Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani
Kamishina mwandamizi Jafari Ibrahimu akifafanua jambo kwa waandishi wa
habari ofisini kwake kuhusina na watuumiwa wa ujamabzi waliokamatwa
pamoja na siraha ambazo wamezikamata baada ya kufanya operesheni katika
mapori(Picha na Victor Masangu)
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Pwani Kamishina mwandamizi Jafari Ibrahimu akifafanua jambo kwa
waandishi wa habari ofisini kwake kuhusina na watuumiwa wa ujamabzi
waliokamatwa pamoja na siraha ambazo wamezikamata baada ya kufanya
operesheni katika mapori(Picha na Victor Masangu)
………………………………………………….
VICTOR MASANGU, PWANI
KUFUATIA kukithiri kwa wimbi la
matukio ya uharifu pamoja na kuvamia vituo vya polisi Jeshi la polisi
Mkoa wa Pwani limefanya msako mkali katika mapori mbali mbali na
kufanikiwa kuwanasa watuhumiwa wa ujambazi 27 pamoja na risasi
153,bunduki 2 mabomu 3 ambavyo walikuwa wakivitumia katika matukio ya
uharifu.
Akizungumza na wa waandishi wa
habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishina mwandamizi Jafari
Ibrahimu amesema kwamba watuhumiwa hao wamekamatwa baada ya kufanyika
operesheni katika magenge yaliyopo vichakani na kuwakuta watuhumiwa hao
wakiwa wamejificha.
Kamanda amesema kwamba
wameamua kufanya operesheni hiyo kutokana na kuongezeka kwa uharifu
katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Pwani na kuwakamata watuhumiwa hao
ambao wengine walikutwa na vifaa mbali mbali ikiwemo visu
mapanga,pamoja na nyaya tatu za milipuko ya mabomu.
Aidha Kamanda huyo amebainisha
kwamba katika zoezi hilo pia waliweza kukamata madawa ya kulevya aina
aya bangi gunia 18 na mirungi kilo 124,lita 88 za pombe ya moshi pamoja
na mitambo yake mitatu ya kutengenezea noti bandia 370 na meno ya tembo.
Katika hatua nyingine Kamanda
huyo amesema kwamba wanafunzi wawili wa familia moja katika shule ya
msingi mgogodo iliyopo Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani wamepoteza
maisha baada ya chumba chao walichokuwa wamelala kuteketea kwa moto na
kwamba chanzo cha moto huo ni kibatali.
Mkoa wa pwani umekuwa na
matukio ya uharifu mbali mbali ikiwemo kuvamiwa kwa vituo vya polisi
ikiwemo kituo cha Kimazichana Wilayani mkuranga ,Ikiwiriri ,kituo
kidogo cha mloka,pamoja na tukio la kufanya jaribio la kutaka kuvamia
kituo cha polisi Kibiti vyote vilivyopo Wilayani Rufiji.
No comments:
Post a Comment