Pages

KAPIPI TV

Wednesday, November 4, 2015

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI WILLIAM LUKUVI AAGA RASMI SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akipokea ngao yenye picha ya chui ikiwa ni ishara ya tuzo ya Shirika la Nyumba la Taifa kwa Waziri huyo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu kwa kuonyesha utendaji uliokuwa wa kasi usiochoka wakati Waziri Lukuvi alipotembelea katika Shirika hilo kuaga rasmi.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akipokea kadi ya pongezi ya Shirika la Nyumba la Taifa kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Jamii, Susan Omari kwa kuonyesha utendaji uliokuwa wa kasi usiochoka wakati Waziri Lukuvi alipotembelea katika Shirika hilo kuaga rasmi.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza na Wakurugenzi na Mameneja wa Makao Makuu ya Shirika hilo wakati Waziri Lukuvi alipotembelea katika Shirika hilo kuaga rasmi.
Baadhi ya mameneja wa Makao Makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wakifuatilia mazungumzo wakati Waziri Lukuvi alipotembelea katika Shirika hilo kuaga rasmi.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza na Wakurugenzi na Mameneja wa Makao Makuu ya Shirika hilo wakati Waziri Lukuvi alipotembelea katika Shirika hilo kuaga rasmi.
Waziri Lukuvi akizungumza na Wakurugenzi na Mameneja wa Makao Makuu ya Shirika hilo wakati alipotembelea katika Shirika hilo kuaga rasmi kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu.

Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani, Fatma Chillo akizungumza kwa niaba ya Wakurugenzi na Mameneja wa Makao Makuu ya Shirika hilo kumshukuru Waziri huyo wakati Waziri alipotembelea katika Shirika hilo kuaga rasmi.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi ameiagiza Menejimenti ya Shirika hilo kuhakikisha inaendeleza kasi ya ujenzi wa nyumba za makazi na biashara bila kusahau misingi iliyoliunda shirika hilo.

Akizungumza leo wakati akiaga rasmi Shirika hilo alisema amejifunza mengi katika uwepo wake ndani ya Wizara na hasa dhamira na utendaji wa kasi wa Shirika hilo na akaiagiza menejimenti ya Shirika hilo kufanya kazi bila kuchoka likihakikisha linapigania makazi bora kwa kila mtanzania.

"Kabla ya kuingia katika Wizara , na hata nilipoingia sikuwa nafahamu kwa kina kwamba Shirika la Nyumba limebadilika kutoka lile la kuangalia nyumba za msajili wa majumba na kuwa sasa limejenga nyumba nyingi na kuziuza kwa Watanzania, sasa nimefahamu kwa kujifunza kwamba Shirika letu hili limebuni utaratibu unaolifanya lifanye kazi kwa kasi kubwa kibiashara lakini pia likibakia na 'human face', "alisema Lukuvi.

Alisema Serikali inafahamu changamoto linazokabiliana nazo Shirika hilo za ulipaji wa VAT mara mbili na gharama za miundombinu kama maji, umeme na barabara ambazo mara kadhaa zimekuwa zikirudi kwa mnunuzi wa mwisho na kwamba zinafanyiwa kazi pia akaliagiza Shirika na mamlaka hizo kukaa pamoja na kuweka mipango yao pamoja ili angalau kuliwezesha Shirika kuwafikia Watanzania wengi.

Waziri Lukuvi alisema kuwa Serikali inaitambua sekta ya nyumba kuwa ni sekta mtambuka kwa kuwa hukuza uchumi, huongeza ajira na kusaidia kudumisha amani ya nchi yetu. Hivyo, alilihimiza Shirika hilo liendelee na mipango yake kabambe ya kujenga nyumba za gharama nafuu ili kuwawezesha wananchi wengi kumiliki nyumba.

Alisema wananchi wengi wakimiliki nyumba utakuwa mkakati mmojawapo wa kupunguza umaskini nchini maana wananchi hao wataweza kutumia nyumba zao kupata mikopo benki ya kuendeleza shughuli zao za kiuchumi.

Akiungumzia Serikali ya awamu ya Tano ijayo alisema kama kuna watumishi wa umma ambao walikuwa wakifanya mambo kwa mazoea katika awamu zilizopita basi awamu hii wahakikishe wanakuwa mguu sawa kwani Serikali ya Magufuli ambayo inaingia madarakani ni serikali isiyotaka mchezo wala lele mama na kwamba wala rushwa, na wazembe watatafuta mlango wa kutokea.

Akimkaribisha Waziri Lukuvi, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu alisema Shirika hilo linatekeleza miradi yake ili kuhakikisha linaweka makazi bora kwa Watanzania

Alisema kwa shirika hilo lonafanya hivyo kwa kuwa sekta ya nyumba ni sekta mtambuka katika maendeleo ya uchumi. 

Sekta ya nyumba husaidia kuleta maendeleo ya haraka ya sekta zinginena kutoa ajira. Taifa linalozingatia sekta ya nyumba huwezesha nchi yao kuwa na amani, kwani mtu mwenye makazi bora, huthamini uwepo wa amani.

No comments: