Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Hiiti Sillo (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya TFDA Dar es Salaam leo, wakati akitoa tahadhari ya uwepo katika soko wa vipodozi vyenye viambato vilivyopigwa marufuku na Serikali. Kulia ni Mkurugenzi wa Dawa na Bidhaa Nyongeza, Fimbo Mitangu.
Mkurugenzi wa Dawa na Bidhaa Nyongeza, Fimbo Mitangu (kushoto), akizungumza katika mkutano huo huku akionesha moja ya kopo lenye kipodozi vilivyopigwa marufuku. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Uendelezaji Huduma wa TFDA, Chrispin Severe
Mkurugenzi wa Usalama wa chakula, Raymond Wigenge (kushoto) na Mkurugenzi wa Huduma za Maabara wa TFDA, Charys Ugullam (kulia), wakiwa kwenye mkutano huo na wanahabari.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
1.
MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) ni Wakala wa Serikali ulio chini ya Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii wenye jukumu la kudhibiti ubora, usalama na ufanisi wa bidhaa
aina ya chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba.
2.
TFDA
inautaarifu umma kuwa kupitia mfumo wake wa ufuatiliaji ubora na usalama wa
bidhaa kwenye soko, imebaini uwepo wa vipodozi vyenye viambato vilivyopigwa
marufuku aina ya “steroids” zinazojulikana kitaalam kama “clobetasol propionate”, “hydrocortisone”
na “triamcinolone”.
3.
Jumla ya Vipodozi aina tofauti 36 vya jamii ya krimu (creams) na losheni
(lotion) vimebainika kuwa na viambato
hivyo vilivyopigwa marufuku baada ya kufanya uchunguzi wa kina wa matoleo 57 yaliyochukuliwa kwenye soko na
viwanda vilivyotengeneza.
4.
Vipodozi
hivyo vimetengenezwa na makampuni manne (4) yaliyoko hapa nchini na kiwanda
kimoja (1) kilichoko nje ya nchi kama ifuatavyo:-
Na.
|
Jina la kiwanda
|
Idadi ya vipodozi
|
Idadi ya matoleo
|
1.
|
Chemi
& Cotex Industries Limited - Dar es Salaam
|
6
|
7
|
2.
|
Mamujee Products Limited - Tanga
|
11
|
20
|
3.
|
Tanga Pharmaceutical & Plastics Limited - Tanga
|
15
|
24
|
4.
|
Tridea
Cosmetics Limited - Dar es Salaam
|
3
|
5
|
5.
|
Johnson & Johnson (Pvt) Ltd, Rattray Road, East London,
South Africa
|
1
|
1
|
Jumla
|
36
|
57
|
5.
Steroids aina ya “clobetasol propionate”, ‘hydrocortisone’’ na “triamcinolone” hutumika kama dawa
kutibu magonjwa mbalimbali ya ngozi yajulikanayo kitaalam kama eczema, herpes labialis, psoriasis, contact
dermatitis, alopecia areata, vitiligo, lichen sclerosus, lichen planus na mycosis fungoides. Steroids hizi
hazitakiwi kutumika zaidi ya wiki mbili na lazima mgonjwa apate ushauri wa
daktari kabla ya kutumia dawa hizi.
6.
Baadhi
ya madhara yanayotokana na kutumia dawa hizi ni pamoja na muwasho na kuvimba
kwa ngozi (allergic contact dermatitis), ngozi
kuwaka moto (burning sensation), ngozi
kukatikakatika (skin cracking), ngozi
kubabuka (fissuring) ngozi kukosa
chembembe aina ya melanin inayoleta kinga
na hivyo kuifanya ngozi kuwa nyeupe isivyo kawaida (hypopigmentation), madhara
kwenye mifupa (osteoporosis), kizunguzungu (dizziness), ngozi kukauka (skin dryness), shinikizo la damu
kwenye macho (glaucoma), vinyweleo vya
ngozi kupata athari (folliculitis), kuwashwa mara kwa mara (excessive itching, pruritus, erythema and
irritations), vidole kufa ganzi (numbness
of fingers), ngozi kusinyaa (skin
atrophy) na ngozi kubanduka (skin peeling/maceration).
Madhara mengine ni pamoja na ngozi kuwa nyekundu (skin redness), kusikia kichefuchefu (nausea), kichwa kuuma (headache),
kushindwa kupata usingizi (insomnia),
kutoka jasho jingi (sweating), kupata
chunusi kubwa kwenye ngozi (acne),
kuchoka (fatigue), kuongezeka uzito (weight gain), mapigo ya moyo kutoenda
sawa (uneven heartbeats) na kuona
maluweluwe (blurred vision).
7.
Kufuatia
hali iliyojitokeza na kwa kuzingatia madhara yanayoweza kusababishwa na
matumizi ya steroids kwa muda mrefu,
TFDA imechukua hatua zifuatazo:
a. Kuzuia kwa muda wa
miezi sita (6) utengenezaji wa vipodozi aina ya krimu, losheni na jeli kwenye
viwanda vinne (4) vilivyohusika.
b. Kuwaelekeza wenye
viwanda vilivyohusika kuviondoa vipodozi vilivyokutwa na steroids kwenye soko na kuviteketeza kwa gharama zao wenyewe.
c. Kufuta usajili wa
vipodozi 31 vilivyokuwa vimesajiliwa.
d. Kuwaelekeza Mameneja
wa Ofisi za Kanda za TFDA kufanya ukaguzi katika maeneo yao kwa kushirikiana na
Ofisi za Halmashauri ili kuondoa katika soko vipodozi vyote vilivyohusika.
8.
Pamoja
na hatua hizo, TFDA inatoa maelekezo yafuatayo:-
a. Wananchi wote wasitumie
vipodozi husika kwa kuwa vina madhara ya kiafya. Wananchi wanaaswa kuangalia
lebo za vipodozi walivyonavyo majumbani na wakiona vina majina yaliyoainishwa waache
kutumia vipodozi hivyo mara moja.
b. Wasambazaji na wauzaji
wote kurudisha vipodozi vilivyohusika kwa watengenezaji au kwa waliowauzia ili
hatua za uteketezaji ziendelee.
9.
TFDA
inaendelea kufuatilia vipodozi vingine vyote ili kujiridhisha na ubora na
usalama wake kwa watumiaji. Vile vile itaendelea na kazi yake iliyopewa ya
kulinda na kudumisha afya ya jamii kwa kuhakikisha bidhaa aina ya chakula,
dawa, vipodozi na vifaa tiba zinazotengenezwa hapa nchini au kuingizwa kutoka
nje ya nchi ni bora, salama na zenye ufanisi unaotakiwa.
10.
TFDA
itawachukulia hatua kali za kisheria wale wote wanaojihusisha na uvunjaji wa Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Sura
219 na inawaomba wananchi wote kuendelea kutoa taarifa pale wanapobaini
uwepo wa bidhaa (chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba) duni au bandia kwenye
soko la Tanzania.
ORODHA YA VIPODOZI VILIVYOBAINIKA KUWA NA VIAMBATO VILIVYO PIGWA MARUFUKU
Na.
|
Jina la kipodozi
|
Namba ya usajili
|
Toleo
|
Tarehe ya kuishamatumizi
|
Sehemusampuliilipochukuliwa
|
Aina ya kiambatokilichokutwa
|
Chemi&Cotex Industries Limited, Dar es Salaam
|
||||||
1.
|
Lovely Body Cream - Lemon
|
TAN15 CP 0095
|
12&16
|
Feb-18
|
Kwenye soko&Kiwandani
|
ClobetasolProprionate
|
2.
|
Baby Soft Body Lotion
|
Haijasajiliwa
|
08
|
Dec-16
|
Kwenye soko
|
ClobetasolProprionate
|
3.
|
Siri Moisturizing Cream- Cocoa Butter
|
TAN13 CP 3118
|
26
|
Jan-18
|
Kiwandani
|
ClobetasolProprionate
|
4.
|
Siri Moisturizing Cream- Lemon
|
TAN13
CP 3120
|
03
|
May- 18
|
Kiwandani
|
ClobetasolProprionate
|
5.
|
Lovely Body Cream - Lemon
|
TAN15
CP 0094
|
16
|
Mar-18
|
Kiwandani
|
ClobetasolProprionate
|
6.
|
Lovely Body Cream - Papaya
|
TAN15
CP0096
|
10
|
May-18
|
Kiwandani
|
Hydrocortisone
|
Mamujee Products Limited, Tanga
|
||||||
7.
|
Beauty Care Aloe Vera Beauty Cream
|
Haijasajiliwa
|
00283
|
Sep-15
|
Kwenye soko&Kiwandani
|
ClobetasolProprionate
|
No comments:
Post a Comment