Pages

KAPIPI TV

Tuesday, July 21, 2015

KAMANDA WA POLISI MKOA WA PWANI JAFARI IBRAHIMU AZUNGUMZIA JUU YA SILAHA ZILIZOKAMATWA


ki1
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishina mwandamizi Jafari Ibrahimu akifafanua jambo kwa waandishi wa habari ofisini kwake kuhusina na watuumiwa wa ujamabzi waliokamatwa pamoja na siraha ambazo wamezikamata baada ya kufanya operesheni katika mapori(Picha na Victor Masangu)
ki2
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishina mwandamizi Jafari Ibrahimu akifafanua jambo kwa waandishi wa habari ofisini kwake kuhusina na watuumiwa wa ujamabzi waliokamatwa pamoja na siraha ambazo wamezikamata baada ya kufanya operesheni katika mapori(Picha na Victor Masangu)
………………………………………………….
VICTOR MASANGU, PWANI
 
KUFUATIA kukithiri kwa wimbi la matukio ya uharifu pamoja na kuvamia vituo vya polisi  Jeshi la polisi Mkoa wa Pwani  limefanya msako mkali katika mapori mbali mbali  na  kufanikiwa kuwanasa watuhumiwa  wa ujambazi  27 pamoja na   risasi 153,bunduki 2  mabomu 3  ambavyo  walikuwa wakivitumia katika matukio ya uharifu.
 
Akizungumza na wa waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishina mwandamizi Jafari Ibrahimu amesema kwamba watuhumiwa hao wamekamatwa baada ya kufanyika operesheni katika magenge yaliyopo vichakani na kuwakuta watuhumiwa hao wakiwa wamejificha.
 
 Kamanda amesema kwamba  wameamua kufanya  operesheni  hiyo  kutokana na kuongezeka kwa uharifu katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Pwani na kuwakamata watuhumiwa hao  ambao wengine walikutwa na vifaa mbali mbali ikiwemo visu mapanga,pamoja na nyaya tatu za milipuko ya mabomu.
 
Aidha Kamanda huyo amebainisha kwamba katika zoezi hilo pia waliweza  kukamata madawa ya kulevya aina aya bangi gunia 18 na mirungi kilo 124,lita 88 za pombe ya moshi pamoja na mitambo yake mitatu ya kutengenezea noti bandia 370 na meno ya tembo.
 
 Katika hatua nyingine Kamanda huyo amesema kwamba wanafunzi wawili  wa familia moja katika shule ya msingi mgogodo  iliyopo Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani wamepoteza maisha  baada ya chumba chao walichokuwa wamelala kuteketea kwa moto na kwamba chanzo cha moto huo ni kibatali.
 
 Mkoa wa pwani umekuwa na matukio ya uharifu mbali mbali ikiwemo kuvamiwa kwa vituo vya polisi ikiwemo kituo cha  Kimazichana Wilayani mkuranga ,Ikiwiriri ,kituo kidogo cha mloka,pamoja na tukio la kufanya  jaribio la kutaka kuvamia kituo cha polisi Kibiti vyote vilivyopo Wilayani Rufiji.

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA LASAIDIA MASHINE KWA VIJANA WALIOACHA KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA


 Vijana walioacha kutumia dawa za kulevya katika eneo la Kigogo Luhanga, Jijini Dar es Salaam  wakishangilia baada ya Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC, Bw. Muungano Saguya alipokabidhi msaada wa mashine tatu za kufyatulia matofali kwa Mlezi wao, Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Mashariki na Pwani Luhanga, Rev. Richard Hananje anayelea  takribani vijana 150 hivi. Shirika limetoa msaada wa mashine hizo tatu za kufyatulia matofali ya kufungamana zenye thamani ya shilingi milioni moja na nusu kwa vijana hao na mtaji  ili waweze kujishughulisha na kazi za kujiongezea kipato na kusahau utumiaji wa madawa ya kulevya.

Vijana walioacha kutumia dawa za kulevya katika eneo la Kigogo Luhanga Jijini Dar es Salaam  wakishangilia kwa pamoja na Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC, Bw. Muungano Saguya na Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Mashariki na Pwani Luhanga, Richard Hananje ambaye ni Mlezi wa kikundi hicho chenye vijana takribani 150 hivi. Shirika limetoa msaada wa mashine ili kuunga mkono juhudi za Kituo hicho za kuokoa maisha ya vijana wanaojihusisha na madawa ya kulevya. 
 Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa, Bw. Muungano Saguya akikabidhiana mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana na Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Mashariki na Pwani Luhanga, Richard Hananje  kwa ajili ya kuwapatia vijana walioacha kutumia dawa za kulevya katika eneo la Kigogo Luhanga Jijini Dar es Salaam. Shirika hilo limetoa msaada wa mashine hizo za kufyatulia matofali ya kufungamana kwa vijana hao ili waweze kujishughulisha na kazi za kujiongezea kipato.
Afisa Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa, Edith Nguruwe akijadiliana jambo na baadhi ya vijana walioacha kutumia dawa za kulevya katika eneo la Kigogo Luhanga Jijini Dar es Salaam, baada ya Shirika hilo kutoa msaada wa mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana kwa vijana hao ili waweze kujishughulisha na kazi za kujiongezea kipato.
Vijana walioacha kutumia dawa za kulevya katika eneo la Kigogo Luhanga Jijini Dar es Salaam wakimsikiliza Meneja wa Huduma kwa Jamii, Muungano Saguya (hayupo Pichani) baada ya Shirika hilo kutoa msaada wa mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana kwa vijana hao ili waweze kujishughulisha na kazi za kujiongezea kipato.
Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa, Muungano Saguya akizungumza na vijana walioacha kutumia dawa za kulevya katika eneo la Kigogo Luhanga Jijini Dar es Salaam, baada ya Shirika hilo kutoa msaada wa mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana kwa vijana hao ili waweze kujishughulisha na kazi za kujiongezea kipato.
  Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa, Muungano Saguya akizungumza na vijana walioacha kutumia dawa za kulevya katika eneo la Kigogo Luhanga Jijini Dar es Salaam, baada ya Shirika hilo kutoa msaada wa mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana kwa vijana hao ili waweze kujishughulisha na kazi za kujiongezea kipato.
Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa, Muungano Saguya akijadiliana jambo na mmoja wa vijana waathirika wa madawa ya kulevya ambao wamebadilika kabisa tabia na sasa wanafanya shughuli mbalimbali za kujipatia kipato.
  Vijana walioacha kutumia dawa za kulevya katika eneo la Kigogo Luhanga Jijini Dar es Salaam wakimsikiliza Meneja wa Huduma kwa Jamii, Muungano Saguya  baada ya Shirika hilo kutoa msaada wa mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana kwa vijana hao ili waweze kujishughulisha na kazi za kujiongezea kipato.
  Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa, Muungano Saguya akizungumza na vijana walioacha kutumia dawa za kulevya katika eneo la Kigogo Luhanga Jijini Dar es Salaam, baada ya Shirika hilo kutoa msaada wa mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana kwa vijana hao ili waweze kujishughulisha na kazi za kujiongezea kipato.
  Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa, Muungano Saguya akimkabidhi kiasi cha pesa kwa Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Mashariki na Pwani Luhanga, Richard Hananje kwaajili ya kuwasaidia vijana walioacha kutumia dawa za kulevya katika eneo la Kigogo Luhanga Jijini Dar es Salaam, baada ya Shirika hilo kutoa msaada wa mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana kwa vijana hao ili waweze kujishughulisha na kazi za kujiongezea kipato.
 Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Mashariki na Pwani Luhanga, Richard Hananje akizungumza na vijana walioacha kutumia dawa za kulevya katika eneo la Kigogo Luhanga Jijini Dar es Salaam, baada ya Shirika hilo kutoa msaada wa mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana kwa vijana hao ili waweze kujishughulisha na kazi za kujiongezea kipato.
Afisa Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa, Edith Nguruwe akijadiliana jambo na baadhi ya vijana walioacha kutumia dawa za kulevya katika eneo la Kigogo Luhanga Jijini Dar es Salaam, baada ya Shirika hilo kutoa msaada wa mashine za kufyatulia matofali ya kufungamana kwa vijana hao ili waweze kujishughulisha na kazi za kujiongezea kipato.

"MKUFYA ATANGAZA NIA YA UBUNGE JIMBO LA TABORA MJINI KUPITIA CHADEMA"


WARSHA YA KUPUNGUZA VIFO NA MAJERUHI WA AJALI ZA BARABARANI YAFANYIKA JIJINI DAR-ES-SALAAM

????????????????????????????????????
Kamishina Msaidizi wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Johansen Kahatano akifungua rasmi warsha ya waandishi wa habari ya kupunguza ajali na vifo vinavyotokana na ajali za barabarani iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la AMEND na kufadhiliwa na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya EU warsha hiyo imefanyika kwenye jengo la Umoja House jijini Dar es salaam.
????????????????????????????????????
Gianluca Azzon Mwakilishi wa EU Nchini Tanzania akiwasilisha mada katika warsha ya waandishi wa habari ya kupunguza ajali na vifo vinavyotokana na ajali za barabarani iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la AMEND na kufadhiliwa na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya EU warsha hiyo imefanyika kwenye jengo la Umoja House jijini Dar es salaam.
????????????????????????????????????
Tom Bishop kutoka shirika lisilo la Kiserikali la AMEND akiwasilisha mada katika warsha ya waandishi wa habari ya kupunguza ajali na vifo vinavyotokana na ajali za barabarani iliyoandaliwa na shirika hilo na kufadhiliwa na Jumuiya ya umoja wa Ulaya EU warsha hiyo imefanyika kwenye jengo la Umoja House jijini Dar es salaam.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wataalamu na taasisi mbalimbali za serikali, Umoja wa Ulaya na Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na waandishi wa habari wakifuatilia mada mbalimbali katika warsha hiyo.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wataalamu na taasisi mbalimbali za serikali, Umoja wa Ulaya na Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na waandishi wa habari wakifuatilia mada mbalimbali katika warsha hiyo.
????????????????????????????????????
Kamishina Msaidizi wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Johansen Kahatano akimkabidhi cheti cha ushiriki wa warsha hiyo Mkurugenzi wa mtandao wa Fullshangweblog Bw. John Bukuku.
????????????????????????????????????
Kamishina Msaidizi wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Johansen Kahatano akimkabidhi cheti cha ushiriki wa warsha hiyo Kibuda Chalila Mwandishi mwandamizi wa Michuzi Media.
????????????????????????????????????
Kamishina Msaidizi wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Johansen Kahatano akimkabidhi cheti cha ushiriki wa warsha hiyo Mwandishi wa habari wa magazeti ya serikali TSN Bi. Regina Kumba.
????????????????????????????????????
Washiriki wa Warsha hiyo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika warsha hiyo
????????????????????????????????????
Na Mwandishi Wetu
Imeelezwa kuwa suala la usalama barabarani ni ni jukumu la kikosi cha usalama barabarani hali ambayo jamii imejengeka na utamaduni huo na kusahau suala hilo ni jamii nzima katika mapambano ya kupunguza ajali za barabarani.

Hayo ameyasema leo Kamishina Msaidizi wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Johansen Kahatano wakati wa mafunzo kwa waandishi habari juu ya kuhabarisha jamii katika suala la usalama barabarani iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU)
Kahatano amesema kuwa kikosi cha usalama barabarani kimekuwa kikitoa elimu juu ya usalama barabarani kwa wananchi pamoja na madereva katika kuzingatia sheria zilizowekwa katika kuondokana na ajali zinazotokana na makosa ya kibinadamu.

Amesema jamii ikipata mwamko wa katika kutambua sheria za usalama barabarani kuna uwezekano wa kuondokana na ajali ambazo zinapoteza watu pamoja na kuacha watu wengine wakiwa na ulemavu wa kudumu.

“Kikosi cha usalama barabani pekee yake hakiwezi ni wakati umefika kwa jamii kuweka suala hili kwenye vichwa vyao kuwa wanamchango katika wa kusukuma gurudumu katika kupambana na ajali katika sehemu zao”amesema Kahatano.

Katika kuhamasisha masuala ya Usalama Barabarani ,Mwandishi wa Citizeni Mkinga Mkinga amesema ni wakati umefika kwa waandishi kutambua umuhimu wetu wa kutoa taarifa za kuelimisha wananchi juu ya usalama barabarani.

Umoja wa Ulaya utaendelea kushirikiana na Tanzania katika mradi wa uboreshaji wa miundombinu katika mashule ili kuweza kuondokana na ajali za wanafunzi katika maeneo ya karibu na barabara.

"LEMBELI AITOSA CCM,AJIUNGA RASMI CHADEMA"


Aliyekuwa Mbunge wa Kahama kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), James David Lembeli (kushoto) akiingia ukumbi wa Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Dar es Salaam leo asubuhi akiwa ameongozana na mtoto wake, Wizilya Lembeli wakati akienda kutangaza kuondoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kahama mkoani Shinyanga, James David Lembeli, akizungumza na waandishi wa habari Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Dar es Salaam leo asubuhi wakati akitangaza kuondoka katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Pamoja na kutangaza nia ya kugombea ubunge kupitia chama hicho.
 Lembeli akizungumza na wanahabari.
 Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
 Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.

Wanahabari wakimsikiliza Lembeli. Suleiman Msuya

Na Mwandishi Wetu

ALIYEKUWA Mbunge wa Kahama James Lembeli, amehamia rasmi Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akitokea Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Tukio hilo la kuhama lilifanyika jijini Dar es Salaam leo asubuhi katika Hoteli ya Blue Pearl, Ubungo Plaza ambapo aliambatana na mwanae ambaye alijitambulisha kwa jina Wizilya James.

Akizungumzia uamuzi wake huo Lembeli alisema amekuwa ndani ya CCM kwa miaka yake yote lakini kutokana na vitendo vinavyofanyika ndani ya chama hicho ameaona akae pembeni.

Lembeli alisema, ndani ya CCM ili ufanikiwe kupita michakato yote sahihi ni lazima utoe rushwa au kuiba kura jambo ambalo yeye analipiga vita hivyo kutofautiana na viongozi wa chama ngazi ya Wilaya.

"Ndani ya CCM rushwa imekuwa ibada inasumu kali kuliko ukimwi hivyo nimeshindwa kuvumilia naona Chadema wana viashiria vinavyofanana na mimi ngoja tukafanye kazi," alisema Lembeli.

Alisema katika harakati za kupata wagombea katika jimbo la Kahama kila mwaka ni lazima rushwa itumike lakini chama kimekuwa kimya na kuwabeba wale watoa rushwa.

Mbunge huyo alisema ushahidi wa watu kutoa rushwa hasa katika kipindi hiki umeonekana lakini wahusika wameendelea na hatua zingine bila kukemewa.

"Mimi mwaka 2010 nilikuwa nimekatwa lakini huruma ya Rais Jakaya Kikwete nilirejeshwa sasa nimeona hakuna sababu ya kuendelea kulazimisha kama viongozi hawakutaki," alisema.

Alisema iwapo angechukua fomu CCM mkakati ambao ulikuwepo ni kumkata kwa kile ambacho wanaamini kuwa amekuwa akisimamia misimamo ambayo ina madhara kwa Serikali.

Lembele alisema kutokana na dhana hiyo ni vema aende katika chama ambacho kinaonekana kuwa wabunge wake wanauchungu na nchi yao na sio kubebana kusiko na sababu.

"Kufanya kosa sio kosa lakini kurudia kosa ni kosa kubwa sana hivyo siwezi kurudia kosa la 2010 hivyo huku Chadema ndiko sahihi," alisema.

Alisema ukiona mwenzako ananyolewa ni vema kujiandaa kwa kutia maji nywele jambo ambalo ameliona na ameamua kufanya hivyo.

"Siwezi kutoa rushwa kwa sababu sijafunzwa hivyo na hata wananchi wa Kahama wanajua kuwa mimi sio mtoa rushwa hivyo ukiwa hutoi rushwa CCM ni ngumu kukubalika jambo ambalo linafanya kuwa rushwa iwe mbaya kuliko ukimwi," aliongezea.

Akizungumzia kugombea ubunge kupitia Chadema, alisema atafanya hivyo kwani ukweli ni kuwa anakubalika kwa wananchi wote kutokana na misingi yake ya utumishi.

Alisema mpaka anafanya uamuzi huo ameshafanya utafiti ambapo anaamini kuwa atashinda tena kwa kishindo kwani wananchi wa jimbo hilo wanamkubali.

Lembeli alisema kimsingi jimbo la Kahama wapinzani wapo tangu yeye akiwa Mbunge, hivyo anaamini kuwa iwapo atafanikiwa kushinda hatapata wakati mgumu kufanya kazi.

"CCM imefanya mambo mengi ambayo kimsingi hayana afya ndani ya chama ukiwa wa kwanza kwa kura ndani ya CCM unakuwa wa mwisho hali ambayo inakatisha tamaa na hilo lilitokea 2010 na Chadema wakapata ushindi," alisema

Pia alisema amepokea simu na meseji nyingi ambazo kutoka kwa wananchi zinamtaka agombee kupitia chama Chadema hivyo pamoja na ukweli kuwa ni uamuzi mgumu ila hawezi kula matapishi.

Alisema ilimchukua masaa 10 kumuelezea mama yake juu ya uamuzi huo lakini baadae alielewa hivyo kwa sasa ana baraka zote za mama na familia kwa ujumla.

Kuhusu uhusiano na 4U Movement

Akizungumzia kuhusu uamuzi huo kuhusishwa na kundi la 4u Movement, alisema kimsingi kundi hilo analiona kupitia mitandoa ya kijamii ila hana uhusiano nalo na hahitaji kuwa katika hao.

Lembeli alisema wananchi wa Kahama ni watu makini wanajua nini cha kufanya hivyo uamuzi ambao watafanya utakuwa ni kwa uelewa wao na sio kwa msukumo wa kundi hilo linalotajwa kuwa ni wafuasi wa Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa.

Kuhusu Katiba iliyopendekezwa Lembeli alisema yeye ni muumini wa Serikali tatu na alionesha hilo katika vikoa vyote vya bunge lile ambapo alikuwa katika kamati namba moja.

Alisema kutokana na ukweli huo ni dhahiri kuwa ameenda chama ambacho wanafanana kifra kwani bila Serikali tatu hatma ya Tanzania itakuwa mashakani.

"Kwa hili siwezi kubadilika mimi msimamo wangu hadi leo ni Serikali tatu ambapo pia ni msimamo wa Chadema hivyo wengi ndio walishinda lakini mimi sio mmojawapo," alisema.

Aidha Lembeli alitumia muda huo kufafanua ni kwanini alitoa hoja ya kutaka Lowassa na wengine ambao wamekutana na majanga ndani ya bunge wasafishwe ambapo alisema haki haikutendeka kusafisha watu baadhi na wengine kuachwa.

Lembeli alisema katika taarifa ya Operasheni Tokomeza haikusema mawaziri fulani wanamakosa ila iliweka bayana kuwa kulinga na nafasi zao wanapaswa kuwajibika kisiasa.

Alisema mfumo wa kusafisha watu fulani na wengine kuwaacha sio mzuri kwani hauendani na misingi ya haki za binadamu ni ubaguzi.


Kwa upande wa mtoto wake wa pili Wizilya James Lembeli alisema wanamuunga mkono baba yao kwa uamuzi huo na kuwa wako nyuma yake.

Alisema uamuzi ambao amechukua baba yake ni mgumu hasa ukilinganisha na kipindi husika lakini hakuwa na njia nyingine kwani ni mtu wa siasa.

Akizungumzia ujio huo Ofisa Habari wa Chadema ambaye ndiye alimpokea Lembeli alisema kimsingi mwanachama huyo mpya alikiwa ni mpinzani kiroho hivyo hawana shaka naye.

Makene alisema wanaamini kuwa wamepata mtu ambaye anapenda mabadiliko kwani alionekana ndani ya bunge na nje kwa kusimamia rasilimali za nchi bila uoga.

Alisema Chadema itaendelea kupokea wanachama wapya kutoa CCM na vyama vingine hadi Julai 25 kwani lengo lao ni kuhakikisha kuwa nchi inafikia kwenye mabadiliko chanya.

Lembeli amekuwa Mbunge wa jimbo la Kahama, tangu mwaka 2005 hadi 2015 ambapo awali alikuwa  mwandishi na mtumishi katika shirika la Hifashi ya Taifa (Tanapa).

NEW MUSIC VIDEO : EMANUEL AUSTIN FEAT. BEN POL -RUKA JUU


MFAHAMU EMANUEL AUSTIN MTANZANIA MWANAMUZIKI AISHIYE UJERUMANI.

Emanuel  Austin alizaliwa 27.10.1990 Jijini Dar es salaam Tanzania, na ilipofika mwaka 1996  alihamia Ujerumani Kuishi na wazazi wake, Kipaji chake cha kucheza na kuimba kilianza kuonekana mapema.
Akiwa na Miaka mitano Emanuel Austin alianza kuigiza kama anacheza movie pamoja na rafiki zake wa Kiafrika akiwemo Gregory Msuya na Michael Jackson.  Alipofika umri wa Miaka 15 alianza kupenda na kuimba muziki wa Kugani yani ‘Hip hop’
Baadaye alitafuta baadhi ya wenzake ambao aliona wanaweza kuingia studio na kufanya muziki wa Kughani yaani Rap baadhi ya marafiki zake walikuwa ni pamoja na Miguel Amil Matos, Bernado Ernest na Patrick Kitchens ambapo kwa Mara ya kwanza walifanya vizuri.
Mnamo mwaka 2002 wazazi wake na Emanuel walianzisha Mradi mkubwa wa shule kwa ajili ya kufundisha Salsa huko Großkrotzenburg  jirani na  Frankfurt , ambapo yeye binafsi alijifunza Salsa na sasa amekuwa ni mwalimu mzuri wa Mtindo huo. Na kuanzia mwaka 2005 Emanuel  na baba yake wamekuwa wakiendesha programu ya kuwafundisha watoto salsa.
Kipaji cha nyota Mwanamuziki Emanuel Austin kilianza kuonekana wakati ameanza kuimba Lebo ya MarciRecords moja ya sehemu ambayo inawaunganisha wanamuziki mbalimbali na vijana ambao wanavipaji katika sanaa ya Muziki, akiwa huko Emanuel alishinda tuzo ya Msanii anayechipukia ndani ya Mji wa Hanau, Ujerumani  mwaka 2006.
Mwaka 2007 Emanuel alifanya video yake ya kwanza kupitia wimbo wake wa Put your hands up wimbo uliotoka katika album yake ya Put your Hands up, Album hiyo ilitengenezwa na Muandaaji wa Muziki Dj Verde.
Mwaka 2008 Emanuel alifanya ngoma nyengine ambapo alitoa audio pamoja na video , ngoma hiyo ilikwenda kwa jina la Master of the Game, chini ya usimamizi wa mwandaaji wa Muziki Axel Breitung hii ilikuwa ni nyimbo ambayo ilimuongezea umaarufu zaidi na kusikika katika chanel maarufu za Televisheni kama VIVA na MTV.
Kutokana na mafanikio hayo makubwa Emanuel alianza kuandaa matukio mbalimbali ikiwa ni pamoja na matamasha ya muziki , Mwaka 2008 Emanuel aliamua kufungua darasa la mafunzo ambapo ilikuwa ni Shule ya Muziki inayoitwa Tanzschule Weiss iliyopo Offenbach, ambapo wanafundisha Hip hop, Kuwafundisha watoto kucheza na Salsa Cubana na anampango wa kuanzisha shule ya Muziki Nchini Tanzania.
Kwa sasa Emanuel Austin anafanya kazi katika moja ya shule kubwa ya Muziki wa Dance nchini  Ujerumani  ambapo wachezaji maarufu wa Dance kama Don Omar wapo humo , hata hivyo Emanuel huja nyumbani Tanzania kila mwaka  na sasa Amekuja na ngoma mpya ambayo amemshirikisha Ben Pol inaitwa ruka juu.

Kufahamu zaidi juu ya Emanuel Austin   Mfuate hapa
.
www.instagram.com/emanuelaustinofficial 
www.facebook.com/emanuelaustin 
YouTube : Emanuel Austin 
Twitter: emanuelaustin27 

www.twitter.com/emanuelaustin27

"DOGO" AJITOSA UDIWANI KUPITIA CHADEMA KATA YA KORONGONI MJINI MOSHI.

Mpambanaji aliyejitambulisha kwa mwandishi wa blog hii kwa jina la Liberatus Oba Mawalla "Dogo" (pichani juu) amechukua na kurudisha fomu za kugombea udiwani kata ya Korongoni wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Amesema endapo atapata ridhaa hatapenda wamuite mheshimiwa na badala yake anataka wapiga kura wake wamuite ndugu. Angalia picha zaidi hapa chini

Dogo akiwa na wanachama hicho

Msafara kuelekea kurudisha fomu ukijipanga.

Hapa ni furaha tupu.

Dogo akiwa na vijana wa chama hicho.

Akisaini wakati akichukua fomu.

Hapa ni ushindi tu.


Msafara huo kurudisha fomu.

Ni alama ya vidole viwili chadema .



Ni furaha tu kwa kwenda mbele.




Dogo ndani ya mchuma akienda kurudisha fomu.

Ni kama wanasema ushindi ni lazima.

Msafara huo wa kwenda kurudisha fomu.

Dogo akipongezwa na vijana wenzake.

JERRY SLAA AREJESHA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA UKONGA

IMG_9354
Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM taifa, Jerry William Silaa akionyesha fomu aliyojaza kwa ajili ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge Jimbo la Ukonga katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 Mwaka huu nchini kote, wakati aliporejesha fomu hiyo katika ofisi za CCM wilaya ya Ilala aliyoikabidhi kwa Katibu Msaidizi wa CCM wilaya ya ILALA (kushoto).
Jerry Slaa aliongozana na Mwenyekiti wa tawi la Gulukakwalala ambako ndio nyumbani kwake, Mwenyekiti wa CCM kata ya Gongo la Mboto pamoja na wazee wa jimbo la Ukonga.
IMG_9341
Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM taifa, Jerry William Silaa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla fupi ya kurejesha fomu yake ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge Jimbo la Ukonga katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 Mwaka huu nchini kote.
IMG_9348 IMG_9317
Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM taifa, Jerry William Silaa akiwa meza kuu na baadhi ya viongozi na wazee wa Ukonga aliombatana nao wakati wa kurejesha fomu.