Pages

KAPIPI TV

Tuesday, March 24, 2015

RUHUSUNI WANAUME WADI ZA LEBA KUPUNGUZA KUCHOCHEA UZAZI SALAMA - KOMBO

DSC_0036




DSC_0069




DSC_0194



DSC_0112
DSC_0158
DSC_0171
DSC_0274
DSC_0204
DSC_0218
DSC_0220
DSC_0222
DSC_0228
DSC_0294
DSC_0305
DSC_0240
DSC_0250
DSC_0252
DSC_0254
DSC_0256
DSC_0258
DSC_0261
DSC_0048
DSC_0053
DSC_0040
DSC_0268
DSC_0025
DSC_0080
DSC_0316
DSC_0026
DSC_0021
DSC_0321
DSC_0327
DSC_0331
DSC_0336
DSC_0341
DSC_0346
DSC_0350
DSC_0359

Monday, March 23, 2015

23 UYUI WAHITIMU MAFUNZO YA WASAIDIZI WA KISHERIA VIJIJINI

    
Katibu Msaidizi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Bw.Salvatory Kilasara akitoa maada ya maadili ya viongozi wa Umma wakati wa kuhitimisha  mafunzo ya Wasaidizi wa kisheria wilaya ya Uyui yaliyofanyika kwa muda wa siku 25.
Baadhi ya Wasaidizi wa kisheria wakipokea vyeti vya kuhitimu Mafunzo ya Sheria mbalimbali za nchi.




Tabora

JUMLA ya vijana 23 wakiwemo wanawake 9 na wanaume 14 wamehitimu mafunzo maalumu ya ‘Wasaidizi wa Kisheria’ vijijini yaliyoendeshwa katika wilaya ya Uyui mkoani Tabora na taasisi ya Jamii Salama Development Volunteers (JSDV) yenye makao yake makuu mjini Tabora.

 Mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Denmark (DANIDA) kupitia Mfuko wa Huduma za Kisheria (Legal Services Facility-LSF) yaliendeshwa kwa muda wa siku ishirini na tano (25) chini ya usimamizi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (Tanganyika Law Society).

Akizungumza katika hafla ya kufunga mafunzo hayo jana, Katibu Msaidizi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Bw.Salvatory Kilasara alisema mafunzo waliyopata vijana hao ni msaada mkubwa kwa jamii hasa kule vijijini ambako wananchi walio wengi hawana mtu wa kuwapa mwongozo au msaada wa kisheria utakaowawezesha kupata haki zao kama inavyostahili.

Ili wafanikiwe katika kazi hiyo ya utoaji msaada wa kisheria kwa wananchi ikiwemo kusuluhisha migogoro ya wananchi hususani kule vijijini, Kilasara aliwataka wahitimu hao kuwa waadilifu, kufanya kazi kwa weledi, kuweka mbele maslahi ya jamii na kuendelea kujifunza zaidi kwa wanasheria wengine.

Aliwataka kuongeza mshikamano zaidi na taasisi ya JSDV, halmashauri ya wilaya Uyui na jamii kwa ujumla, aidha aliasa vijana hao kusaidia kuelimisha jamii juu ya utokomezaji vitendo vyote vya ukatili na unyanyasaji kijinsia ikiwemo vitendo vya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.

Mwakilishi wa Tanganyika Law Society (TLS) Seleman Pingoni alipongeza jitihada na utayari wa vijana hao kuitetea jamii inayowazunguka, hivyo akawataka wasiwe watendaji wa ofisini tu bali wawatembelee wananchi mbalimbali kule vijijini na kutoa mwongozo wa elimu ya sheria katika jamii na sio kuwa mahakimu.

Naye Mkurugenzi Mkazi wa JSDV Pascal Kilagula alisema vijana hao sasa wameiva na wako tayari kuitumikia jamii na kama taasisi wana matarajio makubwa juu yao, hivyo akawataka kuonyesha ufanisi wa hali ya juu.

Aidha Kilagula alibainisha kuwa mkakati wa kuanzisha kituo cha sheria katika kijiji cha Isikizya wilayani Uyui kwa ajili ya kuwasaidia wananchi uko mbioni kuanza na kituo hicho kitaendeshwa na vijana hao waliohitimu mafunzo ya msaada wa kisheria chini ya usimamizi wa TLS.

Awali akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wenzake Bi.Theresia Kyejo alieleza kuwa wamepata elimu na uelewa wa kutosha utakaowasaidia kutoa msaada wa kisheria kwa jamii na sasa wana ujasiri na ari kubwa ya kuwatumikia wananchi hasa baada ya kufanikiwa kutatua na kusuluhisha jumla ya migogoro 340 katika kata mbalimbali wilayani humo katika kipindi cha mafunzo hayo.

ZIARA YA MKURUGENZI MKUU WA NHC KATIKA MIKOA YA SINGIDA, TABORA NA SHINYANGA

1
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu ukitembelea jengo la NHC lililoungua mwaka jana mjini Singida ambapo Shirika linajenga upya jengo jingine katika kiwanja hicho kilichoko katikati ya mji huo.
Jana Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia kyando Mchechu ameanza ziara yake ya kutembelea Mikoa ili kuhimiza utendaji kazi wa viwango na kujionea utekelezaji wa miradi ya nyumba za gharama nafuu katika mikoa atakayotembelea ya Singida, Shinyanga, Tabora, Kigoma, Sumbawanga,Katavi na Mbeya. Picha na Muungano Saguya-Shinyanga
New Picture (2)
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu ukiwa eneo la Unyankumi na kupewa maelezo ya mradi wa nyumba za gharama nafuu na Meneja wa NHC Mkoa wa Singida Bw. Ladislaus Bamanyisa ulipotembelea mradi huo kukagua ujenzi wake.
New Picture (3)
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akikagua nyumba za gharama nafuu eneo la Unyankindi Singida na kukuta mmoja wa wanunuzi wa nyumba hizoakiwa amejenga ukuta usilingana na viwango vilivyowekwa na NHC katika miliki zake inazojenga.
New Picture (4)
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu na ujumbe wake wakiwa na mfanyakazi aliyestaafu utumishi wake NHC Dr. Allan Kabogo (wa pili kutoka kulia) walipomkuta eneo la Misigiri Wilaya ya Iramba akiwa anajishughulisha na biashara na huduma za kitabibu. Ujumbe huo ulifurahishwa kuona mstaafu wa NHC anaishi maisha ya furaha na matumaini makubwa.
New Picture (5)
Meneja wa NHC Mkoa wa Tabora Bw. Erasto Chilambo akitoa maelezo ya awali kwa ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu ulipotembelea mradi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Igunga jana.
New Picture (6)
Nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Igunga zikiwa katika hatua ya linta tayari kukamilishwa na kuuzwa kwa wananchi wa Wilaya hiyo na maeneo mengine watakaohitaji.
New Picture (7)
Utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa nyumba za gharama za nafuu unaotekelezwa na NHC katika mikoa 23 hivi sasa unatoa ajira kwa wananchi wanaozunguka maeneo ya miradi hiyo kama wananchi hawa walivyonaswa na kamera ya NHC Wilayani Igunga jana.
New Picture (8)
Meneja wa NHC Mkoani Tabora Bw. Erasto Chilambo akiwatembeza viongozi wa Shirika waliotembelea mradi wa nyumba za gharama nafuu unaotekelezwa na NHC Wilayani Igunga kwa ajili ya kuuzia wananchi.
New Picture (9)
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akionyeshwa kisima cha maji kinachotumiwa na vikundi vya vijana vya Vijana Tujiajiri na Miti ni Uhai Wilayani Nzega ambavyo vilipewa msaada na NHC wa mashine za kufyatua matofali yanayofungamana.
New Picture (10)
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akiangalia namna mchanga wa kufyatulia matofali yanayofungamana unavyoandaliwa alipotembelea vikundi vya vijana vya Vijana Tujiajiri na Miti ni Uhai Wilayani Nzega jana. Vikundi hivi vilipewa mashine ya kufyatulia matofali na NHC kama sehemu ya kusaidia vijana ajira nchini.
New Picture (11)
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akitoa mchango wa kununua sementi kwa vikundi vya vijana vya Vijana Tujiajiri na Miti ni Uhai Wilayani Nzega ambavyo vilipewa msaada na NHC wa mashine za kufyatua matofali yanayofungamana.Vikundi hivyo sasa vinapata kazi za kuwatengenezea wateja mbalimbali matofali hayo na hivyo kuwa na ajira endelevu.
New Picture (12)
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake wakionyesha na Meneja wa Mkoa wa Tabora Bw. Erasto Chilambo ramani yaeneo lililopewa NHC ili kujenga nyumba za gharama nafuu Wilayani Nzega.
New Picture (13)
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akipewa maelezo na Msimamizi wa mradi wa nyumba za gharama nafuu Bw. Mwikuka juu ya hatua zilizofikiwa katika ujenzi wa nyumba 50 zinazojengwa na NHC eneo la Zongomela Wilayani Kahama.
New Picture (14)
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akisalimiana na mafundi ujenzi alipotembelea mradi wa nyumba 50 za gharama nafuu zinazojengwa na NHC eneo la Zongomela Wilayani Kahama.
New Picture (15)
Mkurugenzi wa Usimamaizi wa Mikoa na Utawala Bw. Raymond Mndolwa akishiriki ujenzi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Kahama mara baada ya Uongozi wa Shirika kutembelea mradi huo jana.
New Picture (16)
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akisisitiza umuhimu wa kupunguza gharama za ujenzi wa nyumba za gharama nafuu unaofanywa na NHC ili kuwawezesha wananchi wengi kumudu bei ya nyumba hizo alipotembelea nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Kahama ili kuukagua mradi huo jana.
New Picture (17)
Mkurugenzi wa redio Kahama FM Bw. Marco Mipawa akimpa maelezo Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu alipotembelea studio hizo ili kufafanua namna wananchi wanavyoweza kununua nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC eneo la Zongomela Wilayani Kahama jana. Ujenzi wa nyumba hizo utakamilika mwezi Agosti mwaka huu na kuuzwa kwa wananchi.
New Picture (18)
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akiongea na wafanyakazi wa NHC Mkoa wa Shinyanga(hawapo pichani) akisisitiza watende kazi zao kwa mtizamo wa kibiashara na kuongeza tija na kwamba hatasita kumuondoa kazini mtumishi yeyote wa Shirika ambaye atashindwa kufikia malengo aliyopewa.
New Picture
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akibatilisha eneo la kujenga nyumba ya biashara mjini Singida kwa Msimamizi wa mradi huo kutoka kampuni ya B.H Ladwa inayojenga jengo hilo. Kwa sasa jengo hilo litajengwa mbele ya jengo la Singida Motel ili kuweza kuvutia wafanyabiashara watakaopanga katika jengo