Pages

KAPIPI TV

Monday, January 5, 2015

RAIS JAKAYA KIKWETE AKIREJESHA KIWANDA CHA CHAI CHA MPONDE LUSHOTO KWA WANANCHI

1Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Bumbuli Mh. Januari Makamba wakati alipowasili jimboni humo katika wilaya ya Lushoto. akiwa katika ziara ya siku mbili ambapo amefanya mkutano wa hadhara katika kata ya Mponde na kuwataarifu wananchi na wakulima wa Chai kuhusu maagizo ya Rais Jakaya Kikwete juu ya kukirejesha kiwanda cha Chai cha Mponde kwa wananchi , Awali kiwanda hicho kilikuwa kinamilikiwa na Mwekezaji Yusuf Mulla na kilifungwa kutokana na mgogoro wa wakulima wa Chai na mwekezaji huyo . Rais Jakaya Kikwete amechukua uamuzi huo baada ya katibu Mkuu wa CCM Ndugu Andulrahman Kinana kusikiliza kero hiyo ya wananchi wakati alipofanya ziara ya mkoa wa Tanga na kuahidi kufuatilia ili kuhakikisha suluhisho la kudumu linapatikana na wakulima hao wanapata haki yao. Mgogoro huo umedumu kwa muda wa miaka kumi na kiwanda hicho kimefungwa kwa muda wa miezi ishirini kabla ya Rais Jakaya Kikwete kufikia uamuzi wa kukirejesha kwa wananchi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-BUMBULI-LUSHOTO) 2Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ukiwasili katika eneo la mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Mponde katika jimbo la Bumbuli wilayani Lushoto. 3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akielekea kwenye eneo la Mkutano mara baada ya kushuka kwenye gari. 4Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mwenyekiti wa Wakulima wa Chai Bw. Almasi Kassimu ambaye alikuwa kiungo kikubwa katika kupatikana kwa suluhisho hilo. 5Baadhi ya wananchi wakiwa wamefurika kwenye eneo la mkutano wa hadhara. 6 7Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Mhe. Majid Hemed Mwanga akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo kijiji cha Mponde mkoani Tanga. 8Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mh. Mrisho Gambo akisalimia wananchi katika mkutano huo. 9 Mmoja wa wananchi kijiji cha Mpond akipiga makofi huku akiwa amevaa sanamu 10Mkuu wa mkoa wa Tanga Mh. Magalula Said Magalula akisalimiana na wananchi na kujitambulisha kwao kama mkuu wa mkoa huo. 11Mbunge wa jimbo la Lushoto Henry Shekifu akiwahutubia wanamponde. 12Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa na wakulima wa Chai Mponde wakati alipofika kijijini hapo ili kuwataarifu juu ya rais Jakaya Kikwete kuamuru Kiwanda cha Chai cha Mponde kurejeshwa kwa wananchi. 13 14Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Chai Tanzania Injinia Mathias Asenga aliyekuwa akiwaeleza wanachi juu ya kumalizika kwa mgogoro huo. 15Mbunge wa jimbo la Bumbuli Mh. Januari Makamba akimshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa uamuzi wake wa kukirejesha kiwanda hicho kwa wananchi na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwa kushughulikia mgogoro huo mpamka kufikia mwisho. 16Mbunge wa jimbo la Bumbuli Mh. Januari Makamba akiendelea kuzungumza na wananchi katika mkutano huo. 17Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati alipokuwa akiongea na wananchi katika mkutano huo wa hadhara.

No comments: