Pages

KAPIPI TV

Showing posts with label DC KINONDONI PAUL MAKONDA. Show all posts
Showing posts with label DC KINONDONI PAUL MAKONDA. Show all posts

Thursday, June 11, 2015

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI PAUL MAKONDA APIGA MARUFUKU UCHIMBAJI MCHANGA MTO MBEZI NA KAWE


 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akizungumza na wakazi wa Mbezi na Kawe Ukwamani ambao nyumba zao zilibomoka kutokana na mmomonyoko wa ardhi uliosababishwa na shughuli za kibinadamu kama vile uchimbaji wa mchanga katika mto huo hali iliyosababisha kingo za mto huo kupanuka hadi kwenye makazi ya watu. Makonda aliwatembelea wakazi hao Dar es Salaam jana.
 DC Makonda akiwa ameongozana na viongozi mbalimbali wakati alipo watembelea waathiriwa hao.
 Wananchi wakiwa katika maeneo hayo yaliyoathiriwa na mmomonyoko huo.
 Baadhi ya nyumba zilizobomoka kutokana na mmomonyoko huo.
Na Dotto Mwaibale

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amepiga marufuku uchimbaji mchanga katika mto Mbezi na Kawe Ukwamani kutokana na uharibifu wa mazingira ambao umesababisha nyumba zilizo kando ya mto huo kubomoka kutokana na mmomonyoko wa ardhi.

Makonda alipiga marufuku wakati akizungumza na wananchi walioathiriwa na mmomonyoko huo alipofika kuwapa pole na kuona jinsi ya kuwasaidia Dar es Salaam jana.

"Wakati tunaangalia namna ya kuwasaidi naomba kuanzisha leo shughuli za uchimbaji wa mchanga katika mto Mbezi ukome na mtu atakaye bainika anaendelea kuchimba mchanga atachukuliwa hatua za kisheria" alisema DC Makonda.

Makonda alisema wataalamu wa Manispaa hiyo watafika katika eneo hilo ili kuona nini kifanyike kupunguza tatizo hilo kwa siku za mbele kama walivyofanya maeneo ya Tegeta yaliyokumbwa na mafuriko ambapo kutajengwa karavati kubwa ili maji yaweze kupita.

Katika eneo hilo nyumba zaidi ya 100 zimebomoka kutokana na kusombwa na maji wakati wa mvua za maisha huku zikiwaacha wakazi wa maeneo hayo wakiishi katika chumba kimoja na wengine wakikosa makazi. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)