Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw.Nehemia Kyando Mchechu wa kwanza kulia mbele akitembelea
eneo la ujenzi wa nyumba za gharama nafuu zitakazojengwa katika
Halmashauri ya Busekelo Mkoani Mbeya alipotembelea Halmashauri hiyo
Septemba 3 mwaka huu .Picha na Saguya wa NHC.
|
Thursday, September 4, 2014
MKURUGENZI NHC ATEMBELEA ENEO LA MRADI WA NYUMBA ZA WATUMISHI HALMASHAURI YA BUSOKELO MBEYA
MGODI WA NORTH MARA WACHANGIA BILIONI 7.5 KATIKA SHUGHULI ZA JAMII
Mwenyekiti
wa Jopo la Majaji kwa ajili ya kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais ya
Huduma za Jamii na Uwezeshaji Prof. Samwel Wangwe (kushoto) akisalimiana
na Afisa Mahusiano wa Mgodi wa North Mara Bw. Zakayo Kalebo (kulia)
mara baada ya jopo hilo kuwasili kwenye mgodi huo.
Meneja
Mahusiano wa Mgodi wa North Mara Bi Fatuma Mssumi (mbele) akielezea
shughuli za mgodi wa North Mara mbele ya jopo la majaji waliotembelea
mgodi huo ili kuendelea na zoezi lake la kumtafuta mshindi wa Tuzo ya
Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji.
Afisa
Uhusiano wa Kijiji cha Matongo Bw. Magesa Wanjara akionesha jinsi ya
kutumia bomba la kisima cha maji kilichofadhiliwa na mgodi wa North Mara
mbele ya timu ya majaji, sekretarieti na wajumbe wengine.
Mwenyekiti
wa Umoja wa Kikundi cha Vijana cha Nyakegema Bw. Zacharia Mwita ( wa
pili kutoka kulia) akitoa maelezo mbele ya timu ya majaji na wajumbe
wengine kuhusu mchango wa mgodi wa North Mara kwa kikundi hicho kupitia
mradi wake wa mboga za majani. Kikundi hicho kina jumla ya vijana 578
kutoka katika vijiji saba vinavyouzunguka mgodi huo.
Mwenyekiti
wa Jopo la Majaji kwa ajili ya kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais ya
Huduma za Jamii na Uwezeshaji Prof. Samwel Wangwe (kushoto) akisalimiana
na Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Ingwe Bw. Alfred Joseph mara
timu hiyo ilipofanya ziara kwenye shule hiyo iliyofadhiliwa na mgodi wa
North Mara.
……………………………………………
Na Greyson Mwase, Tarime
Imeelezwa kuwa mgodi wa North Mara
uliopo wilayani Tarime mkoani Mara umechangia jumla ya shilingi bilioni
7.5 katika kipindi cha mwaka 2013 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya
maendeleo katika vijiji saba vinavyouzunguka mgodi huo.
Akizungumza mbele ya timu ya
majaji kwa ajili ya kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii
na Uwezeshaji chini ya mwenyekiti wake Prof. Samwel Wangwe Meneja
Mahusiano wa Mgodi huyo Bi Fatuma Mssumi alitaja vijiji hivyo kuwa ni
pamoja na Nyangoto, Nyamwaga, Nyakunguru, Kerende, Kewanja, Genkuru na
Matongo.
Bi Mssumi alisema kuwa kupitia
sekta ya elimu, mgodi ulichangia madawati 2700 yenye thamani ya shilingi
milioni 251.9 kwa ajili ya shule mbalimbali za msingi na sekondari na
kuongeza kuwa mgodi ulijenga shule ya sekondari ya Ingwe kwa shilingi
bilioni 1.1 miradi ambayo imekamilika.
Alisema kuwa mgodi ulifanya
ukarabati pamoja na ujenzi wa shule ya sekondari ya Kemambo kwa gharama
ya shilingi milioni 905.5, na shule ya msingi ya Bong’eng’e kwa gharama
ya shiligi milioni 827.
Aliongeza kuwa mgodi huo katika
awamu yake ya kwanza ulichangia shilingi milioni 605. 8 kwa ajili ya
ujenzi wa shule ya sekondari ya Nyamwaga mradi ambao bado unaendelea.
“ Pia mgodi uligharamia shilingi
milioni 12.7 kwa ajili ya wanafunzi waliofanya vizuri kusoma katika
shule na vyuo mbalimbali”, alisema Bi Mssumi
Aliongeza kuwa nia ya kuwekeza
katika elimu katika wilaya ya Tarime ni kuhakikisha wanajenga msingi
utakaopelekea kupatikana wataalamu kwa ajili ya kufanya kazi katika
mgodi huo.
Akielezea mchango wa mgodi huo
katika sekta ya afya Bi Mssumi alitaja miradi mingine kuwa ni pamoja na
ukarabati na ujenzi wa zahanati ya Genkuru uliogharimu shilingi milioni
61.2, upimaji wa macho kwa wanakijiji 3,000 kwa shilingi milioni 19
pamoja na upimaji wa virusi vya Ukimwi kwa wanakijiji 1067 uliogharimu
shilingi milioni tano.
Aliendelea kusema kuwa mgodi huo
ulitoa msaada kwaajili ya upasuaji kwa wanakijiji 11 ambapo jumla ya
shilingi milioni 12.2 zilitumika
Akielezea sekta ya maji Bi. Mssumi
alisema kuwa mgodi ulichimba visima katika vijiji sita kwa thamani ya
shilingi milioni 888.3 pamoja na usambazaji wa maji katika vijiji vya
Nyangoto, Kewanja, Matongo na Kerende uliogharimu shilingi bilioni 1.2
Alisema kuwa mgodi pia ulifanya
ukarabati katika kituo cha afya cha Nyangoto kwa gharama ya shilingi
milioni 481.7 pamoja na usafi katika vijiji vya Nyangoto, Kerende,
Kewanja na Nyamwaga uliogharimu shilingi milioni 544.4
Alisisitiza kuwa ili kuhakikisha
kuwa wachimbaji wadogo wananufaika na sekta ya madini kupitia kujiajiri
mgodi huo ulichangia shilingi milioni 91.4 kwa kikundi cha wachimbaji
wadogo Tarime kwa ajili ya ununuzi wa mashine kwa ajili ya kusaga
kokoto.
Bi Mssumi aliongeza kuwa hatua
iliyofikiwa sasa ni mkandarasi kufanya kazi ya kutoa umeme kutoka mgodi
wa North Mara hadi mashine ilipo ili ianze kazi mara moja.
Alisema kuwa mgodi pia
ulifadhili miradi mbalimbali kwa gharama ya shilingi milioni 252.5
pamoja na vikundi vya kijamii/kidini kwa gharama ya shilingi bilioni 1.8
Akizungumzia mchango wa mgodi huo
katika sekta ya miundombinu Bi Mssumi alisema kuwa mgodi huo ulikarabati
barabara yenye urefu wa kilomita 47.9 kwa gharama ya shilingi milioni
469 pamoja na uunganishaji wa umeme kwa kushirikiana na Shirika la Umeme
Nchini (Tanesco) katika vijiji vya Kerende na Matongo kwa gharama ya
shilingi milioni 472
Alitaja miradi mingine kuwa ni
pamoja na ujenzi wa kituo cha polisi uliogharimu shilingi milioni 555.5
na ujenzi wa mahakama ya mwanzo Nyamongo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa
nyumba za wafanyakazi wa mahakama hiyo kwa shilingi milioni 182.9 mradi
ambao haujakamilika bado.
Akizungumzia changamoto katika
utekelezaji wa miradi hiyo, Bi. Mssumi alisema kuwa kumekuwepo na tatizo
la wanavijiji kuhujumu miundombinu ya maji iliyowekwa hali inayopelekea
mgodi huo kuingia gharama kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu hiyo.
“Wapo wanakijiji wasio waaminifu
ambao huharibu miundombinu ya maji kwa makusudi ili kufanya biashara ya
maji jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya vijiji hivyo”
Alisisitiza Bi. Mssumi.
MAJAMBAZI WATANORAIA WA BURUNDI WAUWAWA KIGOMA WAKUTWA NA MABOMU 3 SILAHA 2 RISASI 64
Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma Kamishina Msaidizi Japhari Muhamed akionyesha siraha walizokuwa nazo majambazi waliouwawa leo alfajiri. |
Mabomu, bunduki na vyakula vyenye nembo ya kutoka nchi ya Burundi walivyokutwa navyo majambazi |
Silaha walizokuwa nazo majambazi katika eneo la tukio Kigoma |
Na Magreth Magosso,Kigoma
Jeshi la
Polisi Mkoa wa Kigoma limefanikiwa kuyauwa Majambazi watano raia kutoka nchi ya Burundi leo(jana) alfajiri
katika Barabara Kuu ya Kasulu Kibondo eneo la pori la malagarasi wakiwa tayari
kuteka mabasi ya abiria mbalimbali yaendayo
mikoani.
Pia walikuta
mfuko wa salfeti uliokuwa na mabonu matatu ya kutupa kwa mkono,silaha za moto mbili moja aina ya AK 47 yenye namba
UA40501997,SMG namba 691220 ,magazine tatu pamoja na risasi 64.
Akifafanua
hilo jana ofisini kwake kigoma Ujiji Kamishna Msaidizi wa polisi Jaffari
Mohamed alisema Septemba ,3,mwaka huu saa 11.45 alfajiri askari polisi wakiwa wamejipanga katika eneo
la tukio hilo waliwakuta wakiandaa silaha zao tayari kufanya mashambulizi kwa
walengwa.
“tulibaini
njama hizo kutoka kwa wadau wetu,askari
walipofika eneo hilo walishuhudia harakati zao badae nao walibaini askari wetu na walianza kufyatua risasi bila
mpangilio mungu ni mwema tumeyauwa na
maiti zipo hospitali ya wilaya ya kasulu”alianisha Mohamed.
Alisema wananchi kwa kushirkiana na wajumbe wa vikao
vya kamati ndogo na kubwa za ulinzi hasa polisi jamii zimechangia kufanikisha
hayo ambapo hivi karibuni wilaya ya buhigwe majambazi watano raia wa nchi hiyo waliua
watu wanne na kujeruhi saba kwa kutupa bomu katika basi la abiria.
Kwa upande
wa Naibu kamishna idara ya uhamiaji wa hapa Ebrosy Mwanguku alibainisha
kuwa,changamoto ya matukio ya uhalifu katika mkoa huo ni kutokana na uhalisia
wa mipaka ambayo ina vipenyo vingi visivyo na vituo vya uhamiaji na askari
polisi hali inayochangia wahalifu kutoka huko kushambulia raia wa hapa.
Naye Mkuu wa
wilaya ya kasulu Danny Makanga alisema kupitia vikao vya ujirani mwema unaoshirikisha
nchi tatu ambazo zinapakana na kigoma(Drc Kongo,Burundi
) wahakikishe wanakusanya silaha zilizozagaa nchini kwao ili kuheshimu madhimio
12 yaliyoadhimiwa katika kikao cha Agost,15,mwaka huu.
Ubalozi
mdogo wa Burundi Johnbosco Ngayikengurukiye alipoulizwa kwa nini raia wa Burundi
hukutwa katika matukio yasiyorasmi hasa uhamiaji haramu na uhalifu akiri
changamoto hiyo inamumiza kichwa na kubainisha ukosefu wa ardhi na ajira chachu
ya hayo.
Jamboleo
limebaini bidhaa zilizokutwa katika kiroba cha majambazi hayo ni mikate iliyookwa
kiasili na juisi iliyosindikwa `Zaam Zam Orange'ambayo ni moja yakinywaji kiwanda cha Mona`s,ambavyo huvila pale wanapohisi njaa katika safari ya kuja hapa.
Hivyo changamoto ya mipaka mikubwa isiyokuwa na idara nyeti za ulinzi kuingia kinyemela usiku kwa usiku na kufanya
uhalifuambapo hitaji la vituo ni 14 ni chachu ya kuimarisha ulinzi lakini kwa sasa kigoma
ina vituo viwili tu venye huduma hiyo hali inayochangia majanga ya uhalifu
kushamiri kila kukicha.
Wednesday, September 3, 2014
UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU HAPA NCHINI UNAANZIA PALE MTU ANAPOKAMATWA NA VYOMBO VYA DOLA
SULEIMAN MSUYA
TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHGG) imesema asilimia kubwa ya ukiukwaji wa haki za binadamu hapa nchini unaanzia pale mtu anapokamatwa na vyombo vya dola kwenye mahojiano pamoja na mahabusu.
TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHGG) imesema asilimia kubwa ya ukiukwaji wa haki za binadamu hapa nchini unaanzia pale mtu anapokamatwa na vyombo vya dola kwenye mahojiano pamoja na mahabusu.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Huduma za Kisheria
(CHGG) Nabor Assey wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii leo
jijini Dar es Salaam.
Assey alisema utafiti unaonyesha kuwa wengi wao wanakamatwa
pasipo utaratibu, kudhalilishwa, kuteswa, kubambikiwa kesi, kuwekwa muda
mrefu bila kufikishwa mahakamani na kuwepo mazingira magumu ya dhamana
jambo linalokiuka haki za binadamu zilizoainishwa katika ibara ya12
mpaka 24 ya Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na sheria zingine za
nchi na mikataba ya kimataifa iliyoridhiwa.
Mkurugenzi huyo utafiti huo unaonyesha kuwa asilimia 50 ya watu
wanaoshikiliwa maeneo mbalimbali nchini ni mahabusu ambao ama
wanasubiri kufikishwa mahakani au kesi zao zinaendelea katika mahakama
mbalimbali bado hawajahukumiwa.
“Napenda kuweka wazi kuwa hii ni Idara huru ya Serikali
tunachokisema hapa ni katika juhudi za kusaidia serikali kutatua
changamoto ambazo zinaikabili jamii yake hasa katika masuala ya haki za
binadamu” alisema.
Assey alisema ni wazi kuwa vyombo vya dola hasa jeshi la polisi
limekuwa likishutumiwa kwa ukiukwaji wa haki za binadamu hali ambayo
inahitaji elimu zaidi ambayo inaweza kusaidia kutatua tatizo hilo.
Alisema ni vema dhana halisi ya jina la polisi (Police Force)
kubadishwa na kuwa (Police Service) ili kuwapatia uelewa kuwa wanapaswa
kutoa huduma na sio kutumia nguvu zaidi kama njia ya kukabiliana na
tatizo.
Mkurugenzi huyo alisema pia kuna mapungufu katika mfumo wa
sheria za jina za Tanzania akitolea mfano ibara ya 13(6) (e) ya Katiba
ya Tanzania ya 1977 inakataza utesaji kwa watuhumiwa na kuelekeza
mamlaka za nchi kutunga sheria kwa minajili hiyo.
Alisema bado kuna upungufu katika sheria kwani kifungu cha 29
cha sheria ya ushahidi sura ya 6 ya sheria za Tanzania kinakata
ushahidi uliopatikana kwa shinikizo la aina yoyote kutumika kama
ushahidi halali mbele ya mahakama.
Assey alisema pamoja na sheria hizo kuonyesha ukatazo bado
hazijaonyesha ni hatua gani atachukuliwa mtumishi yeyote ambaye
atabainika kufanya vitengo vinavyokiuka haki za binadamu.
Alisema Tume yao ipo katika mchakato wa kuhakikisha kuwa vyombo
vya usalama vinapatiwa elimu yakutosha juu ya nini majukumu yao pale
ambapo wanamshikilia mtu ambaye amefanya kosa.
Mkurugenzi huyo alisema jitihada hizo zinatakuwa zikishirikisha
wananchi hasa kwa kudai haki zao ambazo hazipo kisheria ambao
wanaonekana kuwa waathirika wakubwa kutokana na vyombo vya dola hasa
Jeshi la Polisi
Tuesday, September 2, 2014
NISHATI NA MADINI WAIMARISHA MKAKATI WA UTUNZAJI MAZINGIRA
Afisa
Mazingira kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Emmanuel Shija
akiwasilisha mada kuhusu ‘Uchimbaji mdogo wa Madini na Mazingira’ wakati
wa semina ya mafunzo kwa Maafisa Mazingira wa Wilaya kutoka Kanda ya
Ziwa. Semina hiyo ya siku nne inafanyika jijini Mwanza (Septemba 1-4,
2014) na imeandaliwa na Kitengo cha Mazingira cha Wizara husika.
Katibu
Mtendaji wa TAREA (Tanzania Renewable Energy Association) Tawi la Kanda
ya Ziwa, Bw. Jacob Ruhonyora akizungumzia uzoefu wake kuhusu faida za
matumizi ya nishati jadidifu,kwa Wajumbe wa semina ya mafunzo ya mambo
ya mazingira inayoendelea jijini Mwanza kuanzia Septemba 1, 2014. Semina
hiyo ya siku nne imeandaliwa na Kitengo cha Mazingira cha Wizara ya
Nshati na Madini.
Afisa
Misitu Mkuu kutoka Kitengo cha Mazingira – Wizara ya Nishati na Madini
(Kulia), Theodory Silinge akitoa ufafanuzi kuhusu umuhimu wa kuhimiza
jamii kutumia nishati mbadala wakati wa semina ya mafunzo kwa Maafisa
Mazingira wa Wilaya kutoka Kanda ya Ziwa, inayofanyika jijini Mwanza,
Septemba 1 – 4, 2014 Afisa
Sheria kutoka Wizara ya Nishati na Madini Renatus Damian, akiwasilisha
mada kuhusu masuala ya sheria katika utunzaji mazingira wakati wa semina
kwa Maafisa Mazingira wa Wilaya kutoka Kanda ya Ziwa, inayofanyika
jijini Mwanza Septemba 1 – 4, 2014.
Afisa
Mazingira kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Nassor Abdullatif
(Kushoto), akiwasilisha mada kuhusu umuhimu wa kufanya Tathmini ya
Mazingira (Environmental Impact Assessment – EIA) kabla ya kuanza
utekelezaji wa mradi wowote katika siku ya pili ya semina kwa Maafisa
Mazingira wa Wilaya kutoka Kanda ya Ziwa, inayofanyika jijini Mwanza
Septemba 1 – 4, 2014.
AMERICAN SENATORS VISIT SERENGETI NATIONAL PARK
Director
General of TANAPA Mr. Allan Kijazi (right) welcomes the Chairperson of
the US Senate Committee on Agriculture, Nutrition and Forestry and
Michigan Senator Ms. Debbie Stabenow during the arrival of the US
Senators delegation at Serengeti National Park.
A cheetah hunting in the bush of Serengeti
Five American Senators have
started a two days visit in Serengeti National Park as part of the
official program in the country. The delegation led by the Senator of
Michigan Ms. Debbie Stabenow who is also the Chairperson of the US
Senate Committee on Agriculture, Nutrition and Forestry will have an
opportunity to witness firsthand the vital role of conservation and good
natural resources management in promoting sustainable economic
development.
The US Senate delegation will also
specifically demonstrate the challenges of combating the Wildlife
Trafficking Crisis and methods for mitigation at the local, regional,
national and the international level.
While in Serengeti, the delegation
will visit sites of local conservation projects, view elephants and
rhinos in their natural habitats, meet with leaders on the front lines
in the war on poaching, and visit community projects that are working to
preserve their natural resources, including threatened species. They
will also learn about human-wildlife conflict and other issues of
importance to local people.
Other Senators in the delegation
includes Ms. Cantwell (Washington); Ms. Amy Klobuchar (Minnesota); Ms.
Heidi Heitkamp (North Dakota) and Ms. Maize Hirono (Hawaii).
LADY JAYDEE AUNGANA NA MARIE STOPES TANZANIA KWENYE KAMPENI YA UZAZI WA MPANGO
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Marie Stopes Tanzania (MST), Uller Muller (kulia)
akikabidhi kisanduku chenye vifaa vinavyohusika na masuala ya uzazi wa
mpango kwa Balozi mpya wa Marie Stopes ambaye pia ni msanii mkongwe wa
muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura ‘Lady jaydee’ katika hafla ya
utiaji sahihi makubaliano hayo katika ofisi za MST, jijiji Dar es
Salaam jana.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Lady
Jaydee, mwana muziki mashuhuri wa kizazi kipya nchini Tanzania, aliibua
shangwe na chereko kwenye hospitali ya uzazi Marie Stopes iliyopo
Mwenge, Dar es Salaam.
Uwepo
wa Jaydee ulitokana na kuungana kwa nyota huyu na Marie Stopes kwenye
kampeni ya “Chagua Maisha” ambayo inalenga kuboresha upatikanaji wa
huduma za uzazi wa mpango katika jamii.
Akiongea
na waandishi wa habari punde baada ya mazungumzo na Mkurugenzi
Msimamizi wa MST nchini Tanzania, Bi Uller Muller, Lady Jaydee
aliwaambia waandishi : “Nina furaha kubwa kuchukuka nafasi hii ya
kipekee kama Balozi wa Marie Stopes kwa sababu wanafanya mengi
kuwawezesha wakina mama kusimama na kujitegemea.
Lengo
kuu la Kampeni hii ya Chagua Maisha nikuhakikisha kila Mtanzania ana
haki ya kuchagua mfumo wa uzazi wa mpango ili kulinda afya zao na
kutimiza malengo yao ya kimaisha, hususan mabinti wadogo”.
Akitafakari
sababu zilizompeleka kuungana na kampeni hii, Lady Jaydee alieleza:
“siku zote nilikuwa naamini kuwa wanawake wana uwezo wa kubadilisha
Tanzania kimaendeleo. Hivyo niliumizwa moyo sana nilipoambiwa hivi leo
kuwa Wanawake wengi hupoteza maisha, na wasichana wengi wanalazimishwa
kuacha masomo kutoka na ujauzito.
Mimi nimeamua kusaidiana na Marie
Stopes kuelimisha jamii nzima wanaweza kubalili fikra na hatima zao, kwa
kutumia uzazi wa mpango”.
Continue reading →RAIS KIKWETE AFUNGUA RASMI NYUMBA ZA MAKAZI ZA MEDELI LEO HII
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembelea mradi wa nyumba za makazi za Medeli zilizopo Mjini Dodoma wenye nyumba 150, kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Rehema Nchimbi (wa kwanza kushoto) Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NHC, Zakhia Meghji na Naibu Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Simbachawene. Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe na Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Christopher Kangoye. (Picha zote kwa hisani ya Shirika la Nyumba la Taifa)
Rais Jakaya Kikwete akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa mradi wa nyumba za makazi za Medeli zilizopo Mjini Dodoma wengine wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC, Nehemia Mchechu, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NHC, Zakhia Meghji.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembelea mradi wa nyumba za makazi za Medeli zilizopo Mjini Dodoma wenye nyumba 150, kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NHC, Zakhia Meghji na Naibu Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Simbachawene. Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe na Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Christopher Kangoye. Majengo ya Nyumba za Makazi za Medeli Mjini Dodoma kama yanavyoonekana pichani. Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NHC, Zakhia Meghji huku Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Christopher Kangoye na Naibu Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Simbachawene wakishuhudia wakati wa ufunguzi rasmi wa mradi wa nyumba za makazi za Medeli zilizopo Mjini Dodoma. Mradi una jumla ya nyumba 150. (Picha zote kwa hisani ya Shirika la Nyumba la Taifa) Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Meneja wa NHC katika Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu, Bulla Boma wakati wa ufunguzi rasmi wa mradi wa nyumba za makazi za Medeli zilizopo Mjini Dodoma. Rais Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na Watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mara baada ya ufunguzi rasmi wa mradi wa nyumba za makazi za Medeli zilizopo Mjini Dodoma.
STAR WA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) 2014, MWANAAFA MWINZAGO AWA KIVUTIO MITAA YA KARIAKOO
Mshindi wa Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 Mwanaafa Mwinzago (Katikati) akisindikizwa na Matron pamoja na Mfanyakazi wa TMT huku akilindwa na Mabaunsa wakati alipopelekwa Katika Mitaa ya Kariakoo kwaajili ya kununua zawadi Kwaajili ya Wazazi wake.
Mfanyakazi wa TMT, Happy Ngatunga (Kushoto) akitoa maelekezo kwa Mabaunsa na Mshindi wa TMT aliyejinyakulia Kitita Cha Shilingi milioni 50 katika fainali ya Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Mlimani City Mwanaafa Mwinzago wakati walipokuwa katika matembezi Kariakoo.
Baadhi ya wafanyabiashara wa Kariakoo wakimpungia Mikono kama ishara ya kumpongeza kwa kuibuka mshindi wa fainali ya Tanzania Movie Talents (TMT) Star wa TMT 2014 kutoka Mtwara, Mwanaafa Mwinzago Wakati alipokatiza kwenye mitaa ya Kariakoo pindi alipokwenda kununua zawadi kwaajili ya wazazi wake
Star Wa TMT 2014, Mwanaafa Mwinzago (katikati) akiwa na furaha mara baada ya kupongezwa na mashabiki waliopata nafasi ya Kumsalimia na kumpongeza wakati akikatiza mitaa ya Kariakoo pindi alipokwenda kununua Zawadi kwaajili ya Wazazi wake
Wanafunzi wa Shule ya Msingi wakimpongeza Star Wa TMT 2014, Mwanaafa Mwinzago kwa kuweza kuibuka mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 kwa kuwabwaga mwenzake 9 na kuondoka na Kitita Cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania wakati walipomuona katika moja ya mitaa ya Kariakoo wakati Star Huyo wa TMT 2014 alipokwenda Kununua Zawadi kwaajili ya kuwapatia wazazi wake ikiwa kama ishara ya Upendo na shukrani kwao.
Matron wa Kambi ya TMT 2014, Kemmy akichagua baadhi ya vitenge kwa Niaba ya Star Wa TMT 2014 Mwanaafa Mwinzago wakati alipopelekwa Kariakoo kwaajili ya Kununua Vitenge kama zawadi kwa wazazi wake.
SIDO KUZINDUA MRADI WA MCHIKICHI
SHIRIKA la
kuhudumia viwanda vidogovidogo Mkoa wa Kigoma (Sido) watazindua Mradi wa Local Investment Climate ifikapo
mosi, Octoba mwaka huu ,ukiwa na lengo la
kuboresha mazingira ya uchakataji wa bidhaa za
wajasiliamali hasa zao la Mchikichi.
Akielezea
hilo jana kwenye kufunga maonyesho ya wajasiliamali Kanda ya kati ambapo mwaka huu yamefanyika kigoma ujiji Meneja wa Sido wa hapa Mackdonald Maganga alisema,mradi utaanza na zao moja muhimu katika
mkoa na kulifanyia utafiti wa kina.
Pia watajenga
kiwanda kidogo cha usindikaji wa zao husika,ambapo kwa hapa zao la mchikichi
litapewa kipaumbele katika mradi mtambukwa kwa lengo la kuboresha zao hilo na
kuteka soko nchi za Afrika Mashariki.
“mchikichi zao
kuu na asili , kwenye maonyesho hayakuwepo
mafuta ya mawese unajua kwa nini kutokana
na mazingira ya uandaaji wa mafuta hayo ni duni , ukiona wanavyofanya huwezi
kuyatumia ,ingawa mawese yanafaida mwilini” alibainisha Maganga.
Mradi huo
unasimamiwa na shirika la Danida ambapo
watatumia shamba darasa kwa walengwa
wachache wenye vigezo, ili kulinyanyua zao hilo kutoka kwenye kiwango duni hadi
ubora wa kimataifa .
Alisema mashirika
ya usajili (Brela) ubora wa bidhaa na chakula (Tfda),(Tbs waweke ofisi kigoma
ili kupunguza umbali na urasimu katika utendaji kazi kwa wadau na
kutoa wito kwa umma watumie fursa zilizopo kujikwamua na umaskini.
Kwa upande
wa Meneja wa Mfuko wa hifadhi wa Nssf Josephat Komba alisema wajasiliamali wa wilaya ya kigoma wanakabiliwa
na bidhaa duni walizonazo ukilinganisha na wilaya ya kasulu na mikoa mingine.
Alisema jamii
itumie fursa za Asasi za kifedha ili
kupanua wigo wa ubunifu,elimu ili
kuhodhi soko la mipakani hasa nchi jirani na kuongeza ajira kwa wakazi ambapo kwa mwaka
2014 januari -agust wamekopesha bilioni 4 kwa vikundi Vinne kikiwemo cha wakulima.
Monday, September 1, 2014
NAIBU IGP AKUTAKA NA MAKAMISHINA WA POLISI KUTOKA NAMIBIA
Naibu
Inspekta Jenerali wa Polisi,Abdulrahman Kaniki akimkabidhi zawadi
Kamishna wa Polisi wa Namibia Bw.Schalk Meuwesen ofisini kwake
jana.Kamishna huyo yupo nchini kwa ziara ya siku tatu akiwa na maafisa
wengine kutoka Namibia kujifunza jinsi Jeshi la Polisi Tanzania
lilivyofanikiwa katika kutekeleza Maboresho yake.(Picha na Frank Geofray
wa Jeshi la Polisi).
Naibu
Inspekta Jenerali wa Polisi,Abdulrahman Kaniki akimfafanulia namna
maboresho ya Polisi yalivyoanza Kamishna wa Polisi wa Namibia Bw.Schalk
Meuwesen ofisini kwake jana.Kamishna huyo yupo nchini kwa ziara ya siku
tatu akiwa na maafisa wengine kutoka Namibia kujifunza jinsi Jeshi la
Polisi Tanzania lilivyofanikiwa katika kutekeleza Maboresho yake.(Picha
na Frank Geofray wa Jeshi la Polisi).
Naibu
Inspekta Jenerali wa Polisi,Abdulrahman Kaniki akiwafafanulia namna
maboresho ya Polisi yalivyoanza Makamishna wa Polisi kutoka Jeshi la
Polisi la nchini Namibia Bw.Schalk Meuwesen na Bw.Abed Kashihakumwa
ofisini kwake jana.makamishna hao pamoja maafisa wengine wapo nchini kwa
ziara ya siku tatu kujifunza jinsi Jeshi la Polisi Tanzania
lilivyofanikiwa katika kutekeleza Maboresho yake.(Picha na Frank Geofray
wa Jeshi la Polisi).
CHADEMA TABORA WAPATA MWENYEKITI MPYA
Na Allan Ntana, Tabora
CHAMA
Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Tabora kimepata safu mpya
ya uongozi baada ya kufanya uchaguzi wake mkuu katika ngazi ya mkoa hapo
jana katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Ualimu Tabora.
Katika
mkutano huo wa uchaguzi nafasi zilizokuwa zinagombewa ni Mwenyekiti wa
CHADEMA Mkoa na Katibu wa Mkoa na Mwenyekiti na Katibu wa Baraza la
Vijana Chadema (BAVICHA), Baraza la Wanawake (BAWACHA) na Baraza la
Wazee.
Aliyeibuka
kidedea katika nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Tabora ni Bw.
Francis William Msyuka aliyepata kura 46 na kumshinda mgombea mwenzake
Bw.Hassan Said aliyepata kura 17 kati ya kura zote 66 zilizopigwa huku
kura 3 zikiharibika.
Na
aliyeibuka kidedea katika nafasi ya Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Tabora ni
Bw.Alinanuswe Mwakilima ambaye alipigiwa kura za ndio 57 na hapana 2
kati ya kura zote 61 baada ya kukosa mpinzani katika wajumbe wote
waliohudhuria mkutano huo.
Waliochaguliwa
kuongoza mabaraza ya chama hicho katika ngazi ya mkoa ni, BAVICHA,
Mwenyekiti ni Lazaro Damson na Katibu wake ni Daud Ndelwa, BAWACHA
Mwenyekiti ni Sada Kabezi na Katibu wake ni Anna Nyawacha na Baraza la
WAZEE Mwenyekiti ni Joseph Tanganyika na Katibu wake ni Vicent Ndeuka.
Msimamizi
wa Uchaguzi huo Christopher Nyamwanji ambaye ni Mratibu wa chama hicho
Kanda ya Magharibi aliwapongeza wajumbe wote waliohudhuria mkutano huo
kwa kufanikisha zoezi hilo la kikatiba ndani ya chama kwa utulivu na
amani huku akiwataka kukitumika chama hicho kwa moyo mmoja pasipo
kuruhusu roho za usaliti kama walivyofanya viongozi waliokuwepo.
Naye
diwani wa kata ya Bukene wilaya ya Nzega Omar Shehe kupitia chama hicho
ambaye alikuwa Mwenyekiti wa mkutano huo wa Uchaguzi aliwataka viongozi
hao kudumisha amani, mshikamano na uzalendo ndani ya chama hicho na
kujiepusha na makundi ili kuwaunganisha vizuri wanachama katika mkoa huo
hasa ikizingatiwa kuwa uchaguzi mkuu hauko mbali sana huku akiwaasa
kutogopa changamoto za hapa na pale.
Akitoa
shukrani zake Mwenyekiti mpya wa chama hicho Mkoa wa Tabora Francis
William Msyuka alisema kazi kubwa iliyoko mbele yake ni kutengeneza
mshikamano mzuri kwa viongozi wote na wanachama wa chama hicho kuanzia
ngazi ya shina, wilaya, jimbo na mkoa na kuhamasisha maendeleo katika
kila eneo husika sambamba na kukutana na wananchi ili kusikiliza kero
zao.