Pages

KAPIPI TV

Thursday, December 11, 2014

UN YATAKA SERIKALI KUFANYIA KAZI MIANYA INAYOTISHIA HAKI ZA BINADAMU

HUMAN RIGHTS DAY 2014
Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bibi Mary Massay akitambulisha meza kuu wakati wa maadhimisho ya Siku ya haki za binadamu yaliyoenda sambamba na mkutano wa kujadili utekezaji wa makubaliano ya haki za binadamu nchini na maandalizi ya ripoti ijayo yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog).

Na Mwandishi wetu
MRATIBU Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez ameitaka serikali ya Tanzania pamoja na mafanikio makubwa katika kufanikisha amani na kutia saini mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu, kufanyia kazi maeneo kadhaa ambayo bado yanatishia sifa nzuri ya taifa hili.

Maeneo hayo ni mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, wanawake vikongwe na ukatili kwa watoto.

Alisema taifa hili ambalo limekuwa kimbilio la wakimbizi,kuukubali kuwa makao ya mahakama mbili kubwa za kimataifa zinazoshughulikia haki za binadamu (ICTR na African Court of Human rights) sasa linashuhudia madhila kwa baadhi ya wananchi wake ambao huuawa kwa imani za kijinga.

Akizungumza katika siku ya mataifa ya haki za binadamu mjini hapa, Mratibu huyo pamoja na kutoa ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, alisema ili Tanzania iweze kutekeleza kwa umakini kauli mbiu ya mwaka huu “haki kwa wote siku zote 365” maeneo yaliyotajwa yanastahili kufanyiwa kazi kwani ni changamoto kubwa.
IMG_6700
Mgeni rasmi Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mh Ali Hassan Rajab akizungumza wakati wa akifungua mkutano wa kujadili utekezaji wa makubaliano ya haki za binadamu nchini na maandalizi ya ripoti ijayo ulioenda sambamba na maadhimisho ya siku ya haki za binadamu duniani.

Alisema Tanzania ambayo imetia saini na kuridhia mikataba ya haki za binadamu kama ya kuwatambua walemavu, kukabili ubaguzi dhidi ya wanawake (CEDAW) na ule wa kulinda haki za watoto (CRC) inaposherehekea siku ya haki za binadamu inakabiliwa na doa hilo la ukatili miongoni mwa watu wake.

Alisema ipo haja ya kuimarisha usalama wa makundi hayo kwa kuhakikisha kwamba mashauri yao mahakamani yanamalizika na haki kuonekana kutendeka .
Alisema familia ambazo zimepoteza watu wake kwa namna ya kikatili wanahitaji si tu kuona haki inatendekea bali wahusika wake wakichukuliwa hatua na ulinzi kwa makundi hayo ukiimarishwa.

Aidha alisema kwamba anapata maumivu makubwa anaposikia kuwapo na taarifa nyingi za ukatili kwa watoto na kuendelezwa kwa mila mbaya zinazofunika haki za msingi huku wahusika wakiwa hawachukuliwi hatua au upelelezi ukidaiwa bado kukamilika.
DSC_0110
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisoma hotuba kwenye maadhimisho ya siku ya haki za binadamu duniani yaliyoenda sambamba na mkutano wa kujadili utekezaji wa makubaliano ya haki za binadamu nchini na maandalizi ya ripoti ijayo.

Alisema kitendo cha kuchelewesha haki kutokana na upelelezi kutokamilika au kushindikana kutokana na kukosekana kwa fedha au familia zenyewe kushindwa kutafuta haki kutokana na kutokuwa na fedha kunavuruga jina zuri la nchi hii ambayo ina makabila mengi na tamaduni tofauti.

Alisema pamoja na ukweli kuwa matendo hayo kisheria ni haramu kukosekana kwa utashi kwa viongozi kukabiliana na changamoto zilizopo na kuachwa kwa mila mbaya kunawafanya wananchi wabaki katika mazingira ya kutotendewa haki.

Alisema mfumo wa sheria lazima uonekane kufanya kazi ili kukabiliana na wavunjaji wa haki za binadamu.

“Ni matumaini yangu kwamba serikali ya Tanzania itaonesha kuwajibika kwake na kuhakikisha inaangalia changamoto hizi na kuziondoa ili kuwezesha kutekeleza haki za binadamu saa 24, siku saba za juma na siku 365 za mwaka” alisema na kuahidi kwamba Umoja wa mataifa katika hilo utaendelea kutoa ushirikiano.
IMG_6647
Mkuu wa Balozi za Umoja wa Ulaya (EU) nchini Tanzania na Afrika Mashariki, Mh. Filiberto Ceriani-Sebregondi akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya haki za binadamu duniani yaliyoenda sambamba na mkutano wa kujadili utekezaji wa makubaliano ya haki za binadamu na maandalizi ripoti ijayo.

Aidha alisema kwamba UN itaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kuimarisha kamisheni ya haki za binadamu na utawala bora (CHRAGG) na taasisi nyingine za kijamii kuhakikisha kwamba kuna mfumo wa kulinda haki za biandamu.

Aidha mratibu huyo ameitaka serikali ya Tanzania kukamilisha uongozi wa CHRAGG na pia kuangalia watetezi wa haki za binadamu wanapata ulinzi wa kutosha dhidi ya watu wanaowatishia maisha.

Naye Mkuu wa Balozi za Umoja ya Ulaya (EU) nchini Tanzania na Afrika Mashariki Filiberto Ceriani-Sebregondi ameitaka serikali ya Tanzania kuangalia mapendekezo matatu iliyokataa ambayo yanagusa haki za binadamu.

Mapendekezo hayo yalikuwamo katika mfumo wa Umoja wa mataifa wa kupitia mambo mbalimbali yanayohusu haki za binadamu (UPR).
DSC_0108
Meza kuu kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bibi Mary Massay, Mkuu wa Balozi za Umoja wa Ulaya (EU) nchini Tanzania na Afrika Mashariki Filiberto Ceriani-Sebregondi, mgeni rasmi Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mh Ali Hassan Rajab na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez katika maadhimisho ya siku ya haki za binadamu duniani yaliyoenda sambamba na mkutano wa kujadili utekezaji wa makubaliano ya haki za binadamu na maandalizi ripoti ijayo.

Balozi huyo alitaja mapendekezo hayo ni pamoja na kufuta adhabu ya kifo, kuweka umri unaoruhusu ndoa na kuchukua hatua za kulinda waandishi wa habari na kulinda utamaduni wa wananchi wake.

Alisema mambo hayo ni sehemu muhimu ya kutekeleza maazimio ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu.

Aidha balozi huyo pia aliitaka serikali kukamilisha kamisheni ya haki za binadamu na utawala bora na kuiwezesha kufanyakazi zake zinazopaswa ikishirikiana na asasi za kiraia na wadau wengine wa haki za binadamu.

Hata hivyo alisema jumuiya hiyo itaendelea kufanyakazi na serikali katika kuhakikisha kwamba haki za binadamu zinazlindwa.

Hata hivyo balozi huyo amesema ni vyema kuendelea kuyafanyia kazi mapendekezo mengine 119 ambayo serikali ilikuwa imeyakubali na kuonesha mafanikio yake katika majadiliano yajayo.
IMG_6732
Pichani juu na chini ni baadhi ya mabalozi, wadau wa haki za binadamu na wageni waalikwa wakifuatilia hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika maadhimisho ya siku ya haki za binadamu duniani yaliyoenda sambamba na mkutano wa kujadili utekezaji wa makubaliano ya haki za binadamu na maandalizi ripoti ijayo.
IMG_6638
IMG_6633
IMG_6630
IMG_6739
Nkason Sarakikya kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali akitoa tathmini ya hali ya haki za binadamu Tanzania kwenye maadhimisho ya siku ya haki za binadamu duniani yaliyoenda sambamba na mkutano wa kujadili utekezaji wa makubaliano ya haki za binadamu na maandalizi ripoti ijayo.
DSC_0193
Balozi Mdogo anayeshughulikia masuala ya habari na siasa kutoka Jumuiya ya Ulaya Tanzania, Bi. Laura REALE, akiuliza swali kuhusiana na uboreshaji wa sheria ya ndoa za utotoni kwenye mkutano wa kujadili utekezaji wa makubaliano ya haki za binadamu na maandalizi ripoti ijayo wakati maadhimisho ya siku ya haki za binadamu duniani.
DSC_0176
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt. Natalia Kanem akizungumza kwenye mkutano huo wa kujadili utekezaji wa makubaliano ya haki za binadamu na maandalizi ripoti ijayo.
IMG_6584
DSC_0186
Dr. Khoti Kamanga kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Kitivo cha sheria akitoa maoni kwenye mkutano wa kujadili utekezaji wa makubaliano ya haki za binadamu na maandalizi ripoti ijayo.
IMG_6762
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu (katikati), Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama pamoja na Afisa Habari wa Umoja wa ulaya Tanzania (EU), Susanne Mbise (kushoto) katika picha ya pamoja.
DSC_0089
Mkuu wa Balozi za Umoja wa Ulaya (EU) nchini Tanzania na Afrika Mashariki, Mh. Filiberto Ceriani-Sebregondi (kushoto) akiteta jambo na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati). Kulia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bibi Mary Massay.
IMG_6556
Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu THRDC Taifa, Bw. Onesmo Olengurumwa akiteta jambo na Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mh. Lennarth Hjelmaker wakati wa mkutano wa kujadili utekezaji wa makubaliano ya haki za binadamu na maandalizi ripoti ijayo ulioenda sambamba na maadhimisho ya siku ya haki za binadamu duniani.
IMG_6533
Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe,Egon Kochanke ( wa pili kushoto) akibadilishana mawazo na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mh. Diana Melrose (wa pili kulia) pamoja na wakili wa serikali ya mapinduzi Zanzibar, Bw. Othman Suleiman wakati wa maadhimisho hayo.
DSC_0128
Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bibi Mary Massay (kushoto) akiongozana na Mkuu wa Balozi za Umoja wa Ulaya (EU) nchini Tanzania na Afrika Mashariki, Mh. Filiberto Ceriani-Sebregondi (katikati) pamoja na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez kuelekea sehemu maalum kwa ajili ya picha ya pamoja na washiriki wa mkutano wa kujadili utekezaji wa makubaliano ya haki za binadamu na maandalizi ripoti ijayo katika kuadhimisha siku ya haki za binadamu duniani.
DSC_0136
Mgeni rasmi Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mh Ali Hassan Rajab (wa pili kulia waliokaa) katika picha ya pamoja na wadau waliohudhuria mkutano wa kujadili utekezaji wa makubaliano ya haki za binadamu na maandalizi ripoti ijayo ulioenda sambamba na maadhimisho ya siku ya haki za binadamu duniani.
DSC_0144
Balozi wa Ireland Nchini Tanzania, Mh. Fionnuala Gilsenan (kulia) akibadilishana mawazo na Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bibi Mary Massay (kushoto) mara baada ya zoezi la picha ya pamoja. Katikati ni Mshauri mwandamizi wa haki za binadamu kutoka Umoja wa Mataifa Tanzania, Chitralekna Massey.

No comments: