Pages

KAPIPI TV

Wednesday, October 1, 2014

WALIMU WAFUNGIA WATENDAJI WA HALMASHAURI - KIGOMA

 
Na Magreth Magosso Kigoma

WALIMU na viongozi wa chama cha walimu katika wilaya ya Kigoma wamevamia ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo  na kufunga lango kuu la kuingia kwa takribani masaa matatu wakitaka serikali isikilize madai yao.

Walimu hao walichukua hatua hiyo kufuatia kitendo cha mkurugenzi Mtendaji wa wilaya hiyo ,Michael Mwandezi kuondoka ofisini kwake muda mfupi baada ya walimu hao kuingia eneo la ofisi za Halmashauri na kuchukua muda mrefu kumsubiri bila mafanikio.

Kitendo hicho kilisababisha huduma mbalimbali zilizokuwa zikitekelezwa na watumishi katika halmashauri hiyo kukwama kwa kipindi cha takribani masaa matatu ambapo walimu hao waliitaka serikali isikilize na kulipa madai yao mbalimbali ambayo hayajalipwa kwa muda mrefu sasa.


Wakieleza sababu za kuchukua hatua hiyo Mwenyekiti wa Chama cha walimu wilaya ya Kigoma Alphonce Mbassa na Mwenyekiti wa CWT mkoa Kigoma,Hussein Mayeye walisema wamekuwa wakipuuzwa na serikali katika kulipwa madai yao kwa muda mrefu na kwamba hatua hiyo ya kuzifunga ofisi za Halmashauri zinaashiria ukomo wa uvumilivu wao.


Wakiongea kwa nyakati tofauti walimu hao Kabembo Samora  na Rukia Juma walisema kwa muda mrefu madai yao hayajapatiwa ufumbuzi na kuweza kulipwa  stahiki zao ambazo wamekuwa wakizifuatilia mara kadhaa bila mafanikio.

Walisema kuwa serikali imekuwa ikipuuza kulipa madai ya walimu hali ambayo imeshusha morali ya wao wa kufundisha na ndiyo moja ya sababu ya kushuka kwa taaluma kwenye shule za msingi na sekondari nchini jambo linalichangiwa na serikali yanyewe ambayo haijaweka mikakati dhabiti ya kusaidia walimu kwenya Nyanja mbalimbali.


Baada ya kufungwa kwa milango ya kuingia katika ofisi za Halmashauri ilibidi polisi wa kutuliza ghasia wafike eneo hilo  ambapo baada ya mashauri na viongozi wa polisi,usalama wa taifa na Katibu tawala wa wilaya ya Kigoma walimu hao walikubali kufungua milango na kuingia kwenye ukumbi wa mikutano kwa ajili ya majadiliano.


Akizungumza katika kikao cha pamoja baina ya viongozi wa CWT,walim,Wakuu wa idara wa Halmashauru ya wilaya ya Kigoma, maafisa kutoka vyombo vya ulinzi na usalama, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauria ya wilaya Kigoma,Michael Mwandezi alisema kuwa serikali imeanza kulipa madai mbalimbali ya watumishi wakiwemo walimu baada ya kufanyiwa uhakiki na kwamba madai yanayosumbua kwa sasa ni yale ambayo usahihi wake wa malipo unatia shaka.

Mkurugenzi huyo aliwaahidi walimu hao kuwa madai yao yatashughulikiwa  baada ya wiki mbili  ambapo Walimu hao wanadai kiasi cha shilingi milioni 80 ikiwemo malipo ya nauli za likizo,matibabu,marekebisho ya kupandishwa madaraja.

No comments: