Pages

KAPIPI TV

Friday, September 23, 2016

WANAFUNZI KISARAWE NA TABORA KUNUFAINIKA NA MSAADA WA MADAWATI KUPITIA KAMPENI YA SIMAMA KAA INAYOFANYWA NA DR.AMON MKONGA FOUNDATION

Stella Pius Afisa Mawasiliano wa Kampuni ya simu za mkononi ya Halotel(Kulia) akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo kuhusu kampeni ya Madawati mkoani Tabora , katikati ni Mwenyekiti wa Dr. Amon Foundation Bw. Amon Mkoga na kushoto ni Ngo Duy Truong Meneja Masoko Halotel
Mwenyekiti wa Dr. Amon Foundation Bw. Amon Mkoga katikati ,  Ngo Duy Truong Meneja Masoko Halotel, Kushoto na Stella Pius  Meneja Mawasiliano wa Halotel wakionyesha kwa waandishi wa habari mfano wa Madawati ambayo watakuwa wanayagawa kupitia kampeni ya Simama Kaa Desk  itakayofanyika mkoani Tabora na Pwani.
 
Mwenyekiti wa Dr. Amon Foundation Bw. Amon Mkoga  ametoa mchango wa madawati  katika kampeni ya uchangiaji madawati  kwa udhamini wa mtandao wa simu za mkononi wa Halotel hii leo katika ukumbi wa Idara ya Habari  Maelezo jijini Dar-es-Salaam.
 
Akizungumza na waandishi wa habari Amon Mkoga amesema kuwa ili kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. John Pombe Magufuli ,wameandaa kampeni ya “Simama Kaa Desk” Kampeni.,  itakayosaidia kupunguza uhaba wa madawati ikidhaminiwa na Kampuni ya Simu ya  Halotel.
 
“Lengo kubwa la kampeni hii ya “Simma Kaa Desk”   ni kuchangia na kupunguza upungufu  wa madawati katika shule za msingi na sekondari  ili kumuunga mkono rais wa  Tanzania Dk. John Pombe Magufuli, Kampeni hiyo  itaanzia katika mkoa wa Tabora na Pwani tukiwa pamoja na Kampuni ya Halotel.”
 
Aidha afisa mawasiliano wa Halotel Stella Pius amesema kuwa Halotel itakuwa pamoja na Dr Mkoga Foundation kuhakikisha kwamba watakuwa bega kwa bega ili kuwasilisha mchango wa madawati katika elimu.
 
“Ikiwa ni pamoja na kuunga mkono uchangiaji wa madawati Haloteli tutahakikisha katika kampeni hii ya Simama Kaa Desk kampeni,  tunawakilisha mchango wetu tukishirikiana na Dr Amoni Foundation kupitia kampeni hii ambapo  tunaamini kuwa ni njia pekee ya kupunguza uhaba wa madawati mashuleni.”
 
Licha ya hayo pia kutakuwa na burudani ya mziki wakati wa kukabidhi madawati hayo ambayo italetwa na  kundi la muziki wa kizazi kipya la Mabaga Fresh la jijini Dar es salaam.
 

AMON MKOGA
MANAGING DIRECTOR
CHIEF PROMOTIONS
P.O BOX 78566
MOBILE 0755 638 004/0784 772628/0655 638 004
EMAIL dramontz2002@yahoo.com
WEBSITE www.chiefpromotions.or.tz
WEBSITE www.mtemimilambofestival.blogspot.com
DAR ES SALAAM
TANZANIA

No comments: