Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa NIC Bw. Justin Mwandu akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma za shirika hilo kupitia mkongo wa taifa wa mawasiliano ambapo matawi yote nchini ya shirika hilo yameunganishwa pamoja na makao makuu ili kurahisisha huduma za bima zinazotolewa na Shirika hilo nchini kote, Amesema kwa sasa baada ya Kampuni ya simu ya TTCL kufanya kazi nzuri ya kuunganisha mtandao wa huduma za NIC nchini kote kupitia mkongo wa mawasiliano wa taifa mteja anaweza kuhudumiwa mahali popote kama vile yuko makao makuu ya NIC Dar es salaam bila kufuata huduma hiyo mbali. Hafla hiyo imefanyika kwenye makao makuu ya NIC mtaa wa Samora jijini Dar es salaam leo, Katika picha kulia ni Mkurugenzi wa shirika la simu Tanzania TTCL Dr. Kamugisha Kazaura. Mkurugenzi wa shirika la simu Tanzania TTCL Dr. Kamugisha Kazaura akielezea kazi nzuri iliyofanywa na shirika lake la TTCL katika kuunganisha matawi ya NIC mikoani na Makao makuu ili kuleta pamoja huduma za bima zinazotolewa na shirika hilo hapa nchini, Kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa NIC Bw. Justin Mwandu. Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa NIC Bw. Justin Mwandu. akipokea cheti kutoka kwa Mkurugenzi wa shirika la simu Tanzania TTCL Dr. Kamugisha Kazaura mara baada ya kukamilisha kazi ya kuunganisha shirika hilo na mkongo wa mawasiliano wa taifa. Mkurugenzi wa shirika la simu Tanzania TTCL Dr. Kamugisha Kazaura na wa tatu kutoka kulia na Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa NIC Bw. Justin Mwandu wa pili kushoto wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa hafla hiyo kutoka kushoto ni Meneja mradi Bw. Mihayo Ngawalina kutoka TTCL , Mtaalam wa Idara ya Teknohama NIC Bw. Sam Kamanga na kushoto ni Peter Ngota Afisa Mauzo na Masoko TTCL. Mtaalam wa Idara ya Teknohama NIC Bw. Sam Kamanga akizungumza na kuuelezea mradi huo wakati wa hafla hiyo kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa NIC Bw. Justin Mwandu na Mkurugenzi wa shirika la simu Tanzania TTCL Dr. Kamugisha Kazaura. Meneja mradi Bw. Mihayo Ngawalina akielezea jinsi mradi huo ulivyotekelezwa na faida zake kwa Shirika la Bima la Taifa NIC. Baadhi ya maofisa na wakuu wa vitengo kutoka Shirika la Bima la Taifa NIC wakifuatilia jambo wakati Meneja mradi wa TTCL alipokuwa aiuelezea. Kutoka kulia ni Maofisa kutoka mashirika hayo Leonard Laibu Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja, TTCL,wa tatu Peter Ngota Afisa Masoko na Mauzo na Sam Kamanga Mtaalam wa Teknohama NIC Leonard Laibu Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja, TTCL kulia na baadhi ya maofisa wa shirika hilo wakiwa katika hafla hiyo. Baadhi ya wanahabari waliohudhuria katika hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment