Ujumbe wa Waziri wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi umemaliza ziara yake nchini Singapore huku ukiwa umejifunza mambo muhimu ikiwemo kuwepo utawala wa sheria katika usimamizi wa ardhi, kutokuwepo rushwa, nidhamu na uaminifu mkubwa wa watumishi wa umma, jamii inayopenda kujitegemea na usalama wa hali ya juu. Yafuatayo ni matukio ya ziara hiyo kwenye Mamlaka ya Uendelezaji wa Mji wa Singapore(URA) kama yalivyoratibiwa na Muungano Saguya.Ujumbe wa NHC ulipokutana na baadhi ya wawekezaji wakubwa wa sekta ya uendelezaji Miliki wa Singapore ili kuwahamasisha kuwekeza vitega uchumi vya hoteli nchini Tanzania. Ujumbe huu umekutana na Bw. Henry Ngo ambaye ni Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bonvest na Hoteli ya Sheraton Singapore ambao pia wamewekeza Zanzibar Hoteli ya Kitalii.
Ujumbe wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa William Vangimembe Lukuvi ukiwa katika Mamlaka ya Uendelezaji wa nchi ya Singapore(Urban Redevelopment Authority –URA) kujionea namna mamlaka hiyo inavyoratibu ukuaji wa sekta ya nyumba kwa kuweka mipango madhubuti ya matumizi bora ya ardhi kulingana na mahitaji ya Taifa hilo linalotegemea zaidi utalii.
Mchoro unaoonyesha ramani ya nchi ya Singapore ulioko Makao Makuu ya Mamlaka ya Uendelezaji nchi hiyo ukionyesha majengo mbalimbali yaliyoko katika nchi hiyo yenye uhaba mkubwa wa ardhi.
Ujumbe wa Tanzania ukiangalia ramani yenye matumizi mbalimbali yaliyotengwa kwenye ardhi ya Taifa la Singapore. Katika nchi hiyo hakuna uwezekano wa mtu yeyote kuvamia kipande chochote cha ardhi kwa kuwa kila ardhi imepangiwa matumizi yake na kusimamiwa na sheria madhubuti.
Ujumbe wa Tanzania ukitizama maeneo yaliyoendelezwa yenye matumizi mbalimbali nchini Singapore kwenye jengo la makumbusho ya kihistoria ya hatua za ukuaji wa mji huo.
Kamishna wa Ardhi Dk Moses Kusiluka(kushoto)na watendaji wa NHC na Wizara wakipata maelezo kwa njia ya video ya namna mji wa Singapore ulivyopangwa kulingana na ardhi iliyopo na mahitaji ya Taifa hilo.
Ujumbe wa Tanzania ukiangalia kwa chini mchoro wenye ramani ya nchi ya Singapore na jinsi matumizi ya ardhi yanavyoratibiwa ulipotembelea Mamlaka ya Uendelezaji nchi ya Singapore jana.
Makamu wa Rais wa Shirika linalosimamia mipango Miji la Singapore Bw. Anandan Karunakaran(aliyeinama) akimueleza Waziri Lukuvi maeneo mapya yaliyotengwa kwa ajili ya uendelezaji mpya wa mji wa Singapore baada ya kufukia vipande vya bahari(land reclamation) ili kukidhi mahitaji ya sasa na ya baadaye ya idadi ya watu wa nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment