Na Magreth Magosso,Kigoma
MTU mmoja Niyubuntu Finias(22) raia wa kijiji cha Kabomyange Nyanzalac Nchini Burundi
amekufa papo hapo, baada ya kuangukiwa na mti uliokuwa nyuma ya nyumba
aliyokuwa amejikinga kutokana na mvua kubwa ilioambatana na upepo mkali .
Mbali na hilo mvua hiyo imeleta janga kwa Watu saba kukosa
makazi ya kuishi na kujeruhi watu wanne
akiwemo mwanafunzi Teddy Kihagilo(8) anayesoma darasa la pili katika shule ya
msingi Ilagala kwa kukatwa na bati visogoni
wengine ni Isihaka Ngozi(5),Rahabu
Fredirick(14) na Damiano Fredirick (15) ambao wanauguza majeraha katika
zahanati ya kijiji hicho.
Tukio hilo limetokea Februari ,13 ,jioni katika Kijiji cha Ilagala kitongoji
cha Lugongoni kilichopo wilayani Uvinza mkoa wa kigoma,ambapo marehemu alikuwa
akilima shamba na alipoona mvua kubwa na upepo mkali alijibanza katika kibanda chake kilichopo shambani, hatimaye
kuangukiwa na mti mkubwa uliokuwepo karibu na kibanda na kupoteza maisha.
Wakizungumza na gazeti hili Kabichi Matisho ni muhanga na
shuhuda Abdala Mpolwe kwa nyakati tofauti walisema janga hilo lilitokea jioni
ya jana(juzi) na kwa sasa wahanga wanaishi kwa wasamaria wema,wakisubiri msaada
wa hifadhi kutoka Serikali ya wilaya ya
Uvinza.
Akifafanua hilo Mwenyekiti wa kijiji cha ilagala Jumanne
Kisiki alisema marehemu ni raia wa nchi ya Burundi alikuwa kibarua wa kulima
shamba hadi mauti yanamkuta na atazikwa
leo(jana) kutokana na sintofahamu ya famila yake na kuwataka wananchi wafichue
wahamiaji wasio rasmi .
Alisema wanasubiri kikao cha kamati ya maafa ili kujadili
hatma ya wahanga hao,huku Diwani wa kata ya ilagala Hamis Mkwafi adai polisi
watashughulikia suala ya maiti na kumwandikia mkuu wa wilaya hiyo barua ya kushiriki kikao cha kamati husika,ili
kunusuru hifadhi ya walengwa.
Akithibitisha hilo Kamanda wa Polisi Kigoma Jafari Mohamed
alisema ni kweli marehemu ni raia wa Burundi na maiti imehifadhiwa katika
zahanati ya ilagala sanjari na zaidi ya kaya sita kupoteza makazi kutokana na mvua hiyo.
No comments:
Post a Comment