kinyume na haki za binadamu.Hata hivyo mtandao huu ulitaka kuhoji hatua ya Uongozi wa Kutayba Saccos kuzuia watoto hao lakini viongozi hawakuwa tayari na hivyo waliamua kujifungia milango ofisini kwao.





MAABARA YA MAFUNZO ITEMBEAYO YAZINDULIWA RASMI

DSC_0080
Mganga Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa jamiii, Dk. Magreth Mhando akisoma hotuba ya uzinduzi wa maabara itembeayo kwa ajili ya mafunzo ya upasuaji. Kulia ni Naibu Balozi wa Ireland nchini, Maire Matthews na kushoto ni Mkurugenzi wa ECSA anayeshughulikia Afya ya jamii Prof Yoswa Dambisya.

Na Mwandishi wetu
Mganga Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Magreth Mhando mwishoni mwa juma alizindua maabara ya upasuaji ya mafunzo inayotembea iliyotolewa kwa chuo kitembeacho cha COSECSA na serikali ya Ireland.
Alifanyakazi hivyo kwa niaba ya Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii, Dk Seif Rashid.
Maabara hiyo ambayo ni mradi wa majaribio wa chuo hicho wenye lengo la kufundisha wapasuaji pale walipo imegharimu dola za Marekani 100,000.
Kwa mujibu wa taarifa za COSECSA maabara hiyo itakuwa nchini kwa miezi kama mitatu kabla ya kwenda Kenya na baadae Malawi.
Mradi huo wenye lengo la kufundisha wapasuaji zaidi kwa kufika eneo ambalo wanafanyia kazi, ni moja ya miradi ya chuo kitembeacho ambacho toka kimeanzishwa mwaka 1990 kimeshatoa wapasuaji 200.
Hafla ya uzinduzi wa maabara hiyo yenye vifaa vya kisasa vya kufundishia na kufanyia upasuaji ikiwamo ya upasuaji kwa kutumia darubini ulifanyika katika hospitali ya kumbukumbu ya Hubert Kairuki.
DSC_0053
Rais wa COSECSA , Profesa Stephen Ogendo akisoma taarifa kwa mgeni rasmi kabla ya uzinduzi.
Akizindua maabara hiyo Dk. Mhando alisema kwamba ni matumaini yake italeta mabadiliko makubwa katika kuwezesha taifa kuwa na wataalamu wengi wa upasuaji.
Aidha alisema changamoto ya kutosajiliwa kama chuo kamili wakati mataifa mengine yamefanya atayafuatilia ili kuweza kuona ya kukiwezesha chuo hicho kutambuliwa rasmi nchini Tanzania.
Maabara hiyo mali ya College of Surgeons of East Central and Southern Africa (COSECSA) iliwasili mapema mwezi huu na jana ndio ilikuwa uzinduzi rasmi ambao ulishuhudiwa na wanafunzi wa upasuaji, wataalamu na maofisa mbalimbali wa afya wakiwemo watu wa Mfuko wa taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Kaimu mkurugenzi wa Mfuko huo Michael Mhando alisema kwamba wamefurahishwa na juhudi za wadau wao katika kuimarisha vifaa tiba na utoaji wa wataalamu.
Alisema anaamini kwamba maabara hiyo ni moja ya mambo muhimu yanayotakiwa kufanywa na wadau ili kuimarisha tiba nchini.
Alisema kwamba wataangalia namna ya kufanya ili kusaidia huduma hiyo kwani inahitajika sana vijijini ambako wengi wa watu hawapati fursa ya kufanyiwa upasuaji hata ule mdogo.
DSC_0130
Baadhi ya wadau wa sekta ya afya na wanafunzi waliohudhuria hafla hiyo.
Maabara hiyo yenye uzito wa tani 30 inatarajia kufanya mafunzo ya upasuaji katika hospitali zenye uhusiano na COSECSA.
Aidha maabara hiyo inaweza kufunza wapasuaji 10 kwa mkupuo mmoja.
Kuletwa kwa maabara hiyo kutoka Ireland ambako kuna uzoefu wa miaka mingi wa kutumia maabara zitembeazo za upasuaji kumefanikishwa na mahusiano yaliyopo kati ya Royal College of Surgeons in Ireland (RCSI), Shirika la misaada la Ireland (Irish Aid) na College of Surgeons of East, Central and Southern Africa (COSECSA).
Maabara ya mafunzo ya upasuaji itembeayo ilianzishwa na RCSI kwa mara ya kwanza duniani mwaka 2006 na kwa uzinduzi uliofanyika dare s Salaam jana umedhihirisha dhamira njema ya COSECSA na RCSI ya kutoa mafunzo bora kwa lengo la kuimarisha afya za wanadamu.
Akizungumza kwenye tukio hilo Rais wa COSECSA , Profesa Stephen Ogendo alisema kwamba kuwepo kwa maabara hiyo kutasababisha mabadiliko makubwa katika utoaji mafunzo katika ukanda wa Afrika Mashariki, kati na Kusini ( ECSA).
Alisema kwamba kutokana na uasili wa maabara hiyo wanafunzi hawatakuwa wanalazimika kufuata kituo cha mafunzo na badala yake kituo hicho kitawafuata pale walipo.
Aidha alisema kwamba muundo na mfumo wa ufundishaji umeshatengenezwa kwa ajili ya kusaidia mafunzo hayo kwa nchi wanachama.
DSC_0023
Naye Mkurugenzi wa ECSA anayeshughulikia Afya ya jamii Prof Yoswa Dambisya alisema kwamba wataendelea kuwa mstari wa mbele kufundisha wataalamu wa afya kwa kutumia mbinu mbalimbali za kisasa na zenye kutoa tija kama kuwepo kwa mabara hiyo.
Alisema kutokana na haja kubwa ya wataalamu wa upasuaji kuwepo kwa maabara hiyo itembeayo kutasaidia kufunza wanafunzi wengi katika eneo ambalo uwiano wa wataalamu na wagonjwa ni mtaalamu mmoja kwa wagonjwa 190,000 ukilinganisha na Uingereza ambako uwiano ni mtaalamu mmoja kwa wagonjwa 2,800.
Alisema raslimali kama ya maabara itasaidia kufunza watu wengi zaidi ili kuendelea kupunguza pengo la wataalamu wa upasuaji.
Alisema pia kwamba takwimu za dunia zinaonesha kuwa asilimia 6.5 ya magonjwa yanatokana na kukosekana kwa huduma za upasuaji.
Alisema vifo vingi vinatokana na kukosekana kwa huduma za upasuaji kuliko Malaria, Ukimwi na kifua kikuu kwa pamoja.
COSECSA ambayo ilianzishwa mwaka 1999 kwa malengo ya kutoa elimu ya upasuaji ilianzishwa na shirikisho la wapasuaji Afrika Mashariki ambalo lina miaka takaribani 60.
DSC_0087
Mganga Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa jamiii, Dk. Magreth Mhando akikata utepe kuzindua maabara ya upasuaji ya mafunzo inayotembea iliyotolewa kwa chuo kitembeacho cha COSECSA na serikali ya Ireland.
DSC_0097
Mmoja wa walimu ambaye ni daktari bingwa wa upasuaji akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Mganga Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa jamiii, Dk. Magreth Mhando aliyemwakilisha Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii na Naibu Balozi wa Ireland nchini, Maire Matthews.
DSC_0146
Wageni mbalimbali wakiangalia namna maabara hiyo inavyofanyakazi.
IMG_2862
Mganga Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa jamiii, Dk. Magreth Mhando (kulia) akishuhudia zoezi la upasuaji kwa vitendo ndani ya maabara hiyo.
DSC_0151
Rais wa COSECSA , Profesa Stephen Ogendo akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kukagua maabara hiyo katika uzinduzi huo.
DSC_0090
Picha ya pamoja baada ya uzinduzi.
DSC_0047
Maabara ya upasuaji ya mafunzo inayotembea iliyotolewa kwa chuo kitembeacho cha COSECSA na serikali ya Ireland.

NAWERA AITAKA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII KUPUNGUZA BEI KUBWA ZA DAWA NCHINI

Elias Nawera
Na Dotto Mwaibale

MWENYEKITI wa Chama cha Walaji na Tiba Tanzania , Elias Nawera, ameitaka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kutatua changamoto ya bei kubwa ya dawa za binadamu wanayotozwa Watanzania.

Nawera alisema sera ya afya inasema kila mtu ana haki ya kupata huduma za afya kwa bei nafuu, lakini bado Watanzania wengi wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kununua dawa kwa bei kubwa.
“Tunaomba Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii aingilie kati suala hili,
wanaoteseka kwa kiwango kikubwa ni watu wa kipato cha chini.

Nimesema hivi baada ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Baraza la Famasia kushindwa kulitafutia ufumbuzi suala hili.

Alitoa kauli hiyo Dar es Salaam juzi, wakati akizungumza na wanahabari, ambapo alifafanua kuwa, amefikia hatua hiyo baada ya kubaini mzigo mkubwa wa gharama za matibabu wanaobebeshwa Watanzania.

Aidha, Mwera alisema kupanda kwa gharama za dawa hakuna uhusiano wowote na kupanda kwa gharama za maisha na kwamba, wizara husika ikifuatilia inaweza kulipatia ufumbuzi suala hilo.(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

"LEO NILIALIKWA NA STAR TV NIKIWA NA PROF.LIPUMBA NA NDUGU RENATUS MKINGA KATIKA KIPINDI TUONGEE ASUBUHI"-DR.KIGWANGALLA



Leo nilialikwa Star TV kwenye kipindi cha Tuongee Asubuhi, pamoja na Prof. Ibrahim Haruna Lipumba na Ndg. Renatus Mkinga. Mjadala ulikuwa mzuri sana. Mzee Mkinga aka-dismiss wagombea wote vijana na wagombea wote wanawake...

Nilishtuka kidogo!
Mzee Mkinga alianza kwa kutufagilia Ndg. January Y. Makamba, mimi na vijana wengine lakini akasema muda bado. Wanawake aliwashukia moja kwa moja tu kuwa hawatoshi na Tanzania haiko tayari kwa Rais mwanamke, na kwamba CCM huwa kuna hila kama zile alizofanyiwa Mzee Sitta ili kufumba fumba Richmond.

Binafsi, niliona kama anatubagua kwa umri na jinsia zetu. Nikadhani si sahihi kufanya ubaguzi wa wazi namna hiyo. Kama unakubali kuwa sisi ni waadilifu na hauna shaka na uadilifu wetu, kinachofuata ni kutazama utayari wetu, uelewa wetu wa changamoto zinazolikabili taifa letu, maarifa yetu ya kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo, na uzalendo wetu. 

Ukiona tunafaa basi unatuchagua. Kwani na sisi tukiamka tukasema wazee wote hawafai sababu uzoefu wao umepitwa na wakati, ni wa kizamani, na kwamba vijana wa sasa wasiwachague tutakuwa tumekosea?

Mzee Mkinga akaelezea kuhusu umuhimu wa uzoefu na kuponda sana kuwa wagombea wa aina yetu hatuna uzoefu wa kutosha, akilinganisha na uzoefu aliokuwa nao Rais Barack Obama wa Marekani kuwa alifanya kazi ya community organizing na useneta kwa muhula mmoja, na uzoefu mkubwa sana kumfanya kuwa Rais, mambo ambayo sisi hatuna. Ofcourse ni mtazamo wake, na ana haki nao, lakini nadhani ni wa juu juu sana.

Nitajizungumzia mimi binafsi na uzoefu - kwamba, wakati nasoma masomo yangu ya udaktari, nilifundishwa mambo mengi sana ya kwenye jamii - sociology, psychology, environmental health, psychiatry, community health, epidemiology, health policy and planning, menejimenti, uongozi, teamwork n.k. - hapa nilipata maarifa ya kutosha ya menejimenti na uongozi. 

Baada ya shule nilifanya kazi kama mtafiti nikapata kuzunguka mikoa yote ya Tanzania, mijini na vijijini, nikifanya kazi na watu - nataka niulize, hivi katika hao wenye 'uzoefu' anaouzungumzia Ndg. Mkinga na wenzake wenye mawazo ya namna hiyo, wanao huu uzoefu kama wangu?

Baadaye nikasoma masomo ya uzamili kwenye afya ya jamii (MPH) na kwenye usimamizi wa biashara (MBA) - hapa nikijikita zaidi kwenye mambo ya utafiti, takwimu, usalama wa afya za watu, uongozi, oganaizesheni na menejimenti ya taasisi kwa upana wake - baada ya masomo haya nikaamua kujiajiri mwenyewe kwa kuanzisha kampuni ambayo tuliikuza na kufikia kuzalisha ajira zaidi ya 500 kwa mwaka (za moja kwa moja - direct), na zaidi ya 10,000 indirectly. 

Nikiwa kiongozi mkuu mwendeshaji wa makampuni haya, na wenzangu, tuliweza, kwa mfano kufufua kilimo cha zao la pamba Nzega na kukuza uzalishaji kutoka kilo 20,000 mwaka wa kwanza wa mradi na kufikia leo hii (mwaka wa saba) takriban kilo milioni 9 za pamba. Mradi huu unagusa karibu watu laki 4. 

 Ni nani katika hao wenye 'uzoefu' anaowasema Mzee Mkinga, ana uzoefu wa namna hii?
Nimetoa mifano hiyo ili kuweka wazi hoja kwamba, kila mgombea katika sisi ana uzoefu wa aina yake, na uzoefu wa mtu mmoja, haufanani na uzoefu wa mwingine, na kwamba unapokuwa Rais haufanyi kazi peke yako na kwamba basi wewe unatakiwa uwe unajua kila kitu, na una uzoefu kwenye kila kitu...la hasha!

Kwenye uongozi huwa kuna kufanya kazi kwa timu, wewe ukitumia ujuzi na mamlaka yako kuwashawishi unaowaongoza wakubaliane na vision yako na Chama chako ili mwende pamoja kutekeleza mission yenu nyote hautokwama - nchi itaenda. tena kwa mimi 'upya' ni asset inayopaswa kukumbatiwa, maana tunataka mambo mapya. 

Cha msingi tupimwe kama tuna uelewa wa namna ya kuongoza, changamoto za Taifa za leo na za kesho, na suluhu tunazopendekeza kwamba je zinaweza kufanya kazi, na kwamba je tuna weza kuwaunganisha watanzania pamoja tukakimbia kutekeleza vision yetu kama taifa?

Kuna wagombea hapa wamekaa serikalini zaidi ya miaka 30 lakini hawana cha kuonesha cha kutisha sana, zaidi wamekaa miaka yote hiyo wakifanya kazi kwa mazoea tu. Mtu hapimwi uwezo wake kwa kukaa kwenye uongozi miaka mingi sana bali kwa nini amefanya katika kipindi alichokaa humo.

Hata ukae miaka mingapi kwenye serikali ama kwenye chama, bado tu kuna vitu vingi sana hautovijua, lakini haimaanishi utashindwa kufanya maamuzi, maana ukiwa Rais unakuwa kiongozi tu wa taasisi yenye watu wengi, lakini utafanya kazi na wataalamu waliobobea kwenye maeneo yao - wewe unatakiwa uwe msikivu na mwenye utayari wa kupokea ushauri, kuuchambua na kuufanyia uamuzi sahihi.

Nasisitiza tena, kwamba, kazi tunayoomba ni mpya, na sote hatujawahi kuifanya, wenye uzoefu ni wanne, aliyetangulia mbele ya haki, wastaafu wawili (Mzee Mwinyi na Mzee Mkapa) na aliyepo madarakani, na wote hawa hawagombei tena mwaka 2015. Na kwamba sisi sote tuna uzoefu kwenye mambo mbalimbali mengine tu, na uzoefu wa mmoja ni tofauti na wa mwingine. 

Tupimwe kwa kushindanisha hoja za nani anakuja na ubunifu wa namna mpya ya kutatua changamoto zetu.

Kuna wagombea wengine wenye 'uzoefu' kweli na wanatumia gharama kubwa sana kuwakusanya watu wawasikilize lakini hawana wanachowaambia!

WADAU WA MODEWJI BLOG WAJUMUIKA KUSHEREHEKEA MIAKA 7 YA MTANDAO HUO NDANI YA VIWANJA VYA SABASABA

IMG_5219
Mdau wa modewjiblog, Ray the hustler (kushoto) aliyeambatana ndugu zake kutembelea banda la Modewjiblog katika picha ya pamoja na Mwandishi wa habari mwandamizi wa mtandao wa Modewjiblog, Andrew Chale.

Na Modewjiblog team
Shamra shamra za miaka Saba za mtandao wa habari nchini wa Modewji blog tayari zimeanza kurindima ndani ya banda la MeTL Group lililopo kwenye maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yaliyoanza jana kwenye mabanda ya SabaSaba katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Wadau mbalimbali wanaoperuzi mtandao wa modewji blog wamekuwa wakimiminika kujionea utendaji wa kazi zinazofanywa na mtandao huu pamoja na kupata picha za pamoja ikiwemo ‘selfie’ ambazo zinakuwa zinarushwa moja kwa moja katika blog na mitandao mingine ya kijamii ikiwemo facebook, twitter na Instagram.
Pia wadu na watu mbalimbali wanakaribishwa kutoa maoni yao namna ya kuboresha zaidi huduma zetu.
Hata hivyo, kwa mujibu wa Meneja mwendeshaji Mkuu wa modewji blog, Zainul Mzige aliweza kutoa punguzo maalum la hofa kwa watu mbalimbali kujitokeza kutangaza na mo dewji blog katika msimu huu wa maonyesho ya Saba saba.
Punguzo hilo ni maalum na litadumu kwa muda wote wa kipindi cha Saba Saba pekee.
Kwa matangazo na maelezo zaidi wasiliana nasi kwa barua pepe : info@modewjiblog.com au zainul@modewjiblog.com
DSC_0582
Afisa Masoko wa taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu iliyochini ya Wizara ya Fedha, (UTT-PID), Kilave Atenaka (katikati) pamoja na Afisa kutoka taasisi hiyo Beatrice Ngode waki-show love na T-shirts za modewjiblog walizokabidhiwa walipotembelea banda la modewjiblog na kujionea shughuli mbalimbali za utendaji kazi wa mtandao huo katika shamra shamra za kusheherekea miaka 7 mtandao huo tangu ulipoanzishwa. Kulia ni Mwandishi wa mwandamizi wa modewjiblog, Andrew Chale.
IMG_5195
Mdau wa Modewjiblog, Bw. Geofrey Tupper (kushoto) akipokea fulana kutoka kwa Mwandishi mwandamizi wa mtandao wa modewjiblog, Andrew Chale mara baada ya kutembelea banda lao katika maonyesho ya saba saba yaliyoanza kutimua vumbi jana jijini Dar es Salaam.
IMG_5204
Mbunifu wa mavazi nchini Ally Rehmtulah (wa pili kushoto) akipata picha ya kumbukumbu na team ya modewjiblog pamoja na mdau wa kampuni ya vifaa vya ki-elektoniki ya LG katika aliptembelea letu katika banda la maonyesho ya saba saba yalioanza kutimu vumbi jana jijini Dar es Salaam.
DSC_0579
Maafisa wa tasisi ya UTT-PID waki-show love na kofia pamoja na T-shirts za modewjiblog mara baada ta kutembelea banda hilo kwenye maonyesho ya saba saba.