Na Magreth Magosso,Kigoma
INADAIWA kuwa,Wabunge 36 kutoka Chama cha CCM na 28 kutoka vyama vya upinzani
watahamia chama kipya chenye miezi tisa tu,Alliance &Transparency For Change Tanzania (ACT) kwa lengo la
kuongeza uwajibikaji katika chama hicho na kuleta mabadiliko chanya ya huduma
za wananchi.
Pia ,ili kukabiliana na uchaguzi mkuu wa kuchagua madiwani,wabunge
na rais ambao utakaofanyika Octoba ,mwaka huu ,ACT kimetayarisha wagombea 92 watakaonyakua viti vya ubunge katika mikoa
27 iliyopo nchini.
Hayo yalibainika jana kigoma ujiji katika mdahalo
ulioandaliwa na asasi ya kiraia ya Meza ya duara ya watanganyika,ambapo Ofisa
habari Taifa wa chama hicho Karama Kaila alisema hivi karibuni wadau wa siasa
watarajie kuwapokea wabunge hao ,ambao wanataka kufanya kazi kwa umoja ,uwazi
na uwajibikaji kwa lengo la kuondoa mfumo hasi wa chama tawala.
Kaila alisema watarudisha hifadhi ya jamii bila kujali tabaka la walionacho na wasionacho ili kuleta
usawa katika jamii sanjari na kuwaeleza wananchi sera na mlengo wa chama hicho
chenye miezi tisa tangu kuanzishwa kwake,huku wakazi wa kigoma kuwa kinara wa
kuimarisha chama hicho.
Alisema kigezo kikubwa cha kuwapokea wabunge husika ni pamoja
na uwajibikaji katika majimbo yao hususani ahadi binafsi walizozitoa kwa
wananchi husika ziwe zimemalizika kwa
wakati kabla ya uchaguzi mkuu kwa njia
ya kintelejinsia ,ili kuondoa dhana ya viongozi wengi waliojiunga na chama
hicho waliharibu majimboni mwao.
“Viongozi wa ACT mkoani humu mkiamua kumwalika Zitto Kabwe
aje kufafanua jambo takuja ,namanisha kisiasa yeye ni wa kwetu ila kisheria si
wetu,tunmasubiri barua ya wahusika ili ajenge chama kwa uhuru na haki bila
bughudha” alisema Ofisa habari huyo
.
Alisema changamoto ya migogoro katika chama itarataibiwa na kusuluhishwa na kamati za
usuluhishi na kusema mzozo wa awali ulitokana na udhibiti wa fedha za chama
,ambapo baadhi ya viongozi walizoea mfumo wa 10% wa kuongeza fedha ya ziada katika
hitaji la manunuzi ,kutokana na udhibiti wa mweka hazina ndio chachu ya
yaliyotokea .
Kwa upande wa Katibu wa Jimbo la kigoma mjini Azizi Ally
alisema miongoni mwa wabunge watakaohamia ni Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini
Zitto Kabwe ,Jimbo la Uvinza Davidi
Kafulila na Felix Mkosamali Jimbo la Muhambwe na kudai wandishi wa habari walijiunga na vyama vya saisa hawatendi haki
katika taluma yao.
No comments:
Post a Comment