Na Magreth Magosso,Kigoma
WAFANYABIASHARA wanaofanya shughuli za uzaji wa bidhaa za
mashambani Soko la Kalenge,Kijijic ha Kalenge Kata ya Kandaga kilichopo
Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Mkoa wa Kigoma,wapo katika wakati mgumu wa
kuondokana na kero ya ukosefu wa Choo kwa kuwa hawana uongozi wa soko hilo
tangu mwaka 1974.
Soko hilo lenye wafanyabishara wapatao
64 wamezungukwa na uchafu na nyasi ndefu
zilizolificha soko hilo,lenye bidhaa kadhaa hasa maharagwe,mahindi,viazi,ndizi,miwa
na mafuta aina ya mawese ,hali
inayochangia eneo kuwa na harufu nzito kutokana na kujisaidia katika nyasi
hizo.
Wakizungumza na Mtandao huu,Siwema Sadick na Naomi
Kadugu kwa nyakati tofauti walisema soko la kalenge ni moja ya soko kongwe linaloingiza
mapato kwa wingi katika halmashauri ,lakini shida ya choo na uchafu ni kero
kubwa na inawatesa kwa miaka kenda.
Walisema mbali na hilo soko
halina uongozi ndio chanzo cha walengwa kukosa ushirikishwaji katika kupanga kipaumbele
cha mradi wa choo katika soko hilo,ilihali hutozwa sh.3,600 kwa mwezi na wakala wa ushuru lakini hafanyi usafi kwa mujibu wa kanuni na
taratibu za uwakala.
Alipohojiwa Mwenyekiti wa Kijiji
hicho Noel Joel akiri soko halina choo sanjari na kamati husika haina jipya
katika hilo,Wakati huohuo Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Uvinza mabaye
pia ni diwani wa kata husika Fiedli
Kumbo alisema shida ni uelewa wa jamii husika.
Alieleza kuwa,mwaka 2013/14 Asasi
ya( Tcrs) ilitoa mafunzo ya mradi wa ujenzi wa choo bora kwa ghrama nafuu na
wananchi wa kata ya kalenge,mlela na kandaga walishirikishwa cha kushangaza
mwisho wa mafunzo walijenga vyoo majumbani kwa wenyeviti na watendaji wa vijiji
hivyo,badala ya kujenga sokoni.
Alibainisha kuwa,wasitegemee
Serikali katika kutatua kila kero,watumie fursa za wadau wa maendeleo kutambua
vipaumbele vyenye tija kwa umma na wasikubali kuburuzwa na watendaji wa vijiji,ambao
ni chachu ya kufubaza maendeleo ya jamii ikiwa hawatajitambua kupitia adha
zinazowakabili.
Kumbo alisema kuhusu swala la
usafi ni jukumu la wakala wa usafi ambaye anapaswa kusafisha soko kila siku kwa
kuwa anakusanya kiasi cha 3,600 ilihali soko limezingirwa na mazingira machafu
na kuwataka wafanye mchakato wa kuchagua viongozi wa kusimamia haki zao za
msingi hasa choo na usafi wa soko.
No comments:
Post a Comment