Pages

KAPIPI TV

Monday, June 29, 2015

KONGAMANO LA SDG’s LAFANYIKA KWA MAFANIKIO DODOMA

IMG_4628
Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida, akitoa maelezo ya kongamano kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kulifungua kongamano kubwa la siku mbili la kujadili namna taifa linavyojiandaa kutekeleza malengo mapya ya Maendeleo endelevu (SDGs) limefanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma ambalo liliandaliwa na taasisi yake.

Na Mwandishi wetu, Dodoma
KONGAMANO kubwa la siku mbili la kujadili namna taifa linavyojiandaa kutekeleza malengo mapya ya Maendeleo endelevu (SDGs) limefanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.

Kongamano hilo lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti ya Masuala ya Uchumi na jamii (ESRF) limelenga kuwakutanisha wataalamu kutoka Tanzania Bara na Visiwani kujadili namna ya kupata fedha za kutekeleza malengo hayo baada ya kumalizika kwa malengo ya maendeleo ya millennia (MDG’s) baadae mwaka huu.

Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa katika kongamano hilo ambapo wataalamu wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo walishiriki ni pamoja na namna ya kupata fedha kwa ajili ya maendeleo baada ya Septemba mwaka 2015 kwa kuangalia rasilimali za ndani.

Mada hiyo imetokana na ukweli kuwa upatikanaji wa fedha za ndani ndio suluhu ya utekelezaji wa malengo mapya kwa kuwa awali kwenye MDG’s utekelezaji wa malengo ulikwamishwa na kukosekana kwa fedha kutoka kwa wafadhili ambao waliahidi kuchangia maendeleo.

Pamoja na kuangalia upatikanaji wa fedha kutekeleza malengo hayo mapya bila kuacha yale ya zamani, washiriki pia waliangalia namna ya kujiandaa katika ufuatiliaji wa malengo ya Maendeleo endelevu (SDG’s).

Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida, akitoa maelezo ya kongamano kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kulifungua katika ukumbi wa mikutano hoteli ya St Gasper mjini Dodoma alisema kuwapo kwa kongamano hilo kumetokana na haja ya kujiandaa kabla ya mkutano wa tatu wa namna ya kutafuta fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Mkutano huo utafanyika mwezi ujao mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Aidha alisema kwamba upo umuhimu wa kuangalia uimarishaji wa ushirikiano wa dunia katika kuimarisha maendeleo endelevu.

Dk. Kida alisema kwamba kongamano hilo ambalo ni sehemu ya maandalizi ya kuingia katika SDGs; na kuwa taasisi ya ESRF kwa miaka mitatu imekuwa likifuatilia katika kuratibu mazungumzo kuhusu hatima yam MDG’s baada ya 2015.

Akifungua mkutano huo Katibu mkuu Hazina Dk. Servacius Likwelile aliwataka washiriki kuhakikisha kwamba wanachambua masuala muhimu yanayohusu maendeleo na kuyawekea mkakati katika mkutano ujao wa Addis Ababa, Ethiopia.

Akisoma hotuba kwa niaba ya Katibu Mkuu, Kamishina wa Fedha kutoka Nje Wizara ya Fedha Ngosha Magonya amesema kwamba amefurahishwa na juhudi za ESRF kuwakutanisha wataalamu kujipanga kwa mikutano ijayo na utekelezaji wa maendeleo endelevu ya SDG’s.
Aidha aliipongeza taasisi ya United Nations Development Programme (UNDP) kwa kusaidia Tanzania kuangalia hali ilivyokuwa katika MDG’s na hali ya baadae.
IMG_4606 IMG_4729
Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha, Ngosha Magonya akisoma hotuba ya ufunguzi wa kongamano hilo kwa niaba ya mgeni rasmi Katibu Mkuu wa wizara hiyo katika hoteli ya St. Gasper mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
IMG_4678
Mtaalamu wa masuala ya uchumi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Dar es salaam, Rogers Dhliwayo akitoa salamu za Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) wakati wa kongamano hilo la siku mbili la kujadili namna taifa linavyojiandaa kutekeleza malengo mapya ya Maendeleo endelevu (SDGs) lililofanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
IMG_4949
Afisa Mwandamizi wa uhamasishaji na uwekezaji kutoka kituo cha uwekezaji nchini (TIC), Lilian Mwamdanga akishiriki kuchangia maoni wakati kongamano kubwa la siku mbili la kujadili namna taifa linavyojiandaa kutekeleza malengo mapya ya Maendeleo endelevu (SDGs) limefanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
IMG_5015
Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)- Programme, Amon Manyama akichangia maoni wakati wa kongamano kubwa la siku mbili la kujadili namna taifa linavyojiandaa kutekeleza malengo mapya ya Maendeleo endelevu (SDGs) limefanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
IMG_4801
Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida na Kamishna Mipango wa Tume ya Mipango Zanzibar, Ahmed Makame Haji wakifuatilia kwa umakini maoni mbalimbali ya wadau yaliyokuwa yakitolewa kwenye kongamano hilo.
IMG_4739
Pichani juu na chini ni washiriki kutoka Tanzania bara na visiwani walioshiriki kongamano hilo la siku mbili ambalo liliandaliwa na taasisi ya ESRF.
IMG_4702
IMG_4756
Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)- Programme, Amon Manyama (kushoto) akizungumza jambo na Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha, Ngosha Magonya ambaye amemwakilisha mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha (wa pili kushoto) wakati akiondoka katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Saint Gasper mjini Dodoma mara baada ya kufungua kongamano kubwa la siku mbili la kujadili namna taifa linavyojiandaa kutekeleza malengo mapya ya Maendeleo endelevu (SDG's) lililofanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma. Wengine katika picha kutoka kulia ni Kamishna Mipango wa Tume ya Mipango Zanzibar, Ahmed Makame Haji, Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida pamoja na Mtaalamu wa masuala ya uchumi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Dar es salaam, Rogers Dhliwayo.
IMG_4778
Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (kushoto) akimsindikiza Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha, Ngosha Magonya ambaye alimwakilisha mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha mara baada ya kufungua kongamano kubwa la siku mbili la kujadili namna taifa linavyojiandaa kutekeleza malengo mapya ya Maendeleo endelevu (SDGs) limefanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
IMG_5066
Picha ya pamoja ya washiriki.

NJOO SABASABA UJUE UMOJA WA MATAIFA, MIAKA 70 YA KUTETEA USTAWI WA DUNIA

DSC_0598
Muonekano wa nje wa Banda la Shirika la Umoja wa Mataifa (UN), Tanzania lililopo ndani ya Karume Hall wanaoshiriki katika Maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam ya sabasaba yaliyoanza kurindima jana kwenye katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Modewji blog team, Sabasaba
Shirika la Umoja wa Mataifa (UN), Tanzania wapo katika maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yaliyoanza kurindima mapema jana.
UN Tanzania ambao wapo katika banda la Karume ndani ya mabanda hayo ya Sabasaba, kutoa elimu inayolenga kuionyesha jamii mafanikio, changamoto na fursa zilizopo katika Umoja wa Mataifa ambapo mwaka huu unafikisha miaka 70 tangu shirika hilo lianzishwe.
“Huu ni mwaka muhimu sana kwani safari ya Umoja wa Mataifa ilianza mwaka 1945, hadi kufikia sasa kuwa umefikia wapi, tupo wapi na tunaelekea wapi katika kushughulikia changamoto za kidunia ikiwemo Amani na usalama, changamoto za maendeleo, changamoto za mabadiliko ya tabia nchi, na changamoto zingine”, alieleza Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama.
Aidha, alibainisha kuwa, UN ambayo imeweza kufikisha miaka 15 ya malengo ya Milenia yaliyokubaliwa na nchi wanachama wa Umoja huo mwaka 2000, yanafikia kilele hapo Desemba 30, mwaka huu hivyo wakuu hao wanchi watakutana tena mwezi Septemba mwaka huu, kupanga malengo mapya ya Maendeleo endelevu (SDGs) ambayo yatakapokubalika yataanza kutumika mwakani.
“Huu ni mwaka muhimu sana. wa kuonyesha hayo mabadiliko, tumekuwa na miaka 15 ya milenia kuna vitu tumefanikiwa na tumekuwa na changamoto. Kwa hiyo malengo hayo yalikuwa ni shirikishi kutoka kwa kada zote”alieleza.
Pia alieleza kuwa katika mkutano mkubwa wa mabadiliko ya tabianchi ambao utakuwa mkutano mkubwa wa 21, utakaofanyika Paris-Ufaransa Disemba mwaka huu. Wakuu wa nchi watakuja na makubaliano ya kuona watafanya nini hivyo makubaliano hayo ni muhimu sana.
Nchi zote duniani zimeona suala la mabadiliko ya tabianchi si la nadharia tena bali ni la wote kuungana kupambana nalo kwani wote tunaathirika.
Hivyo tunawakaribisha sana watanzania kutembelea katika banda letu kujionea na kufahamu na kujifunza na kwa Tanzania mwaka huu tunamalizia program yetu ya kwanza ambayo tunashirikiana mashirika yote kufanya kazi kwa pamoja (Delivering as one) katika kutatua changamoto zinazotukabili hapa Tanzania kwa kushirikiana na serikali.
DSC_0611  
Afisa habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akitoa maelezo ya taarifa mbalimbali zilizoorodheshwa kwenye jarida la vijana lililoandaliwa na Shirika linaloshughulikia idadi ya watu Duniani (UNFPA) kwa mmoja wa wakinamama aliyetembelea banda kwa ajili ya kufahamu shughuli mbalimbali na mchango wa shirika la Umoja wa Mataifa kwa serikali Tanzania.
IMG_5248
Afisa habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akisikiliza swali kutoka kwa raia wa kigeni mwenye asili ya asia aliyetembelea banda la Umoja wa Mataifa katika maonyesho ya sabasaba yaliyoanza kurindima jana katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
IMG_5271
IMG_5240
Afisa habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akiendelea kuwapiga msasa raia hao wa kigeni waliotembelea banda la shirika la Umoja wa Mataifa Tanzania.
IMG_5291
IMG_5286
Afisa habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akisaidiana na mmoja wa wananchi aliyetembelea banda la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya sabasaba kukusanya machapisho na vipeperushi mbalimbali vinavyoelezea shughuli za Umoja wa Mataifa.
IMG_5300
Baadhi ya wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa Tanzania katika hatua za mwisho za kuandaa program mbalimbali zitakazokuwa zikitoa elimu kwa wananchi wakataotembelea banda hilo katika maonyesho ya sabasaba yaliyoanza kutimua vumbi jana katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
IMG_5148
Pichani juu na chini ni meza zilizosheheni ripoti, vitabu na majarida mbalimbali ya Umoja wa Mataifa kwa ajli ya watanzania kujisomea na kuelimika kuhusiana na shughuli na taarifa mbalimbali za ustawi wa kidunia zinazofanywa na Shirika la Umoja wa Mataifa.
IMG_5146

MKE WA MWANAHABARI WA KAMPUNI YA GUARDIAN NA NIPASHE, THOBIAS MWANAKATWE AFARIKI DUNIA KWA KUGONGWA NA GARI NJE YA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE DAR ES SALAAM

 Mke wa Thobias Mwanakatwe, Levina Michael Genda, 
enzi za uhai wake.
 Mwanahabari Thobias Mwanakatwe, aliyefiwa na mke wake.
Mwanahabari Thobias Mwanakatwe, akiwa na mke wake enzi za uhai wake.

Dotto Mwaibale

MWANAHABARI wa Kampuni ya The Guardian na Nipashe, Thobias Mwanakatwe, amepoteza mke wake baada ya kugongwa na gari eneo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam jana usimu majira ya saa 2;30.

Akizungumza na mtandao wa www.habari za jamii.com. Mwanakatwe amesema kifo cha ghafla cha mke wake ni pigo kubwa kwake na familia zote mbili.

Mwanakatwe amesema shughuli za kuuaga mwili wa marehemu zitafanyika kesho kuanzia saa tano na baada ya hapo watausafirisha kwenda kijiji cha Endala Karatu mkoani Arusha kwa mazishi yatakayofanyika kesho kutwa.

Kama kuna yeyote atakaye penda kumtolea chochote mwenzetu Mwanakatwe ili kimsaidie kwa msiba huo anaweza kuwasiliana naye kwa namba hizi za simu-0762-183666, 0655-183666 na 0787184666. Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. (Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)


A HUMBLE TANZANIAN RECOGNISED BY H.M THE QUEEN:





By Ayoub Mzee-London

Meet Angela BenedictoMnagoza, a girl from a humble background  in  Tanzania, a former child domestic worker, who has  achieved  so  much  to  warrant  an  Award  from  her  majesty  Queen  Elizabeth II  in London.

Last year a search was launched to find exceptional young people to receive the first ever Queen’s Young Leaders Awards. Hundreds of applications flooded in from incredible young people all dedicated to making lasting change in their community and beyond.

The award, started by the Queen Elizabeth Golden Jubilee Trust, recognises the contributions of 18-29 year olds from 35 Commonwealth countries. As part of their prize, winners were able able to meet the Queen and Prime Minister David Cameron and take part in a 2 day leadership course in Cambridge.

They were also  givena mentor for a year and able to take a distance learning course to help them to develop their leadership skills.

The award, which is also in partnership with Comic Relief and the Royal Common Wealth Society, had thousands of applications this year and will run for a period of 4 years.

“This programme will celebrate the achievements of these extraordinary individuals and help develop their skills, thus creating a lasting legacy – benefiting the whole of the Commonwealth – to honour the long and successful reign of HM Queen Elizabeth II.”

In  the case  of  Angela BenedictoMnagoza, thanks  for  the  support  from  Anti-Slavery and the local NGOKivuliniin  Tanzania.

Applications to become a 2016 Queen’s Young Leader will open on 22nd June.
HE QUEEN’S YOUNG LEADERS GRANTS SCHEME

Grants will be available to eligible organisations in selected countries across the Commonwealth that are working with young people to transform their lives. 

Projects will be supported that are led by or focused on young people and provide opportunities for them to learn new skills, secure employment, create enterprises or have a say in decisions affecting their future. 

Each project will place young people at the heart of their communities, working with them to help solve the issues that affect their lives.

The Grants will be available to organisations working with young people in UK, Zambia, Sierra Leone, Bangladesh, Jamaica and Solomon Islands.

WHO IS ELIGIBLE?

You are eligible if your organisation:

Is registered in one of the six eligible countries, or is registered in a Commonwealth country and will work through a named partner who is registered in one of the six eligible countries
Has independently audited accounts within the last two years
Has managed grants of equal size before
Is not a Company limited by shares or a Public Limited Company
Has governance structures that involve, or are made up of, young people and beneficiaries of youth-focused projects
Has demonstrable experience of working with young people
Can demonstrate where young people have played a clear role in the planning of projects and activities
Has a child protection policy.


Saturday, June 27, 2015

MAMIA WAJITOKEZA VIWANJA VYA LEADERS CLUB JIJINI DAR ES SALAAM KUMUAGA MHARIRI EDSON KAMUKARA


 Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Mhariri wa Kampuni ya Mwanahalisi, Edson Kamukara wakati ulipowasili viwanja vya Leaders Club Dar es Salaam leo asubuhi, kwa ajili ya kuagwa. Kamukara alifariki dunia juzi na mazishi yake yanatarajia kufanyika nyumbani kwao Muleba mkoani Kagera.

 Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Regnald Mengi (katikati), akiwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk.Wilibrod Slaa kwenye uagaji wa mwili wa Edson Kamukara. Kulia ni Mbunge wa Bukoba mjini, Khamis Kagasheki.
 Mmoja wa waandishi wa habari akiwa amepoteza fahamu wakati wa kuaga mwili huo.
 Wanahabari na waombolezaji wengine wakiwa wamejipanga foleni wakati wa utoaji wa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Edson Kamukara.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwanahalisi, Said Kubenea (katikati), akisaidiwa baada ya kuishiwa nguvu wakati akitoa heshima za mwisho kwa marehemu

 Wanahabari ni huzuni na vilio
 Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akisalimiana na Mbunge wa Bukoba mjini, Balozi Khamis Kagasheki wakati wa kuuaga mwili wa Edoson Kamukara.
 Wanafamilia ya marehemu wakiwa kwenye shughuli hiyo
 Sehemu ya umati wa watu katika shughuli hiyo.
 Mwakilishi wa wanafunzi waliosoma na marehemu Shule ya Sekondari ya Majengo, Joachim Mushi akizungumza kabla ya kutoa rambirambi yao ya sh.500,000.
 Viongozi wa serikali na vyama vya siasa wakiwa kwenye shughuli hiyo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,  Paul Makonda akizungumza katika uagaji wa mwili wa marehemu ambapo alipigania waajiri wa vyombo vya habari kutoa mikataba ya ajira kwa wanahabari.


 Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Regnald Mengi akimfariji Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwanahalisi, Said Kubenea alikuwa akifanyakazi marehemu Edson Kamukara.
 Ni vilio tu kwa wanahabari.
 Shughuli ya uagaji ikiendelea.
 Dada ya marehemu Edson Kamukara akitoa heshima za mwisho.

WAJUMBE WA BODI YA FILAMU WALIOTEMBELEA OFISI ZA PROIN PROMOTIONS NA KUJIONEA MIUNDOMBINU ILIYOWEKEZWA

 Mjumbe wa Bodi ya Filamu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bi.Vicensia Shule(wa kwanza kutoka kushoto) akimwuliza  jambo Mwenyekiti wa makampuni ya Proin Bw,Johnson Lukaza(hayupo pichani) leo jijini Dar es salaam walipotembelea kujionea  miundombinu ya kampuni hiyo.Kutoka kulia ni Makamu mwenyekiti wa  wa Bodi iyo Bw.Sylvester Sengerema na katikati ni  Bw.Bishop Hiluka.
 Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bi,Joyce Fissoo akichangia jambo wakati walipotembelea miundombinu ya Filamu ya Makampuni ya Proin.Bi Fissoo ametoa wito kwa makampuni yanayotengeneza Filamu Tanzania kuendelea kushirikiana na Serikali ili kuimarisha Tasnia ya Filamu na kusaidia katika kupambana na Changamoto mbalimbali.
Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin Bw,Johnson Lukaza akimwonyesha Katibu mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi,Joyce Fissoo  moja ya Kazi walizotengeneza na kuingia Sokoni,Pia aliiomba Serikali kusaidia kuweka sheria kali zitakazo zuia wizi wa Filamu nchini.
Wajumbe wa Bodi ya Filamu Tanzania wakifurahia jambo na Mkurugenzi wa Makampuni ya Proin Bw,Johnson Lukaza(wa tatu kutoka kushoto) walipotembelea miundombinu ya kutengenezea filamu ya Kampuni iyo eneo la Mabibo jijini Dar es Salaam.Wajumbe hao walijionea jinsi Filamu inavyotengenezwa na pia walitembelea eneo kampuni iyo wanapojenga Studio ya kutengenezea Filamu.

WAZEE KIGOMA WAMKABIDHI FOMU YA KUWANIA UBUNGE DR.YAREDI FUBUSA JIMBO LA KIGOMA KASKAZINI

Mjumbe wa Kuchaguliwa Kamati Kuu Taifa CHADEMA, Dkt Yaredi Fubusa akizungumza na wananchi baada ya kukabidhiwa fomu na wazee wa Jimbo la Kigoma Kaskazini
Mwenyekiti wa Wazee Wilaya ya Kigoma, Mzee Yasini Athumani (Mapigosaba) akimkabidhi fomu Mjumbe wa Kuchaguliwa Kamati Kuu Taifa CHADEMA, Dkt. Yaredi Fubusa 
Na Magreth Magosso, Kigoma.
 
WAZEE  wa jimbo la Kigoma Kaskazini  mkoani Kigoma wamechukua dhamana ya kununua fomu kwa ajili ya Mjumbe wa kamati Kuu Taifa chama cha Democrasia na maendeleo CHADEMA Dkt. Yared Fubusa ili aweze kuwania kiti cha ubunge na kutetea haki za wakazi wa Jimbo la Kigoma Kaskazini
 
Walisema hayo wakati wakimkabidhi fomu hiyo  ya kugombea nafasi ya Ubunge  kwa kiasi cha shilingi laki 2.5 lengo likiwa ni kumtaka kijana huyo kuwakomboa wakazi wa jimbo hilo katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo na uchumi wa wakazi hao uweze kupanda kulingana na rasilimali walizonazo katika jimbo hilo.
 
Walisema lengo la kuomba kijana huyo aweze kugombea ni kutokana na kiwango chake cha elimu ambacho kinaweza kuwa msaada kwa wakazi wa jimbo hilo kutetea haki zao ndani ya nchi nan je ya nchi na si kwa maslahi yake binafsi ni kwa maslahi ya wakazi wa jimbo la Kigoma Kaskazini pamoja na uwekezaji aliofanya katika jimbo hilo kijiji cha Kiganza wilaya ya Kigoma Mkoani humo.
 
“ Tumepata wabunge wengi ambao wamepata nafasi hizo na kutoweka, lakini yaredi amekuwa akiishi wa wananchi wa kijiji cha Kiganza kwa muda mrefu licha ya kupata elimu yake nchi ya Marekani, tunaomba utukubalie kupokea fomu hii na ututoe aibu kwa kutuletea maendeleo na sio ukawe mbunge wa Kitaifa” walisema.
 
Akipokea fomu hiyo Dkt. Fubusa ambaye amepata elimu katika nchi ya Marekani ya uchumi na maliasili alisema jimbo la Kigoma kaskazini linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa zahanati, viwanda vya kuzalisha zao la Kahawa ili iwe na ubora na kupata masoko ya ndani nan je ya nchi.
 
Alisema pamoja na sekta ya elimu bado ni changamoto kwa jimbo hilo hivyo akipata fursa ya kuongoza jimbo hilo atahakikisha anasimamia vyema utekelezaji wa maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara ya lami kwa kilomita zilizobaki, kujenga hospitali ya jimbo, viwanda vya michikichi, nanasi pamoja na kuboresha uvuvi katika ziwa Tanganyika.

“ Kuna kitabu nimekitunga cha mambo ya uchumi na maisha ya watu wa jimbo la Kigoma Kaskazini nchini Marekani ikiwa ni  degree yangu ya PHD ya uchumi katika kitabu hiki kuna changamoto na kero za wakazi wa jimbo hili na nimeweka nini kifanyike ili kutatua changamoto na kero na siingii bungeni kwa ubabaishaji lazima nifanye yale niliyoamua kuyatekeleza katika jimbo hili” alisema dkt. Fubusa.

WANAHABARI WAPEWA SEMINA KUHUSU MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA

Kaimu Mkurugenzi Magonjwa Yasiyoambukiza wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Auson Rwehimbiza (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kwenye semina ya siku moja kuhusu magonjwa yasiyoambukiza. Kulia ni Meneja Mradi Shirikisho la Vyama vya Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza (TANCDA
Kaimu Mkurugenzi Magonjwa Yasiyoambukiza wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Auson Rwehimbiza (kulia), akimuelekeza jambo Ofisa Habari wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Catheline Sungura wakati wa semina hiyo.
Ofisa Habari wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Catheline Sungura (kushoto), akielekeza jambo kwenye semina hiyo.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye semina hiyo.

Semina ikiendelea.


Na Dotto Mwaibale

MAISHA ya watu katika nchi zinazoendelea, yapo hatarini kutokana na asilimia 50 ya magonjwa yasiyoambukiza kusababisha vifo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, wakati wa semina ya magonjwa yasiyoambukiza iliyondaliwa mahususi kwaajili ya wanahabari yenye lengo la kukamilisha mkakati pamoja na mpango kazi 2015/2020, Kaimu Mkurugenzi Magonjwa yasiyoambukiza, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Auson Rwehimbiza aliyataja magonjwa yasiyoambukiza ni moyo na mishipa ya damu, kisukari, kansa na magonjwa sugu ya mfumo wa hewa.

Alisema magonjwa hayo yanazidi kuongezeka nchini hasa kwa jamii ya watu waishio mjini na kuongeza kuwa watu wazima wenye umri wa miaka 80 kuwa na magonjwa hayo kwa asilimia 1 hadi 3 na msukumo wa juu wa damu kwa asilimia 5 hadi 10.

"Tathmini ya mwaka 2012 iliyohusisha watu wazima katika wilaya 50, inaonesha viwango vya ugonjwa wa kisukari viliongezeka kwa asilimia 9, huku asilimia 27 kwa msukumo wa juu wa damu," alisema Dk. Rwehimbiza.

Alisema ongezeko hilo limetokana na kuongezeka kwa utandawazi, ukuaji wa miji, kutofanya mazoezi ya mwili, ulaji usiofaa, utumiaji wa tumbaku pamoja na unywaji wa pombe kupita kiasi.

Aidha, alisema Tanzania ilianza kujihususha na magonjwa yasiyokuambukiza kuanzia mwaka 2009 hadi 2015, kwa kuandaa mpango mkakati na mpango kazi ambao ulihusisha utekelezaji wa mpango wa taifa wa kisukari kwa kushirikiana na chama cha wagonjwa wa kisukari nchini.  

"Hadi sasa utekelezaji wa mpango wa taifa wa kuanzisha  kliniki za magonjwa yasiyoambukiza umefikia asilimia 75 katika hospitali za mikoana wilaya na vituo vya afya,". Nakuongeza kuwa asilimia 75 ya elimu zinazotolewa na watoa huduma wa afya katika hospitali za mikoa, wilaya na vituo vya Afya.

Anaongeza kuwa, shirika la afya duniani WHO, liliandaa mpango mkakati ambao ulidhamiria kupunguza viwango vya sasa vya vifo vitokanavyo na magonjwa hayo kwa asilimia 25 ifikapo mwaka 2025 na kupendekeza mapendekezo ya hiari lengo ikiwa kufanikiwa kwa mkakati huo.(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba -0712-727062)