CHAMA Cha Waganga wa Tiba za
asili na mbadala Mkoa wa Kigoma ,umelitaka Jeshi la Polisi mkoani humo, washirikishe
uongozi wa mitaa na kiongozi wa chama cha tiba asilia katika operesheni ya kamatakamata
waganga wapiga ramli chonganishi kwa kuwa,
baadhi ya Askari polisi hujinufaisha na sakata la mauwaji ya albino kwa kuvamia
kaya za waganga na kuomba fedha kiasi
cha sh.200,000 ili wachiwe huru.
Hayo yalibainika kigoma Ujiji
wakati wanachama wa chama hicho,kilichoketi kujadili njia mbadala ya kuepuka tiba hizo na
uhusishwaji wa mauwaji ya vikongwe na walemavu wa ngozi (Albinism) na kulaani
vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia
unaofanywa na baadhi ya waganga washirikina ,ambapo kuwaingilia kimwili wateja kwa madai ni tiba ilihali
mwenyezi mungu ameweka miti na matunda
katika kuboresha afya za watu.
Akielezea hilo Mwenyekiti wa chama (ATME) Abdallah Joseph Mkazi wa
Ujiji alisema kitendo cha baadhi ya askari polisi kwa nyakati tofauti wamekuwa kero kwa waganga
wa tiba hizo,kwani huwavizia katika nyumba na kuwabana kwa maswali yasiyo na
mashiko sanjari na kuomba fedha ili wamwache huru.
Alisema ili jamii itofautishe
baina ya waganga wa tiba asilia na mbadala na waganga washirikina hawana budi
kuanza ujenzi wa Kliniki bora nay a kisasa ambayo itatoa huduma kwa walengwa
kwa mujibu wa sheria na taratibu za kitiba bila kuingilia uhai wa mtu na
atakayekaidi kujiunga na vyma mtambukwa vya kijadi atakuwa na lake.
“hakuna tiba inayoruhusu udhalilishaji
kwa wateja kuwa ni dhambi kubwa kwa
mungu kwa mujibu wa vitabu vya mungu(Qur`an na Biblia) na ni ukiukwaji wa haki
za binadamu na kukiri hakuna tiba ya kuingiliana kimwili baina ya mteja na mganga” alibainisha
Joseph.
Alitaka kitendo cha uogeshaji
utupu kwa wateja katika njia panda na utupaji wa madawa hovyo njiani umepitwa na wakati na kinachangia
kushusha thamani ya tiba asili na kuongeza uchafuzi wa mazingira na kudai mkakati
walionao chama cha (ATME) Tawi la hapa ni ujenzi wa kliniki ya
kisasa , ili kuepuka kero ya mauwaji hayo.
Akifafanua hilo Mjumbe wa dawa
asilia na utunzaji wa mazingira kanda mgharibi Gregori Kassian ambaye ni Mkazi
wa wilaya ya Kibondo kigoma alisema kuna mchakato maalum wa kitaifa wa
kuwaelimisha waganga wafuate sheria na taratibu
za tiba ziwe za uwazi na wajiunge katika vyama ili kuwabaini waganga feki wanaoharibu
umuhimu wao katika jamii.
Alisema ili kukabiliana na aibu
ya utupaji wa madawa katika njia panda wameanzisha ulinzi shirikishi miongoni
mwao ili kubaini wanaohusika na tiba za udhalilishaji wa kijinsia kwa tija ya
kulinda watu wenye ulemavu wa ngozi.Wakatihuohuo Sadick Kimwaga
alitaka watakaobainika kuchangia mauwaji ya vikongwe na albino
wahukumiwe kwa mujibu wa sheria.
Akifunga kikao hicho Mwenyekiti wa
Serikali wa Mtaa wa Rusimbi Pia Katibu wa chama cha walemavu kigoma Bakari
Songoro alisema wapo tayari kutoa
ushirikiano katika maboresho ya tiba hizo na kukiri kigoma Ujiji inaongoza kwa tiba
za njia panda ,ambazo hulazimisha mteja aoge na atupe dawa njia panda, ambapo madawa
hayo uchanganywa na nyembe,pini,sindano ni hatari kwa watoto.
No comments:
Post a Comment