Pages

KAPIPI TV

Monday, July 13, 2015

TAMASHA LA NCHI ZA JAHAZI 2015 KUFANYIKA NGOME KONGWE ZANZIBAR KUANZIA JULAI 18 HADI 26

 Mjumbe wa bodi wa Tamasha la Jahazi, Fatma Allo (kulia), akizungumza katika mkutano na wadau wa filamu na wanahabari Dar es Salaam leo jioni kuhusu tamasha la nchi za jahazi litakalofanyika kuanzia Julai 18 hadi 26 mwaka huu Ngome Kongwe mjini Zanzibar.Kutoka kushoto ni Meneja wa Tamasha, Daniel Nyalusy na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tamasha la Jahazi, Martin Mhando.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tamasha la Jahazi, Martin Mhando (kushoto), akizungumza kuhusu tamasha hilo kubwa la jahazi. Kulia ni  Mjumbe wa bodi wa Tamasha la Jahazi, Fatma Allo.
 Meza Kuu. Kutoka kushoto ni Mratibu John Mchaina 'Simple', Mratibu Rehema Jonas, Mjumbe wa Bodi, Mahabobo Champs, Daniel Nyalusy, Ofisa Mtendaji Mkuu, Martin Mhando na Mjumbe wa Bodi, Fatma Allo.
 Baadhi ya wasanii watakaotoa burudani siku hiyo ya tamasha.
 Wanamuziki na  wasanii wa filamu  wakiwa kwenye mkutano huo wa kutambulisha tamasha hilo.
 Mtayalishaji wa muziki, Cadrake Touch (kushoto), Msanii wa filamu Mzee Chilo na mwanamuziki Elias Barnaba wakiwa kwenye mkutano huo.

Wanahabari na wadau wa filamu wakiwa kwenye mkutano huo. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

No comments: