Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka Bw. Alex Msama akikabidhi vyakula mbalimbali kwa Halima Ramadhan Mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Mwadaliwa kilichopo Tegeta jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, ikiwa ni moja ya misaada inayotolewa katika vituo mbalimbali vya kulelea watoto yatima wakati wa msimu huu wa maadalizi ya Tamasha la Pasaka linalotimiza miaka 15 tangu lianzishwe.
Tamasha hilo Litafanyika jijini Dar es salaam Aprili 7 2015 na kushirikisha waimbaji mbalimbali wa kimataifa na waimbaji wa ndani, Katika Tamasha hilo pia kutakuwa na michezo mbalimbali itakayochezwa ikiwa ni pamoja na kukabidhi zawadi na vikombe kwa washiriki wa Tamasha hilo, Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye ofisi za kampuni hiyo zilizoko Kinondoni jijini Dar es salaam.
Alex Msama amelaani mauaji ya Albino na kuiomba serikali kuweka mkazo katika kushughulikia wahalifu wanaofanya ukatili huu na kuua watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino), ili kukomesha mauaji hayo hapa nchini ambayo yanalitia aibu taifa(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM) Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka Bw. Alex Msama akikabidhi vyakula mbalimbali kwa Honorata Michael Mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Honorata kilichopo Temeke jijini Dar es salaam. Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka Bw. Alex Msama akikabidhi vyakula mbalimbali kwa Rashid Mpinda Katibu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre kilichopo Kinondoni Mosco jijini Dar es Sakaam. Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka Bw. Alex Msama akikabidhi vyakula mbalimbali kwa Soud Said Mwakilishi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Ijanzo Zanda orphanage Centre cha jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka Bw. Alex Msama akikabidhi vyakula mbalimbali kwa Hadija Mwambungu kutoka kituo cha kulelea watoto yatima cha Malaika Kids kilichopo Mwananyamala Mwinjuma jijini Dar es salaam. Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka Bw. Alex Msama akiakihelezea zaidi kwa waandishi wa habari juu ya misaada hiyo iliyotolewa na kampuni yake kwa vituo hivyo wakati huu wa maandalizi ya tamasha la Pasaka. Mmoja wa waratibu wa tamasha hilo Bw Hudson Kamoga akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya tamasha la pasaka. Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka Bw. Alex Msama akiakiwa amewabeba baadhi ya watoto wa kituo cha Honorata wakati alipowakabidhi msaada wa vyakula mbalimbali. Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka Bw. Alex Msama akihojiwa na mwaandishi wa habari wa BBC Bw. Anold Kayanda mara baada ya kukabidhi misaana hiyo ambapo aliiomba serikali kuweka mkazo katika kushughulikia wahalifu wanaoua watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino)ili kukomesha mauaji hayo hapa nchini
No comments:
Post a Comment