Pages

KAPIPI TV

Thursday, August 20, 2015

"UCHOYO NDIO UNAWASABABISHA BAADHI YA WABUNGE TABORA MJINI WASIREJEE MADARAKANI"-MWAKASAKA

Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Jimbo la Tabora mjini Bw.Emmanuel Mwakasaka akiwapungia mkono wananchi wakati wa hafla fupi ya kumpokea katika ofisi za Chama hicho wilaya ya Tabora mjini ambapo pia Chama cha Mapinduzi kilimkabidhi barua ya kumtambua rasmi kuwa ndiye aliyeteuliwa na Chama hicho kuwa mgombea atakayepeperusha bendera katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Katibu wa CCM wilaya ya Tabora mjini Bw.Kanuti Ndaghine akimtambulisha mgombea Ubunge Jimbo la Tabora mjini Bw.Emmanuel Mwakasaka wa kwanza kushoto anayefuata ni aliyekuwa  mgombea wa kura za maoni Bw.Mirambo ambaye alipata fursa ya kutambulishwa katika hafla hiyo fupi.
Baadhi ya wananchi wanaomuunga mkono Bw.Mwakasaka walimpokea kwa mabango yaliyoandikwa ujumbe mzito huku wakiahidi kuendelea kumuunga mkono katika Uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu katika kuhakikisha CCM inapata ushindi mkubwa.
Mgombea wa Jimbo la Tabora mjini Bw.Emmanuel Mwakasaka akizungumza na wananchi waliojitokeza kumpokea wakati wa hafla fupi iliyofanyika nje ya Ofisi za CCM wilaya ya Tabora mjini ambapo Mwakasaka alisisitiza umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi na kupiga vita Uchoyo na Ubinafsi.Aidha Mwakasaka ameahidi kushirikiana na Wananchi pasipo ubaguzi wa aina yoyote katika shughuli mbalimbali za kijamii na kupiga vita umasikini. 
"UMOJA NI USHINDI TUTAKUUNGA MKONO WAKATI WOTE KUANZIA SASA NA HATA BAADAE"
Mwakasaka akiteta jambo na Waswezi
Mapokezi makubwa ya mgombea Ubunge wa Jimbo la Tabora mjini Bw.Emmanuel Mwakasaka katika viwanja vya CCM wilaya ya Tabora mijini.








No comments: