Pages

KAPIPI TV

Thursday, October 2, 2014

BENKI YA CRDB YAZINDUA WIKI YA HUDUMA KWA MTEJA

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia), akiwa na  Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay wakati wakiingia katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya serena jijini Dar es Salaam kuzungumzia Wiki ya Wateja wa Benki hiyo itakayoanza Oktoba 6-11. 
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka (kulia), akiingia katika mkutano huo akiongozana na maofisa wa Benki hiyo.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka (kulia), Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay (katikati) wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei muda mfupi kabla ya kuanza mkutano na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja.
 Maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa jkatika mkutano huo.
 Maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika mkutano huo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki hiyo.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka (kulia), Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay (kushoto) wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyu (kulia) akiwa na maofisa wa Benki hiyo kabla ya kuanza kwa mkutano.
Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma
kwa Wateja wa Benki ya CRDB
, Tully Mwambapa akimkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei kuzungumza na waandishi wa habari kjuhusu Wiki ya Wateja wa Benki ya CRDB.
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumzana waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya wiki ya Wateja wa Benki ya CRDB itakayoanza Oktoba 6-11.

BANDA LA BODI YA UTALII AFRIKA KUSINI KWENYE MAONYESHO YA KIMATAIFA YA SWAHILI EXPO(SITE)

2 (1)
pix2Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika, Bodi ya Utalii Afrika Kusini Bi. Evelyn Mahlaba akifanya mahojiano na mwandishi wa Capital Tv Bi. Yvonne Msemembo kabla ya uzinduzi wa maonesho ya kimataifa ya Utalii Swahili Expo jijini Dar Es Salaam jana.
pix3Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika, Bodi ya Utalii Afrika Kusini Bi. Evelyn Mahlaba akipozi kwenye picha ya pamoja na warembo(ushers) wanaosimamia banda la utalii la Afrika kusini kwenye maonesho ya kimataifa ya Swahili Expo Mlimani City jijini Dar Es Salaam leo.

Wednesday, October 1, 2014

SHIRIKA LA NYUMBA NHC TABORA LATOA MSAADA WA MASHINE ZA MATOFALI KWA VIJANA ZENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 12.9

Mkuu wa wilaya ya Tabora Bw.Suleiman Kumchaya akikabidhi moja ya mashine ya kufyatulia matofali zilizotolewa na Shirika la nyumba la Taifa NHC tawi la Tabora kwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Igunga Bi.Rostica Tuluka,mashine hizo 28  ambazo zina thamani ya shilingi milioni 12.9 zitagaiwa kwa kila ikiwa ni hatua ya NHC kusaidia vijana mkoani Tabora. 
Mmoja kati ya wataalamu wakitoa maelezo namna mashine hizo zinavyofyatua matofali imara na kwa gharama nafuu.
Ufyatuaji tofali
Meneja wa Shirika la nyumba NHC tawi la Tabora Bw.Erasto Chilambo akitoa maelezo mafupi wakati wa hafla ya kukabidhi mashine hizo.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Uyui Bw.Said Ntahondi akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika Kijiji cha Isikizya wilaya ya Uyui.
Picha ya pamoja

Baadhi ya nyumba zilizojengwa na Shirika la nyumba la Taifa katika kijiji cha Isikizya.






PROFESA MUHONGO ASAINI MKATABA WA MRADI WA KUUZIANA UMEME KATI YA ZAMBIA,TANZANIA NA KENYA


unnamed27
Mawaziri wanaoshughulikia Nishati kutoka nchi za Zambia, Tanzania na Kenya wakisaini Mkataba wa Makubaliano kuonesha dhamira ya Serikali ya nchi hizo kujenga miundombinu ya pamoja ya kusafirisha umeme na kufanya biashara ya kuuziana umeme wa ziada baina ya nchi hizo.

Na Anitha Jonas, Maelezo-DSM.
WAZIRI wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter Muhongo jana ametia saini Mkataba wa Mradi kujenga Miundombinu ya kuuziana umeme kati ya Zambia, Tanzania na Kenya (ZTK) katika Mkutano  wa Kumi wa kujadili mradi huo.

Katika utiaji saini Mkataba huo, Profesa Muhongo alisema kuwa mchakato wa kuandaa Mkataba wa mradi huo ulikwishafanyika tangu mwaka 2001 ambapo ulikuwa na vipengele ambavyo kwasasa Mawaziri wa Nishati toka nchi zote tatu wameupitia na umefanyiwa marekebisho.

Profesa Muhonga alisema kuwa katika marekebisho hayo wamebadili kipengele kilichokuwa kinaeleza juu ya uwepo wa Ofisi moja itakayosimamia mradi huo katika nchi zote tatu, na badala yake wamekubaliana kuwa kila nchi ijisimamie yenyewe badala ya kuwa na Ofisi moja pekee itakayosimamia mradi huo.


“Kwa upande wa Tanzania ujenzi wa mradi huu umeshaanza kazi na mpaka hivi sasa asilimia 90 ya vifaa vya ujenzi wa mradi vimeshawasili katika eneo la ujenzi,”alisema Profesa Muhongo.

Akizungumzia maeneo ambayo mradi huo utapita kwa upande wa Tanzania, Profesa Muhongo alisema kuwa, mradi huo utapita maeneo ya mikoa ya Singida- Arusha-Namanga, na Namanga-Isinya kwa Kenya, kwa upande wa Zambia utapita Mbeya–Iringa na Iringa-Singida-Shinyanga. Ambapo unatarajia kusambaza umeme wa kuanzia 400kV.
unnamed28
Mawaziri wanaoshughulikia Nishati kutoka nchi za Zambia, Tanzania na Kenya , Waziri wa Wizara yaMigodi, Nishati na Maendeleo ya Maji  wa Zambia , Christopher Yaruma (kushoto) Waziri wa Nishati na Madini , Profesa Sospeter Muhongo Tanzania (katikati) na Waziri wa Nishati na Petroli Kenya, Davis Chirchir (kulia) wakibadilishana Mkataba wa Makubaliano kuonesha dhamira ya Serikali ya nchi hizo kujenga miundombinu ya pamoja ya kusafirisha umeme na kufanya biashara ya kuuziana umeme wa ziada baina ya nchi hizo mara baada ya kusaini.

Naye Katibu Mkuu wa Nishati nchini Kenya, Mhandisi Joseph Njoroge  alisema kuwa muungano huo wan chi tatu utasaidia kupunguza tatizo la umeme katika nchi zote na Afrika kwa ujumla kwani utapunguza gharama ya umeme pamoja na kuongeza ukuaji wa uchumi katika uzalishaji.

Aidha aliongeza kuwa Serikali yake itahakikisha kuwa Mkataba huo ndani ya siku Thelathini zijazo kabla ya mkutano ujao kuanza, Mwanasheria Mkuu wa Kenya atakuwa umekwisha usaini.

Kwa upande wake Waziri wa Nishati na Madini nchini Zambia, Mh. Christopher Yaruma alisema kuwa nchi yake imeshasaini Mkataba wa kuonyesha dhamira ya kuuziana umeme na nchi ya Malawi, Namibia na Botswana.

Utiaji saini wa Mkataba huo ulihusisha wadau mbalimbali wa maendeleo na wafadhili ikiwemo JICA, COMESA, EU, Korea, Benki ya Dunia, AFD, Ufaransa na Mabalozi wa nchi mbalimbali, ambapo wadau hao wameonyesha nia ya dhati katika kuendelea kuisaidia Serikali hususani katika sekta ya Nishati
Sambamba na hilo, mkutano wa mwendelezo wa mradi huo badaa ya kuwa umesainiwa na viongozi wa Sheria katika nchi husika unatarajiwa tena kufanyika mwanzoni mwa mwezi wa Kumi na moja nchini Lusaka, Zambia.
unnamed29
Mawaziri wanaoshughulikia Nishati kutoka nchi za Zambia, Tanzania na Kenya , Waziri wa Wizara ya Migodi, Nishati na Maendeleo ya Maji  wa Zambia , Christopher Yaruma (kushoto) Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo  Tanzania (katikati) na Waziri wa Nishati na Petroli Kenya, Davis Chirchir (kulia) wakionesha Mkataba wa Makubaliano mara baada ya kusaini.
unnamed31
Sehemu wa wadau waliohudhuria hafla ya kusaini Mkataba  wa Makubaliano kuonesha dhamira ya Serikali ya nchi za Zambia, Tanzania na Kenya kujenga miundombinu ya pamoja ya kusafirisha umeme na kufanya biashara ya kuuziana umeme wa ziada baina ya nchi hizo. Mbali na Wataalamu kutoka katika nchi hizo, hafla hiyo imehudhuriwa uwakilishi wa COMESA,  Mashirika ya Umeme kutoka nchi hizo na  baadhi ya washirika wa Maendeleo wakiwemo Benki ya Dunia, Umoja wa Ulaya, Ubalozi wa Norway, Shirika la Maendeleo la Japani (JICA), African Development Bank (AfDB), Ubalozi wa Ufaransa.

IPTL YAIMWAGIA TASWA MILIONI 20 KUANDAA TUZO ZA WANAMICHEZO

FKB_3692
Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Harbinder Sigh Seth (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 20 kwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Juma Pinto (wapili kulia) ikiwa ni mchango wa IPTL kusaidia maandalizi ya Tuzo za wanamichezo bora nchini. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni ni Makamu Mweyekiti wa TASWA, Egbert Mkoko, Katibu Mkuu, Amir Mhando na Mwanasheria na Mshauri Mkuu wa IPTL,Joseph Makandege na kulia ni Mjumbe wa TASWA, Rehure Richard Nyaulawa.
Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto akizungumza na wanahabari baada ya kupokea fedha hizo.
Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Harbinder Sigh Seth akiwaeleza wanahabari furaha yake ya kuisaidia TASWA kitita hicho cha fedha kusaidia wanamichezo ambapo nae alikiri kuwa ni miongoni mwa wanamichezo na amewahi kuwa Mshindi wa tatu wa Mbio za Magari Afrika.
Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Harbinder Sigh Seth (katikati) akiwaongoza wanahabari kuangalia mitambo ya Kampuni hiyo ambayo inazalisha umeme. Kulia ni Katibu mkuu wa TASWA, Amir Mhando na Kushoto ni Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto.
Waandishi wa habari wakiingia kuangalia uzalishaji wa umeme katika mitambo ya IPTL.

RAIS KIKWETE AFUNGUA RASMI BARABARA YA MWENGE-TEGETA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.
 Wananchi wakifurahia hotuba ya  Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.
  Wapiga picha wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwa tayari tayari kumrekodi Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua  rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Masaki Okada  wakifungua kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam. Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadiki, Meya wa Konondoni Mhe, Mbunge wa Kawe  Mhe Halima Mdee na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Dar es salaam Ndg Ramadhani Madabida
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Masaki Okada  wakifurahia baada ya kufungua kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam. Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadiki, Meya wa Konondoni Mhe, Mbunge wa Kawe  Mhe Halima Mdee na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Dar es salaam Ndg Ramadhani Madabida
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Masaki Okada  wakikata utepe  kuashiria ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam. Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadiki, Meya wa Konondoni Mhe, Mbunge wa Kawe  Mhe Halima Mdee, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Musa Iyombe na viongozi wengine
 Sehemu ya barabara  ya Mwenge-Tegeta yenye urefu wa Km 12.9, ambayo ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Masaki Okada  wakikata utepe  kuashiria ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam. Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadiki, Meya wa Konondoni Mhe, Mbunge wa Kawe  Mhe Halima Mdee, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Musa Iyombe na viongozi wengine
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Masaki Okada  baada ya ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam. Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadiki, Mbunge wa Kawe  Mhe Halima Mdee, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Musa Iyombe na viongozi wengine.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mbunge wa Kawe Mhe Halima Mdee  baada ya ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

KUNDI LA ORIJINO KOMEDY WAJIUNGA NA HUDUMA YA BIMA YA AFYA ITOLEWAYO NA CRDB

CRDB Microfinance Insurance Brokers ambao ni wakala wa bima za aina zote ikiwemo bima ya afya, moto, nyumbani na maisha wakishirikiana na kampuni zaidi ya kumi za bima nchini Tanzania,wamefanikiwa kuwapatia huduma ya bima ya maisha,mazishi na ulemavu wa kudumu Kundi la Wasanii wa Vichekesho la Orijino Komedy Company wao na familia zao kupitia African life Assurance (Tanzania) Ltd na bima ya afya wao na familia zao kupitia Kampuni ya AAR Insurance Tanzania.
CRDB Microfinance wanayo furaha kubwa kwa kuwapatia wasani hao huduma hiyo,kwani siku zote imekuwa ikifahamika kuwa msanii ni kioo cha jamii.Wasanii hao waliofanikiwa kujiunga na huduma hizo ni pamoja na Isaya Mwakilasa ‘Wakuvwanga’, Mjuni Silvery ‘Mpoki’, Lucas Mhuvile ‘Joti’, Alex Chalamila ‘McRegan’ na Kiongozi wa kundi hilo,Sekioni David na wengine ni Herry pamoja na Jonas.
Huduma hii inawahamasisha wasanii wengine,wanahabari,wanamitindo na watanzania wote wa hali zote kutembelea ilipo CRDB Bank tawi lolote nchini Tanzania,ili waweze kupata huduma nzuri ya na haraka ya bima “ndani ya mikono salama” .
Meneja wa CRDB Microfinance Insurance Brokers,Arthur Mosha (kushoto) akimkabidhi Kadi ya huduma ya bima ya maisha,mazishi na ulemavu wa kudumu Kiongoni Mkuu wa Orijino Komedy Company,Sekioni David (kulia) wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo kwenye ofisi za CRDB Mikocheni jijini Dar.
Msanii Lucas Mhuvile ‘Joti’ akipokea kadi yake kutoka kwa Meneja wa CRDB Microfinance Insurance Brokers,Arthur Mosha.
 Msanii Isaya Mwakilasa ‘Wakuvwanga’ (kulia) akipokea kadi yake kutoka kwa Meneja wa CRDB Microfinance Insurance Brokers,Arthur Mosha.(wa pili kulia) ni Meneja Mkuu wa African Life Assurance,Nura Masoud na Kushoto ni Meneja Mkuu wa AAR Insurance,Majala Manyama.
Meneja Uhusiano wa CRDB Microfinance Insurance Brokers,Nargis Mohamed (kulia) akiwa na Msanii wa Kundi la Wasanii wa Vichekesho la Orijino Komedy Company,Mjuni Silvery ‘Mpoki’ katika hafla hiyo.
Picha ya pamoja.

KATIBU MWENEZI (BAWACHA) KAWE AJIUNGA NA ACT


index
Mbunge wa Kawe Mh. Halima Mdee ambaye pia ni Mwenyekiti wa BAWACHA taifa.
……………………………………………………………..
Kipimo Abdallah
ALIYEKUWA Katibu Mwenezi wa Baraza la Wanawake Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA) Jimbo la Kawe, Batuli Kivuma ambaye amejiunga na chama cha Alliance for Change and Transparent (ACT-Tanzania amesema kilichomuondoa CHADEMA ni ukabila ulioota mizizi kwa muda mrefu.
 
Kivuma ambaye awali alikuwa mwanachama wa Chama Cha Wananchi CUF alisema aliamini kuwa chama hicho kinasimamia demokrasia jambo ambalo limeshindikana hasa ukiwa hotekei mkoa wa Kilimanjaro.
 
Alisema tangu ajiunge katika chama hicho amekuwa na juhudi za kukijenga chama hasa Kata ya Msasani na jimbo zima la Kawe ila juhudi zake zimekuwa zikikwamishwa kwa misingi ya ukabila.
 
Katibu Mwenezi huyo wa zamani wa BAWACHA alisema katika kudhihirisha hilo alishiriki kwenye  mchakato wa kugombea nafasi ya Udiwani viti maalum mwaka 2010 ambapo alishinda ila aliondolewa kwa kigezo cha yeye ni Mdigo na wakapewa nafasi hiyo Wachaga.
 
“Kusema ukweli suala la kuhama vyama sio zuri ila inafikia mahali unashindwa kuvumilia kwani nimekuwa nikionewa mara kwa mara katika chaguzi na ukiangalia vizuri msingi wake ni ukabilia ambao unawabeba Wachaga” , alisema.
 
Kivuma  alisema alikuwa akikipenda sana chama hicho lakini ubaguzi uliopo amefikia mwisho wa uvumilivu na kwamba anahitaji kuonyesha jitihada zake kwingine.
 
Alisema suala hilo la ukabila lilikidhiri katika uchaguzi mkuu ambao ulifanyika hivi karibuni hasa katika upande wa BAWACHA ambapo juhudi zilifanywa kuanzia ngazi ya chini hadi Taifa.
 
Mwenezi huyo wa zamani wa BAWACHA alisema hata upatikanaji wa Mwenyekiti wa BAWACHA wa sasa Halima Mdee ulitawaliwa na ukabila ikiwa ni agizo la Mwenyekiti Taifa Freeman Mbowe.
 
“Unajua hili neno demokrasia wanalielewa je bwana kwani kwa ufahamu wangu ni kuhakikisha kuwa jamii inaacha pale inapofanya maamuzi yake ila huku ni kinyume”, aliongezea Kivuma.
 
Kivuma alisema atahakikisha kuwa anakibomoa CHADEMA hasa katika Jimbo la Kawe ambapo amefanya kazi za kisiasa kwa muda mrefu.
 
Kwa upande wake aliyekuwa Mjumbe wa Mtaa Serikali ya Mtaa wa Matofalini Ujiji Kigoma Yassin Mohamed alisema ni vema vyama vikatambua kuwa hakuna uadui baina yao na kuhama chama ni haki ya mtu.
 
Alitolea mfano hali ya kisiasa ilivyokuwa siku za nyuma kati ya chama na CHADEMA na CUF hali ambayo kwa sasa haipo na vinafanya kazi pamoja.
 
Mohamed alisema ameamua kujiunga na ACT-Tanzania na kuondoka CHADEMA ili kupata uhuru wa kupigania demokrasia ya kweli.

UVCCM TABORA WALALAMIKA

Na, Thomas Murugwa, Tabora.

Viongozi wa chama cha Mapinduzi  - CCM wameaswa kutatrua changamoto zinazowakabili wanachama wa jumuhiya ya UVCCM kwani ndiyo nguzo ya chama.

Akizungumza kwenye baraza la vijana lililofanyika kata ya Gongoni  mjini Tabora  mwenyekiti wa UVCCM mkoa Seif Gullamali amesema kuwa kuimarika kwa vijana ndio mafanikio ya CCM.

Mwenyekiti huyo amesema kwamba vijana ndiyo nguzo ya chama hivyo changamoto zinazowakabili inabidi zitatuliwe ili waweze kutumika ipasavyo kuijenga CCM badala ya kuwaacha wakilalamika.

Gullamali amewashauri viongozi wa chama tatwala kutembelea vijana na kuzungumza nao ili kufahamu matatizo yanayowakabili na kuyatafutia ufumbuzi ili wasije wakajigawa katika makundi na hatimaye kuhasi.

Wakisoma risala yao vijana hao walilalamika mkwamba viongozi wa CCM wamekuwa hawatoi msaada kwa jumuiya hiyo  hali ambayo huwafanya vijana kuwa na hali ngumu katika ufanisi wao huku wakiishi kama yatima.

Walitaja changamoto nyingine kuwa ni mahusiano mabaya kati ya viongozi wa chama na jumuiya hiyo kuwa ni majibu yasiyo mazuri pindi vijana wanapotaka kusaidiwa kimawazo au kiuchumi wakibaki wasijue la kufanya.

Naye kamanda wa vijana kata ya Gongoni Kessy Shariff amewaasa wenzake wasikate tamaa na wasiogope kuwania nafasi za uongozi wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwezi Desema mwaka huu.

Kessy amewaambia vijana wenzake kuwa huu si wakati wa malumbano bali wajipime kama wanatosha kuwa viongozi waingie kwenye kinyanganyiro cha kitawaunga mkono.

WALIMU WAFUNGIA WATENDAJI WA HALMASHAURI - KIGOMA

 
Na Magreth Magosso Kigoma

WALIMU na viongozi wa chama cha walimu katika wilaya ya Kigoma wamevamia ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo  na kufunga lango kuu la kuingia kwa takribani masaa matatu wakitaka serikali isikilize madai yao.

Walimu hao walichukua hatua hiyo kufuatia kitendo cha mkurugenzi Mtendaji wa wilaya hiyo ,Michael Mwandezi kuondoka ofisini kwake muda mfupi baada ya walimu hao kuingia eneo la ofisi za Halmashauri na kuchukua muda mrefu kumsubiri bila mafanikio.

Kitendo hicho kilisababisha huduma mbalimbali zilizokuwa zikitekelezwa na watumishi katika halmashauri hiyo kukwama kwa kipindi cha takribani masaa matatu ambapo walimu hao waliitaka serikali isikilize na kulipa madai yao mbalimbali ambayo hayajalipwa kwa muda mrefu sasa.


Wakieleza sababu za kuchukua hatua hiyo Mwenyekiti wa Chama cha walimu wilaya ya Kigoma Alphonce Mbassa na Mwenyekiti wa CWT mkoa Kigoma,Hussein Mayeye walisema wamekuwa wakipuuzwa na serikali katika kulipwa madai yao kwa muda mrefu na kwamba hatua hiyo ya kuzifunga ofisi za Halmashauri zinaashiria ukomo wa uvumilivu wao.


Wakiongea kwa nyakati tofauti walimu hao Kabembo Samora  na Rukia Juma walisema kwa muda mrefu madai yao hayajapatiwa ufumbuzi na kuweza kulipwa  stahiki zao ambazo wamekuwa wakizifuatilia mara kadhaa bila mafanikio.

Walisema kuwa serikali imekuwa ikipuuza kulipa madai ya walimu hali ambayo imeshusha morali ya wao wa kufundisha na ndiyo moja ya sababu ya kushuka kwa taaluma kwenye shule za msingi na sekondari nchini jambo linalichangiwa na serikali yanyewe ambayo haijaweka mikakati dhabiti ya kusaidia walimu kwenya Nyanja mbalimbali.


Baada ya kufungwa kwa milango ya kuingia katika ofisi za Halmashauri ilibidi polisi wa kutuliza ghasia wafike eneo hilo  ambapo baada ya mashauri na viongozi wa polisi,usalama wa taifa na Katibu tawala wa wilaya ya Kigoma walimu hao walikubali kufungua milango na kuingia kwenye ukumbi wa mikutano kwa ajili ya majadiliano.


Akizungumza katika kikao cha pamoja baina ya viongozi wa CWT,walim,Wakuu wa idara wa Halmashauru ya wilaya ya Kigoma, maafisa kutoka vyombo vya ulinzi na usalama, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauria ya wilaya Kigoma,Michael Mwandezi alisema kuwa serikali imeanza kulipa madai mbalimbali ya watumishi wakiwemo walimu baada ya kufanyiwa uhakiki na kwamba madai yanayosumbua kwa sasa ni yale ambayo usahihi wake wa malipo unatia shaka.

Mkurugenzi huyo aliwaahidi walimu hao kuwa madai yao yatashughulikiwa  baada ya wiki mbili  ambapo Walimu hao wanadai kiasi cha shilingi milioni 80 ikiwemo malipo ya nauli za likizo,matibabu,marekebisho ya kupandishwa madaraja.