Na Magreth Magosso,Kigoma.
Mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa Serikali ya Mtaa kupitia
Chama cha (NRA) mtaa wa Vamia Kata ya Buzebazeba Halmashauri ya Manispaa ya
Kigoma Ujiji Mkoa wa KigomaYohana Frank
ameahidi kusimamia na kurejeshwa kwa fedha kiasi cha sh.milioni 600 zilizokusanywa kwa ajili ya kupatiwa hati
miliki za ardhi .
Frank alitoa kauli hiyo wakati akijinadi
katika uzinduzi wa kampeni uliokuwa chini ya Katibu wa NRA Taifa Hamis Kiswaga
uliokuwa ukihamasisha wananchi wachague viongozi
bora wenye uwezo wa kutetea na kusimamia rasilimali za umma .
“tumechoka kuonewa wakazi wa
vamia tuliowapa maisha yetu wanatuchezea akili,haiwezekani mtaa ukose huduma
muhimu za msingi,soko,zahanati na
barabara hazipitiki wakati wa masika,haina mitaro ya kupitisha maji nahaidi haya yataisha kama mtaniunga mkono “
alisema Kamongo.
Alisema Diwani wa kata ya
Buzebazeba kupitia (CHADEMA) Maftah Bahila alichangisha na kukusanya fedha milioni 34 kwenye zaidi ya kaya 40 kwa ajili ya
kupatiwa hati miliki na akaunti ilifunguliwa Exim Benki ikiwa na
wasimamizi watatu lakini mpaka leo hakuna kinachoendelea .
Aliongeza kuwa,wakimpa fursa ya kusimamia
mtaa huo atawafikisha katika vyombo vya sheria ili waeleze wananchi husika
zilipo fedha zao kwa lengo la kuweka wazi
eneo lenye changamoto ambapo linazuia maendeleo ya umma.
Mhanga wa waliochangishwa fedha
Zainabu Ramadhan alisema,Januari,2014,walichangishwa shilingi 60,000 kwa kila
kaya,wanashangaa hadi leo hakuna tarifa yeyote inayowapa matumaini ya kupatiwa
hati miliki ama kurudishiwa fedha hizo,ambapo wengi wao ni wananchi wenye
maisha magumu.
Kwa upande wa Katibu Taifa NRA Kiswaga
alisema kuwa,wakati wakielekea katika uchaguzi wa Serikali za mitaa watasikia
ahadi nyingi na nzuri kutoka kwa wagombea wa vyama vingine ambavyo wa dhamana
ya kuongoza mitaa kadhaa na walishindwa kuwajibika kwa umma kwa mujibu wa
sheria,kanuni na taratibu za kazi na kusihi wampe fursa awajibike na jamii
inufaike na rasilimali zilizopo.
No comments:
Post a Comment