Zaidi ya wahamiaji walowezi 6,000 katika manispaa ya kigoma
ujiji mkoani kigoma,wamefanikiwa kupata hati ya utambulisho wa kuishi kisheria ,kutokana na juhudi ya serikali kwa
kushirikiana na Shirika la Kimataifa la wakimbizi (IOM na U.K AIDS) kuwezesha zoezi la kuwatambua na kuandikisha wageni,linaloendelea
mkoani humo.
Hayo yalibainishwa na Mkuu wa idara ya uhamiaji kigoma Ebrosy Mwanguku kigoma ujiji juzi katika uwanja wa Lake Tanganyika
kwenye uzinduzi rasmi wa kuandikisha raia
walowezi,wakimbizi waliopewa uraia 1980,watoto wa waliopewa
uraia,waliooa/kuolewa na watanzania .
Lengo la kufanya hivyo,ni kutambua uwepo wao na taarifa kuhifadhiwa katika `Kanzi data’ ili kubaini wahalifu wa
matukio ya ujambazi sanjari na kuepusha migogoro ya uraia katika kipindi cha chaguzi
za kugombea nyadhifa mbalimbali za madaraka kama
ubunge,udiwani,uenyeviti wa mitaa na
urais.
Alisema zoezi lipo katika mkoa wa kigoma,Kagera na Geita
kutokana na mikoa hiyo kuwa na changamoto kubwa ya kuwa karibu na nchi jirani
husika,ambapo kwamakundi mtambukwa wanapewa fursa ya kujiandikisha ili
waepukane na adha ya operesheni ya kamatakamata (uhamiaji usio rasmi).
Kamishna wa uhamiaji na udhibiti wa mipaka Abdallah
Khamis akiri walowezi wapo wengi nchini ,ambapo
kipindi cha mwezi uliopita baada ya kutangaza zaidi ya kaya 6000 wamejitokeza
ambapo ni miongoni mwa makundi mtambukwa,na kwa wilaya ya kigoma watu 1050
washapata vitambulisho husika.
Pia walowezi watapaiwa huduma za msingi ndani ya nchi na
kudai kigoma ni chachu ya mafanikio ya mpango huo,ambao ni tija ya kubaini
wahalifu na wanaovamia jukwaa la siasa kinyume cha vigezo vya kufanya hivyo na
kuishukuru( IOM),Uk ,aids kwa kuwezesha zoezi hilo endelevu nchini.
Kwa upande wa
Mwakilishi wa shirika la kimataifa la wakimbizi ( IOM ) Tamara Keating alisema
wahamiaji walowezi na waliopewa uraia mwaka 1980 sanjari na waliooa na kuolewa
na raia wa hapa wakitaka kurudi kwenye asili ya nchi yao watasaidia kuwasafirisha
na mtaji wa kuanzia maisha ya huko.
“fursa hii ni ya
kipekee ambapo mhanga ataandaliwa mazingira mazuri ya kuishi kwenye nchi yake
kwa kuwezeshwa huduma zote za msingi ikiwemo malazi,chakula na fedha za kuanzia
maisha ili wapate yote wanahitajika wajiandikishe kwa muda uliopo wakipuuza
wasilaumiwe” alisema Keating.
Kaimu mkurugenzi idara ya wakimbizi mambo ya ndani Philo
Nondo aliwahimiza walengwa watumie fursa waliyopatiwa na serikali kwa kushirikiana
na( IOM ,Uk.Aids) kufanikisha mchakato
huo,ambao ni chachu ya kuondoa operesheni tokomeza zilizoweka majeraha kwa
baadhi ya wahanga.
Mchungaji wa kanisa la (PEFA) Mwananzambe Bugondo alisema serikali inathamini maisha ya
wahamiaji wasio rasmi,awali waliishi kwa woga hali iliyochangia ashindwe
kuwekeza kwa moyo mkunjufu na kushauri walengwa wa kigoma watumie fursa hiyo.
No comments:
Post a Comment