Na Magreth Magosso,Kigoma
MGOMBEA Ubunge Jimbo
la kigoma Kaskazini Mkoa wa Kigoma kwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)
Dkt,Yared Fubusa amesema ataendelea kuboresha sekta ya elimu kwa kujenga Chuo kikuu
ili kuongeza tija kwa wakazi wa hapo.
Akitoa kauli hiyo mbele ya wananchi
wa Kata ya Kagongo kwenye mkutano wa
hadhara wa Kampeni anaoendelea kuzifanya katika kata na vijiji vilivyopo katika
Jimbo hilo kwa kusihi wananchi wachague kiongozi mwenye makazi ya kudumu ambaye
atashiriki kikamilifu katika mchakato wa kutatua kero zinazowakabili.
Dkt,Fubusa alisema hivi sasa
anamiliki Shule ya `Gombe school of
Environment and Society’(GOSESO)na mwanzilishi wa ujenzi wa Chuo kikuu ,Gombe
University of Tanzania(GUTA) na msimamizi wa tafiti za wanafunzi wa vyuo vikuu
ndani na nje ya Nchi na mwaka huu shule
hiyo imeshika nafasi ya kwanza kwa ufaulu
wa wanafunzi kwa Kanda Magharibi na kitaifa imenyakua nafasi ya 11.
Alisema maendeleo hayaangalii
vyama ,bali yanahitaji kiongozi mwenye utu,uzalendo na ubunifu wa kutumia uwezo
alionao sambamba na elimu na kunufaisha
jamii, na yalete mabadiliko chanya kwa kuondoa hali ngumu za maisha zinazochangiwa na
mfumo mbovu wa serikali husika kushindwa kuwajibika kwa umma.
Dkt,Fubusa alianisha kuwa
changamoto kubwa iliyopo kwenye Serikali ya Chama tawala (CCM) ni mfumo mbovu
katika usimamizi wa rasilimali watu na mali ,ambapo wachache hunufaika na
rasilimali za taifa,Hivyo hushindwa kudhibiti na kuwawajibisha kwa wakati
wanaotuhumiwa na skendo za ubadhirifu wa mali za umma.
Dkt,Fubusa alieleza kuwa,kijiji
cha Kagongo ni miongoni mwa vijiji vilivyopo pembezoni mwa Ziwa Tanganyika
,ambapo ni walinzi wa hifadhi ya Gombe,ambapo haifaidishi wakazi husika katika
kuboresha kero zilizo ndani ya uwezo wao.
Alisema kisheria hifadhi hiyo inapaswa
asilimia ya mapato yake kwa mwaka ili kutatua kero mbalimbali za kijamii kwa mujibu wa sheria ya maliasili hasa misitu
yenye hifadhi za wanyama na kuahidi akipewa ridhaa hapo ,Octoba,25, mwaka huu
atasimamia hilo ili kuondoa kero ya madawati,vitabu vya ziada na kiada ili
kustawisha jamii lengwa.
Aidha alisema anauhakika wananchi
wana uelewa mpana wa elimu ya uraia kwa kuchagua kiongozi bora na sio bora
kiongozi ,ambao wanadiriki kuhama familia zao na kwenda kupanga katika familia
ya kaya nyingine,ilhali kaya yake inatabika na kero ya nishati ya kuzalisha
viwanda,kilimo cha kisasa kupitia mabonde mtambukwa .
Kwa upande wa Kampeni meneja wa
mgombea huyo Alhaji Salum Ndama alisema,wananchi wa jimbo la kigoma kaskazini
hawana budi kufanya mabadiliko , kwa kuchagua mgombea mwenye vigezo muhimu na
kwa Dkt,Fubusa anatosha kwa kuwa ni msomi pekee aliyewekeza katika sekta ya elimu
na anasomesha watoto wenye mazingira
magumu 38 kila mwaka.



No comments:
Post a Comment