Katika
Kijiji cha Usupilo,Kata ya Misheni,wilayani Sikonge,mtoto mwenye umri
wa miaka minne,Agnes Peter,mwenye ulemavu wa viungo huku akiwa hawezi
kukaa,kusimama wala kuzungumza anadaiwa kufungiwa ndani kwa muda wa
miaka miwili pasipo majirani na viongozi kufahamu.
Mama mzazi wa mtoto huyo Sarah
Jumanne(39) anaeleza kwamba alimzaa mtoto huyo na mwanaume aitwaye Peter
William aliyemtelekeza akiwa na mimba ya mwezi mmoja.
Sarah alisema alimzaa mwanae akiwa mzima
na aliugua baada ya miaka miwili baada ya kuugua degedege na kuapata
ulemavu na kuomba asaidiwe kwani alikuwa haelewi nini cha kufanya.
“Nilimzaa akiwa mzima na aliugua degedege
na kupata ulemavu na nikashindwa kufahamu cha kufanya naomba tu
nisaidiwe”Alisema kwa huzuni.
Afisa maendeleo ya Jamii katika
Halmashauri ya wilaya ya Sikonge,Tito Luchagula,alisema unyanyapaa wa
majirani ndio chanzo na kuomba mama huyo asaidiwe.
“Kama mama huyu asingefanyiwa unyanyapaa
asingemficha mtoto wake na naomba asaidiwe kutokana na hali ya mwanae
kuhitaji msaada wa matibabu na uchunguzi zaidi”Alisema
Luchagula alidai jambo la kwanza
watakalofanya ni kumbana baba wa mtoto huyo ili atoe pesa za matumizi na
matibabu ya mtoto wakati jitihada zikifanyika kumsaidia zaidi mtoto
huyo.
Akizungumzia
tukio hilo,Afisa upepelezi msaidizi wilaya ya Sikonge,mkaguzi Joseph
Matui,aliyeongoza zoezi la kumbaini mtoto huyo,anakiri kuwa jamii
inahitaji kuelimishwa zaidi ili kuondokana na tabia ya kuwaficha watoto
wenye ulemavu.
“Jamii inapaswa kuelimika kufahamu watoto
wanapopata ulemavu hawapaswi kuachwa pasipo msaada wowote bali
wanahitaji kupatiwa matibabu”Alisema.
Majirani wa mama huyo hawakuwa tayari
kuelezea kuhusu mtoto huyo huku wengine wakidai walidhani amefariki kwa
vile hawajamuona muda mrefu.
Kujulikana kwa mtoto huyo kumetokana na
taarifa ya msamaria mwema mmoja kwa idara ya maendeleo ya Jamii katika
Halmashauri ya wilaya ya Sikonge kuwa kuna mtoto mwenye ulemavu
anayefungiwa ndani kwa muda mrefu pasipo majirani na viongozi kufahamu.
No comments:
Post a Comment