Na Kibada Ernest –Katavi.
Wazazi 25 kutoka Kata za Ikola ,Karema,Kabungu, ,mpandandogo,Katuma
na Mwese Wilayani Mpanda Mkoani Katavi wamefikishwa
Mahakamani kwa makosa ya kusababisha utoro wa watoto wao mashuleni hivyo
kuchangia kushuka kwa kiwango cha elimu wilayani humo.
Kati ya Wazazi hao 25
waliofikishwa Mahakamani kati yao wazazi watatu wanatoka Kata ya Ikola waliohukumiwa
kwenda jela miezi sita au kulipa faini ya shilingi laki tatu kila mmoja ili iwe
fundisho kwa wazazi wengine.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima ameeleza kuwa wazazi wilayani humo wamekuwa chanzo cha utoro
kwa watoto kwa kuwa wanawaacha watoto wao kukaa nyumbani
bila kuchukua hatua yeyote kuhakikisha watoto wao wanaenda shule iwe wanafunzi
wa shule za Msingi na wale wa Sekondari.
Hivyo wanafunzi kukaa kuacha shule na kukaa, nyumbani huku wazazi wakiwa hawachukue hatua zozote za
kuwarejesha shule,ni kuvunja sheria za nchi, hivyo serikali haina budi kuchukua
hatua za kuwarejesha kwa nguvu shuleni kwa kuwa serikali inapenda watu wake
wote wapate elimu kama ilivyo kwenye sera ya elimu watanzania wote kuhakikisha
wanapatiwa elimu.
Watoto hao walikuwa wakisoma katika shule za sekondari
mpandandogo,Ilandamilumba,Ikola,Karema,Kabungu,na mwese, na wengine wa shule za
msingi lazima wote warudi shule.
Kumekuwepo na utoro
warejareja na ule wa kudumu unaosababishwa na kuacha shule na kwenda,kuolewa ,kuoa,mimba
na wengine kuacha bila sababu za msini huku
wazazi wakiwa hawaoni umuhimu wa
elimu katika jamii hiyo na wanawaacha bila kukemea hali hiyo.
Mapema mwaka jana
mwezi wa Disemba Mkuu wa Wilaya Mkuu Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima alitoa amri
halali kwa wazazi wote ambao watoto wao waliacha shule kutokana na utoro
kuolewa,kuozwa au kwenda kufanya shughuli za kilimo kwenye mashamba ya tumbaku,kuvua
samaki,kuchunga,kwenye maeneo ya machimbo na wengine kusikojulikana kurejea shuleni.
Ambapo alitoa mwezi mmoja
kuanzia mwezi wa Disemba mwaka
2014 hadi kufikia mwezi Januari shule zitakapofunguliwa watoto wote walioacha
shule kuanzia shule za msingi,na sekondari
wahakikishe wazazi wanawarejesha shule vinginevyo watachukuliwa hatua za
kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani.
Kufuatia amri hiyo sasa baada ya shuleni kufunguliwa msako
mkali umeanza nyumba kwa nyumba kuwasaka
watoto ambao ni watoro hawajaripoti shule na wazazi wa watoto hao wamekamatwa
na kufikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma hizo za kutowapelekea watoto wao
shule ikiwa ni kutekeleza amri halali iliyotolewa na mkuu wa wilaya ya Mpanda
Paza Mwamlima
No comments:
Post a Comment