Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk.Agnes Kijazi
(kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake
Dar es Salaam jana, kuhusu mwelekeo wa mvua kwa kipindi cha Januari na
Februari, 2015 nchini. Kushoto ni Mkurugenzi, Huduma za Utabiri,
Dk.Hamza Kabelwa.
Wana habari wakiwa kwenye mkutano huo leo
Habari kwa hisani ya mtandao wa www.habari za jamii.com
SIKU
moja baada ya mvua kubwa kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini na
kusababisha madhara Watanzania wametakiwa kuchukua tahadhari kutokana na
kuendelea kunyesha kwa mvua kubwa za vipindi.
Hayo
yalisemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)
Dk. Agness Kijazi Dar es Salaam jana wakati akiwasilisha tathmini ya
mvua za vuli kuanzia Ocktoba hadi Disemba mwaka huu na mwelekeo wa mfumo
ya hali ya hewa na mvua kwa kipindi cha Januari na Febduari 2015.
Alisema
kutokana na mifumo iliyopo ya hali ya hewa inatarajiwa kusababisha
vipindi vya ongezeko la mvua katika baadhi ya maeneo ya Magharib kwenye
mikoa ya, Nyanda za juu Kusini-Magharibi na mikoa ya Kusini mwa nchi
kuanzia Januari na Febduari 2015.
Hata
hivyo alisema kuwa katika maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa
mwaka hususan Nyanda za Juu Kaskazini-Mashariki, Pwani ya Kaskazini,
Kanda ya Ziwa Viktoria na Kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma mvua zinatarajia
kuisha mwishoni mwa Disemba mwaka huu.
Alisema
matukio ya mvua katika maeneo ya mvua za nje ya msimu yanatarajiwa
katika kipindi cha miezi ya Januari 2015.Hali hiyo inatarajiwa katika
baadhi ya maeneo ya Kaskazini mwa mkoa wa Morogoro, Kusini mwa Mkoa wa
Pwani na baadhi ya meneo ya Mikoa Arusha , Manyara, Kagera, Geita,
Shinyanga na Mwanza.
Dk.
Kijazi alisema katika maeneo mengine yaliyosalia yanatarajia kuwa makavu
huku maeneo ya Magharibi mwa nchi, Kanda ya Kati, Nyanda za Juu
Kusini-Magharibi, Kusini mwa nchi na Pwani ya Kusini ambayo yanayopata
msimu mmoja wa mvua yanatarajiwa kupata mvua za juu ya wastani.
“Izingatiwe
kuwa pamoja na kuwepo kwa uwezekano wa matukio mengi ya mvua kubwa
katika maeneo yatakayopata mvua za juu ya wastani, hali hiyo pia
itajitokeza katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi
chini ya wastani,” alisema.
Aliongeza
kuwa matukio ya vimbunga katika eneo la kusini magharibi mwa bahari
hindi yanatarajiwa kuchangia katika mwenendo wa mvua nchini.
“Maeneo
ambayo hali ya mvua inaweza kuathiriwa zaidi na vimbunga ni pamoja na
kanda ya kati, nyanda za juu kusini magharibi, magharibi mwa nchi na
maeneo ya ukanda wa Pwani,” alisema.
No comments:
Post a Comment