Mjumbe wa Kuchaguliwa Kamati Kuu Taifa CHADEMA, Dkt Yaredi Fubusa akizungumza na wananchi baada ya kukabidhiwa fomu na wazee wa Jimbo la Kigoma Kaskazini |
Mwenyekiti wa Wazee Wilaya ya Kigoma, Mzee Yasini Athumani (Mapigosaba) akimkabidhi fomu Mjumbe wa Kuchaguliwa Kamati Kuu Taifa CHADEMA, Dkt. Yaredi Fubusa |
Na Magreth Magosso, Kigoma.
WAZEE
wa jimbo la Kigoma Kaskazini mkoani Kigoma wamechukua dhamana ya kununua
fomu kwa ajili ya Mjumbe wa kamati Kuu Taifa chama cha Democrasia na maendeleo CHADEMA Dkt.
Yared Fubusa ili aweze kuwania kiti cha ubunge na kutetea haki za wakazi wa
Jimbo la Kigoma Kaskazini
Walisema hayo wakati wakimkabidhi fomu
hiyo ya kugombea nafasi ya Ubunge kwa kiasi cha shilingi laki 2.5 lengo likiwa
ni kumtaka kijana huyo kuwakomboa wakazi wa jimbo hilo katika Nyanja mbalimbali
za kimaendeleo na uchumi wa wakazi hao uweze kupanda kulingana na rasilimali
walizonazo katika jimbo hilo.
Walisema lengo la kuomba kijana huyo aweze
kugombea ni kutokana na kiwango chake cha elimu ambacho kinaweza kuwa msaada
kwa wakazi wa jimbo hilo kutetea haki zao ndani ya nchi nan je ya nchi na si
kwa maslahi yake binafsi ni kwa maslahi ya wakazi wa jimbo la Kigoma Kaskazini
pamoja na uwekezaji aliofanya katika jimbo hilo kijiji cha Kiganza wilaya ya
Kigoma Mkoani humo.
“ Tumepata wabunge wengi ambao wamepata
nafasi hizo na kutoweka, lakini yaredi amekuwa akiishi wa wananchi wa kijiji
cha Kiganza kwa muda mrefu licha ya kupata elimu yake nchi ya Marekani,
tunaomba utukubalie kupokea fomu hii na ututoe aibu kwa kutuletea maendeleo na
sio ukawe mbunge wa Kitaifa” walisema.
Akipokea fomu hiyo Dkt. Fubusa ambaye amepata
elimu katika nchi ya Marekani ya uchumi na maliasili alisema jimbo la Kigoma
kaskazini linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa zahanati,
viwanda vya kuzalisha zao la Kahawa ili iwe na ubora na kupata masoko ya ndani
nan je ya nchi.
Alisema pamoja na sekta ya elimu bado ni
changamoto kwa jimbo hilo hivyo akipata fursa ya kuongoza jimbo hilo
atahakikisha anasimamia vyema utekelezaji wa maendeleo ikiwemo ujenzi wa
barabara ya lami kwa kilomita zilizobaki, kujenga hospitali ya jimbo, viwanda
vya michikichi, nanasi pamoja na kuboresha uvuvi katika ziwa Tanganyika.
“ Kuna kitabu nimekitunga cha mambo ya uchumi
na maisha ya watu wa jimbo la Kigoma Kaskazini nchini Marekani ikiwa ni degree yangu ya PHD ya uchumi katika kitabu
hiki kuna changamoto na kero za wakazi wa jimbo hili na nimeweka nini kifanyike
ili kutatua changamoto na kero na siingii bungeni kwa ubabaishaji lazima
nifanye yale niliyoamua kuyatekeleza katika jimbo hili” alisema dkt. Fubusa.
No comments:
Post a Comment