Pages

KAPIPI TV

Monday, November 24, 2014

TARATIBU ZA TIBA YA RAIS MH. JAKAYA MRISHO KIKWETE ZAKAMILIKA

D92A4106
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoka katika hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore Maryland baada ya kutolewa nyuzi katika mshono baada ya kufanyiwa upasuaji wiki iliyopita.Rais Kikwete anatarajiwa kurudi tena hospitalini hapo Jumatatu kwa ukaguzi wa maendeleo ya kidonda na ushauri .Kulia kwake ni Daktari wa Rais Profesa .Mohamed Janabi
………………………………………………………………….
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI LEO
Taratibu za matibabu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, zimekamilika leo, Jumatatu, Novemba 24, 2014.

Taratibu hizo za matibabu za Mheshimiwa Rais Kikwete zimekamilika kiasi cha saa 12 asubuhi ya leo wakati madaktari bingwa katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko mjini Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani, walipomfanyia hatua ya mwisho ya tiba.

Hata hivyo, Rais Kikwete ataendelea kupumzika na kuangaliwa kwenye Hoteli Maalum inayohusiana na Hospitali ya Johns Hopkins kwa siku mbili hadi tatu kabla ya kuanza safari ya kurejea nyumbani.

Kama kila kitu kitakwenda kama ilivyopangwa na madaktari, Rais Kikwete anatarajiwa kurejea nyumbani Jumamosi, Novemba 29, 2014.

Rais Kikwete aliondoka nchini Alhamisi ya Novemba 6, 2014, kwenda kufanyiwa uchunguzi wa afya yake lakini madaktari katika Hospitali ya Johns Hopkins waliamua kumfanyia upasuaji wa tezi dume Jumamosi ya Novemba 8, 2014.

Rais Kikwete anaendelea kuwashukuru Watanzania kwa sala na maombi yao ya kumtakia heri ya kupona haraka na kurejesha afya njema katika kipindi chote cha ugonjwa wake.
Imetolewa na:
 
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu – Dar es Salaam. 24 Novemba,2014

NHIF YATOA HUDUMA YA USHAURI NA UPIMAJI WA AFYA KWA WASHIRIKI WA MASHINDANO YA SHIMUTA-TANGA

Afisa Masoko na Elimu kwa Umma wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bi. Catherine Kameka akiwasajili baadhi ya washiriki wa mashindano ya SHIMUTA waliofika kupata huduma za upimaji wa afya katika banda la NHIF.
Dr. Mashaka Cosmas akimpa ushauri Bw. Jesse John  watimu ya TANESCO baada ya kupata vipimo katika banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya katika mashindano ya SHIMUTA yanayofanyika katikaViwanja vya MkwakwaniTanga.
Afisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Kichanta Damian akimpima urefu mmoja wa washiriki wa mashindano ya SHIMUTA aliyekuja kupata huduma ya upimaji katika banda la Mfuko waTaifa wa Bima ya Afya

 Sr. Mwanaisha Mngulwa akimpima shinikizo la damu Bw. Anord Semu wa timu ya CBE aliyefika katika banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kupata huduma hiyo.

Baadhi ya washiriki wa SHIMUTA wakisubiri kupata vipimo katika banda la Mfuko waTaifa wa Bima ya Afya.