Na Magreth Magosso,Kigoma
WANAWAKE wajawazito katika kijiji cha Nyanganga wilaya
ya Uvinza Mkoa wa Kigoma ,wanalazimika kulala chini baada ya kujifungua kwa
kukosa vitanda vya kupumzika katika zahanati ya nyanganga.
Hali hiyo inatokana na uwepo wa
kitanda kimoja cha mbao ambacho ni chakavu ambapo huwalazimika kuwalaza vichanga
wanaozaliwa kwa siku hiyo.
Akizungumza na Jamboleo katika
zahanati hiyo Muguzi wa hapo Mwatatu Mustafa akiri wazazi hutandika kanga chini
baada ya kujifungua kutokana na ukosefu wa vitanda na magodoro ,ambapo tangu
mwaka 2009 alikuta hali hiyo na kitanda kilichopo hutumia kuwalaza watoto.
“wanawake wa huku wanazaa ,ambapo
kwa siku napokea vichanga watano hadi sita,inabidi walale chini ili watoto
walale kwenye kigodolo hiki kama unavyokiona ,
nipo mimi na mganga tu,tunashirikiana na wakunga wa jadi kuwangalia wazazi,hitaji la haraka ni
magodoro matano na vitanda pia” alibainisha Mustafa.
Aidha alisema shida ni mganga wa
kituo hicho kushindwa kufika katika vikao vya kijiji ili kubainisha adha ya
uhaba wa vitanda sanjari na kuvuja kwa nyumba za wauguzi hao,ambapo hulazimika
kuweka beseni vitandani pindi inyeshapo
mvua.
Kwa upande wa wazazi waliokutwa hapo
Eliza Julias na Meri Dafidel kwa nyakati tofauti wakili kulala chini na kwa
siku zaidi ya wajawazito watano hujifungua na ili kulinda afya za watoto
hulazimika kuwalaza watoto katika kitanda kimoja kilichopo na kutandika khanga
zao chini ili wapate kusinzia na uchovu wa kujifungua.
Baadhi ya wakunga wa jadi
waliokutwa hapo Zainabu Ntabindi na Catalina Paulo waliongeza kwa kusema mbali
na kulala chini ,zahanati haina chumba
cha kupumzikia walengwa sanjari na ,Serikali ya wilaya kushindwa kutimiza motisha ya doti moja ya kanga,sabuni na sukari
kwa wakunga wa jadi wanaosaidia uzazi salama kwa mama na mtoto.
Hivyo,Katibu Itikadi na Uenezi wa chama
cha
NRA Taifa Hamis Kiswaga alitoa
godoro tatu ,shuka mbili na vitanda vitatu ili kupunguza adha husika na kumtaka
Mbunge wa Jimbo la kigoma kusini David Kafulila atimize ahadi yake ya vitanda
100 alivyoahidi mwaka 2010 akiwa ana tija ya kuendelea kuwa mbunge jimboni
mwake .
No comments:
Post a Comment