Na Magreth Magosso,Kigoma
UCHAGUZI wa Serikali za Mitaa katika baadhi ya vijiji katika
halmashauri ya wilaya ya Uvinza
na Kasulu Mkoa wa Kigoma umesogezwa mbele kutokana na changamoto ya uzembe wa
uongozi husika kushindwa kuwajibika kwa mujibu wa sheria,kanuni na
taratibu za maandalizi ya uchaguzi huo.
Mbali na hilo wagombea wa nafasi ya uenyekiti wa chama Cha
ccm Kashindi Godei na mgombea wa Chama cha ACT Musa Kafungo na Katibu mwenezi wa ACT Anzuluni Kibera
pamoja na mpiga kura Hamis Kandoga washikiliwa kwa masaa mawili kwa kosa la
kurumbana eneo la kituo.
Sababu kubwa ya kusogezwa mbele ni sintofahamu ya uraia wa
wagombea,majina ya wagombea kuwekwa katika nembo za bendera zisizo zao,ukosefu
wa vifaa na makaratasi ya kupiga kura hayakidhi hitaji la wapiga kura ambapo
inadaiwa ni uzembe wa wakurugenzi na timu ya wasimamizi wa mambo hayo.
Vituko wilaya ya Uvinza kijiji cha Kalago inadaiwa msimamizi
wa eneo hilo leo asubuhi asimamisha
uchaguzi kutokana na mashaka ya uraia wa
mgombea nafasi ya uenyekiti Chama cha
ACT aliyejulikana kwa jina moja la Mbwasu na Chama cha Chadema Shabani Matope .
Akifafanua hilo Katibu wa Chadema Mkoa Shaban Madede alisema
leo (jana) watakuwa na kikao cha
kujadili hujuma dhidi ya kusimamishwa kwa zoezi hilo ambapo sababu zake
hazina mashiko na walipomtaka msimamizi atoe barua aliyopewa na Mkurugenzi wa
Uvinza juu ya tuhuma hizo alidai asiyeridhika aende mahakamani .
Alisema katika kijiji cha Kapalamsenga mgombea wa chama cha
ccm kupitia nafasi ya uenyekiti alitaka kugombea wakati aliwekewa zuio wiki
iliyopita juu ya uraia wake na idara ya uhamiaji ilibaini si raia wa hapa na hakujibu pingamizi hadi leo siku ya kupiga kura alitaka agombee hivyohivyo
kwa shinikizo la chama tawala na ndio sababu ya msimamizi kuhairisha uchaguzi.
Katika kata ya Manyovu sababu ya vijiji vyake viwili kusimamishwa ni kuchanganywa kwa
majina ya wagombea kwa mujibu wa vyama vyao na bendera zao sivyo ndivyo na kudai hayo yote ni hujuma dhidi ya vyama
vya siasa na serikali ya chama tawala.
IAwali ngazi ya vijiji ilibainisha kwa weledi wagombea wote
wa vyama vya upinzani ajabu leo siku ya tukio majina yanabandikwa holela bila kuzingatia chama cha mgombea
Wakati huohuo Katika wilaya ya Kasulu sintofahamu kubwa ni uwekaji wa majina
hayalingani na vyama vyao.
Akielezea hilo Katibu mwenezi wa wilaya husika Masoud Kitoe
alisema kijiji cha nyakitonto wagombea
wa chama cha ccm hayakuenea waliweka majina saba badala ya 11 wakati ya
wagombea wa upinzani yapo sawa,
Kijiji cha Kalela msimamizi atoa masharti kwa wapiga kura
kuwa waweke tiki moja kati aya majina ya wagombea na s inane kwa mujibu wa
kanuni,sheria na taratibu ya idara ya uchaguzi
ilihali vifaa hakuna na walioteuliwa kusimamia wengi wao ni walimu.
Katika kijiji cha Nyamidaho ,Kulugongo,Rungwe mpya ,Kigondo,Kwaga
na Mwilavya Kabulanzwili,nyenge ,Kagerankanda,Kasengezi hivi vilikubwa na adha ya vifaa kutokuwepo na maeneo yaliyopelekwa
maboksi ya kupigia kura kulikuwa hakuna makaratasi ya kupiga kura.
Mfano kijiji cha
Kasengezi waliojiandikisha walikuwa 2,000 na karatasi zilikuwa 600
tu,hali iliyochangia uchaguzi kuahirishwa hadi jumapili ijayo (Desemba,20,2014)
Huku viongozi wa vyama husika wakiitupia lawama halmashauri husika.
Ifahamike kuwa,wilaya ya kasulu ina Mitaa ipatayo
109,Vitongoji 389,Vijiji 70 na Kata 33
na vilivyofanikiwa kufanya uchaguzi bila vikwazo ni vijiji Vitano tu,ambavyo ni
Muzye,Mganga,Nyatenda na Rungwe mpya
na Nyumbigwa.
Zaidi ya wakazi 6,000
wa mtaa wa Nyakaseke walisusia uchaguzi
mapema mwa mwezi uliopita kwa
sababu ya kugombea mpaka eneo la soko la kijiji cha Rungwe mpya yenye wakazi
16,500 ambapo kila mtaa ulidai eneo la soko ni lao .
Kitendo cha kupewa wakazi wa mtaa wa Rungwe mpya kijiji cha
Nyakaseke walionya uongozi wa halmashauri husika wasithubutu kuwapeleka masuala
ya uchaguzi ,inagwa inadaiwa baadhi ya vyama vya siasa walishawishi
wafanye hivyo.
Akithibitisha hilo Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Danny Makaga amekiri zoezi kwenda mrama
kutokana na baadhi ya vijiji na kata kushindwa kupata vifaa,majina kukosewa
kulingana na vyama husika,na kushindwa kubaini idadi ya vijiji vilishindwa
kufanya uchaguzi siku ya Desemba
,12,mwaka huu.
No comments:
Post a Comment