Wasimamizi
wa Uchaguzi wakielekeza namna ya kupiga kura wapiga kura walijitokeza
kupiga kra mkoani Katavi Uchaguzi wa Seriklali za Mitaa.
(Picha zote
na Kibada Kibada –Katavi)
|
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kupiga kura wakiwa wamepanga mstari katika moja ya Vituo vya kupigia kura kitongoji cha Mnyagala Kata ya Kabungu Halmashauri ya Mpanda Mkoani Katavi. |
Mojawapo ya wapiga kura mwanamama ambaye jina halikuweza kufahamika mara moja kipiga kura kumchagua mwenyekiti wa mtaa wa Kashaulili Halmashauri ya Mji wa Mpanda kama alivyokutwa na MPIGA PICHA |
Akina mama
waliojikusanya pamoja kusubiri nafasi ya kupiga kura kuwachagua viongozi wao
kwenye uchaguzi wa serikkali za mitaa kamawalivyokutwa Kituo cha Sabato
|
Uchaguzi wa
Serikali za Mitaa Katika Mkoa wa Katavi umekamilika kwa wananchi kujitokeza
kupiga kura kwa kufuata taratibu kanuni na sheria zinazoongoza uchaguzi wa
serikali za Mitaa ingawa kulikuwa na changamoto za hapa na pale kama kuchelewa
kufika kwa karatasi za kupigia kura na vituo vingine uchaguzi kuahirishwa
dakika za mwisho kutokana na Mgombea kukosa Sifa ya kugombea .
Akizungumzia
kuahirishwa kwa uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nsanda Kata ya Ugalla
kwa kile kilichoelezwa kuwa Mgombea kukosa Sifa ya kugombea baada ya kuwa kuwa
amehukumiwa kifogo cha mwaka mmoja jela siku moja kabla ya uchaguzi hivyo
kukosa sifa ya kuweza kugombea na nafasi hiyo kubaki wazi hadi hapo
itakapotangazwa tena na mamlaka husika ya uchaguzi wa serikali za mitaa.
Afisa
uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi Betwel Ruhega
ameeleza kuwa kwa mjibu wa taratibu mgombea anapokuwa amepatikana na kosa la
jinai na kuhukumiwa kifugo tena cha mwaka mmoja hivyo anakuwa amepoteza sifa za kugombea
uongozi hivyo hafai kuwa kiongozi tena
kwa mjibu wa taratibu.
Ruhega
akaeleza kuwa aliyekuwa Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Kitogoji cha Nsanda
amekosa sifa baada ya kufugwa na siku moja kabla ya uchaguzi hivyo nafasi hiyo
kuwa wazi,kwa mjibu wa utaratibu inabidi kuahirisha ili kutoa nafasi kwa chama
kupendekeza na kuteua jina la mgombea mwingine wa nafasi hiyo ya mwenyekiti.hivyo
uchaguzi umeahirishwa hadi utakapotangazwa tena kwa mjibu wa Kanuni taratibu na
sheria za uchaguzi.sitanislau makungu
chadema
A kaongeza
kuwa maeneo mengine mambo yameenda kama yalivyopangwa na wananchi wamejitokeza
kwa wingi kupiga kura na hivi wanasubiria matokeo.
Na taarifa zilizopatikana
kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Kata ya Mpandandogo wagombea nafasi ya
Uenyekiti wa Kitongoji Igagala B’ wamegongana kura hivyo inabidi uchaguzi huo
urudiwe upya.
Kwa Mjibu wa
Afisa Uchaguzi wa Halmashauri ya Mpanda Charles Linda amesema wagombea wa
Nafasi ya Mwenyekiti wa Kitongoji cha
Igagala C Kijiji cha Igalala Kata ya Mpnda Ndogo wamegona kwa kupata kura sawa
hivyo inabidi uchaguzi urudiwe upya .
Linda
amewataja waliolingana kura kuwa ni
Mgombea wa Nafasi ya Mwenyekiti kuptia tiketi ya CCM Isaya Daud na Stanslaus Makungu kupitia tiketi ya Chama
cha Demokrasia na Maendeleo.
Katika hatua
nyingine wapiga kura wa kituo cha kupigia kura Mnyagala walilazimika kusubiri
kuanza kupiga kura majira ya saa nane mchana baada ya kuchelewa kuwafikia
karatasi za kupigia kura hivyo
kurazimika kusubiri hadi zilipo fika karatasi hizo wakaanza kupiga kura.
Kwa Mjibu wa
Msimamizi wa Kituo cha kupigia kura Steven
Msomi alieleza kuwa wananchi walijitokeza tangu asubuhi kusubilia kupiga
kura na hawakuchoka na hamasi ilikuwa kubwa hasa akina mama na vjiana wengi
wamehamasika na kujitokeza kwa wingi.na hali ya usalama ni shwari.
Katika
maeneo mengine Mkoani humo uchaguzi umeendeshwa kwa amani na usalama hadi
kufungwa kwa vituo vya kupigia kura kullikuwa hakuna taarifa zozote
zilizoripotiwa zinazohusiana na uvunjifu wa amani.
No comments:
Post a Comment