Pages

KAPIPI TV

Friday, July 17, 2015

BI. CHIKULUPI NJELU KASAKA ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE WA VITI MAALUM,VIJANA MBEYA ATOA VIPAUMBELE VYAKE

Bi. Chikulupi Njelu Kasaka 
Mgombea Ubunge Viti Maalum Vijana Mbeya Bi. Chikulupi Njelu Kasaka (Kushoto) akikabidhiwa Fomu ya Kuomba Ridhaa kuteuliwa kugombea Ubunge wa Viti maalum Vijana Mbeya na Katibu wa UVCCM Mkoa wa Mbeya Bi. Aida Mamu
 Kushoto ni Bw. Moses Mwakibinga Katibu wa Hamasa na Chipukizi Wilaya ya Chunya, Bi. Chikulupi Njelu Kasaka (Kushoto)  na Katibu wa UVCCM Mkoa wa Mbeya Bi. Aida Mamu Baada ya kukabidhiwa Fomu

                  MFAHAMU BI. CHIKULUPI NJELU KASAKA


*Anaitwa Chikulupi Njelu Kasaka.

*Ni Mwanasheria (wakili) kitaaluma.


*Ni mfanyakazi wa Bunge la JMT
.
*Sasa anawania Ubunge wa Viti-maalum (vijana).


*WASIFU WA MGOMBEA: BI. CHIKULUPI KASAKA

ELIMU:
Chikulupi Kasaka ni mzaliwa wa Chunya na babu na Bibi ni wakazi wa Kijiji cha Mtanila katika Wilaya ya Chunya.

 Chikulupi alizaliwa mwaka 1986 na kuanza elimu ya msingi mwaka 1994 katika shule ya Chunya Kati. Chikulupi alimaliza elimu ya msingi Mkoani Tabora na kuchaguliwa kwenda shule ya Serikali ya Sekondari ya Wasichana Msalato iliyopo Dodoma ambapo alisoma kidato cha kwanza mpaka cha nne mwaka 2000-2004. Mwaka 2005-2007 alijiunga na Shule ya Serikali ya Sekondari ya Wasichana Loleza iliyopo Mkoani Mbeya. Alishaguliwa kijunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2007 kusomea Shahada ya Kwanza ya Sheria na kumaliza mwaka 2011. Mwaka 2013 alijiendeleza kwa kujiunga na mafunzo ya uanasheria kwa vitendo na kumaliza mwaka 2014 katika chuo kiitwacho Law School of Tanzania ambapo baadaye niliapishwa kuwa wakili.

UZOEFU KATIKA UONGOZI:
Chikulupi aliwahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi akiwa anasoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Alikuwa Mbunge katika Serikali ya wanafunzi - DARUSO.

 Chikulupi alichaguliwa mwaka 2009 kuwa Makamu wa Rais wa Umoja wa Wanafunzi wa Afrika Mashariki uitwao East Africa Community Students Union -EACSU.

 Pia alikuwa Afisa Mahusiano ya Umma katika Taasisi ya wanafunzi wa Sheria iitwayo University of Dar es Salaam Human Rights Association –UDHRA. Mwaka 2010 alishiriki mafunzo ya Uongozi kwa Vijana yaliyofadhiliwa na Shirika la Kijeruman liitwalo Friedrich Ebert Stiftung –FES.

 Pia mwaka 2014 alishiriki mafunzo ya Viongozi Vijana toka barani Afrika nchini Marekani ambao alisomea masomo ya Public Management katika chuo cha Howard kilichopo Washington. Pia nilipata fursa ya kukutana na Rais Barack Obama ambae ni mwanzilishi wa mafunzo haya.

UZOEFU NDANI YA CHAMA/UVCCM:
Chikulupi Kasaka alijiunga na CCM hasa katika jumuiya ya UVCCM mara tu baada ya kumaliza elimu ya sekondari 2006. 
Alipokuwa anasomea Shahada ya Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alijikita katika shughuli mbalimbali za kuimarisha chama na mwaka 2010 alichaguliwa Mwenyekiti wa UVCCM tawi ya Abiyan-Chuo Kikuu. Na mjumbe wa Shirikisho la Vyuo Vikuu wanaCCM, Mkoa wa Dar es Salaam.

KAZI:
Mara baada ya kumaliza chuo kikuu Julai 2011 Chikulupi alifanya kazi katika Shirika la Wakimbizi katika Mradi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam uitwao International Migration Management Program (IMMP). 

Mwaka 2012 aliajiriwa na Serikali kama Hakimu Mkazi daraja 2, katika Mahakama ya Mwanzo Makongorosi-Chunya, Mbeya. Mwishoni mwa mwaka 2012 nilijiunga na utumishi wa Chama Makao Makuu ya CCM Dodoma. 

Nilipangiwa kufanya kazi za Chama katika Upande wa Bunge hasa za kisheria. Tangu kipindi hicho mpaka sasa Chikulupi anafanya kazi kama Msaidizi wa Katibu wa Wabunge wote wa CCM, Bungeni Dodoma.

VIPAUMBELE:
Chikulupi Kasaka anaomba ridhaa yako ili aweze kuwawakilisha vijana wa Mkoa wa Mbeya katika nafasi ya Uongozi wa Kitaifa kupitia ngazi ya Ubunge wa Viti Maalum-Vijana. 

Kama mkazi wa Mbeya naamini vijana wa Mbeya wanauwezo, nguvu, bidii na jitihada katika shughuli zao za kila siku. Lakini mimi nitapigania kuwapatia vijana wa Mbeya fursa nyingi zaidi katika vipaumbele vifuatavyo: 

ELIMU, AJIRA, MICHEZO, UTALII na AFYA.
ANAOMBA UMUUNGE MKONO KWA FURSA ZAIDI KWA VIJANA WA MKOA WETU WA MBEYA.


ANSWAR-SUN WASWALI IDD EID FITRI JANGWANI DAR ES SALAAM LEO

 Amiri wa Jumuiya ya Answari Suna Tanzania, Shekh. Juma Omari Poli (kulia), akiswalisha Swala ya Iddi katika viwanja hivyo.
 Shekh Hamid Abdallah, akitoa mawaidha wakati wa ibada ya Swala ya Idi katika Viwanja vya Jangwani Dar es Salaam leo.

Waumini wa dini ya kiislam wakiwa kwenye ibada hiyo.
 Waumini wa madhehebu ya Anwar-Suni wakiswali katika viwanja hivyo.

SKYLIGHT BAND YAENDELEA KUUNGURUMA NDANI YA KIOTA KIPYA CHA LUKAS PUB MASAKI,USIKOSE LEO

 
Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower akishusha mistari na kucheza huku waimbaji wenzake Sony Masamba (wa pili kutoka kushoto), Ashura Kitenge(wa pili kutoka kulia) pamoja na Sam Mapenzi wakisebeneka Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Lukas Pub jijini Dar.
Mwimbaji wa Bendi ya Skylight Shuu akiimba pamoja na msanii mwenzake Kasongo Junior haya ni Majembe mapya ya bend ya Skylight
Ilikuwa noma sana siku ya Ijumaa iliyopita maana ilikuwa sio ya kupitwa basi mchuke na ndugu, jamaa au rafiki yako leo uje kuona vitu vitamu kutoka kwenye Bendi ya Skylight
Mashabiki wa Bend ya Skylight wakiendelea kuserebuka.
Sony Masamba akiendelea kutoa burudani huku akisindikizwa na waimbaji wenzake ndani ya kiota kipya cha Lukas kilichoko Masaki jijini Dar.
Sakata rhumba na Skylight band hapana chezea hatareee ukigusa lazima unase
Mwimbaji wa Bendi ya Skylight Shuu akitoa burudani kwa mashabiki wa bendi hiyo ( hawapo pichani) uku akisindikizwa na waimbaji wenzake Sony Masamba (kushoto) pamoja na Ashura Kitenge.(kulia)
Katika bend ya Skylight ni full burudani.
Skylight Band ni mwendo wa kutoa raha sana tukutane Ijumaa hii ndani ya kiota cha Lukas pub Masaki jijini Dar kwa kuburudika na band hii
Ndani ya Skyligt band ni full burudani.
Ilifika time ya Nigeria Flavour….. Sam Mapenzi akitoa burudani huku akisindikizwa na wanamziki wenzake waliokuwa wakimpa support ya nguvu kwenye ngoma za Nigeria ambao ni Joniko Flower (wa kwanza kushoto), Ashura Kitenge(wa pili kutoka kulia) pamoja na Sony Masamba.
Mashabiki wakiendelea kuserebuka nyimbo za Skylight.

NANI KUAGA SHINDANO LA TMT 2015 #MPAKAKIELEWEKE WIKI HII?

 Baadhi ya washiriki wakiwa kazini katika kutengeneza filamu mfupi
 Baadhi ya washiriki wakiwa makini huku sura zao zikiwa na majonzi na wasiwasi juu ya washiriki gani wanaooaga shindano kwa wiki hii.
 Baadhi ya watazamaji waliojitokeza katika kushuhudia mtanange wa washiriki wanaaga mashindano katika wiki hii na kushuhudia wanaoingia katika jua la utosi
 Walimu wa Washiriki wa Shindano la TMT 2015 #mpakakieleweke kutoka Kushoto Ni Mwl Issa na Dkt Mona Mwakalinga wakifuatilia kazi ya wanafunzi wao katika kipindi cha TMT 2015 #mpakakieleweke
 Majaji wa Shindano la TMT 2015 #mpakakieleweke wakifurahia show ya washiriki wa TMT waliobahatika kuendelea na shindano hilo mara baada ya washiriki wengine kuaga mashindano hayo kutokana na kura kutotosha.
 Mahosti wa Kipindi cha TMT 2015 #mpakakieleweke wakifurahia kazi yao wakati wa kipindi cha TMT kinachorushwa kila jumapili saa tatu na nusu usiku kupitia kituo cha ITV
Baadhi ya washiriki wa TMT 2015 #mpakakieleweke wakiwa mbele ya majaji tayari kwa kutaja waliongia hatua ya jua la utosi.
Na Josephat Lukaza.
Shindano la TMT 2015 #mpakakieleweke limeingia hatua nyingine tena mara baada ya washiriki wengine kuaga shindano hilo . Katika hatua hiyo ya mchujo hali imezidi kuwa ngumu kwa washiriki kutokana na shindano kuwa gumu kwao kila wiki. Mpaka sasa jumla ya washiriki wanne wameshaaga shindano hilo huku mchuano ukiwa mkali kwa washiriki waliobakia.
Ili kuweza kumbakiza mshiriki umpendae unachotakiwa kufanya ni Kumpigia kura kadri uwezavyo ili kumnusuru na kuaga shindano ambalo limejizolea umaarufu mkubwa ndani na nje ya Nchi ya Tanzania kutokana na ubora wake na uwajibikaji na ubunifu wa shindano hilo
Jinsi ya kumpigia kura mshiriki umpendae unachotakiwa kufanya ni Kuandika ujumbe mfupi wa Maneno TMT ikifuatiwa na namba ya mshiriki halafu tuma kwenda namba 0784 36 77 38.
Kufahamu ni nani na nani wameaga shindano hili kwa wiki hii basi usikose kufuatilia kipindi cha TMT 2015 #mpakakieleweke kupitia kituo cha runinga cha ITV kila siku ya Jumapili saa tatu na nusu usiku.
Shindano la TMT limepigwa Tafu na I-View Studio, Precision Air, Global Publishers, Paisha, Cam Gas, Radio One na ITV pamoja na Pepsi

THE STARS BAND KUZINDULIWA RASMI EID MOSI NDANI YA MZALENDO PUB

IMG-20150715-WA0008
Na Andrew Chale, Modewjiblog
Bendi mpya ya muziki wa dansi ijulikanayo kama The Stars Band iliyo chini ya Anneth Kushaba inatarajiwa kuzinduliwa rasmi Jumamosi ya Julai 18, siku ya Idd-Mosi ndani ya kiota cha Mzalendo Pub, Kijitonyama jijini Dar es Salaam huku ikitarajiwa kusindikizwa na mwanamuziki Barnabas pamoja na bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’
Kiongozi wa Stars Band, Kushaba anasema kuwa, tayari wapo katika mazoezi mbalimbali na ‘crew’ nzima ya bendi hiyo ambayo inaunganisha wanamuziki wenye uzoefu mkubwa katika uimbaji, upigaji vifaa na kushambulia jukwaa ndani na nje ya Tanzania.

“Wadau wa burudani ni nafasi ya kipekee kujitokeza kushuhudia uzinduzi wa bendi yao mpya iliyojaa kila aina ya burudani kuanzia uimbaji, kumiliki jukwaa na vyombo vilivyopangika.. burudani itakayoanza kuanzia saa moja jioni hadi majogoo” anasema Kushaba.

Anaongeza kuwa, uzinduzi huo pia utapambwa na bendi ya Fm Academia ‘Wazee wa NGWASUMA na mwanamuziki Barnabas Classic huku kiingilio mlangoni kitakuwa sh 10,000.

Kushaba anasema kuwa, miongoni mwa wanaounda bendi hiyo wapo wakali katika upande wa uimbaji kama Mao Santiago, Felly Kano, Alawy Junior, Khajanito (Khadija Maumivu) na Aneth Kushaba.

Kwa upande wa vyombo bendi hiyo inaundwa na mpiga drum wa zamani wa Twanga Pepeta, James Kibosho akiwa pamoja na Zaid Sato (Base), Othuman Majuto, Sebastian na Denis ‘Keyboard’, pamoja na Chacha ‘Tumba’.

Stars Band ndio inakuwa bendi ya kwanza ya dansi nchini kuja na mitindo mipya ya Utamaduni na bongo fleva (None stop!!) jukwaani.
Stars Band pia baada ya uzinduzi huo itakuwa inapiga kila Jumamosi ndani ya kiota hicho cha Mzalendo Pub.

RIDHIWANI KIKWETE KUTETEA KITI CHAKE CHA UBUNGE JIMBO LA CHALINZE, ACHUKUA FOMU

????????????????????????????????????
Mh. Ridhiwani Kikwete mbunge wa jimbo la Chalinze akisalimiana na Diwania wa Kata ya Bwilingu Bw, Ahmed Masser wakati alipowasili katika eneo la mkutano uliofanyika mji mdogo wa Chalinze jana ukiwa na lengo la kuelezea utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya CCM uliofanywa na Mbunge huyo kwa kipindi cha mwaka mmoja katika huduma za Afya, Elimu, Maji, Miundombinu, Uchumi, Michezo na amaendeleo mengine ya kijamii.
Mh. Ridhiwania Kikwete ametanganza rasmi jana katika mkutano huo nia yake ya kutetea jimbo la Chalinze ambapo leo mchana anatarajiwa kuchukua fomu katika ofisi za CCM wilaya ya Bagamoyo tayari kwa kuanza mchakato wa kuwania tena ubunge wa jimbo la Chalinze ili kuendeleza yale aliyokwishayaanza kutekeleza katika kipidi cha mwaka mmoja alipokuwa madarakani.
????????????????????????????????????
Mh. Ridhiwani Kikwete mbunge wa jimbo la Chalinze akisalimiana na wananchi mbalimbali wakati alipowasili katika eneo la mkutano mjini Chalinze.
????????????????????????????????????
Mh. Ridhiwani Kikwete mbunge wa jimbo la Chalinze akizungumza jambo na Katibu wake Bw. Idd Swala huku Diwani wa Kata ya Bwilingu Ahmed Nasser akisikiliza kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Bw.ndugu Majid Mwanga.
????????????????????????????????????
Mh. Ridhiwani Kikwete mbunge wa jimbo la Chalinze akizungumza jambo na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Ndugu Majid Mwanga.
????????????????????????????????????
Diwani wa Kata ya Bwilingu Ahmed Nasser akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Chalinze jana.
????????????????????????????????????
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Ndugu Majid Mwanga akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Chalinze jana.
????????????????????????????????????
Mh. Ridhiwani Kikwete mbunge wa jimbo la Chalinze akizungumza na wananchi mjini Chalinze wakati alipotangaza nia yake ya kutetea tena ubunge wa jimbo hilo.
????????????????????????????????????
Wananchi wa Chalinze wakimsikiliza Ridhiwania Kikwete mbunge wa jimbo hilo hayupo pichani wakati alipokuwa akitangaza nia yake ya kutetea tena kiti cha ubunge wa jimbo la Chalinze.
???????????????????????????????????? ???????????????????????????????????? ???????????????????????????????????? ????????????????????????????????????

Thursday, July 16, 2015

MSANII MAARUFU WA FILAMU AJIUNGA NA ACT WAZALENDO


Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa (kushoto) akimkabidhi kadi msanii maarufu wa filamu nchini, Mohamed Mwikongi jina la sanaa 'Frank' alipotambulishwa mara baada ya kujiunga na chama hicho.
Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa (kushoto) akimkabidhi kadi msanii maarufu wa filamu nchini, Mohamed Mwikongi jina la sanaa ‘Frank’ alipotambulishwa mara baada ya kujiunga na chama hicho.
Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa (kushoto) akimkabidhi aliyekuwa Mwenyekiti wa kitengo cha vijana Taifa wa NCCR Mageuzi, Deo Meck alipotangazwa kujiunga na chama hicho rasmi leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa (kushoto) akimkabidhi aliyekuwa Mwenyekiti wa kitengo cha vijana Taifa wa NCCR Mageuzi, Deo Meck alipotangazwa kujiunga na chama hicho rasmi leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa (kushoto) akimkabidhi kadi na katiba msanii maarufu wa filamu nchini, Mohamed Mwikongi jina la sanaa 'Frank' alipotambulishwa mara baada ya kujiunga na chama hicho.
Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa (kushoto) akimkabidhi kadi na katiba msanii maarufu wa filamu nchini, Mohamed Mwikongi jina la sanaa ‘Frank’ alipotambulishwa mara baada ya kujiunga na chama hicho.
Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa akizungumza na waandishi wa habari leo alipowapokea baadhi ya wanachama wapya wa ACT-Wazalendo. Kushoto ni Katibu wa Kampeni na Uchaguzi, Mohamed Masaga na kulia ni Deo Meck mwanachama mpya wa ACT Wazalendo.
Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa akizungumza na waandishi wa habari leo alipowapokea baadhi ya wanachama wapya wa ACT-Wazalendo. Kushoto ni Katibu wa Kampeni na Uchaguzi, Mohamed Masaga na kulia ni Deo Meck mwanachama mpya wa ACT Wazalendo.
Msanii maarufu wa filamu nchini, Mohamed Mwikongi jina la sanaa 'Frank' akizungumza na waandishi wa habari alipotambulishwa mara baada ya kujiunga na chama hicho.
Msanii maarufu wa filamu nchini, Mohamed Mwikongi jina la sanaa ‘Frank’ akizungumza na waandishi wa habari alipotambulishwa mara baada ya kujiunga na chama hicho.
MSANII maarufu wa filamu nchini, Mohamed Mwikongi jina la sanaa ‘Frank’ amejiunga na chama kipya cha siasa cha ACT Wazalendo. Frank amejiunga na chama hicho leo jijini Dar es Salaam akitokea Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Katika hafla hiyo ya utambulisho kiongozi mwingine ambaye ni Mwenyekiti wa kitengo cha vijana Taifa wa NCCR Mageuzi, Deo Meck pia amejiunga na chama cha ACT Wazalendo na kukabidhiwa kadi za chama hicho.
Akiwakabidhi kadi za ACT-Wazalendo, Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa leo Makao Makuu ya ACT alisema wamewapokea wanachama hao wapya kwa mikono miwili na wapo tayari kushirikiana nao ndani ya chama hicho. Alisema kuna idadi kubwa ya vigogo kutoka vyama vingine ambao tayari wameomba kujiunga na chama chao na taratibu zinafanywa kutambulishwa.
“…tendo hili la leo la kuwakaribisha vijana hawa ni mwanzo wa kuwatambulisha wanachama mbalimbali wakiwemo wabunge na viongozi wa vyama waliojiunga nasi baada ya kuvunjwa kwa Bunge. Tayari tunao baadhi ya watu waliokuwa wabunge na wameshajiunga nasi na mchakato wa kuwatambulisha unaendelea katika maeneo mbali mbali nchini,” alisema Mtemelwa.
Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa (kushoto) akimtambulisha aliyekuwa Mwenyekiti wa kitengo cha vijana Taifa wa NCCR Mageuzi, Deo Meck alipotangazwa kujiunga na chama hicho rasmi leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa (kushoto) akimtambulisha aliyekuwa Mwenyekiti wa kitengo cha vijana Taifa wa NCCR Mageuzi, Deo Meck alipotangazwa kujiunga na chama hicho rasmi leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa kwenye mkutano wa ACT Wazalendo.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa kwenye mkutano wa ACT Wazalendo.

Akizungumzia mchakato wa uchukuaji fomu kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho, Mtemelwa alisema Julai mosi mwaka huu Chama Cha ACT-Wazalendo kilifungua rasmi pazia la uchukuaji fomu za kugombea nafasi mbalimbali zikiweno za Udiwani, Ubunge na Urais.

Alisema tangu kuanza kwa uchukuaji huo wa fomu kumekuwa na mwitikio mkubwa wa wanachama kuchukua fomu na hadi sasa kuna baadhi ya majimbo na kata zina watia azma kuanzia wanne mpaka tisa jambo ambalo alidai ni faraja kwa ACT Wazalendo.

“Kati ya majimbo 265 yakiwamo majimbo mapya 26 yaliyoongezwa hivi karibuni na Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), ACT-Wazalendo tumeshakuwa na waweka azma zaidi ya mmoja katika majimbo 226 kwa nchi nzima na tunaamini mpaka kufikia mwisho wa uchukuaji fomu ndani ya Chama majimbo yote 265 yatakuwa yanawatia azma mbalimbali wanaosubiri kupitishwa na chama kwa ajili ya uchaguzi mkuu,” aliongeza Naibu Katibu Mkuu huyo wa ACT Wazalendo.

Alibainisha kuwa kichama mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu kwa nafasi ya udiwani ni julai 24, kwa nafasi ya Ubunge mwisho ni Julai 31 na kwa nafasi ya Urais mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni Agosti Mosi, 2015. 

“Kwa ngazi ya Taifa Halmashauri kuu itakutana Agosti 13 kwa ajili ya kuteua jina la mgombea Urais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, pamoja na kupendekeza majina ya wagombea Urais kwenye mkutano mkuu. Agosti 13, Mkutano mkuu utamchagua mtu atakayepeperusha bendera ya Chama cha ACT Wazalendo katika mbio za urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”

“Hivi karibuni tumepokea taarifa kutoka katika miji ya Tarime na Rorya Mkoani Mara kuwa kuna watu wanapita na kutangaza kuwa Chama chetu kimezuiwa kushiriki Uchaguzi kwa muda wa miezi sita.  
Tumebaini lengo la upotoshaji huu ni kuwakatisha watanzania tamaa juu ya ukuaji wa Chama Cha ACT-Wazalendo pamoja na dhamira yake nzuri ya kuirudisha nchi katika misingi iliyoachwa na hayati Mwalimu Julius Nyerere.

“Tunawataarifu wananchi kuwa Chama chetu kitashiriki uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu kwa kuweka wagombea wa nafasi zote na Chama hakitakuwa tayari kuona sehemu yoyote ya nchi mgombea wa CCM anapita bila kupingwa,” alisisitiza Naibu Katibu Mkuu huyo wa ACT Wazalendo. *Imeandaliwa na www.thehabari.com