Pages

KAPIPI TV

Thursday, August 13, 2015

"WANAOKATWA CCM HAKUNA SABABU ZA KUHAMA CHAMA!!!"-SEIF GHULAMALI

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Tabora na Mgombea Ubunge wa Jimbo jipya la Manonga wilayani Igunga Bw.Seif Ghulamali,amenaswa kwenye mtandao wa kijamii akitoa maoni yake kuhusu hatua inayochukuliwa na Chama cha Mapinduzi katika kuwaengua baadhi ya wagombea wanaokosa sifa ya kuteuliwa kuwania nafasi za Urais,Ubunge na Udiwani.

"Sioni sababu ya Jina langu kukatwa na hata likikatwa naweza nikawa na sababu Maana nilishinda kura za Maoni,Lakini kwa wale wanaokimbia Chama kwa Kushindwa kura za Maoni Ambapo Wananchi huko Vijijini ndio Wapiga kura na wanasikika wakisema safari hii hatukuhitaji, Tafsiri yake wamekukata Wananchi wenyewe sasa ukihama chama na waliokukata ni haohao Wananchi unakutana nao tena kwa chama kingine kwenye Uchaguzi Mkuu nasema hivi Wananchi WANAKUKATA TU. Hata uhame Chama utakatwa tu na hao hao waliokukata Mwanzo".

No comments: