TABORA WALIA NA MGOMO WA UUZAJI WA PETROLI
Baadhi ya waendesha Bodaboda mjini Tabora wamekusanyika kusuburi kununua mafuta ya Petroli katika moja ya vituo vya kuuzia mafuta hapa mjini Tabora.
Tabora mjini: Mji ambao unatajwa kuwa ni miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa watu kutumia usafiri wa baiskeli na pikipiki.
Baadhi ya watumiaji wa usafiri wa vyombo vya moto ikiwemo pikipiki hapa mjini Tabora wamejikuta wakiwa katika wakati mgumu kutumia usafiri huo kutokana na kukosekana kwa mafuta ya Petroli mjini hapa
Kwa muda wa siku tatu mfululizo kumekuwa na hali ya msongamano katika vituo vya kuuzia nishati hiyo ya Petroli baada ya kudaiwa kuwa wauzaji na wamiliki wa vituo vya mafuta wapo katika mgomo wakishinikiza kupandishwa kwa bei ya bidhaa hiyo muhimu.
Uchunguzi wa mtandao huu umebaini kuwa bei iliyopo sasa ya lita moja kwa shilingi 2,140/= imedaiwa kuwatia hasara wauzaji hao na hivyo kuendesha mgomo wa kimya kimya ambao hauna ukomo.
Taarifa zilizoenea kutoka kwa baadhi ya wamiliki wa vituo vya kuuzia mafuta zimedai kuwa,wauzaji hao wamekuwa wakinung'unikia hilo huku wakidai kuwa thamani ya shilingi inaendelea kushuka wakati wao mafuta waliyonayo wakiendelea kupata hasara kwa kuuza bei hiyo ya shilingi 2,140 kwa lita.
Baadhi ya waendesha pikipiki maarufu bodaboda wamekuwa wakionekana kukusanyika katika vituo vya kuuzia mafuta ambapo baadhi ya vituo vimelazimika kupunguza msongamano walau kwa kuuza lita mbili tu kwa kila pikipiki.
''Kwakweli haya ni mateso na manyanyaso kwetu hebu serikali ingejaribu kuliangalia hili''mmoja kati ya waendesha Bodaboda alisikika akilalamika huku akidai kuwa amepanga foleni kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa tisa mchana ndio akafanikiwa kununua lita mbili za Petroli.