Pages

KAPIPI TV

Tuesday, February 24, 2015

PSPTB YAFANYA SEMINA YA UTAFITI KWA WANAFUNZI WA BODI YA WATAALAMU WA UNUNUZI NA UGAVI

Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi PSPTB imeendesha mafunzo kwa wanafunzi wa fani ya ununuzi na ugavi wanaofanya tafiti kama sehemu ya mafunzo yao ya shahada ya
Ununuzi na ugavi.

Mafunzo hayo yalifunguliwa tarehe 16 Februari 2015 na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi Dr. Clemence Tesha, ambaye aliwaasa wanafunzi hao wazingatie mafunzo hayo ili kuongeza ubora wa kazi za utafiti watakazofanya kwa ajili ya kupata shahada ya juu ya ununuzi na ugavi. Aidha, alisisitiza kuwa wanapaswa kuzingatia maadili katika kufanya utafiti, jambo ambalo ndio msingi na matakwa ya Bodi. 

wanafunzi wanatakiwa kufanya utafiti wao wenyewe na sio kuchukua kazi zilizofanywa na wanafunzi/watafiti wengine au kufanyiwa na watu wengine maana kufanya hivyo ni kuvunja sheria.

Pamoja na kuwajengea uwezo wa kufanya utafiti, pia wanafunzi wanajengewa uwezo wa kujiamini, kuandika ripoti na kujieleza na hata kuwasilisha ripoti katika sehemu zao za kazi. Hivyo lengo kuu la semina hii ni kuwajengea uwezo wa kuandika, kujieleza na kutoa huduma bora kwa taifa, kwani ufaulu wa mwanafunzi, unategemea sana uwezo wake wa kuitetea kazi yake, ambapo katika mtihani huo mwanafunzi atawasilisha kazi yake mbele ya wataalam, ili kupima uwezo wake.
New Picture (88)Mr. Godfred Mbanyi, Mkurugenzi wa Mafunzo PSPTB akitoa neno katika ufunguzi wa semina ya utafiti iliyofanyika kwenye ukumbi wa TEC Kurasini Dar es Salaam tarehe 16/2/2015
New Picture (89)
Mkurugenzi wa mafunzo Mr. Godfred Mbanyi akimkaribisha Mkurugenzi mtendaji wa PSPTB Dr. Clemence TEsha kufungua semina ya utafiti katika ukumbi wa TEC Kurasini Dar es Salaam. Tarehe 16/02/2015
New Picture (90)Picha ya pamoja ya Mkurugenzi mtendaji wa PSPTB na washiriki wa semina ya Utafiti iliyofanyika Katika ukumbi wa TEC Kurasini Dar es Salaam tarehe. 16/2/2015.
New Picture (91)Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB Dr. Clemence Tesha(aliyeketi katikati), mwezeshaji wa semina Dr. Eli Tumsifu (aliyeketi kushoto) na Mr. Godfred Mbanyi Mkurugenzi wa mafunzo (aliyeketi kulia) katika picha ya pamoja na washiriki wa semina
New Picture (92)Washiriki wa Semina ya utafiti wakimsikiliza mwezeshaji Dr. Eli Tumsifu toka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwenye semina ya utafiti iliyofanyika katika ukumbi waTEC Kurasini Dar es Salaam tarehe. 16-20 Februari 2015
New Picture (93)Dr. Eli Tumsifu akiwa na washiriki wa semina ya utafiti ya PSPTB ndani ya ukumbi wa TEC Kurasini Dar es Salaam tarehe 16-20 Februari 2015
New Picture (94)Washiriki wa semina ya utafiti ya PSPTB wakiwa na Mkurugenzi mtendaji wa PSPTB Dr. C. Tesha (aliyeketi katikati), Dr. Eli Tumsifu Mkufunzi wa semina (aliyeketi kushoto) na Mkurugenzi wa mafunzo wa PSPTB Mr. Godfred Mbanyi (aliyeketi kulia) wakati wa semina yautafiti iliyofnyika 16-20 Februari 2015 katika Ukumbi wa TEC Dar es Salaam.

No comments: