Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo Desemba 26, 2014
kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ya kuwaaga jumla ya watoto
55 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo kati ya 104, waliofadhiliwa na
Lions Club ya jijini, kwa ajili ya kwenda kutibiwa nchini India. Watoto
hao 55 wa awamu ya kwanza wanaanza kuondoka nchini leo.
Rais
wa Lions (Host) Club ya Dar es Salaam, Mathew Levi, akizungumza wakati
wa hafla fupi ya kuwaaga watoto 55 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo
kati ya 104, kwa ajili ya kwenda kutibiwa nchini India. Watoto hao 55 wa
awamu ya kwanza wanaanza kuondoka nchini leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akivishwa Beji ya miaka 50 ya Lions Club na Makamu wa Gavana wa Club
hiyo, kwa nchi za Tanzania na Uganda, Hyderali Gangji, wakati wa hafla
fupi ya kuwaaga watoto wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo wanaokwenda
nchini India kutibiwa. Hafla hiyo ilifanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye
Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na
Makamu wa Gavana wa Club hiyo, wakati
wa hafla fupi ya kuwaaga watoto 55 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo
kati ya 104, kwa ajili ya kwenda kutibiwa nchini India. Watoto hao 55 wa
awamu ya kwanza wanaanza kuondoka nchini leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo Desemba 26, 2014
kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ya kuwaaga jumla ya watoto
55 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo kati ya 104, waliofadhiliwa na
Lions Club ya jijini, kwa ajili ya kwenda kutibiwa nchini India. Watoto
hao 55 wa awamu ya kwanza wanaanza kuondoka nchini leo.
Badhi ya watoto hao wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo, wakiwa na mama zao wakati wa hafla hiyo.
Badhi ya watoto hao wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo, wakiwa na mama zao wakati wa hafla hiyo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimkabidhi zawadi mtoto, Nabil Hahya (4) kutoka Jijini Dar es Salaam,
mmoja kati ya watoto 55 wa awamu ya kwanza kati ya 104 wenye matatizo ya
ugonjwa wa Moyo wanaokwenda kutibiwa nchini India, wakati wa hafla fupi
ya kuwaaga watoto hao iliyofanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli
ya Serena Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mama wa motto huyo, Amina
Yahya.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiinua glasi juu kumtakia heri Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha
ya pamoja na baadhi ya wadau wa Lions Club, baada ya hafla fupi ya
kuwaaga watoto hao.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa Lions Club, baada ya
hafla fupi ya kuwaaga watoto hao.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa Lions Club, baada ya
hafla fupi ya kuwaaga watoto hao.
Shirika
la Nyumba la Taifa (NHC) limechangia kiasi cha takribani shilingi
milioni 29 katika kuokoa maisha ya watoto wenye maradhi mbalimbali ya
moyo nchini ambao wanaondoka leo kwenda India kwa upasuaji. Watoto hao
53 wameagwa na Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal.
Akizungumza
na wazazi wa watoto hao waliofika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam leo Dk Bilal alililipongeza Shirika la Nyumba la Taifa pamoja na
wadau mbalimbali waliojitolea kuhakikisha wanakabiliana na tatizo la
moyo ambalo linaongezeka kwa kasi.
"Kama
Serikali hatuwezi kukabiliana na tatizo hili peke yetu hivyo
nawapongeza wadau mbalimbali binafsi na taasisi zilizojitolea kwaaajili
ya kuokoa maisha ya Watanzania wenzao, ni jambo linalotia faraja na ni
desturi ya Watanzania kusaidiana,"alisema.
Alisema
Serikali inaendelea na jitihada mbalimbali za kukabiliana na tatizo
hilo ikiwa ni pamoja na kujenga taasisi za kukabiliana na tatizo hilo
nchini ili kusudi hudma ziweze kuwafikia Watandania wengi zaidi.
Naye
Mratibu wa magonjwa ya moyo katika Klabu ya Lions ya Dar es Salaam, Dk.
Rajni Kanabar, alisema wagonjwa hao watatibiwa katika hospitali
mbalimbali nchini India.
Alisema
safari ya wagonjwa hao imeratibiwa kwa pamoja na Klabu ya Lions ya
Dar-es-Salaam (Host), Regency Medical Centre na Wizara ya Afya ya
Zanzibar.
Alisema
katika kundi hilo, watakuwamo wauguzi wawili na madaktari wawili na
wanatarajiwa kurudi nyumbani baada ya wiki nne zijazo.
Dk.
Kanabar alisema wagonjwa 15 watatibiwa katika hospitali ya Jaypee
Health Care Heart Institute iliyoko mji wa New Delhi na wengine 27
watatibiwa katika taasisi kubwa ya Fortis Escorts Heart iliyoko New
Delhi, India.
"Watafanyiwa
upasuaji ambao utagharimu Dola 2,500 za Marekani kwa kila mgonjwa na
watapewa Dola 500 kwa ajili ya kujikimu wakiwa huko," alisema Dk.
Kanabar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Hospitali ya Regency Medical Centre.
Alisema
hospitali ya Escorts ni miongoni mwa hospitali kubwa duniani kwa
matibabu ya moyo na imekuwa ikiwafanyia upasuaji wagonjwa wa moyo kutoka
Tanzania kwa punguzo kubwa la gharama za matibabu hayo.
Aliishukuru
Wizara ya Afya ya Zanzibar kwa kuchangia nauli za ndege kwa wagonjwa 33
na kutoa Dola 500 kwa kila mgonjwa na Ubalozi wa India ambao viza za
bure kwa wagonjwa wote kupitia balozi wa nchi hiyo hapa nchini, Debnath
Shaw.
Dk.
Kanabar aliwataja wengine waliochangia kuwa ni Bank M iliyochangia
Dola 10,000 gharama za upasuaji wa wagonjwa wanne, Shirika la Nyumba la
Taifa limechangia shilingi milioni 29 na
Klabu ya Lions Dar es Salaam (Host) Dola 16,500, Pradeep Kumar wa
Bengaluru, India Dola 16,400, Regency Medical Centre Dola 12,500,
wanafunzi wa British Columbia University Vancouver, Canada na Jumuiya
ya Theosophical ya Dar es Salaam Dola 10,000.
Wengine
ni Riyaz Hassan Ali wa Karim Foundation Marekani Dola 9,000, Familia ya
Mohamed Gulam Dewji Dola 5,000, Africarriers Dola 5,000, Lakhan Pal wa
Dar es Salaam Dola 2,500, Nashrin Sarkai wa Marekani Dola 5,000, Hazi
Abbas wa Dar es Salaam Dola 2,500, Lion Siraz Jessa wa Dar es Salaam
Dola 2,500, Lion Mohamed Laljee, Lion Yusuf Dalal, Lion Karim Meetha,
Lion Nazmu Dola 3,500, Guru Sikh Sabha wa Dar es Salaam Dola 5,000,
Harun Zacharia, Salim Turkey Dola 5,000, Dk. Kiran Nad Pallavi Patel wa
Global Foundation Marekani Dola 10,000, Habib African Bank ya Dar es
Salaam Dola 3,000 na Prem Kapoor & Family ya Mwanza Dola 3,000
na Gavana wa District 411B.
No comments:
Post a Comment