Pages

KAPIPI TV

Thursday, April 30, 2015

WANAZUONI WAJADILI MUSTAKABALI WA TANZANIA DEMOKRASIA YA VYAMA VINGI

 Jaji Francis Mtungi akifunguja mkutano wa wadau wa siasa  wa uimatishaji demokrasia ya vyama vingi
Mkurugenzi UNDP Philippe Poinsot  akizungumza katika mdahalo
Dk bana akizungumza katika mdahalo
jaji Mutungi akiwa na Mkurugenzi UNDP Poinsot
IMG_4917
IMsimamizi wa mdahalo Prof Bernadetta Killian
Profesa Ruth Meena akizungumzia ushiriki wa kijinsia katika demokrasia ya vyama vingi
Profesa Rugumamu akizungumza
IMG_4861
IMG_4879
wanamdahalo wakiwa makini

Wednesday, April 29, 2015

POLISI YAUWA MAJAMBAZI MATATU KIGOMA WAKUTWA NA RISASI 22,BOMU 2

Na Magreth Magosso,Kigoma


WATU  WATANO  Mkoa wa Kigoma ,wamekufa katika matukio  mawili tofauti  likwemo Jeshi la Polisi mkoani humo kuua Majambazi watatu  na kukamata Mabomu Mawili ya kutupa kwa mkono katikaki ya mpaka wa wilaya ya Kibondo na   Kakonko .


Akifafanua Matukio hayo Kamanda wa Polisi mkoani humo Fernand Mtui alisema kuwa, Aprili,29,2015 saa 8.10 usiku katika mto wa Kahambwe uliopo katikati ya mpaka wa wilaya ya kibondo na Kakonko Askari polisi wakiwa katika operesheni endelevu ya kuimarisha usalama wa mkoa walishtukia kundi la watu wasio na idadi kamili .


Kamanda Mtui alisema walipolikaribia kundi hilo walishtukia wakirushiwa risasi na watu hao,ambapo askari polisi wakajibu mapigo ya ana kwa ana hatimaye majambazi matatu wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 hadi 30 kupoteza maisha katika sakata hilo.


Alibainisha kuwa,baada ya kuona wenzao wamekufa majambazi walikimbia na kutupa mfuko uliokuwa na mabomu mawili aina ya defensive na Ofensive yenye namba Y3PM/2 na silaha aina ya 47 ikiwa na magazine yenye risasi 10 na risasi 22 zilifungwa katika kitambaa maalum.


Aidha alisema silaha hiyo inabeba risasi 22 ,hivyo walitumia risasi 19 katika zoezi hilo na mpaka sasa maiti za majambazi hayo zipo katika hospitali ya wilaya ya kibondo na bado hawajatambuliwa majina na  makazi yao .


Katika tukio la pili watoto wawili  Rashid Juma(3) na Mwajuma Juma(1) wamepoteza maisha baada ya kuungua kwa nyumba waliyokuwa wamelala wakati wazazi wakiwa wamekwenda shambani.


Kamanda Mtui alisema tukio hilo lilitokea  saa 1.00 asubuhi katika kijiji cha Chnkabwimba tarafa ya Mahembe  Wilaya ya Kigoma ,baada ya mtoto mkubwa wa familia hiyo anayesoma darasa la kwanza kusahau kuzima kibatari  na moto kunguza neti na hatimaye nyumba yote kuteketea na kusabisha vifo hivyo.


Hivyo amewasihi  walezi na wazazi wawe makini na watoto hasa katika msimu wa kilimo.ambapo wazazi huwaacha watoto ndani na kukimbilia shambani bila tahadhari kitendo kinachochangia vifo visivyotarajiwa.

MKUU WA WILAYA YA KISARAWE MH. SUBIRA MGALU AZINDUA RASMI SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2015 KIJIJI CHA KISANGA

 Mwenyekiti wa Kijiji cha Kisanga kata ya Masaki Wilayani Kisarawe Bwana Mohamed Shomoi Mlembe akimkaribisha Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh. Subira Mgalu kuzundua Rasmi Shindano la mama shujaa wa chakula 2015 msimu mpya , pamoja na wageni wote waliofika katika sherehe Hizo.
Mgeni Rasmi katika Sherehe za Uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh. Subira Mgalu akizundua Rasmi Shindano hilo, na kuwasihi wakinamama wa Kisarawe wachukue fomu za kushiriki kwa wingi, pia aliwashukuru Shirika la Oxfam kwa kukichagua kijiji cha Kisanga kuwa wenyeji wa Mashindano hayo.
 Eluka Kibona, Meneja Utetezi na Ushawishi wa Oxfam akielezea Historia na Madhumuni ya shindano la Mama shujaa wa Chakula
 Kikundi cha sanaa cha Dhahabu wakitoa Burudani ya Shairi wakati Sherehe hizo zikiendelea ambapo maudhui makubwa yalikuwa ni Ushiriki wa mwanamke katika kumiliki Ardhi na Haki zake
Diwani wa wa kata ya Masaki Mh. Pily Kondo Changuhi akishukuru shindano la Mama Shujaa wa Chakula kufanyika katika kijiji cha kisanga na kuwahakikishia washiriki wote kuwa kijiji kipo salama na watashirikiana pamoja kwa mambo yote wakati wa shindano hilo.
 Baadhi ya wakazi wa Kisarawe na wageni waalikwa wakiwa katika Sherehe hizo za uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula
Mwakilishi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Dkt. Eugania Kapanabo Akiongea na wageni walikwa katika uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula ambapo aliwashukuru Oxfam kwa Kuanzisha mashindano hayo pia kuona umuhimu wa akina mama kuhusishwa katika kilimo, Umiliki wa Ardhi na Haki zao za msingi na kusisitiza hii ni Njia moja wapo ya kumkwamua Mama kiuchumi.
 Mwenyekiti wa Mtandao wa Kijinsia Ngazi ya Kati Kisarawe Bi. Veronica Sijaona akiwasihi wakina Mama wa Kisarawe kushiriki kwa wingi na kuchukua fomu ili waweze kuungana na akina mama wengune pindi Shindano la Mama Shujaa wa Chakula litakapo anza
 Mmoja wa wanakijiji cha Kisanga akijaza fomu ya ushiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula Msimu wa 2015
Baadhi ya wanakijiji cha Kisanga wakiwa katika Sherehe hizo za Uzinduzi wa Mama Shujaa wa Chakula
 Mh Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Subira Mgalu akiungana na wageni waalikwa pamoja na wanakijiji kusherekea uzinduzi Rasmi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 litakalofanyikia katika kijiji cha Kisanga Kata ya Masaki Wilayani Kisarawe.


Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh. Subira Mgalu amezindua Rasmi Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 linaloendeshwa na Shirika la Oxfam kupitia kampeni ya Grow lenye lengo la Kumuwezesha Mwanamke katika kilimo na kumkwamua kiuchumi.

Akizungumza katika Sherehe hizo Mh. Subira Mgalu amesema kuwa amefurahishwa na Mashindano hayo kufanyikia wilayani kwake katika kijiji cha Kisanga na kuwasihi wakina mama wengi kuchukua fomu za ushiriki, na kusisitiza kuwa wakina mama wa Kisarawe sio wavivu na kuwataka washiriki ipasavyo ili zawadi na mshindi wa kwanza atokee katika wilaya hiyo. Aliongeza kuwa Shindano hilo linampa mwanamke uwezo wa kutambua haki zake hasa za umiliki wa Ardhi na kuongeza kuwa ni shindano ambalo mshiriki anahitaji kuwa mbunifu,mwenyeuzoefu ili waweze kubadilishana mawazo na kuwa na mbinu za kisasa za kilimo bora.

Nae Mwakilishi kutoka Oxfam Eluka Kibona alitambulisha rasmi kuwa kijiji cha Kisanga ndicho kitakuwa wenyeji wa shindano hilo na kuwa shindano hilo linatarajia kuanza rasmi mwanzoni mwa mwezi wa Nane na kurushwa moja kwa moja na Kituo cha Televisheni cha ITV na zawadi ya Mshindi wa kwanza kuwa Shilingi Milioni Ishirini za Kitanzania ambapo Mshindi atapata kwa njia ya kununuliwa vifaa na zana za Kilimo.

Eluka  alizungumzia historia fupi ya shindano hilo ambalo sasa ni mwaka wa nne kuendeshwa na kusisitiza kuwa lengo kuu ni kumfanya mwanamke atambulike katika jamii kuwa nao wakiwezeshwa katika kilimo wanaweza pia wanaweza kumiliki hata ardhi na kuongeza kuwa shindano hilo linawapa wakina mama njia za kisasa za kuendesha Kilimo.

Pia Diwani wa Kata ya Masaki Mh. Pily Chamnguhi aliwasihi akina baba wa Kisarawe kuwaruhusu wake zao na watoto wao wa kike kuchukua fomu kwa wingi na kushiriki katika shindano hilo kwa kuwa hiyo ni moja ya Fursa ambazo watazipata kupitia Shindano la  Mama Shujaa wa Chakula.

WAMILIKI WA REDIO ZA KIJAMII WATAKIWA KUBORESHA REDIO ZAO ILI JAMII ITAMBUE MCHANGO WAKE

DSC_0088
Mwezeshaji wa warsha ya Viongozi wa vituo vya redio jamii ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wakati (ASMET), Bw. Ramadhan Ahungu akiendesha mafunzo ya masoko na mpango biashara kwa viongozi wa redio jamii nchini wakati kuhitimisho la warsha ya awamu ya kwanza ya mradi wa Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) wa kuzipa uwezo Redio hizo katika matumizi ya Tehama na Mawasiliano iliyoratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO ambayo imefanyika katika kituo cha Redio jamii Sengerema Telecentre mkoani Mwanza.
Na Mwandishi wetu, Mwanza
WAMILIKI wa redio za jamii wametakiwa kujenga taswira njema za redio zao ikiwa wanataka redio zao zitamanike na kutumiwa na wadua mbalimbali wa maendeleo nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Mwezeshaji wa warsha ya Viongozi wa vituo vya redio jamii Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wakati (ASMET), Ramadhan Ahungu.
Akizungumzia malengo ya warsha hiyo na madhumuni yake alisema kwamba kuwapo kwa mpango wa biashara ndani ya redio hizo hakutakuwa na maana kama wasipozingatia ujenzi wa taswira utakaowafanya wadau kuvutiwa na redio hizo.
Alisema kuna umuhimu wa suala hilo kwani kusipojengeka kwa mahusiano bora kati yake na jamii, watu binafsi na taasisi za kiraia zenye malengo tofauti katika kuhudumia wananchi, redio hizo hazitakuwa na biashara ya kufanya.
Ahungu pamoja na kusifia mtindo uliotumika kuwezesha redio hizo kuandaa mipango kazi ya biashara yenye lengo la kusimamia masoko na fedha alisema warsha imefanikiwa kuwaweka karibu zaidi na wadau wamiliki wa vyombo hivyo.
Warsha hiyo ni hitimisho ya awamu ya kwanza kwa ufadhili wa mradi wa Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) wa kuzipa uwezo redio za jamii katika matumizi ya Tehama na mawasiliano inayoratibiwa na Shirika la Kimataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO iliyofanyika katika kituo redio cha Sengerema Telecentre mkoani Mwanza.
Alisema katika warsha hiyo wamiliki hao walijifunza uandaaji wa mipango ya biashara, kutunza fedha, utafutaji masoko, uhakiki wa mipango ya biashara na vipindi vya redio kwa lengo la kuona namna ya kuvifanya kuleta biashara.
Naye Meneja wa kituo cha Redio Jamii Kahama FM ya Shinyanga, Marco Mipawa akizungumzia mafunzo hayo alisema yamemsaidia sana katika kuhakikisha kwamba kituo chake kinakuwa bora na kinachovutia watangazaji.
Alisema mafunzo hayo yamewafanya wajitambue kwani yamefanyika mfululizo kwa mara 5 na kuwafanya wabadilike.
Aidha Meneja wa kituo cha Redio Jamii FADECO ya wilayani Karagwe, Adelina Lweramula alisema kwamba anashukuru mafunzo kwa kuwa yamewafanya kuondoa mawazo vichwani na kuweka mipango kazi katika karatasi na kuwezesha wafanyakazi nao kufuatilia.
DSC_0219
Meneja wa kituo cha Redio Jamii FADECO ya wilayani Karagwe, Adelina Lweramula akichangia hoja wakati wa mafunzo hayo yaliyomalizika jana kwenye kituo cha Redio Jamii Sengerema-Telecentre mkoani Mwanza.
DSC_0229  
Meneja wa kituo cha Redio Jamii Kahama FM ya Shinyanga, Marco Mipawa akiuliza swali kwa mkufunzi wa warsha ya mafunzo ya masoko na mpango biashara (hayupo pichani) wakati wa kuhitimisha warsha ya awamu ya kwanza inayofadhiliwa na mradi wa SIDA kwa kushirikiana na UNESCO iliyomalizika jana katika kituo cha Redio Jamii cha Sengerema-Telecentre mkoani Mwanza.
  DSC_0067
Pichani juu na chini ni Viongozi wa Redio Jamii nchini walioshiriki mafunzo ya masoko na mpango biashara yanayofadhiliwa na mradi wa Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) wa kuzipa uwezo Redio hizo katika matumizi ya Tehama na Mawasiliano na kuratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO ikiwa ni hitimisho la warsha ya awamu ya kwanza ya mradi huo yaliyofanyika katika kituo cha Redio Jamii Sengerema-Telecentre mkoani Mwanza.
DSC_0064 DSC_0082
Mwezeshaji wa warsha ya Viongozi wa vituo vya redio jamii Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wakati (ASMET), Ramadhan Ahungu akiendelea kuwapiga msasa viongozi hao namna ya kutafuta masoko na kuboresha mpango biashara.
DSC_0236
Mwezeshaji wa warsha ya Viongozi wa vituo vya redio jamii Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wakati (ASMET), Ramadhan Ahungu (kulia) akibadilishana mawazo na Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph (wa pili kulia) wakati wakijiandaa kwa zoezi la picha ya pamoja. Kushoto ni Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu akizungumza jambo na baadhi ya viongozi wa vituo vya Redio Jamii nchini.
DSC_0246
Picha ya pamoja ya Wakufunzi na washiriki wa warsha ya mafunzo ya masoko na mpango biashara iliyomalizika jana katika kituo cha Redio Jamii Sengerema-Telecentre mkoani Mwanza.

SKYLIGHT BAND KUANZA WEEK END ALHAMIS HII NDANI YA MZALENDO PUB

IMG-20150428-WA0053

BALOZI WA UMOJA WA AFRIKA AMINA SALUM ALI ATOA RAMBI RAMBI KWA KIFO CHA BRIGEDIA JENERAL HASHIMU MBITA

Balozi Amina Salum Ali

Na mwandishi wetu, Washington, DC
Balozi wa kudumu wa Umoja wa Afrika, Mhe. Amina Salum Ali leo ametoa salamu za rambi rambi kwa Brigedia Jenerali mstaafu Hashim Mbita aliyefariki  siku ya Jumapili April 26, 2015 asubuhi na kuzikwa siku ya Jumanne April 28, 2015 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Balozi Amina Salum Ali alisema amepokea kwa majonzi na simanzi kubwa taarifa za kifo cha mmoja wa watumishi wa miaka mingi wa Serikali, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (TPDF), aliendelea kwa kusema Brigedia Jenerali msataafu Hashim Mbita atakumbukwa Tanzania, bara nzima la Afrika na dunia kwa jumla kama mmoja wa makamanda mahiri aliyeshiriki kikamilifu katika uondoshaji wa utawala wa ukoloni barani Afrika, hususan utawala wa kidhalimu wa makaburu Zimbabwe na Afrika ya Kusini na hatimaye kuachiwa huru kwa aliyekuwa Rais mzawa wa kwanza nchini Afrika Kusini, hayati Nelson Mandela.

Mzee Mbita alijitoa mhanga kuongoza mapambano ya ukombozi wa Afrika, Atakumbukwa milele kwa kurudisha heshima ya Muafrika.

Brigedia Jenerali msataafu Hashim Mbita ni mfano uliotukuka kwa watanzania na Afrika.Aliiongoza vizuri sana kamati ya ukombozi ya Umoja wa Afrika Mungu amlaze pema peponi, Amin.

Balozi Amina Salum Ali yupo safarini kuelekea Tanzania.

NHIF YAENDELEA NA KAMPENI YA KUHAMASISHA WANANCHI KUJIUNGA NA CHF KATIKA KIJIJI CHA CHUMO KILWA

1Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) Bw, Rehani Athumani akikabidhi mashuka kumi kwa Khatib Said mwenyekiti wa kijiji cha Chumo Wilayani Kilwa mkoani Lindi yaliyotolewa na mfuko huo kwa ajili ya zahanati ya kijiji hicho wakati wa mwendelezo wa kampeni ya uhamasishaji wananchi kujiunga na huduma ya Afya ya Jamii CHF inayotolewa na NHIF, Ambapo wananchi mbalimbali walipima afya kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza na kujiunga na huduma hiyo kwenye uwanja wa shule ya msingi ya Chumo, Katikati ni Meneja wa NHIF mkoa wa Lindi B. Fortunata Raymond.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-CHUMO-KILWA) 2Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) Bw, Rehani Athumani akipongezwa na Khatib Said Mwenyekiti wa kijiji cha Chumo Wilayani Kilwa mkoani Lindi baada ya kukabidhi mashuka kumi yaliyotolewa na mfuko huo kwa ajili ya zahanati ya kijiji hicho wakati wa mwendelezo wa kampeni ya uhamasishaji wananchi kujiunga na huduma ya Afya ya Jamii CHF 3Hatbal Badru mtaalam maabara akiendelea kuwapima afya wananchi mbalimbali wakati wa utoajiwa huduma hiyo. 5Kikundi cha waigizaji kikitoa maigizo kama mafunzo kwa wananchi juu ya umuhimu wa huduma za CHF. 6Wananchi wakiendelea kupata huduma hiyo 7Salvatory Okum Afisa Matekelezo kutoka makao makuu ya NHIF akizizitiza jambo wakati akihamasisha wananchi kujiunga na huduma za Afya ya Jamii CHF 8Wananchi wakiendelea kupata huduma hiyo 9Abdul Gaucho wa kijiji cha Chumo Uso kwa Uso na Othman Michuzi wa Mtaa kwa Mtaa Blog. 10Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) Bw, Rehani Athumani akijadiliana jambo na Mwanaisha Lindu Diwani wa Viti maalum Kilwa wakati alipotembelea na kujionea shughuli za uhamasishaji wananchi wa kijiji cha Chumo kujiunga na huduma ya Afya ya Jamii CHF 11Meneja wa NHIF mkoa wa Lindi Bi. Fortunata Raymond akishiriki kuchezo ngoma ya Wamatumbi wilayani Kilwa. 12Wananchi wakiwa wamejipanga kwenye mstari tayari kwa kupima afya zao. 13 
Paul Marenga Afisa Matekelezo mfuko wa Bima ya Afya mkoa wa Lindi akimpima urefu Bi. Mwanaisha Lindu Diwani wa viti maalum wilaya ya Kilwa wakati wa kampeni hiyo. 14Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) Bw, Rehani Athumani akizungumza na wananchi wakati wa kampeni hiyo iliyofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Chumo. 15Mwalimu Chatherine Ngeleja wa shule ya Msingi Chumo kulia na ndugu yake Beata Ngeleja wakisubiri kupata huduma wakati wa kampeni hiyo. 16Meneja wa NHIF mkoa wa Lindi Bi. Fortunata Raymond akihamasisha wananchi kujiunga na huduma ya afya ya jamii CHF wakati wa kampeni hiyo iliyofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Chumo.

KONGAMANO LA UHURU WA HABARI WPFD KUFANYIKA MOROGORO MEI 2-3, WADAU ZAIDI YA 200 KUSHIRIKI

MISATAN Chairperson Simon Berege addresses the media during a press conference to introduce World Press Freedom Day 2015
Mwenyekiti wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari duniani (WPFD) yatakayofanyika tarehe 2 mwezi Mei mwaka huu mkoani Morogoro.
Na Modewjiblog team
Wanahabari na wadau wa habari wanatarajiwa kukutana Mkoani Morogoro kwa siku mbili kwa kusanyiko la maadhimisho ya siku ya Uhuru wa habari duniani (WPFD), litakalofanyika katika hoteli ya Nasheera, Mjini Morogoro.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mwenyekiti wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika), Ndugu Simon Berege alieleza kuwa, kusanyiko hilo la wandishi wa habari na wadau wa habari litafanyika mjini humo Mei 2-3, mwaka huu.
“Hii ni mara ya kwanza WPFD kuadhimishwa mkoani Morogoro na mwakani itafanyika mkoa mwingine nia ni kufanya kila mkoa kupata nafasi ya kuadhimisha siku hiyo.
Wakati wa maadhimisho hayo wadau watakumbuka gharama za waandishi wa habari kukusanya taarifa mbalimbali na kuwapatia wananchi, gharama ambazo wakati mwingine ni uhai wao au hata kunyimwa uhuru’ alieleza Berege.
Aidha siku hiyo watakumbukwa wale waliopoteza maisha kutokana na harakati za kutafuta habari kwa ajili ya umma.
Siku ya WPFD, ambayo huadhimishwa duniani kote kila mwaka ilianzishwa na Umoja wa Mataifa kwa lengo la kuadhimisha kanuni za uhuru wa habari na kuwakumbuka wale waliokufa wakijaribu kutekeleza kanuni hizo.
Kwa maneno mengine WPFD ni jukwaa linalotumika na waandishi wa habari na wadau wengine katika kutoa kauli za kushawishi serikali mbalimbali kutunga sheria rafiki za vyombo vya habari ambazo zitahakikisha uwapo wa uhuru wa habari.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Usalama wa habari katika ulimwenguj wa dijiti: Uandishi bora, Usawa wa jinsia na faragha’.
Berege alibainisha kuwa, kwa kuzingatia kauli mbiu hiyo, WPFD 2015 itaangalia masuala matatu muhimu: Ikiwemo Uandishi bora na ulio huru katika dunia ya dijiti. Humu itajadiliwa uwingi wa vyombo vya habari na athari zake katika majukumu ya uandishi na uwajibikaji kwa umma, masuala ya kujiwabisha wenyewe, changamoto katika habari za uchunguzi, kauli za uchochezi na vyombo vya habari na mafunzo ya habari.
Pia suala lingine ni juu ya Wanawake na menejimenti ya vyombo vya habari; na namna vyombo vya habari vinavyomuona mwanamke huku la mwisho likiwa ni suala la Usalama wa waandishi wa habari hasa katika maeneo yenye vurugu na jinsi ya kuhami vyanzo vya habari dhidi ya ufichuaji wa kidijiti.
Katika kongamano hilo pia litatoa nafasi ya kujadili na kutoa maazimio kuhusu sheria zilizopitishwa na bunge na zile ambazo zimetamkwa kwa mara ya kwanza. Sheria hizo ni pamoja na za Cybercrime Act, Statistics Act, Media Services Bill and the Access to Information Law.
Hata hivyo, imeelezwa kuwa, Wakati wa kongamano hilo walioathirika kwa kuvunjwa kwa uhuru wa habari watatoa ushuhuda wao.
Pia taarifa ya hali ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika iliyoandaliwa na MISA itazinduliwa rasmi.
Aidha, katika tukio hilo, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Bw. Alvaro Rodriguez huku wadau zaidi ya 200 wakiwemo wadau wa habari na maendeleo pamoja na wawakilishi kutoka serikalini na mashirika mbalimbali ya kimataifa, mabalozi, wabunge, vyama vya kijamii, asasi zisizokuwa za kiserikali, waandishi maveterani,wakuu wa vyuo vya habari na waandishi wa habari.
Tukio hilo limeandaliwa kwa pamoja na Media Institute of Southern Africa-Tanzania Chapter [MISA (T) Chapter], Media Council of Tanzania [MCT], Tanzania Media Fund [TMF], Union of Tanzania Press Clubs [UTPC], United Nations Tanzania Office, UNESCO.
Wengine ni Konrad-Adenauer-Stiftung Tanzania [KAS], Media Owners Association of Tanzania [MOAT], Tanzania Editors’ Forum [TEF], Tanzania Media Women’s Association [TAMWA), Morogoro Press Club na Tanzania Communication Regulatory Authority [TCRA).
Aidha kamati ya maandalizi ya WPFD 2015 imewezesha tukio hilo kwa kushirikisha pia Government Employees Pensions Fund [GEPF], Alliance One Tanzania, IPP Group of Companies, European Union (EU) na Tanzania National Parks [TANAPA].
TMF Director Ernest Sungura clarifies a point during the conference
Mkurugenzi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) ambao ni miongoni mwa wadau wa maandalizi ya maadhimisho hayo Bw. Ernest Sungura akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) uliofanyika katika hoteli ya Holiday Inn jijini Dar es Salaam leo. Kulia Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa ambao ni miongoni mwa wadhamini wa maadhimisho hayo, Usia Nkhoma Ledama.
Ms Jane Mihanji, UTPC Vice President tells why it is important for journalists to be at centre stage during celebrations
Makamu Rais wa Umoja wa Vilabu vya Waancdishi wa habari nchini (UTPC), Jane Mihanji akisisitiza umuhimu wa wanahabari kuhudhuria maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari duniani (WPFD) ambayo kitaifa yanatarajiwa kufanyika mkoani Morogoro Mei 2 mwaka huu. Katikati ni Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa ambao ni miongoni mwa wadhamini wa maadhimisho hayo, Usia Nkhoma Ledama na kushoto ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) ambao ni miongoni mwa wadau wa maandalizi ya maadhimisho hayo Bw. Ernest Sungura.
KAS's Richard Shaba and TAMWA's Godrida Jola listen to questions from journalists
Miongoni mwa wadau wa maandalizi ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari duniani (WPFD) Bw.Richard Shaba kutoka KAS Tanzania na Mwakilishi kutoka TAMWA, Godrida Jola wakisikiliza maswali kutoka kwa wanahabari (hawapo pichani).
A cross section of journalists covering the press conference
Sehemu ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini waliohudhuria mkutano huo.
Journalists at the press conference  

Sunday, April 26, 2015

JESHI LA POLISI KIGOMA LAWAMANI LEO

 Na Magreth Magosso,Kigoma
 
CHAMA Cha Waganga wa Tiba za asili na mbadala Mkoa wa Kigoma ,umelitaka Jeshi la Polisi mkoani humo, washirikishe uongozi wa mitaa na kiongozi wa chama cha tiba asilia katika operesheni ya kamatakamata waganga wapiga ramli chonganishi  kwa kuwa, baadhi ya Askari polisi hujinufaisha na sakata la mauwaji ya albino kwa kuvamia kaya za waganga  na kuomba fedha kiasi cha sh.200,000 ili wachiwe huru.
 
Hayo yalibainika kigoma Ujiji wakati wanachama wa chama hicho,kilichoketi  kujadili njia mbadala ya kuepuka tiba hizo na uhusishwaji wa mauwaji ya vikongwe na walemavu wa ngozi (Albinism) na kulaani vitendo vya  udhalilishaji wa kijinsia unaofanywa na baadhi ya waganga washirikina ,ambapo  kuwaingilia kimwili wateja kwa madai ni tiba ilihali  mwenyezi mungu ameweka miti na matunda katika kuboresha afya za watu.
 
Akielezea hilo Mwenyekiti  wa chama (ATME) Abdallah Joseph Mkazi wa Ujiji alisema kitendo cha baadhi ya askari polisi  kwa nyakati tofauti wamekuwa kero kwa waganga wa tiba hizo,kwani huwavizia katika nyumba na kuwabana kwa maswali yasiyo na mashiko sanjari na kuomba fedha ili wamwache huru.
 
Alisema ili jamii itofautishe baina ya waganga wa tiba asilia na mbadala na waganga washirikina hawana budi kuanza ujenzi wa Kliniki bora nay a kisasa ambayo itatoa huduma kwa walengwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za kitiba bila kuingilia uhai wa mtu na atakayekaidi kujiunga na vyma mtambukwa vya kijadi atakuwa na lake.
 
“hakuna tiba inayoruhusu udhalilishaji kwa  wateja kuwa ni dhambi kubwa kwa mungu kwa mujibu wa vitabu vya mungu(Qur`an na Biblia) na ni ukiukwaji wa haki za binadamu na kukiri hakuna tiba ya kuingiliana  kimwili baina ya mteja na mganga” alibainisha Joseph.
 
Alitaka kitendo cha uogeshaji utupu kwa wateja katika njia panda na utupaji wa  madawa hovyo njiani umepitwa na wakati na kinachangia kushusha thamani ya tiba asili na kuongeza uchafuzi wa mazingira na kudai mkakati walionao  chama cha  (ATME) Tawi la hapa ni ujenzi wa kliniki ya kisasa , ili kuepuka kero ya mauwaji hayo.
 
Akifafanua hilo Mjumbe wa dawa asilia na utunzaji wa mazingira kanda mgharibi Gregori Kassian ambaye ni Mkazi wa wilaya ya Kibondo kigoma alisema kuna mchakato maalum wa kitaifa wa kuwaelimisha waganga  wafuate sheria na taratibu za  tiba ziwe za uwazi na wajiunge katika   vyama ili kuwabaini waganga feki wanaoharibu umuhimu wao katika jamii.
 
Alisema ili kukabiliana na aibu ya utupaji wa madawa katika njia panda wameanzisha ulinzi shirikishi miongoni mwao ili kubaini wanaohusika na tiba za udhalilishaji wa kijinsia kwa tija ya kulinda watu wenye ulemavu wa ngozi.Wakatihuohuo  Sadick Kimwaga  alitaka watakaobainika kuchangia mauwaji ya vikongwe na albino wahukumiwe kwa mujibu wa sheria.
 
Akifunga kikao hicho Mwenyekiti wa Serikali wa Mtaa wa Rusimbi Pia Katibu wa chama cha walemavu kigoma Bakari Songoro  alisema wapo tayari kutoa ushirikiano katika maboresho ya tiba hizo na kukiri kigoma Ujiji inaongoza kwa tiba za njia panda ,ambazo hulazimisha mteja aoge na atupe dawa njia panda, ambapo madawa hayo uchanganywa na nyembe,pini,sindano ni hatari kwa watoto.