Pages

KAPIPI TV

Saturday, December 6, 2014

SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF) YATANGAZA RASMI RATIBA YA MASHINDANO KOMBE LA TAIFA LA WANAWAKE YATAKAYOANZA DESEMBA 28 MWAKA 2014

 Rais Wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Mh Jamal Malinzi akizungumza na wanahabari leo katika ofisi za TFF kuhusu kampuni ya Proin Promotions ltd kudhamini Mashindano ya mpira wa miguu kwa wanawake yajulikanayo kama Kombe la Wanawake Taifa, mashindano hayo yanatarajiwa kuanza tarehe 28 Disemba kwa kushirikisha timu kutoka Mikoa yote ya Tanzania. Mashindano hayo yatazinduliwa Mkoani Mwanza kwa kuzikutanisha timu za Mwanza na Mara. Kushoto kwa rais wa TFF ni Rose Kissiwa ambae ni mwakilishi wa Chama cha Mpira wa wanawake Tanzania.Na Kulia ni Mkurugenzi wa Makampuni ya Proin , Johnson Lukaza ambao ndio wadhamini wakuu wa Kombe la Wanawake Tanzania
 Rais wa TFF akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusiana na Kombe la Wanawake Taifa ambapo ni mashindano ya mpira wa miguu kwa wanawake yaliyodhaminiwa na Kampuni ya Proin Promotions Ltd.
 Mkurugenzi wa Makampuni ya Proin , Johnson Lukaza akizungumzia jinsi kampuni ya Proin Promotions Ltd ilivyoona umuhimu wa kuchangia katika kuinua soka la wanawake nchini na kuamua kudhamini Shindano hilo lijulikanalo kama Kombe la Wanawake Taifa ambalo litaanza rasmi tarehe 28 kwa mechi ya uzinduzi kati ya Mwanza na Mara huko Mkoani Mwanza
 Meneja Biashara wa Shirikisho la Soka Nchini Tanzania (TFF) Peter Simon akizungumzia juu ya ratiba ya mashindano hayo yajulikanayo kama Kombe la Wanawake Taifa ambapo timu za wanawake kutoka mikoa yote ya Tanzania zitashiriki katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Kampuni ya Usambazaji na utenegenezaji wa Filamu za Kitanzania ijulikanayo Kama Proin Promotions Ltd
Bi Rose Kissiwa, Mwakilishi wa Chama cha Mpira wa Wanawake Tanzania akizungumzia juu ya udhamini uliotolewa na kampuni ya Proin Promotions Ltd katika kufanikisha Mashindano ya Mpira wa miguu kwa Wanawake yajulikanayo kama Kombe la Wanawake Taifa ambapo uzinduzi wa Mashindano hayo yatafanyika Jijini Mwanza kwa kuzikutanisha TImu za Mwanza na Mara.Picha zote na Josephat Lukaza  wa http://www.josephatlukaza.com

Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini Tanzania (TFF) leo imemtambulisha rasmi Kampuni ya Proin Promotions Ltd kuwa mdhamini mkuu wa Mashindano ya Mpira wa Miguu kwa wanawake yajulikanayo kama Kombe la Wanawake Taifa ambapo mashindano hayo yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi tarehe 28 Disemba 2014 katika Uwanja wa CCM kirumba jijini Mwanza kwa kuzikutanisha timu za Mwanza na Mara.

Akizungumzia Udhamini huo uliotolewa na Kampuni ya Proin Promotions Ltd, Rais wa TFF jamal Malinzi amesema kuwa Anawashukuru kwanza Proin Promotions Ltd kwa kuona umuhimu pia wa kukuza vipaji vya mpira wa miguu kwa wanawake hapa nchini kwa kudhamini mashindano ya Kombe la Wanawake Taifa ambapo katika mashindano hayo timu kutoka mikoa yote ya Tanzania zitashiriki na hatimaye kuja kupata Mshindi. Mbali na Mashindano hayo Mechi zote za Mashindano hayo zitarekodiwa na kuweza kurushwa katika vituo mbalimbali vya habari ambapo watanzania watapata nafasi ya kuwapigia kura wachezaji bora katika kila nafasi na kuwawezesha kushinda.

Akizungumzia Swala hilo Mkurugenzi Wa Makampuni ya Proin Promotions Ltd, Bw Johnson Lukaza amesema kuwa mpaka sasa Mazungumzo bado yanaendelea na wamiliki wa Vituo vya Televisheni ili kuona uwezekano wa wao kurusha Mashindano hayo na kuwawezesha watanzania kuwapigia kura wachezaji. ameongezea kwa kusema kuwa Mara tu mazungumzo hayo yakimalizika na kuweza kupata nafasi kutoka kituo chochote cha Televisheni ambacho kitakubali kurusha mashindano hayo basi umma wa watanzania watatangaziwa.

Proin Promotions Ltd ambao  ndio wadhamini wakuu wa Mashindano hayo ya Kombe la Wanawake Taifa inatoa nafasi pia kwa makampuni mengine katika kujitoa na kuungana nao ili kuweza kukuza vipaji vya mpira wa miguu kwa wanawake lengo likiwa ni kuboresha Timu ya Taifa ya wanawake Tanzania.

No comments: